Category Archives: Uncategorized

Tofauti kati ya Simu za Waterproof na simu za Water resistance

Linapokuja swala la simu kuingia maji, inaweza kuwa ni moja ya vitu watu hawapendi litoke hata kidogo. Ila kutokana na kazi tunazofanya au mazingira ambayo mtu upo, jambo hili linaweza tokea. Na simu ikiingia maji wote tunajua kinachoweza kutokea ni kuharibika kwa simu pamoja na kupoteza vitu vya muhimu vilivyo kwenye simu.
Ili kuzuia jambo hilo lisitoke, Makampuni ya simu huwa yanatoa simu ambozo zinasifa ya kuzuia maji kuingia kwenye simu. Simu hizi mara nyingi hutangazwa kuwa ni “Waterproof” au “Water resistance”. Na watu wengi wakiwa wanataka kununua simu wakiona imetajwa kuwa ni “Waterproof” au “Water resistance” huwa wanajua ni simu zisizo ingia maji.

Kitu muhimu kujua hapa ni kwamba kuna utofauti kati ya Simu zinazosemwa kuwa ni “Waterproof” na simu zinazosemwa kuwa ni “Water resistance”. Na hapa chini The bestgalaxy tunaenda kukufungua kitu muhimu juu ya utofauti huo.

Tofauti kati ya Simu za Waterproof na simu za Water resistance

Simu za waterproof na simu za water resistance zina tofauti katika jinsi zinavyozuia maji. Simu za waterproof zina uwezo wa kuzuia maji kuingia ndani yake kabisa. Lakini simu za water resistance zinakua na kiwango cha kuzuia maji kwa kiasi flani au namna flani.

Kiufupi simu hadi imeitwa “Waterproof” ni haiwezi ruhusu maji kupenya ndani kabisa. Lakini simu ikiitwa “Water resistance” huwa inaweza kuzuia maji lakini inategemeana na wingi wa maji, joto la maji, aina ya maji, muda iliokaa ndani ya maji au kina cha maji. Na unapotumia simu za Water resistance haushauliwi kuziweka kwenye maji makusudi maana zinaweza kuingia maji. Kuzuia maji kwake kuna kunailinda simu yako isiharibike pale unapo idondosha kwa bahati mbaya kwenye maji au sababu nyingine zisizo za makusudi.

Inasemekana kwamba simu nyingi huwa ni Water resistance na sio Waterproof. Na Kuna Makampuni yanaweza kuziita simu zao Waterproof kwa lengo la kibiashara lakini zikawa zinastahili kuitwa Water resistance na sio Waterproof. Kutokana na jambo hili, haushauriwi kujiamini sana kiasi cha kuiweka weka kwenye maji simu yako hovyo baada ya kuambiwa ni Waterproof.

Simu za Waterproof na Water resistance huwa zinawekwa vimipira na gundi kwenye nafasi ambazo maji yanaweza kupita. Mara nyingi simu za muundo huu huwa ni ngumu kuzifungua zinapotaka kurekebishwa kifundi na pia zikifunguliwa tu, huwa zinapoteza uwezo wake wa kuzuia maji. Mbali na jambo hil, simu hizi zinaweza poteza uwezo wa kuzuia maji baada ya kudondoshwa chini na kujigonga au kutumia kwa muda mrefu.

Ingress protection ratings (IP ratings) ni kipimo cha uwezekano wa kifaa cha kielectric ikiwemo simu zuia maji(vimiminika) na vumbi. Mfano wa IP rating ni “IP68” na imetajwa kuwa samsung galaxy s24 ultra inauwezekano huo. Namba ya kushoto “6” ni uwezekano wa kuzuia vumbi alafu namba “8” ni uwezekano wa kuzuia maji. Simu hii inafahamika kama ni “Waterproof” kutokana na uwezekano huo japo bado haushauriwi kujiachia nayo kwenye maji au vimiminika. Mwisho ningependa ufahamu kuwa Samsung Galaxy S24 ultra ni simu ya kwanza toka Samsung iliojikita kwenye Ai (akili bandia).

Sifa za mwanaume anaefaa kuwa mume

Ni ngumu kusema moja kwa moja mwanaume anaefaa kuwa mume anatakiwa awe vipi. Na ni ngumu kwasababu katika maisha, hii dhana ya “Mwanaume anaefaa kuwa mume” inafanya watu wazingatie kuangalia sifa za mwanaume. Sifa hizi huwa zinatofautiana kutokana na tamaduni, imani, na mtazamo wa mtu binafsi.
Lakini, kuna sifa muhimu ambazo mara nyingi akiwanazo mwanaume huwa zinaweza kuwa ni viashilia vya kuwa anaweza kuwa mume bora kwako katika ndoa. Baadhi ya sifa hizo tumezizungumzia hapa chini. Kama utakua ni mwanamke ambae unahitaji kujua kuhusu hili ni vema ukachukua muda wako kusoma. Kama wewe ni mwanamke hii inaweza kukusaidia katika safari yako ya kupata mume sahihi (husband material).

Sifa 5 za mwanaume anaefaa kuwa mume

Muaminifu

Mwanaume muaminifu kwako ni mwanaume ambae anaweza kuwa bora kuwa mume. Ni ngumu kuwa na mume ambae sio muaminifu katika ndoa maana kunaweza fanya uwe na wasi wasi ambao unaweza pelekea kukosa amani katika ndoa. Unaweza jikuta unamchunga kila mahari na bado unakutana na mambo mengi ya kukuumiza.
Mwanaume mwaminifu anaweza akakufanya usiwe na wasi wasi nae sana katika ndoa na hii inafanya uwe na amani nae na sio kumtilia mashaka kila mara. Na hata akiteleza unaona kabisa ni bahati mbaya.

Mvumilivu na mwepesi wa kusamehe

Mwanaume mwenye uwezo wa kuvumilia ni mwanaume anaefaa kuwa mume. Ndoa inamambo mengi sana ambayo yanahitaji uvumilivu na kuyasamehe. Kuna muda mwanamke unaweza kosea katika ndoa na kama mume wako sio mvumilivu au mwepesi wa kusamehe, inaweza kuwa ni hatari. Tukiwa kama binadamu, ni lazima tukosee katika mambo mbalimbali katika maisha. Hivyo ni vema kuwa na mtu anaeweza kuvumilia au kutusamehe. Na unatakiwa kujua kuwa uvumilivu sio muhimu kwenye kukoseana tu, hata kwenye kupambana na maisha tu bado unahitajika.

Mambo muhimu kufanya kwa mpenzi mwenye hasira au ukorofI BONYEZA HAPA>>>

Anakufurahisha na unampenda

Unaweza kuwa na mwanaume ambae anahitaji kuwa mme wako au unahitaji kuwa mume wake lakini unapaswa kujiuliza “Anakufurahusha na unampenda?”. Usije ukajitupa kwa mtu ambae hakufurahishi wala humpendi kwa dhati ili tu uitwe mke wake na wewe umuite mume. Ni vema ukaangalia kwanza kama mnafurahia ukaribu wenu kabla hamjaitwa mume au mke. Angalia pia kama mnapendana kweli kabla hamjaingia kwenye ndoa.

Anaejali kuhusu wewe na hali ya maisha yake

Unajiuliza anaejali kuhusu wewe na maisha yake kivipi? Sawa, hii tunaweza sema ni jambo muhumu sana. Mwanaume anaekujali wewe ni mwanaume Bora kuitwa mume. Kujali kunaweza kusanya mambo kama kukusikiliza, kuwa karibu na wewe, kukusaidia kwenye baadhi ya mambo na kuonesha uhitaji wa uwepo wako kwenye maisha yake.
Akiwa anajali kuhusu hali ya maisha yake pia ni jambo zuri maana ukimuita mume utakua upo ndani ya maisha yake. Kujali kuhusu maisha yake au hali ya Maisha yake kunaweza jumuisha kuwa na ndoto anazozipambania, kujua alipo na anataka kwenda wapi kimaisha, kutatua changamoto za maisha yake na kuwa dereva mzuri wa maisha yake.

Anaweza kuwa rafiki yako

Hakuna furaha kama kuwa na mume ambae ni kama rafiki yako. Yani mnaishi kwa amani, manajuana tabia na mapungufu yenu, mnatunziana siri na mnashirikiana kwenye mambo mbalimbali kama marafiki mulio shibana na sio watu mnaoogopana sana au kuwa kama maadui Kila muda.
Ukitaka kupata mume kama huyu ni vema ukajiuliza mwanaume unaetaka awe mume anaweza kuwa rafiki yako au laa.

Mwisho; Ni hayo tu tulioyazungunzia hapa lakini kunavitu vingi zaidi ya hivyo unaweza angalia kupata mwanaume sahihi kuitwa mume. Ni vema kufahamu pia, baadhi ya wanaume hubadili tabia wanapoingia kwenye kuitwa “mume” hivyo nivema ukachagua unaempenda ili isiwe rahisi kuvumilia na kutojutia.

Kuwa mjanja! Tufuate kwenye akaunti zetu mpya za kijamii ; Instagram na Facebook

Call of Duty Warzone Mobile: Mambo ya kujua kuhusu game hili

Kuna muda Activision ilituacha na game moja tu zuri la Call of Duty ambalo tunaweza kulicheza kwenye simu. Game hilo linaitwa “Call of Duty mobile” na Activision walilitoa katika mwaka 2019. Katika mwaka wa 5 toka game hilo litoke na kuwa na mafanikio makubwa duniani, wakaamua kuongeza game lingine la Call of Duty iitwalo “Call of Duty warzone Mobile”. Game hili kilikua likisubiriwa na watu wengi sana maana lilikua linapatikana katika platform nyingine za game. Lilikua rasimu kwenye vifaa vingine vya games lakini halikua rasimi kwa simu/mobile. Activision walilitoa game hili rasimi tarehe 21 mwezi wa 3 mwaka 2024.

Call of Duty Warzone Mobile

Call of duty warzone Mobile ni First-person shooter game ambalo lina mode ya Battle Royale ambayo inawakusanya watu au wachezaji zaidi ya 120 katika eneo moja wapambane kubaki hai. Ni game la kivita la mtandaoni(online) unaloweza cheza kama timu au peke yako(solo). Kama ilivyo kwenye mechi za magame mengine ya Battle Royale, mshindi ni anaebaki hai peke yake au timu inayobaki hai pekee.

Sasa ukitaka kuona raha ya Mode hii, anza na kujiuliza kama unaweza kuwekwa sehemu moja na zaidi ya watu 120 wanaopambana alafu ukabaki mzima peke yako au na timu yako? Ukihisi unaweza, pakua na kujaribu katika game hili.

Kulipakua na kulicheza

Ili kulipakua/kudownload game la Call of Duty warzone Mobile kwenye simu yako ni lazima simu ikidhi vigezo. Simu inahitajika kuwa na GB 4 hadi 8 za RAM alafu pia Adreno 618 GPU au GPU nyenye uwezo zaidi ndio zanaweza kukuwezesha kulicheza. Hayo ni kwaajili ya simu za Android tu tena Android 13 na kuendelea.
Kwenye iOS huku, kifaa chako kinatakiwa kuwa na iOS 17.0 au zaidi na GB 3 za RAM.

Simu yako ikiwa na uwezo huo ndio utaweza kulipakua gemu la Call of Duty warzone Mobile na kulicheza. Linapatikana katika Play store kwaajili ya mtu wa Android na pia inapatika kwenye Appstore kwa watu wa iOS. Lakini kabla ya yote unakiwa kujua kuwa game hili linaweza kuchukua kama GB 5 hivi katika nafasi ya simu yako. Kwaiyo hakikisha unanafasi ya kutosha na hata kwenye internet pia uko vizuri.

Endelea kuwa karibu na The bestgalaxy na usisahau kusoma na kujifunza vitu vingine vingi katika sehemu hii.

Kutatua tatizo la “CONNECTING TO ONLINE SERVICES” kwenye Warzone mobile BONYEZA HAPA>>>

Mambo ya kuepuka baada ya kuachana na Mpenzi wako

Muhusiano ya mapenzi yanaweza kuanza vizuri, yakakua, na watu wanaopendana wakawa na ndoto kubwa kwenye mahusiano hayo. Lakini katika safari ya kuelekea kutimiza ndoto zao katika upendo au maisha ya kua pamoja, kuna mambo mengi hutokea na kuyumbisha mahusiano ya mapenzi. Baadhi ya mahusiano huwa yanadumu na kuendelea kusonga mbele pamoja na mambo mengi yanayoyumbisha.


Lakini pia Kuna mahusiano huwa yanavunjika na kushindwa kuendelea kusonga mbele kabisa. Kuvunjika kwa mahusiano huwa kunazalisha watu wenye mitazamo tofauti juu ya mapenzi na tabia tofauti pia. Hapa ndio utasikia “mapenzi ya kweli hamna… siji kupenda tena” na mambo mengine kama hayo. Mitazamo hiyo mara nyingi huja baada ya maumivu yaliosababishwa na kuachana. Maumivu baada ya kuvunjika kwa mahusiano yanaweza kukusukuma ufanye vitu vingi sana.

Japo kuachana na mpenzi hufanya mtu awe na maumivu lakini kuna vitu au mambo ambayo ni vema kuyaepuka.

Mambo ya kuepuka baada ya kuachana na Mpenzi wako

Kufanya vitu ili kumuumiza

Baada ya kuachana, kunaweza kuwa na mawazo mengi sana ya kukusukuma kufanya vitu vitakavyo muumiza mtu ulieachananae. Msukumo huu unaweza kukufanya usiwe makini na kupelekea ufanye maamuzi mabaya ambayo utayaona kama yanamuumiza lakini kwa upande mwingine yana haribu maisha yako wewe. Mfano mzuri ni kujihusisha na wapenzi wengi baada ya kuachana na Mpenzi uliempeda; unaweza hisi unamuumiza ulieachana nae kwa kumuonesha kuwa watu wengi wanakuhitaji lakini kwa upande mwingine ni maamuzi hatari kwako na sio kwake. Unaweza pata magonjwa, unaweza poteza muda wako na vuruga vitu vingine ulivyopanga kufanya maishani.

Kujilaumu au kumlaumu

Baada ya kuachana na Mpenzi wako unaweza kuwa ni mtu wa kujilaumu sana au kumlaumu ulieachana nae. Lakini kujilaumu au kumlaumu hakuwezi fanya kitu zaidi ya kukuletea maumivu pindi unapofikilia. Ni vema kujisamehe wewe na yeye pia alafu ukakubali hali na kuendeleza maisha yako. Chukulia kama yaliopita yote yalipangwa kuwa hivyo kwenye maisha yako na mambo mengi mazuri yanakuja mbele ya maisha yako. Usijishushe thamani kwaajili ya mtu asiyeona thamani yako. Wewe bado ni wathamani na unapaswa kujipenda na kujithamini hata kama umeachana na mtu unaempenda.

Kufuatilia mambo yake

Kufuatilia mambo ya mtu ulieachana nae, kunaweza fanya ukawa unaumia zaidi. Ni vema kama umeachana na mtu, ukaacha kumfuatilia mambo yake maana utakua unaumia pindi atakapokua anafanya vitu vinavyo uumiza moyo wako. Epuka kumfuatilia kwa siri maana utakua unatumia kwa siri hivyo hivyo.

Uamuzi mzuri wa kufanya baada ya kuachana na Mpenzi wako na kuona hakuna uwezo wa kurudiana ni kukubaliana na hali halisi, kujipenda na kuendelea na maisha yako mpaka utakapo taka kuingia kwenye mahusiano tena. Asante kwa muda uliotumia kusoma makala hii na natumaini umejifunza kitu. Endelea kuwa karibu na The bestgalaxy kwa mambo mengine zaidi ya tuliozungumzia hapa.

Kuwa mjanja! Tufuate kwenye akaunti zetu mpya za kijamii ; Instagram na Facebook

Jinsi ya kupata Namba zilizofutika kwenye Simu

Kwenye simu huwa tunatuza namba na siku hizi Smartphone huturuhusu kutunza katika Email mbali na kuzitunza katika Laini na Simu yenyewe. Mara nyingi mtu unashariwa utunze namba za simu kwenye simu yako katika Email. Email ni sehemu nzuri ya kutunza namba zako maana huwa Inazitunza namba in cloud na kuzifanya iwe rahisi kuzipata hata utakapo ibiwa au kupoteza simu. Yani hata kama umeibiwa simu, ukiwa na taalifa za Email yako uliotunzia namba tu, unaweza ingiza email hiyo kwenye simu yako nyingine na ukapata namba za simu ulizotunza. Taalifa za Email tunazoziongelea ni Email yenyewe na Password yake tu.

Ukiona dalili hizi ujue akaunti yako ya Facebook si salama BONYEZA HAPA>>>


Katika ukurasa huu wa The bestgalaxy, hatuta zungumzia kuhusu utunzaji wa namba za simu zaidi ya hapa. Ila tunaenda kueleza jinsi ya kupata Namba za simu zilizofutika.

Jinsi ya kupata Namba za simu zilizofutika

Ikiwa umefuta namba yoyote kwenye simu yako na haipo tena kwenye Lain, Email na hata katika simu yenyewe, tambua bado unanafasi ya kuipata namba hiyo. Namba iliofutika kwenye simu inaweza kuwa katika akaunti yako ya Facebook iliopo kwenye app ya Facebook ya simu yako.

Ukiwa na app ya Facebook kwenye simu yako, huwa wanaomba ruhusa ya kuchukua namba za simu ulizotunza kwenye simu yako ili wazitumie kuiweka akaunti yako ya Facebook karibu na watu unaowajua. Hii ni moja ya sababu ambazo hupelekea kuwaona watu unaowajua kwenye Facebook.
Ukiruhusu ruhusu Facebook ichukue namba za simu kwenye simu yako, hata zikifutika kwenye simu, bado zitakuepo ndani ya akaunti yako ya Facebook. Kama uliiruhusu Facebook kuchukua namba za simu, unaweza fuata yafuatayo ili kupata Namba zilizofutika kwenye Simu yako.

  • Ingia katika Facebook na ubonyeze vimistari vitatu gusa “Settings”
  • Ingia kwenye settings alafu nenda kwenye “Accounts center”.
  • Ingia kwenye “Your Information and permissions” na ubonyeze kwenye “Upload contacts”
  • Chagua account yako ya Facebook utakayoiona Pele alafu utapelekwa kwenye ukurasa uliona orodha ya majina ya namba ambazo Facebook imeyatunza.
  • Baada ya hapo utakua ukigusa tu majina ili kuona namba. Kwenye orodha ya namba hizo unaweza kuziona namba ya simu iliofutika kwenye simu yako.

Kama haukuiruhusu Facebook kuchukua namba za simu kwenye simu yako, unaweza usiikute namba ambayo unaihitaji. Ni hayo tu tulio kuandalia hapa ila usiache kutembea The bestgalaxy.

sms za mapenzi kiingereza na kiswahili

Mapenzi ya siku hizi huwa yanahusisha sana sms kwasababu watu wengi kipindi hiki huwa wanawasilina kwa sms(ujumbe). Mara nyingi hapa The bestgalaxy tumekua tukizungumzia sms za mapenzi na hapa Kwenye ukurasa huu pia tunaenda kuangalia upende huu huu wa sms za mapenzi lakini tunajikita katika sms za mapenzi katika lugha mbili. Lugha hizi ni Lugha ya kiingereza na kiswahili. Yani tunaenda kuangalia sms za mapenzi kwa kiingereza na kiswahili.

Kuna sababu zinaweza kufanya ukawa unatumia lugha ya kiswahili lakini ukataka kumtumia mwenza wako sms ya mapenzi ya lugha ya kiingereza (English). Unaweza fanya hiyo ili kuonesha utofauti tu unapochati na mpenzi wako, unaweza kufanya hivyo pia kwasababu mpenzi wako ni mtu asie elewa kishwahili sana au anapenda kiingereza tu.

Jinsi ya kufanya mpenzi wako akuwaze kila mara BONYEZA HAPA>>>

Kama upo vizuri katika lugha ya kiingereza, unaweza tuliza kichwa na kusuka sms itayo ugusa moyo wa mpenzi wako ikiwa katika kiingereza/English. Lakini kama haupo vizuri sana au unataka kutunza muda, unaweza tumia hizi chini kwa mwanamke au mwanaume.

Ujumbe/SMS za mapenzi 5 za Kiingereza na Kiswahili

Every time I’m with you I feel like my dream has come true. I cherish you always.
Kila wakati ninapokuwa na wewe nahisi ni kama ndoto yangu imetimia. Nakupenda daima.

I love you so much. In your arms, I have found my home. You complete my life in ways I never imagined. I don’t need to lose you in my life my love.
Nakupenda sana. Katika mikono yako, nimepata nyumba yangu. Wewe unanikamilisha maisha yangu katika njia ambazo sikuwahi kufikiria. Sihitaji kukupoteza kwenye maisha yangu mpenzi wangu.

Dalili za mahusiano yanataka kuvunjika na jinsi ya kuokoa BONYEZA HAPA>>>>

Your love is the melody that fills my heart with joy. Thank you for your love honey . I love you.
Mapenzi yako ni melody(wimbo) inayojaza moyo wangu na furaha. Asante kwa upendo wako honey. Nakupenda.

With you, every day is an adventure. Loving you is the greatest journey of my life. I enjoy having you in my life.
Nikiwa na wewe, kila siku ni safari. Kukupenda ni safari kubwa zaidi ya maisha yangu. Nafurahia kuwa na wewe maishani.

Honey, i need you to know that you are the reason I believe in love. Your presence lights up my world.
Honey, nataka ujue kuwa wewe ndiye sababu ya kuamini katika mapenzi. Uwepo wako unang’arisha ulimwengu wangu.

Mwisho; Ni hayo tu tuliokuandalia hapa. Lakini kabla ya kutuma sms za kiingereza unashauriwa kufikilia kama mwenza wako hupendelea kiingereza au laa. Maana kwa watu waliozoea kiswahili hata wakiwa wanajua kiingereza kunaweza kuwa na ugumu wa maneno ya kiingereza kuugusa moyo wake. Yani wanaweza wanajua kiingereza lakini wakasisimuka zaidi wakiambiwa “Nakupenda” kuliko “I love you”.

Kuwa mjanja! Tufuate kwenye akaunti zetu mpya za kijamii ; Instagram na Facebook

WOWCube: Ni kifaa gani hiki na kinatumikaje?

Kama umewahi chezea “Rubik’s Cube” basi unaweza kuielewa zaidi WOWCube. “Rubik’s Cube” ni kifaa kilichoundwa na ErnÅ‘ Rubik mnamo mwaka 1974. Ni kifaa chenye puzzle au fumbo ambalo linajumuisha kurejesha sura sita za maraba katika usawa baada ya kuvurugwa. Kuna Cube nyingine zanaubo mbali na mraba. Rubik’s Cube imekuwa maarufu zaidi ulimwenguni na inachezwa na mamilioni ya watu ulimwenguni.

Sasa WOWCube(WOWCUBE® Entertainment System) ni kifaa ambacho ni kama “Rubik’s Cube” lakini kipo kidigitali zaidi. WOWCube ipo kisasa zaidi kiasi ambacho inaitwa kifaa cha kucheza games. Kina kuruhusu kucheza games nyingi na unakua unacheza kwa kukizungusha, kukitikisa na kugusa screen. Kifaa hiki kina screen ndogo 24 ambazo zinakufanya uone vitu au games unachocheza.
Unakua unakichaji kama unavyochaji vifaa vingine vya kuchaji vya kidigitali alafu unaweza kukiunganisha na simu ya smartphone kwakutumia Bluetooth. Haijali ni simu ya Android au iOS, zote zinaweza kufanya kazi na hiki kifaa.


Kuna app yake unatakiwa uiingize kwenye simu ya smartphone unayoiunganisha nacho. App hiyo inaitwa WOWCube connect na kazi yake kubwa ni kukupa uwezo wa kuendesha kifaa cha WOWCube. Kupitia app hiyo unaweza ingiza games pamoja na app mpya kwenye kifaa cha WOWCube na kurekebisha vitu kama mwanga ili kuwa vile wewe unapenda.

Mbali na hayo, WOWCube pia inauwezo wa kuonesha notifications za kwenye simu ukiunganisha, tarehe (kalenda kwa ujumla), unaweza soma comics na kujifunza mambo mengine. Ni kifaa kizuri kwa watoto na wakubwa pia. Pre order kwenye website ya WOWCube, imeandikwa unaweza pata kwa kama dora 549 za kimalekani hivi. Hiyo ni pre-order.

Moja ya stori kuhusu jina lake lilivyotokea; wanasema kabla hakijaitwa WOWCube, watu alipokua wakioneshwa walikua wanamshangao wa “Wow”. Basi baada ya mishangao hiyo kuwa mingi, wakaamua kukiita “WOWCube”.

Athari za mwanaume kutumia pesa kutafuta mpenzi

Kwa sasa watu husema “Mapenzi ni pesa” na moja ya mambo ambayo huongelea ni kwamba ukiwa na pesa ni rahisi kupata mpenzi. Kwa wanaume, wanasema pesa inaweza kukufungulia mwanaume nguvu kubwa ya kuweza kuwavutia wanawake.
Na wewe ni mmoja kati ya watu wanao amini hayo? Sawa, ila ukweli ni kwamba pesa inaweza kufanya uvutie wanawake. Kuna wimbo wa zamani sana wa kiingereza wa Cyndi Lauper uitwao “Money Changes Everything”, yaani “Pesa hubadilisha kila kitu”. Wimbo huu kuna sehemu ni kama mwanamke anamuacha mwanaume wake na kuzifuta ahadi zote kisha kujielezea kwenye pesa huku akimwambia “…Tuliapishana upendo wa milele. Nilisema, ndio, najua, lakini tulipofanya hivyo, kulikuwa na jambo moja ambalo hatukuwa tukiwaza nalo ni pesa. Pesa hubadilisha kila kitu…”.

Wimbo wa Cyndi Lauper uitwao “Money Changes Everything”


Lakini sio wanawake wote hua hivyo, kuna wengine wamekulia katika hali za juu za kimaisha kiasi ambacho pesa haiwashtui sana na wengine wanawaogopa au wameisha fanyiwa vitu wasivyo penda na wanaume wenye pesa mpaka wakatenganisha mapenzi na pesa kwenye vichwa vyao.

Ukiwa mwanaume mwenye pesa na uwezo au mwanaume ambae hujifanya unapesa ili kuwakamata wanawake, hiyo inaweza kuwa ni njia rahisi kwako ya kuwavutia wanawake. Lakini njia hii ya kutumia pesa au kujifanya mwenye uwezo, inathari zake mnapokua kwenye mahusiano(au ndioa kabisa).

Athari 3 za mwanaume kutumia pesa kutafuta mpenzi

Kupotea kwa hisia za upendo.

Ukitumia pesa kumvutia mwanamke ambae anavutiwa na pesa au hali yako ya juu ya kimaisha unaweza jikuta unapoteza hisia za upendo mnapoendelea kuwa Katika mahusiano. Hii inaweza kutokea endapo mwanaume utatulia na kuona mwanamke amejisahau na kuweka mbele kukutoa pesa kuliko kuonesha upendo. Yani unaweza kufikia wakati ukaona kama hauna mwenza ila una mtu mnafanya nae biashara hivi na sio mahusiano. Hali hii inaweza fanya usijihisi kupendwa wala kupenda kabisa.

Kufilisika au kupoteza uwezo wako.

Mwanaume kutumia pesa kumvutia mwanamke ambae amevutiwa na pesa inaweza sababisha ukafirisika au kupoteza muelekeo wa kimaisha pindi mukiingia kwenye mahusiano. Hii inaweza tokea kama mwanamke atakua si mshauri mzuri au atakua mtu anae bomoa uwezo wako ili kujijenga yeye bila kujali chochote kuhusu wewe. Mbaya zaidi unaweza potea kimaisha alafu ukaachwa bila mwanamke huyo kujali hali yako.

Kunyanyaswa na kudanganywa.

Unaweza itumia pesa kuingia kwenye mahusiano na mtu asiekupenda kwa dhati na baada ya muda akachoka tu kukuigizia upendo pamoja na uwepo wa pesa. Hapa unaweza nyanyaswa kihisia au ukawa unadanganywa wazi wazi. Unaweza bambeleza sana mambo yawe mazuri lakini unakua haueleweki.

Mwisho; Sio Kila mwanamke unaempata kwa kuvutiwa na pesa au uwezo wako anaweza fanya mambo hayo. Ni baadhi tu ambao wako hivyo. Wanawake wengine unaweza kuwapata kwa kuvutiwa na pesa zako lakini wakakupenda na kuwa na mchango mkubwa katika maisha yako mukiwa kwenye mahusiano. Kikubwa ni kuwa makini ili kuepuka athari tulizo zungumzia. Endelea kuwa karibu na The bestgalaxy.

Jinsi ya kutumia bando kidogo unapokua Instagram

Mtandao wa instagram ni moja ya mitandao huwa inatajwa sana katika upande wa mitandao yenye kutumia sana data au bando la internet kwenye simu. Katika uzoefu wako wa kutumia mtandao huu kutoka Meta, unahisi unatumia sana bando la internet? Mh sijui kwa upande wako unawazo gani lakini ukweli ni kwamba mitandao ukiwemo instagarm ambayo hujihusisha na video huwa inatumia sana bando.

Instagram ina video ambazo hua zinajiplay bila hata uamuzi wa mtumiaji na video hizi hua zinachukua bando zinapojiplay. Mbali na video, picha zenye ubora pia zipo katika Instagram na picha zenye ubora hua zinachukua bando kuliko zisizo na ubora. Lakini hatuwezi sema mambo hayo kwenye instagram ni mabaya maana ndio kati ya mambo hufanya mtu ufurahie kutumia mtandao huu. Kama jambo la bando linakuumiza sana unawezafanya yafuatayo kutumia bando kidogo unapokua Instagram.

WhatsApp yako inatatizo? Jifunze jinsi ya kutatua hapa>>>>

Jinsi ya kutumia bando kidogo unapokua Instagram

Njia rahisi na rasmi ya kupunguza matumizi ya data au bando lako la internet ni kutumia App ya Instagram Lite. App ya Instagam Lite ni app ambayo imeundwa tofauti na jinsi ilivyo App ya Instagram ya kawaida. App hii ni ndogo kuliko app ya kawaida na imepunguzwa baadhi ya mambo au vipengele ambavyo hutumia bando lako ikiwemo ubora wa picha na video . Hivyo, unapoitumia app ya  Instagram Lite unakua unatumia bando kidogo kuliko ambavyo ungetumia app ya Instagram ya kawaida. Haitumi bando lako sana app hii na inaweza fanya vizuri hata kama mtandao wa internet kwenye simu yako haupo vizuri.

Kama hautataka kutumia app ya Instagram lite basi ni unaweza punguza matumizi ya data kwa kuwasha kipengele cha Data saver ambacho hupatika kwenye app ya Instagram ya kawaida. Kuwasha kipengele hiki, gusa vimistari vitatu vilivyo juu upande wa profile yako ya Instagram. Baada ya hapo ingia kwenye “Data usage and media quality” na uwase sehemu ya Data saver utakayoiona hapo.

Mbali na njia hiyo, unaweza punguza pia idadi ya video unazoangalia au ukapunguza muda unaotumia katika mtandao huu ili kupunguza matumizi ya bando lako.

Katika matumizi yako ya simu usifanye vitu hivi GUSA HAPA>>>

Sms za kubembeleza mpenzi wako

Kubembeleza mpenzi wako sio kuwa mjinga. Ni moja katika ya mambo muhimu kufanya unapokua kwenye mahusiano ya mapenzi na mtu anaekupenda. Na kubembeleza hua kuna nyakati zake na sio kila wakati. Unaweza hitajika kumbembeleza mpenzi wako baada ya tukio lililomuumiza hisia zake, baada ya kuchukizwa, kuonesha hali ya kukataa jambo unalohitaji au unapohitaji kumtuliza moyo wake na kumuweka sawa katika penzi lenu.
Kuna baadhi ya watu husema “mimi sjui kubembeleza kwenye mapenzi” au “mimi siwezi kubembeleza kwenye mapenzi” lakini unapaswa kufahamu kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kubembeleza hawaujui.

Jinsi ya kufanya mpenzi wako akuwaze kila mara BONYEZA HAPA>>>


Kubembeleza mpenzi wako huonyesha upendo na kujali kwako kwake. Yani kunajinsi anahisi unamjali. Kubembeleza mpenzi wako pia kunaweza kuimarisha uhusiano wenu kwa kufanya muwe na maelewano ya amani. Kubembeleza mpenzi wako kunaweza kusaidia kukuza uhusiano wa kimwili na kihisia kati ya wewe na mpenzi wako. Kubembeleza mpenzi wako kunaweza kusaidia kujenga imani kati yenu pia.
Huo ni muhimu wa kubembeleza katika mahusiano ya mapenzi ila kabla hatujaendelea, ukizidi sana kubembeleza inaweza kuwa sio jambo zuri tena. Lakini katika ukurasa huu tunaenda kuangalia sms za kubembeleza mpenzi.
Kutokana na utandawazi, watu hutumia sms kuwasiliana na wapenzi wao. Sasa ukiwa mmoja wa watu hawa, kuna sms ambazo mtu unaweza mtumia mpenzi kubembeleza kwenye mambo mbali mbali kwenye mahusiano yenu. Sms hizo unaweza tulia na kuziandika mwenyewe au unaweza angalia sms zitakazo kufaa hapa chini na kuzitumia.

Maneno ambayo hautakiwi kusema kwa mwenza wako BONYEZA HAPA>>>

Sms za kubembeleza mpenzi wako

  • Wewe ndiye wangu mahabuba unaejua kunipa huba. Mwanamke ambae moyo umeushika. Nitabaki na wewe milele, sitochoka kukupenda malaika.
  • Kuna muda nakaa nawaza jinsi gani naweza fanya ili nioneshe moyo wangu unakupenda kiasi gani ili tu uondoe mashaka juu ya upendo wangu kwako kipenzi. Natamani hata kukupeleka kwa wangu wazazi. Nakupenda sana mpenzi.
  • Usije choka kunipenda honey. Na mimi siwezi choka kukupenda pia. Siwezi hata kuelezea jinsi nafurahi kuwa na wewe dear. Ninapokwambia “nakupenda” moyo wangu ndio unanituma kukuambia.
  • Amini kuwa mimi nakupenda wewe japo wanaonitamani ni wengi. Moyoni mwangu kuna chumba chako wewe, sina vyumba vya wengi na humo upo wewe tu mpenzi.
  • Tumekua hatuelewani sana katika siku hizi. Yawezekana ni shetani amekuja kutuchezea. Hebu tumshinde kwa kuanza siku ya leo vizuri kipenzi. Pamoja na yote tunayopitia, tambua sitamani kukupoteza. Moyo wangu bado unakupenda.
  • Nisikupende wewe ili nimpende nani kwenye hii Dunia? Kuwa na wewe ni ndoto niliokua nasubiri kutimiza hapa chini ya jua. Hakuna anaeweza kuniamsha kwenye ndoto hii zaidi yako. Na sitamani itokee maana nakupenda sana.
  • Ivi katika maisha yako umewahi ona penzi lililodumu kwa kusikiliza sana maneno ya watu? Mimi sijawahi, ila nimeona watu wanaodumu kwa kusikilizana tu. Hebu tupuuze ya watu twende mbele mpenzi wangu, nakupenda wewe tu.
  • Nyakati za usiku wewe hua mwezi na wakati wa mchana wewe unakua jua langu. Kiufupi umekua msaada kila wakati ili nisipote kwenye giza. Nakupenda sana mpenzi.
  • Wewe ni wapeke maishani na ninakupenda, sifikirii kukusaliti na wala sifikirii kukutenda. Nakuomba tuendelee kupendana kila siku siku habbity wangu.
  • Unataka kuondoka kwenda wapi? Unataka kunicha na nani mwenzio? Unataka kuniumiza kweli? Atatibu nani majeraha unayota kuniachia? Hebu tumia dakika chache kufikilia tulipotokea. Kumbuka kuwa nakupenda sana mpenzi wangu.

Mwisho; Sms hizi zinaweza tumika na wanawake au wanaume. Kikubwa unapotumia, hakikisha inaendana na hali yenu ya mahusiano au mazungumzo.