Category Archives: Uncategorized

Avunja rekodi ya Dunia kwa kuubadili mwilini wake

Rolf Bochholz ni mjerumani alieingizwa katika kitabu cha rekodi za dunia (Guinness World Record ) Kama mtu aliefanya mabadiliko mengi zaidi kwenye mwili wake. Mjerumani huyu anatumia jina la @robuchholz katika Instagram.

Rolf amefanya zaidi ya mabadiliko 516 katika mwili wake ikiwemo kuutoboa mwili wake,kuchora tattoo na pandikiza nyama katika paji lake la uso zinaonekana kama mapembe. 
Ametoboa vitobo vingi sana kuzunguka mdomo wake, katika pua na pajilake la uso ambayo huvimia kuweka vipuri. Anatattoo nyingi sana katika mwili wake na pia amepandikiza nyama upande wa kulia na wakushoto wa paji lake la uso zinazomfanya  aonekane kama ni mtu mwenye mapembe.

Rolf Buchholz alianza safari yake ya kufanya mabadiliko ya mwili wake akiwa na umri wa miaka 40 ambapo alianza kwa kuchora tattoo na kujitoboa vitobo kwaajili ya kuingiza vipuri.
Rolf anaamini kuwa mabadiliko anayoyafanya katika mwili wake hayambadilishi yeye kwa chochote maana unaobadilika ni mwili tu na si yeye. Pamoja na kufanya mabadiliko zaidi ya 516 katika mwili wake lakini hajatosheka hata kidogo.

Jinsi ya kuanza kulipwa kwenye channel yako ya YouTube kirahisi (Okoa muda)

Kama una YouTube channel na unabambana jinsi ya kuikuza na kuanza kulipwa basi hii ni kwaajili yako.
Ili mtu aanze kulipwa YouTube inabidi awena vigezo vya kuanza kulipwa. Vigezo viwili muhimu na vigumu kwa baadhi ya watu ni:

  • Video zako ziwe zimeangaliwa kwa masaa 4000.
  • Uwe na Subscribers 1000 au zaidi.


Ukiachilia mbali vigezo hivyo unatakiwa pia kuwa na video ulisotengeneza mwenye. Ukiwa na vigezo hivyo unaweza kuomba YouTube na waanze kukulipa.

Sasa wewe kwenye YouTube channel yako unavigezo hivyo?

Kama vigezo vya Subscribers 1000 na Masaa vimekua ni vigumu kwako basi sisi tutakusaidia kupata vigezo hivyo kirahisi bila kupoteza muda.
Tunaweza kuoneza Subscribers 1000 na Masaa 4000 ndani ya siku tatu TU kwenye Channel yako ya YouTube. Na tukikuongezea utakua na uwezo wa kuomba YouTube wakulipe bila Tatizo.

Tumeleta njia hii kama bure tu Kwa watu wanao pambana kwenye YouTube. Ila itabidi ulipie ghalama ambazo tutatumia kukutimizia hivyo viwango.

Kama unataka subscribers 1000 ni Tsh 150,000 tu.
Masaa wanayotaka YouTube ni 4000. Sisi tunafanya kuongeza masaa 1000 Kwa Tsh 37,000 tu. Yani kutaka yote 4000 utagalamia Tsh 148,000 tu.

Unaweza kuwa unaineza masaa 1000 Kila mwezi,. Yani Kila mwezi Tsh 37,000…


Kwaiyo hapo ni wewe tu nakuanza kulipwa. Na ukumbuke kua baada ya kuanza kulipwa utakua unaendelea kuongeza Subscribers huku ukiwa unakua Hela ya kazi unayoifanya. Na YouTube channel yako inapanda thamani kwani hata ukitaka kuiuza utauza bei kubwa maana inalipwa na YouTube.


Kama unahitaji kufanyiwa wepesi huu basi tucheki WhatsApp Kwa kugusa kitufe hapa chini. Tutakushauri pia.

The Bestgalaxy: Jinsi ya kuweka app yetu kwenye simu yako, tupate kirahisi!

Mahali hapa watu wajanja hujifunza vitu mbali mbali kuhusu teknolojia, mapezi na maisha kiujumla. Nikukumbushe tu kuwa unaweza swali, maoni au ujumbe wako kwenye WhatsApp Kwa kugusa HAPA>>>

Mbali hayo pia unaweza jiunga nasi kwenye WhatsApp tukawa tunataalifu kwa njia ya WhatsApp kuhusu vitu vitu vipya tunavyovitoa kwaajili yako. Ukitaka kujiunga na huduma hii, save Namba hii: 0622 586 399 Kwenye simu yako Kisha itumie ujumbe “Niunge na The Bestgalaxy kwenye Whatsapp”

Njia rahisi ya kuipata website hii ni kuiweka kama app kwenye simu yako. Unaiweka vipi? Fuata maelekezo yafuatayo:

Nenda kwenye Ukurasa wetu wa kwanza kabisa Kwa kugusa HAPA>>> Kisha kutakua kama picha inavyoonekana hapa chini👇

Gusa vidoti vitatu vilipo upande wa juu wa app yako. Kama jinsi inavyoonesha picha hii👇

Baada ya kugusa zitakuja chaguzi nyingiii. We gusa sehemu ilioandikwa “Add to home screen” kama inavyoonesha picha hii 👇

Baada ya kufanya hivyo, gusa Nemo “Add” kama picha inavyoonekana hapa chini 👇

Ukisha gusa add app yetu itakua katika simu yako kama unavyoona hapa chini 👇

Kwa kufanya hivyo utakua unauwezo wa kutembelea mahali hapa kirahisi kabisa. Usisahau kuwasiliana nasi na kutujuza mambo gani unahitaji zaidi toka kwetu.

Unaweza soma maelezo zaidi kuhusu the bestgalaxy hapa>>>>

Soma Stori 2 Fupi za Vichekisho (Vunjambavu)

KIKUNDI CHA WATALII kilitembelea mto wa kufugia mamba na walikuwa wakielea kwenye meli ndogo katikati ya mamba wenye njaa. Ikasikika sauti ya mmiliki wa eneo hilo ikisema: “Atakaye ruka kwenye maji na kuogelea kutoka nje atazawadiwa dola milioni 10”. Kila mtu kimya, ghafla mwanaume mmoja akajirusha majini. Alikimbizwa na mamba kwa bahati nzuri alitoka salama. Akatangazwa mshindi. Wakati anarudi hotelini na mkewe akamwambia mkewe “Aisee sijajirusha mwenyewe majini, kuna mtu alinisukuma nikapambana niokoe maisha yangu”. Mke wake akatabasamu na kusema “Ni mie ndio nilikusukuma”. Wewe ungemfanyaje kama ni mkeo? Anyway, “Nyuma ya kila mwanaume mwenye mafanikio kuna mwanamke anayemsukuma kufikia mafanikio”.🤣🤣🤣

UMEMUAGA mkeo unaenda kazini, ukapita kwa mchepuko wako, wakati unajimwaya-mwaya na mchepuko, mume wa mchepuko akagonga mlango, ikabidi ufichwe uvunguni mwa kitanda.
Wakati bado upo uvunguni ka mchepuko kakamuaga mume wake kwamba, kanaenda saloon, mume wa ka-mchepuko naye akaona ndo muda wa kuita mchepuko wake, akauita ukaja, wakajimwayamwaya kwa sana muda huo wee bado upo uvunguni. Mara mchepuko wako akarudi kutoka saloon, akagonga mlango, ikabidi mume wa mchepuko wako aufiche uvunguni mchepuko wake.
Kucheki hivi kumbe mchepuko wenyewe ndo mke wako uliyemuaga unaenda kazini, kwa hiyo wewe na mke wako wote mkawa mmefichwa uvunguni…Ukisikia vita ya tatu ya dunia, ndo hii sasa.

Magemu ya magari ya kucheza kwenye simu

Tukizungumzia magemu ambayo watu hupenda kuyacheza basi hatuwezi acha kuyataja magame ya magari. Magemu ya magari yamekua yakipendwa na watu wengi sana Duniani kwakua ni magemu mazuri Sana na humfanya mchezaji afurahie uchezaji wake. Hapa nimekuandalia orodha fupi ya magemu mazuri ya magari unayoweza kuyacheza kwenye simu yako ya Android. 

1. Real Racing 3

Kama unapenda magemu mazuri na bora ya magari hakikisha haukosi game la Real Racing 3 katika simu yako. Gemu hili huchezwa Online na Offline yaani unaweza cheza kwa kutumia data au bila data. Ukitumia data(Online) utakua ukishindana na watu halisi wanao cheza gemu hilo muda huo katika nchi mbalimbali hivyo kila gari utakaloliona humo jua linaendeshwa na mtu alieshika simu kama wewe. 
Kama ilivyo kawaida ya magemu ya online, gemu hili linamuonekano mzuri sana uliobeba uhalisia wa mashindano ya magari. Kuna aina nyingi sana za magari mazuri na yenye kasi Sana. Linakupa uwezo wa kubadili kamera utakavyo.
Real Racing 3 ni moja ya magemu yapatikanayo playstore na hupatikana kwa MB 40 tu lakini ukishalipakua na kulifungua utatakiwa ulisubiri lipakue data zake na inashauriwa uwe na nafasi isiopungua Gb2.5. Unaweza kulipakua kirahisi  kwa kugusa INSTALL

Magame ya Mazuri ya Truck ya kucheza kwenye simu BONYEZA HAPA>>>

2. Asphalt 8 airborne

Ni gemu zuri sana la magari lililochini ya Gameloft. Gemu hili limetengenezwa likiwa kama ni muendelezo wa magemu ya Asphalt.Katika orodha ya magemu ya magari yenye ubora wa hali ya juu katika muonekano, hauwezi acha kuliweka gemu hili kwakua linamuonekano mzuri Sana.Gemu hili huchezwa Online yaani kwa kutumia data pia huchezwa offline nikiwa na maana bila kutumia data.Ukitumia data(Online) utakua ukishindana na watu halisi wanao cheza gemu hilo muda huo katika nchi mbalimbali.Gemu la Asphalt 8 airborne hupatikana playstore kwa GB 1.6   na unaweza kulipata kirahisi kwa kugusa INSTALL


3. Drift Max Pro




Ni gemu la magari ambalo mpaka sasa linachezwa na zaidi ya watu milioni 50 ulimwenguni. Gemu hili linahusu mashindano ya kuyaburuza magari. Pia lipo vizuri kwenye upande wa ubora wa muonekano ukilinganisha na baadhi ya magemu mengine ya magari.Kama unapenda kushindana online na watu toka sehemu mbalimbali za dunia basi gemu hili pia linakupa nafasi ya kucheza na watu wengine online. Hupatikana kwa MB 361 katika Playstore na unaweza kulipata kirahisi kwa kugusa INSTALL

Battle Of Agents: Gemu kuchezwa na watu wawili au zaidi bila data/internet  GUSA HAPA>>>




4. GT Racing 2

GT Racing 2 ni gemu lingine toka Gameloft ambalo unaweza kulicheza bure kabisa na bila kutumia data (Offline) lakini pia kama utahitaji kushindana na watu wengine toka sehemu mbalimbali  za dunia kutika kuendesha magari basi utalazimika kutumia data. Gemu hili mpaka sasa limechezwa na watu wengi sana hapa duniani na wamelisifu kuwa ni lenye muonekano mzuri na linawafanya wahisi uhalisia wa mchezo wa magari.Linapatikana playstore kwa GB 1.1 na unaweza kulipata kirahisi kwa kugusa INSTALL

5. Asphalt 9 Legends

Hili ni gemu toka kwa watiotengeneza gemu la Asphalt 8 airborne na limetengenezwa kama muendelezo wa magemu ya Asphalt. Linaweza chezwa na kila mtu kwasababu lina Controls nyepesi kiasi ambacho hata mtoto mdogo anaweza kuzielewa. Katika gemu hili kuna gari za nyingi na zenye kasi sana. Mpaka sasa linachezwa na watu zaidi ya milioni 50 na wengi hulipenda kwasababu linamuonekano bora.Huchezwa kwa kutumia data na linakukutanisha na watu toka sehemu mbalimbali za dunia ili kushindana katika kuendesha magari. Hupatikana playstore na unaweza kulipata kirahisi kwa kugusa INSTALL

Unasumbuliwa na kelele za sms za Magroup ya WhatsApp? Fanya hivi

Wengi tumekua tukitumia WhatsApp katika kuwasiliana na ndugu na jamaa zetu kutoka sehemu mbalimbali za dunia. Pia tumekua tukijiunga katika Magroup (Vikundi) ambavyo nia na madhumini yake ni kutujumuisha kwa pamoja ili tuweze kujadili au kubadilishana mambo mbalimbali. 
Kuwa na group si tatizo ila tatizo huja pale group linapokuwa na watu wengi wanaochati kipindi wewe hauna muda wa kuchati kutokana na sababu mbalimbali na kukupelekea kuona sms za wengine kuwa kero kwakua huingia kwa kelele mfululizo.
Kama unagroup ambalo husababisha kelele kutokana na message zake, unaweza lifanya yafuatayo ili kulifanya liingize message kimya kimya;

  • Nenda katika ukarasa wako wa WhatsApp kisha lishikilie group lenye kelele kwa muda usiopungua sekunde tatu Kama inavyooneshwa hapo chini.
  • Ukishikilia kwa muda wa sekunde tatu group litajipiga tiki na maeneo ya juu ya WhatsApp kutatokea chaguzi: katika chaguzi hizo utaona alama ya spika iliokatwa. Alama hii inamaanisha kulikarisha kimya group hivyo utaigusa alama hiyo kama picha inavyokuonesha hapa chini. 
  • Baada ya kuigusa alama hiyo utaletewa chaguzi uchague group hilo liwekimya kwa muda gani kwaiyo utachagua masaa8, wiki 1 au milele kisha utagusa neno “Ok” kama inavyooneshwa katika picha.

Baada ya kufanya hayo utakua umetatua tatizo la kelele maana sms za group hilo zitakua zinaingia kimya kimya. Na unachotakiwa kujua ni kwamba kama utachagua masaa8 basi baada ya masaa8 group litakua linaingiza sms kwa kelele kama kawaida na hata ukichagua wiki, wiki likiisha kelele zitakua palepale ila ukichagua milele hutaskia kelele za group hilo mpaka utakapo lishikilia tena group hilo na kugusa kialama cha sipika isiokatwa ili kuliweka huru.
Kama ni mtu ambae unamagroup mengi au unamagroup ya ajabu ajabu unaweza tumia njia hii kuepuka kelele na kulifanya group lisije kuleta taalifa za sms za ajabu ajabu.

Jinsi ya kuangalia mpira live kwenye simu (Bure)

Kama ni mpenzi wa muda wa kuangalia mpira wa miguu wa nje ya nchi, nadhani umeshawahi kosa kuangalia  mechi ulioipania kwasababu mbalimbali ikiwemo kuwa mbali na Tv. Teknolojia inazidi kukua kila siku na kuturahisishia mambo. Sasa unaweza angalia mechi Kali za mpira wa miguu kupitia simu yako mubashara(Live) ukiwa popote. hapa tutakujuza jinsi ya kuangalia mpira wa nje karibu mechi zote kwenye simu yako BURE.

Simu ikiingia maji unatakiwa kufanya nini? GUSA HAPA>>>

Ikiwa unahitaji kuangalia mpira live kwenye simu yako, utahitajika kuwa na app maalumu kwaajili ya kuangalizia mpira. App hizi zipo nyingi sana katika playstore(Android) lakini mimi nakushauri uchukue app nyepesi na isiokula sana Mbs iitwayo Live Football Tv.

App ya Live Football Tv ni app ya kuangalia mpira live kwenye simu yako. Mpaka Sasa inatumiwa na zaidi ya watu Milioni ulimwenguni na wanaisifu kwa kuonesha mipira mingi bila matatizo. Mbali na kukuonesha mechi live(mubashara), huwa inakupa matokeo na video za matukio muhimu ya mechi zilizomalizika kwaiyo Kama haukua na bando la kutosha kuangalia mpira mzima, unaweza angalia video ya goli lilivyofungwa tu. Pia inakupa nafasi ya kuangalia vipindi vingine vya kimichezo bure toka Ptv sports. 

App hii ya kuangalia mpira live haipatikani Playstore kwasasa ila unaweza kitafuta Google na kuipakua. Pia Unaweza ipakua kirahisi kwa kugusa hapa>>> INSTALL. Na baada ya kuipakua, hauitajiki kujisajili au kufanya Jambo lolote la kujiunga ili kuitumia. Ni kuifungua na kuinjoi…

Fahamu kuwa: App nyingi zinazowezesha kuangalia mpira bure huendelewa Playstore kutokana na Kuvunja sheria za Playstore. Ikiwa app nilioitaja nayo itaondelewa basi unaweza ipakua app nyingine nje ya Playstore Kwa kugusa HAPA>>>

Jinsi ya kuangalia mechi za Tanzania kwenye simu GUSA HAPA>>>

Je, ni Mbs ngapi zinahitajika kuangalia mpira mzima(Dk90) kwenye simu?

Hili ni swali ambalo wengi hujiuliza, wanapohitaji kuanza kuangalia mpira kupitia simu. Ukweli ni kwamba, kadri video inavyokua na muonekao mzuri ndivyo Mbs huwa zinalika nyingi. Itakua ni vizuri zaidi Kama hautakua na chini ya Mb900 ili kutokua na wasiwasi wa bando kuisha.

Magemu ya Mpira ya kucheza kwenye simu GUSA HAPA>>>

{“remix_data”:[],”remix_entry_point”:”challenges”,”source_tags”:[“local”],”origin”:”unknown”,”total_draw_time”:0,”total_draw_actions”:0,”layers_used”:0,”brushes_used”:0,”photos_added”:0,”total_editor_actions”:{},”tools_used”:{“ai_enhance”:2,”square_fit”:1,”transform”:1},”is_sticker”:false,”edited_since_last_sticker_save”:true,”containsFTESticker”:false}

Jinsi ya kutumia internet BURE kwenye simu yako

Kama unavyojua kuwa Kwa sasa vifurushi vya internet vimepanda sana ukilinganisha na kipindi cha nyuma. Lakini habari njema ni kwamba, unaweza kutumia internet BURE kabisa bila hata Bando. Hii ni kweli japo baadhi ya watu huwa hawaani kitu hiki… Lakini ukweli nikwamba kutumia internet BURE inawezekana.

Kunanjia nyingi sana ambazo mtu unaweza zitumia kupata internet BURE kwenye simu yako. Leo nataka kushea na wewe njia ambayo nimeitumia kupata internet BURE kabisa na inafanya kazi 100% kama unatumia laini ya Tigo… Lakini hii ni for education purpose… Hebu angalia picha hii inayokuja onesha nikiangalia YouTube bure bila bado..

Pata BAND0 kubwa la internet Kwa Bei rahisi GUSA HAPA>>>

Kwanini bando lako la wiki la internet huisha ndani ya siku Moja/mbili? GUSA HAPA>>

Sasa kama unahitaji app ni BURE kabisa. Unachotakiwa takiwa kufanya ni kuipakua(Download) kwenye simu yako Kisha install kwenye simu. Baada ya hapo utatakiwa kuifungua ukiwa na bando la internet alafu itaingiza data zake Kwa muda wa sekunde chache tu. Ikisha Ingiza data zake utatakiwa kuweka laini ya Tigo ambayo Haina Bando. Ukishafanya hivyo ifungue tena iyo app na uguse kitufe kichoandikwa “Connect”. Baada ya kuconnect utaanza kutumia internet bila bando. Jaribu kwenda YouTube au Google kucheki kama Iko sawa.

Kama uataka kujifuza mambo mengi kuhusu simu yako na mambo ya teknolojia, usiache kutembelea website hii… Tutakujuza vitu vingi kuhusu Technology.

Mtu akiku “Block” WhatsApp unaweza fanya hivi kuchati nae GUSA HAPA>>>

NJIA HII INAWEZA KUTOFANYA KAZI KWA SASA!

Movies za kutafsiliwa GUSA HAPA>>>>

Magemu mazuri ya kucheza kwenye simu (Android)

Kama wewe ni mpenda magemu na unatumia simu yako ya Android kucheza magemu basi hapa tumekuandalia orodha ya magemu machache ambayo unaweza ya cheza na ukafurahia zaidi muda wako wa kucheza magemu kwenye simu yako. Kama ndio kwa Mara ya kwanza unataka kujifunza au kuanza kucheza magemu ya Android basi ni vema ukaangalia magemu yalio katika orodha hii na ukaangalia linalo kufaa kisha ukalipakua.

Call of Duty mobile

Hili ni gemu zuri sana la kivita ambalo limetolewa na Activision. Gemu la Call of Duty mobile ni gemu lililochezwa na watu Wengi na Mpaka sasa linaendelea kuchezwa na mamilioni ya watu ulimwenguni. Kama unapenda magemu ya kivita basi gemu hili unaweza kulifulahia zaidi lakini unachotakiwa kujua nikwamba game hili ni la Online. Kwa lugha nyingine tunaweza kusema gemu hili linahitaji internet ili kulicheza. Kitu kizuri kuhusu magemu hili ni kwamba unaweza kucheza na watu wengine na pia Kuna mode ningine za kucheza zinazoweza kufanya usichoke kulicheza. Ili kulipata kirahisi gusa HAPA

Jinsi ya kutengeneza Avatar kwenye Facebook (Katuni)

Bus Simulator Indonesia

Bus Simulator Indonesia ni moja ya magame ambayo huchezwa na watu wengi sana na mpaka sasa limechezwa na watu wasiopungua Milioni 50 na wengi hulifahamu kwa jina lake la BUSSiD. Ni game lililotolewa mwaka 2017. Game hili ni la Online yaani ili kulicheza utahitajika kutumia data. Kama nimpenzi wa game za muundo huu basi hakikisha unapakua game hili maana ni game zuri sana.Kitu unachotakiwa kukifahamu ni kwamba mazingira na magari yalio katika game hili yanayofana na mazingira ya Indonesia ndiomana likawa na jina Indonesia.Linaweza kuchezwa na watu zaidi ya mmoja (Online). Linapatika playstore kwa MB zisizopungua 272. Unaweza kulipakua kirahisi kwa kugusa HAPA

Traffic Rider

Kama ni mtu unaependa magame mazuri na unavutiwa zaidi na game za pikipiki basi game la Traffic Rider ni game litakalokufurahisha zaidi.
Game hili mpaka Sasa limechezwa na watu zaidi ya Milioni 7 ulimwenguni na asilimia kubwa ya watu hao wamelipenda.
Linamuonekano mzuri, Sauti zenye uhalisia na majira yenye uhalisia maana kuna hadi mission za usiku. Kadr unavyoendesha kasi pikipiki na kuovertake magari ndivyo unavyojiongezea idadi ya Scores. Lina missions zaidi ya 70 na kuna zaidi ya pikipiki 20 tofauti tofauti.Traffic Rider ni game lipatikanalo Playstore na lina MB90 tu. Hukubali mpaka katika simu zenye RAM 1 bila shida yoyote. Kama utahitaji kulipata kirahisi game hili gusa HAPA

Jinsi ya kutengeneza Pesa kwa kucheza games mtandaoni BONYEZA HAPA>>>


Occupation 2.5

Ni gemu ambalo unalicheza ukiwa Kama mtu ambae upo kwenye mji uliochafuka na kila mtu naeishi katika mji huo anaishi kwa hofu kubwa kutokana na uwepo wa wafu wanaotembea yaani Zombies na baadhi ya viumbe vingine visivyo na urafiki na binadamu. Ni moja ya magame mazuri yanayopatikana kwa Mbs chache katika playstore. Lina nyumba zinaingilika na unawachezesha wahusika zaidi ya mmoja katika mji huo. Unaweza kulipata kirahisi game hili kwa kugusa HAPA

EA Sports UFC

Unapenda magemu ya kupigana? Kama Unapenda magemu ya kupigana basi gemu la EA Sports UFC ni game ambalo halitakiwi kukoswa kwenye simu yako. Gemu hili ni moja ya magemu mazuri sana ya kupigana. Lina muonekano mzuri mno ambao utakufanya ufurahie kulicheza. Linahusu kupigana kwa kutumia ngumi na mateke.

Ukiona dalili hizi Jua Account yako ya Facebook  imedukuliwa na si salama GUSA HAPA>>>>

Limekusanya wapiganaji wengi maalufu duniani ambao utatakiwa kuwafungua kutokana na uchezaji wako. Gemu hili linaweza kuchezwa Offline na Online. Ukiwa unacheza Online unakua na uwezo wa kucheza na watu wengine toka sehemu mbalimbali za dunia na utatakiwa kupambana nao na kufanya wapoteze dira kwa vitasa(ngumi) na mateke ya mitindo mbalimbali ili uibuke mshindi. Unaweza lipata katika playstore kwa kugusa HAPA

Overkill 3

Hili ni gemu zuri sana la Action ambalo mpaka sasa limechezwa na watu zaidi ya milioni 5. Linamuonekano mzuri na watu wengi wanalipenda kutokana na muonekano wake unaofanana na Caver Fire. Gemu hili huchezwa bila data (Offline) pia linaweza kuchezwa na watu zaidi ya mmoja kwa kutumia data (Online).Inashauriwa anaecheza gemu hili awe na miaka 16 na kuendelea. 
Overkill 3 ni gemu lipatikanalo Playstore kwa kama MB 401 ivi na unaweza kulipata kirahisi kwa kugusa INSTALL

Takashi Ninja Worriror: Shadow of last samurai



Hili ni moja ya magemu mazuri sana ambayo kwa sasa yako trend katika playstore. Gemu hili ni la kijapani na linamuhusu kijana Takashi ambae anaingia katika kulipa kisasi kutokana na watu wake kufanywa vibaya. Ukilipakua utaweza kulicheza muda wowote na bila kukugharimu chochote maana gemu hili huchezwa bila data (Offline) pia hupatikana kwa MB chache sana zisizopungua MB 87.
Unaweza kulipata kirahisi katika playstore kwa kugusa  INSTALL

Modern Strike Online

Ni moja ya magemu bora ya kivita ambayo huchezwa Online tu. Limechezwa na watu wengi sana wasio pungua Milioni hamsini(50).Gemu hili ni moja ya magemu yanayofanana na gemu la Call of duty hivyo kama unapenda magemu ya jamii ya Call of duty, usiache kucheza game hili.
Katika game hili unaweza cheza na marafiki zako Online kwa kiunda timu ya kuwaangamiza maadui au mukashindana kuua maandui ili atakaewaua maadui wengi awemshindi.
Modern Strike Online ni gemu lipatikanalo Playstore kwa MB zisizopungua MB 494. Unaweza lipata kirahisi kwa kugusa INSTALL

Movies za kutafsiliwa GUSA HAPA>>>>

Real Moto

Kama ni wewe ni mpenzi gemu za mashindano ya pikipiki basi real moto linaweza kuwa bora sana kwako. Game hili huchezwa bila kutumia data yaani ni gemu la Offline. Limechezwa na zaidi ya watu Milioni kumi(10). Utaweza kutunza kumbukumbu zote za gemu hilo kwenye email yako ili simu ikipotea uendelee  kucheza palepale ulipoishia kucheza gemu hilo pindi utakapopata simu nyingine na kuiingiza email yako.
Gemu hili hupatikana playstore  kwa MB 143. Unaweza kulipata kirahisi sana kwa kugusa INSTALL

Garena Free Fire

Garena Free Fire linatumia data na lipo hivi; Unamchagua mtu wako utakaemchezesha kisha unatupwa katika eneo moja na wenzako 49 wanaocheza gemu hilo muda huo duniani ili mupigane na uwemzima. Kwaiyo kila mtu utakaemuona katika gemu hili ni mtu anaepambania maisha na anaecheza kama wewe.
Zaidi ya watu Milioni 500 ulimwenguni wanalicheza Gemu hili kupitia vifaa vyao vya Android. Ni gemu linalopendwa na watu wengi kutokana na kuwa dogo kuliko magemu mengine ya muundo huu ambayo ni PUBG na CODM. 
Unaweza kulipakua katika playstore kwa MB 674 pia unaweza rahisisha upatikanaji wake kwa kugusa INSTALL

Battle Of Agents: Gemu kuchezwa na watu wawili au zaidi bila data/internet  GUSA HAPA>>>

Rarry Fury: Extrime racing

Kama unapenda gemu za magari usiache kupakua gemu hili lenye utofauti mkubwa na magemu ya magari yanayotamba kila mwaka. Game hili ni moja kati ya magame yanayopendwa na watu na mpaka Sasa limepakuliwa na zaidi ya watu Milioni 50. Linauhalisia wa kufurahisha wa mashindano ya Rarry.
Ukiachilia mbali muonekano wa game hili kuwa mzuri pia game hili linawezwa chezwa na mtu mmoja Offline au zaidi ya moja Online.Lina chukua kama MB 120 kulipakua na linapatikana katika playstore. Unaweza lipata kirahisi kwa kugusa INSTALL

eFootball

Ukiongelea gemu kali za mpira wa miguu katika mwaka huu huwezi acha game hili. Gemu hili limepakuliwa na watu wengi sana hapa duniani na hii ni kwasababu liko vizuri. Kama umeshawahi cheza magemu ya PES basi tambua kuwa “eFootball” ni lile lile PES ila wamebadilisha jina tu.

Linachezwa Online na inashauriwa kuwa na mtandao usiosumbua ili uweze kulifaidi gemu hili bila usumbufu.Hupatikana playstore kwa GB 1.6 pia unaweza kulipata kirahisi sana kwa kugusa INSTALL

Simu ikiingia maji unatakiwa kufanya nini? GUSA HAPA>>>

Real Boxing


Hili ni gemu la mchezo wa ngumi ambalo mpaka sasa limechezwa na watu wasiopungua Milioni 10 ulimwenguni. Lipo vizuri  sana kwanzia muonekano hadi sauti za vitasa(Ngumi). Kama ni mpenzi wa magemu ya kupigana, usikubali kuliacha gemu hili maana ni gemu lenye uhalisia wa mchezo wa kupigana wa Boxing.
Inashauriwa anaecheza game hili asiwe na miaka chini ya kumi na sita (16+). Game la Real Boxing hupatikana playstore kwa kama MB 291 ivi na unaweza kulipata kirahisi kwa kugusa INSTALL

Jumanji: Epic run

Kama unaijua vizuri filamu ya Jumanji au gemu la Tempo Run basi unaweza kulipenda zaidi hili gemu maana limeundwa kutokana na filamu ya Jumanji na muundo wake unafanana na gemu maarufu liitwalo Tempo Run.Ni gemu ambalo hujezwa bila data na mpaka Sasa linachezwa na zaidi ya watu million 10 duniani. Mchezaji wa gemu hili anatakiwa kuwa na umri usiopungua miaka 12.Linapatikana playstore kwa MB 154 na unaweza kulipata kirahisi kwa kugusa INSTALL

Unafahamu sumu ya Nge huuzwa bei ghali ulimwenguni?

Nge ni mmoja wa wanyama wenye sumu kali sana na sumu yake inaweza sababisha mtu kupooza mwili au kupoteza maisha japo baadhi ya aina za Nge huwa hawana sumu zenye athari kubwa.
Kuna zaidi ya aina 1800 za Nge ulimwenguni na kila Nge hutoa sumu tofauti. Nge huwa na miguu nane, macho 6 hadi 12 na mkia mrefu wenye mwiba ambao huutumia kudunga windo na kuiingiza sumu ndani yake.
Nge wadogo huwa wadudu wadogo wadogo lakini kuna Nge wakubwa ambao hula mijusi na panya.

Mbali na sumu ya Nge kuwa ni hatari lakini imekuwa na umuhimu mkubwa katika maswala ya afya ya binadamu. Wanasayansi hutumia sumu hii kutengeneza madawa ya kutibu na kuzuia magonjwa mbalimbali hasa matatizo ya ubongo na kupambana na kansa.Kwa sasa sumu ya Nge ni moja ya vimiminika vinavyouzwa bei ghali ulimwenguni ambapo inakadiliwa kwa Gramu moja tu ya sumu ya Nge inaweza kuwa zaidi ya Tsh 16,000,000.


Lakini sababu kubwa ya sumu hii kuwa ghali sio umuhumu wake bali ni mchakato ambao unatakiwa kufanyika ili kuiandaa na uzalishwaji wake ni mgumu kwakua Nge huzalisha kiasi kidogo mno cha sumu kila baada ya wiki mbili.