Sote tunafahamu kuwa Maisha yanaweza kuwa na changamoto nyingi, lakini mara nyingi mabadiliko madogo yanaweza kuleta tofauti kubwa. Kila mmoja wetu anajitahidi kufikia sehemu anayohitaji au mafanikio. Lakini katika safari ya kufikia hayo, changamoto zinaweza kuwa zinaonekana nyingi na kubwa kiasi ambacho watu huona kabisa hawawezi kutimiza wanayo yahitaji. Watu hufikia kwenye hali hii baada ya kufikia hatua ya kuona wapo mbali sana na wanachokihitaji. Yani kunaweza kuwa na umbali mkubwa sana kati ya sehemu mtu anahitaji kuwa na sehemu alipo. Au umbali kati ya mtu anaehitaji kuwa na mtu aliopo.
Makala hii itakupa mwongozo juu ya mambo madogo muhimu ambayo, ukiyabadilisha, yanaweza kubadilisha Maisha yako. Mambo haya ni mambo madogo sana lakini yakibadilishwa yanaweza kukufanya uwe mtu unaetaka kuwa au kukufikisha sehemu unayoitaka kuwa.
Ukiyajua mambo haya, utapata mwanga na njia za kuboresha maisha yako kwa kubadilisha Maisha yako kuwa vile unahitaji.
Jinsi ya kulinda Ndoto zako Maishani zisife BONYEZA HAPA>>>
Badilisha maisha yako kwa kubadilisha vitu hivi vidogo
Mambo unayofuatilia
Mambo tunayofuatilia huwa yana athari kubwa kwenye maisha yako. Mambo haya yanaweza kuwa ni vitu tunavyosikiliza, tunavyoangalia na hata tunavyosoma.
Mfano; kunamtu alianza kufuatilia mpira kwa kuangalia kwenye Tv, kwenye simu alafu akaanza kwenda mpaka uwanjani kushapikia na sasa amepewa nafasi za juu katika timu ya mpira anayoishabikia. Sehemu aliopo ni zao la vitu anavyo fuatilia.
Sasa huo ni mfano tu lakini unaonesha jinsi gani kitendo cha kufuatilia vitu kwa kusoma, kusikia au kuangalia kunaweza ingilia maisha yako.
Kama wewe ni mtu unaependa mafanikio ya jambo flani basi usisahau kufuatilia vitu kuhusu jambo hilo kwenye maisha yako. Yani unaweza jifunza toka kwa watu unapotaka kuwa kama wao, soma au angalia video zinazohusu jambo unalohitaji na hata kusikiliza pia.
Mawazo unayowaza au mtazamo wako
Unawaza nini? Ni kibaya au kizuri? Kama ni kibaya, tafuta njia ya kuanza kuwaza vitu vizuri maana Mawazo yanaweza athiri maisha yako. Anza kwakuto jiwazia vibaya wewe, kisha usiwawazie vibaya watu wengine alafu usiwaze vibaya kuhusu vitu unavyohitaji.
Ukiwaza vibaya kuhusu kitu unachotaka kukifanya au kukipata hautaweza weka nguvu ya kutosha kukipata au kukifanya. Mfano ukitaka kuanza biashara huku unawaza “Biashara hii hailipi. Inaowalipa wote itakua wanatumia dawa, sio bure” basi kunajinsi unaweza kuwa hautumii akili yako sana kwenye kufanikiwa kwenye biashara mbali na kuwaza kupata dawa ya biashara.
Usiwe na mawazo ya kushindwa kwenye kichwa chako. Na ili usiwe na mawazo ya kushindwa mara kwa mara, unatakiwa uwe na mtazamo mzuri juu ya jambo lako alafu amini kuwa upo kujifunza.
Mfano; Ukiwa unataka kufanya biashara anza na “Biashara hii watu wengi haiwalipi lakini nataka kuwa kati ya wale inaowalipa. Ngoja nianze kujifunza kwa kuifanya huku nikiwaangalia waliofanikiwa wanafanya nini”. Kwa kuwaza hayo, unaweza kuwa mmoja wa waliofanikiwa maana utajifunza kitu sahihi wanachokifanya mbali na kuhisi tu kichwani mwako.
Ukiachana na upande huo, epuka mawazo yoyote mabaya maana huwa na athari kwenye maisha halisi. Yaelekeze Mawazo yako kwenye vitu vya msingi unavyovihitaji. Tenga muda wa kutulia na kuwaza kwa upana kuhusu maisha yako na vitu unavyo hitaji.
Tofautisha kati ya kuwaza kuhusu mambo yako na kupata “Msongo wa Mawazo”. Baadhi ya watu hawajipi muda wa kuwaza mambo yako wakiamini kuwa huo ndio msongo wa Mawazo. Waza kuhusu maisha yako, vya kubadilisha vibadilishe na vya kukubaliana navyo, vikubali. Jifunze kutoka kwa muhusika mkuu kwenye simulizi ya SUKARI YA DADA alivyokua akitulia kufikilia maisha yake.
Mambo unayoongelea sana
Unapenda kuongea kuhusu nini? Unapenda kuongea na nani? Mambo hayo yanaweza kuwa na mchango mzuri kwenye maisha yako? Kama hakuna basi kunajinsi unatakiwa kubadilika.
Baada ya kuongea na mtu, akili yako inaweza kuwa imeongeza vitu na huyo mtu anaweza kuwa ameongeza kitu kwenye akili yake pia. Vitu hivyo vinaweza kuwa na athari kwenye maisha yenu wote.
Mfano; Mkikutana mmnao penda vilevi na kuongelea vilevi, mnaweza ondoka mmejuzana kuhusu vilevi msivyovijua alafu kichwani mkawa na mawazo ya kuvijaribu vilevi hivyo. Na mnaweza hata kujaribu kweli mkija kuviona.
Lakini watu wa biashara mkiongelea mambo ya mafanikio ya biashara, mnaweza kuwa mmeondoka na mbinu au taalifa muhimu kuhusu biashara. Na pia mnaweza tumia mambo hayo kwenye harakati za kibiashara.
Unapoongea na watu, pata muda wa kusikiliza, uliza maswali na utoe baadhi ya mambo unayoyajua pia.
Ni vema ukawa na maongezi ya vitu vitakavyo kujenga na ili kumpata mtu anaeongea mambo hayo inabidi uwe na tabia ya kuongea mambo hayo. Hii inaweza kukufungulia hata fulsa mbalimbali zinazoweza badilisha maisha yako.
Huu ndio mwisho wa makala hii. Kiufupi ni vitu huonekana vidogo kwenye maisha ya binadamu lakini ni vitu vyenye matokeo makubwa kwenye maisha yake. Endelea kuwa karibu na The bestgalaxy.