Category Archives: mengineyo

Mambo yanayokwamisha Watu kukimbiza Ndoto zao



Ikiwa wewe ni kijana mwenye miaka 20 na kuendelea, kuna mambo muhimu sana unatakiwa kujua kuhusu safari ya kufikia ndoto zako.
Kila mtu huwa na ndoto kubwa maishani, lakini ni wachache sana wanaoweza kuzitimiza.


Sababu kubwa inayofanya wengi washindwe si kwa sababu hawana uwezo, bali ni kutokana na kutoanza kuzikimbiza kabisa. Hapa chini tunakupa baadhi ya mambo yanayokwamisha watu wengi kukimbiza ndoto zao. Unaweza kuyapitia ili kuwa na kuelewa kwenye mapambano ya kukimbiza ndoto zako.

Jinsi ya kulinda ndoto zako zisife maishani BONYEZA HAPA>>>

Mambo yanayokwamisha Watu kukimbiza Ndoto zao



1. Kusubiri Wapate Kitu cha Kuanzia

Watu wengi wana mawazo makubwa ya biashara, miradi au mipango ya kubadilisha maisha yao, lakini hawachukui hatua kwa sababu wanasubiri kupata mtaji au kusaidiwa na mtu mwingine ili waanze.
Hii ni moja ya sababu zinazowafanya watu wengi wabaki pale pale walipo kwa miaka mingi, wengine mpaka wanazeeka bila kufanikisha kitu.

Ukweli ni kwamba, ni nadra sana kuona mtu kakupa mkono wa kukuanzishia. Badala ya kusubiri, tafuta njia zako mwenyewe za kuanza hata kidogo.

Usiseme “Nahitaji mtu anipatie milioni 1 ili nifike mbali kibiashara” alafu ukatulia. Bali sema “Nipo napambana kupata pesa kidogo kidogo mpaka nifike kwenye hiyo milioni 1 ili nifike mbali kabisa kibiashara” huku ukifanya hivyo kweli.

Matendo madogo yanayoanza leo, yanaweza kuwa mwanzo wa mafanikio makubwa kesho.




2. Kubadilisha Malengo Mara kwa Mara

Watu wengi huanza mwaka wakiwa na lengo moja, lakini wakifika katikati ya mwaka wanakuwa tayari wamebadilisha mawazo mara kadhaa.
Ni vizuri kuwa na mawazo mapya, lakini kama kila wazo linakufanya usimalize uliloanza, unakuwa unajizungusha pale pale tu bila hatua yoyote.

Kila ndoto inahitaji msimamo na umakini. Usiruhusu malengo mapya yakupotezee mwelekeo wa lengo kuu ulilojiwekea.
Tambua unachokitaka, kisha kifuate bila kuyumbishwa na vitu vidogo vidogo njiani.



3. Kutaka Kuelewa Sana Kabla ya Kuanza Kufanya

Kuna watu hutumia muda mwingi sana kufikiri na kupanga, badala ya kuchukua hatua.
Wanataka kuelewa kila kitu kabla ya kuanza, na matokeo yake wanabaki kufikiri tu bila kufanya chochote cha maana. Kwenye hili; wataalam huwa wanasema “Overthinking Kills Success“, wakiwa na maana “Kufikilia Sana Kunaua Mafanikio”.

Mfano: Wakati wewe unawaza kuanzisha biashara kubwa ya kuuza samaki nchi nzima bila matendo yoyote, mtu mwingine anaamua kuanza kuuza samaki mtaani kwake tu kisha anaanza kuingiza pesa kila siku huku akikua taratibu kibiashara.

Mipango ni mizuri, lakini matendo ndio yanayoleta mabadiliko kwenye maisha.



4. Kutoamini Kwenye Mawazo Yao

Watu wengi wana mawazo mazuri sana, lakini tatizo ni kwamba hawaamini ndani yao kuwa mawazo hayo yanaweza kuleta mafanikio.
Kukosa imani kunazalisha hofu, na hofu inaua ndoto.

Kama huwezi kuamini unachokiwaza, hutachukua hatua, na hutawahi kujua mwisho wake hata kama ni mzuri.


Ndoto hazitimii kwa miujiza, bali kwa hatua ndogo zinazochukuliwa kila siku. Maisha yanabadilika pale unapochukua hatua.

Zingatia haya kwa mtoto wako kabla hajakua kiakili (maisha)

Malezi ya mtoto ni jukumu zito linalohitaji umakini na uelewa wa kina. Mara nyingi wazazi hulenga tu chakula na mavazi, lakini kuna mambo ya ndani zaidi yanayoweza kuathiri maisha ya mtoto kwa muda mrefu.


Kabla mtoto hajakomaa kiakili, ni muhimu kuzingatia mambo mengi sana lakini hapa nakukumbusha mambo matatu tu. Mambo haya ni madogo lakini kuyafanya ukiwa kama mzazi ni kumsaidia mtoto wako.

Mambo 3 ya Kuzingatia kwa Mtoto Kabla Hajakua Kiakili

  1. Mtazamo Wake wa Maisha na Pesa

Mtoto anapokuwa mdogo, kile anachoona na kusikia kutoka kwa mzazi ndicho kinamjengea tabia na mtazamo wa maisha.

Ukimfundisha thamani ya kujituma, kutunza kidogo alichonacho na kuepuka matumizi yasiyo ya lazima, unamjenga awe na nidhamu ya kifedha ndani yake. Unaweza fanya hivyo kwa kumfundisha mtoto kujizuia kutumia pesa zake za pipi, kumpa pesa kumwambia atumie pesa kiasi kidogo na mambo mengine yatakayo msaidia.
Siku moja pia uwe unamtupia maneno chanya kuhusu ambayo umegundua kuhusu kuishi Maisha na kutafuta pesa. Maneno hayo machache yanaweza kujenga mtazamo mzuri utakaomsaidia kukua vizuri kiasi cha kufanikiwa baadae.
Malezi haya humsaidia baadaye asijikute katika changamoto za madeni au matumizi mabaya ya fedha pia.

  1. Imani za Kidini

Imani ni msingi wa maadili ya mtoto. Wazazi wanapomfundisha mtoto wao dini, wanamjengea moyo wa heshima, upendo, na uwajibikaji. Dini humsaidia mtoto kuelewa tofauti ya mema na mabaya na kumpa mwongozo wakati wa changamoto.

Bila misingi hii, mtoto anaweza kukua akiwa na mawazo au maswali mengi yanayomchanganya katika kila changamoto. Hali hii inaweza kumfanya apate ugumu wa kudhibiti hasira, hisia za mwili, tamaa, na hata kushindwa kuendana vizuri na jamii.

  1. Afya ya Meno

Afya ya meno mara nyingi hupuuzwa, lakini ni jambo muhimu kwa maisha ya mtoto. Tabia ndogo kama kufundisha mtoto kupiga mswaki mara mbili kwa siku na kumpeleka kwa daktari wa meno kwa ukaguzi wa mara kwa mara huokoa gharama kubwa za kiafya baadaye. Mtoto akiwa mdogo anakua hana akili ya kutunza meno yake lakini wakati huo ndio meno yenye matatizo yanaweza kutolewa na nakuota tena kirahisi.

Kwaiyo yatunze meno ya mtoto mpaka atakapokua mkubwa kabisa na kujua umuhimu wa meno. Wengi wakikua huwa wanaumia sana wanapoona mwanzo wa matatizo ya meno yao ni wazazi kutozingatia wakiwa wadogo. Na wazazi wengi wanasahau kuhusu hili.

Mtoto ni kioo cha malezi ya wazazi wake. Kabla hajakomaa kiakili, hakikisha unamjengea msingi wa mtazamo mzuri wa maisha na pesa, imani ya kidini, na afya bora ya meno.

Jinsi ya kuzuia kichefuchefu au kutapika kwenye Gari

Kusafiri kwa gari kunaweza kuwa furaha au mateso kulingana na jinsi mwili wako unavyokabiliana na mwendo. Kwa baadhi ya watu, changamoto kubwa ni motion sickness; hali ya kichefuchefu kinachosababishwa na ubongo kuchanganyikiwa kutokana na taarifa tofauti kutoka kwenye macho na masikio kuhusu mwendo. Kuna wengine tatizo hili huanza hata kukusikia harufu flani ndani ya gari.

Kutapika ukiwa kwenye gari kunaweza kukukuta kutokana na kichefuchefu hiki. Lakini uzuri ni kwamba unaweza kupunguza au kuondoa kabisa kichefuchefu ukiwa safarini. Hapa chini kuna njia  zenye maelezo ya kutosha unazoweza kutumia ili kufanya hivyo.

Ujumbe mzuri wa kumtumia mpenzi wako kwa sms BONYEZA HAPA>>>

Njia za kuzuia kichefuchefu au kutapika kwenye gari

1. Kaa Sehemu Sahihi

Kiti cha mbele ni rafiki yako. Ukiwa kwenye kiti hicho, mwili wako hupata mtikisiko mdogo ukilinganisha na viti vya nyuma, na unaweza kuona barabara kwa uwazi zaidi. Hii inarahisisha ubongo wako kulinganisha mwendo unaouona na ule unaouhisi, hivyo kupunguza kichefuchefu.

2. Tazama Mbele, Si Pembeni

Kuangalia mbele husaidia ubongo wako kuelewa vizuri mwendo wa gari. Ukigeuka mara kwa mara pembeni au nyuma, macho yako yatatuma taarifa zinazokinzana na hisia za mwili, na matokeo yake ni kichefuchefu.

3. Pata Hewa Safi

Hewa yenye joto kali au harufu mbaya inaweza kuongeza kichefuchefu. Fungua dirisha kidogo ili upepo baridi uingie, au washa kiyoyozi. Ikiwa kuna harufu ya mafuta, vyakula vizito, au manukato makali ndani ya gari, jaribu kuiepuka kwa kugeuza uso au kukaa karibu na chanzo cha hewa safi.

4. Kula Mlo Mwepesi Kabla ya Safari

Kula chakula kizito kabla ya safari ni kama kualika matatizo. Vyakula vya mafuta, vya kukaanga au vyenye harufu kali huongeza uwezekano wa kutapika. Badala yake, kula vyakula vidogo na vyepesi kama biskuti kavu, mkate, au matunda yasiyo na tindikali nyingi. Lengo ni kuhakikisha tumbo haliko tupu kabisa, lakini pia halijazidiwa.

5. Jaribu Tangawizi au Peppermint

Tangawizi ni tiba ya asili inayojulikana kupunguza kichefuchefu. Unaweza kunywa chai ya tangawizi, kutafuna biskuti yenye tangawizi, au kutumia pipi ya tangawizi. Peppermint pia husaidia kwa kutuliza misuli ya tumbo na kupunguza hisia za kutapika. Weka pipi ndogo mfukoni kabla ya safari.

6. Fanya Mapumziko

Kama safari ni ndefu, kuendelea kukaa kwenye gari kwa muda mrefu huongeza dalili za motion sickness. Simama kila baada ya saa 1-2, tembea kidogo, pumua hewa safi, na nyoosha miguu. Hii itasaidia mwili wako kupata mwendelezo mpya wa hisia na kupunguza kizunguzungu.

7. Epuka Pombe na Kafeini Nyingi

Pombe inaweza kusababisha upungufu wa maji mwilini na kuathiri usawa wa mwili, huku kafeini nyingi ikiongeza wasiwasi na mapigo ya moyo. Yote haya yanaweza kuchochea kichefuchefu. Ni vema kunywa maji ya kawaida au juisi nyepesi badala yake.

8. Tumia Dawa za Kuzuia Motion Sickness

Kwa watu wanaopata tatizo hili mara kwa mara, dawa maalum kama Dramamine, Avomine, au Bonamine zinaweza kusaidia. Ni vizuri kutumia dawa hizi dakika 30 hadi saa 1 kabla ya safari. Kumbuka, tumia dawa baada ya ushauri wa daktari au mfamasia, hasa kama unatumia dawa zingine.


Mwisho; Kama dalili zimeanza, jaribu kupumua kwa utaratibu kupitia pua, kisha utoe pumzi taratibu kwa mdomo. Weka macho yako kwenye kitu kisichohama mbele yako, na epuka kufumba macho kabisa. Njia hii inaweza kuzuia kutapika ndani ya dakika chache bila dawa.

Simulizi ya “Punda” ni mfano mzuri wa kutosikiliza watu katika Maisha

Moja kati ya simulizi ambayo huongelewa sana katika mifano ya maisha ni hii simulizi ya Mume, Mke, na Punda. Kama uijui vizuri simulizi hii, tulia uisome hapa chini;

Kulikuwa na mume na mke waliokuwa wakisafiri kijijini kwao wakiwa na punda. Njiani, walikutana na watu wa aina mbalimbali waliokuwa na maoni yao kuhusu safari yao.

Mume na mke walitembea kwa mguu huku wakiwa wamechukua punda wao akiwa amefungwa kwa kamba shingoni. Walionekana wamechoka, lakini walikuwa wakifurahia mazungumzo yao. Walipokutana na kundi la watu wa kijiji flani, walihisi macho yakiwatazama sana.

“Mna akili kweli? Mna punda lakini mnatembea kwa miguu! Kwa nini msimpande?” mmoja wa watu akasema huku akicheka.

Mume akatazama mke wake na akasema, “Labda wana ongea cha maana hawa. Hebu tubadilike.”

Mume alipanda punda huku mke akitembea pembeni. Baada ya muda, wakakutana na kundi jingine la watu.

“Angalia huyu mwanaume! Anawezaje kumpanda punda huku mke wake maskini anatembea? Hana hata huruma!” mmoja wa wanawake akasema kwa sauti ya lawama.

Mume aliona haya na kushuka. “Basi wewe panda sasa,” alimwambia mkewe.

Mke akapanda punda, alafu mume akaanza kutembea kwa miguu. Njiani, wakakutana na kundi jingine la watu waliokuwa wakifanya kazi shambani.

“Jamani! Angalia huyu mwanamke hana hata aibu. Anampanda punda huku mume wake mzee anatoka jasho akitembea!” mmoja wa wanaume akasema kwa dhihaka.

Mume na mke walitazamana na kuamua wote wapande punda.

Wote wawili walipanda punda na kuendelea na safari yao. Hawakufika mbali, wakaanza kusikia watu wakiwazungumzia tena.

“Hawa watu hawana huruma! Wote wawili wanampanda punda huyu mdogo. Wanataka kumuua kwa uzito wao?” mmoja wa wazee akasema huku akitikisa kichwa chake.

Mume na mke vichwa kikawaka moto, waliona bora wambebe huyo punda mgongoni ili wasisemewe tena. Wakafunga miguu ya punda kwa kamba vizuri na kumbeba kama mzingo. Walipokuwa wakivuka daraja, watu waliwaangalia kwa mshangao na kucheka sana.

“Jamani, angalia hawa wajinga! Wamegeuza mambo. Badala ya punda kuwabeba wao, wao ndio wanambeba punda!”

Kwa aibu, waliishiwa nguvu, punda akaanguka mtoni. Mume na mke wakakaa kimya huku wakitazama punda akizama majini…

Simulizi hii inamaana gani kwenye Maisha?

Simulizi hii inakumbusha kuwa katika Maisha, Haijalishi unafanya nini, watu watasema tu. Unaweza kufanya jambo kwasababu zako nzuri tu lakini wakaangaliwa kwa ubaya. Kiufupi, unapokua na ndoto au mambo mbalimbali unayotaka maishani, maneno ya watu usiruhusu yakuyumbishe au kukupoteza kama ilivyokua kwa wenye Punda.

Ushauri kwa aliesema pesa zake hazioni BONYEZA HAPA>>>

Vichekesho vya Maandishi unavyoweza kusoma

Kucheka ni njia bora ya kupunguza mawazo yanayotukumba kila siku. Katika maisha haya yenye changamoto nyingi, kila mtu anahitaji muda wa kupumzika na kufurahia vitu vidogo vinavyoweza kuleta tabasamu. Hakuna njia bora ya kufurahia muda wako wa kupumzika kama kuangalia video au kusoma vichekesho vya maandishi, vinavyoweza kukuchekesha na kukufanya usahau magumu ya maisha kwa muda.

Utafiti unaonyesha kwamba kucheka kuna faida kubwa kiafya, kama vile kupunguza msongo wa mawazo, kuongeza kinga ya mwili, na kuboresha hali ya moyo. Kicheko pia huimarisha mahusiano ya kijamii kwa sababu huleta furaha na mshikamano miongoni mwa watu unaocheka nao. Kwa hivyo, kama unatafuta kitu cha kukuchekesha na kukupa muda wa kuburudika, basi uko mahali sahihi.

Katika makala hii, tumekusanya orodha ya vichekesho vya maandishi vinavyovutia na kuchekesha, ambavyo unaweza kusoma popote ulipo. Jiandae kwa kucheka kupitia vichekesho hivi vya maandishi!

Soma Vunjambavu za vichekesho BONYEZA HAPA>>>

Vichekesho vya Maandishi vya kuvunja mbavu

  1. Mtoto katika maombi

Kila mara mtoto alikua akiambiwa kuwa anaeleta au kuwapa chakula ni Mungu. Siku moja, Mama yake alimwambia huyo mtoto aombee chakula kabla ya kula. Mtoto akaanza:
“Mungu, tunashukuru kwa chakula hiki. Naomba pia ulete chips na soda kesho maana ugali na mboga za majani kila siku zinachosha!”
Watu wote mezani walicheka sana.

  1. Mtoto na Mwalimu

Mwalimu alianza kuuliza kila mwanafuzi darasani “Kwa nini unahitaji kujifunza hesabu?”
Mtoto mmoja akajibu “Ili mama yangu asitumie hela zangu vibaya nikimpa anishikie”
Darasa zima likacheka

  1. Bibi na TikTok

Bibi Fatuma alikuwa sio mjanja na hakuielewa teknolojia ya TikTok. Wajukuu wake walimshawishi ajaribu. Alianza na video kutaka kutengeneza video akiwa anacheza live. Badala ya kubonyeza kitufe cha kuanza kurekodi, aliweka simu mfukoni na kuanza kucheza peke yake huku akipiga makelele ya nyimbo za zamani.
Baada ya muda mrefu, aliwauliza wajukuu:
“Mbona hakuna mtu ana-like video yangu?”
Wajukuu alipo fikilia kuwa bibi yake alichofanya, alicheka sana.

  1. Mtu na mpenzi wake wanaoongea kwenye simu

MKAKA: Hi uwapi swity?
MDADA: Niko home
MKAKA: Unafanya nini?
MDADA: Nakula
MKAKA: Unakula nini?
MDADA: Mama katengeneza macaroni, ambayo kanyunyizia chiizi na sausage fulani imported ambazo baba amenunua supermaketi Masaki, na saladi, kisha ntateremsha na Epo juisi…

Mara ghafla ikasikika sauti ya mama yake “Hivi we Gulo kaka yako atakula nini na we umemaliza ugali na maharage yote?”

  1. Ndoa nyingine

Mtaani kwetu kuna jamaa mmoja anaitwa chogo, ana mtoto mmoja anaitwa “emma” pamoja na mke wake.. leo bwana katoa kali; Alikua amekaa nje ya nyumba yake kwenye kibalaza, alikua ameshikilia cheti cha ndoa yake.. akanza kukitazama sana, ikafika kipindi mke wake ikabidi avunje ukimya na kumuuliza “Baba emma, mbona unakitazama sana hicho cheti..?” bwana chogo akajibu huku akilia, akitoa sauti ya upole “NATAFUTA EXPIRE DATE YA HIKI CHETI CHETU..” Mke wake hoi akazimia…!

Jinsi ya kutengeneza Pesa zaidi kwenye unachokifanya (Biashara au Huduma)

Tunafanya mambo mbalimbali ili kuingiza pesa kwenye maisha yetu. Karibu kila mtu ana Kazi, Biashara au Huduma ambayo humuwezesha kupata kipato cha kuendesha maisha yake. Kipato kinaweza kuwa kikubwa au kidogo lakini maisha huitaji pesa, hivyo watu hupambana sana katika vyanzo vya mapato yao ili kuishi. Katika kupambana huko, baadhi ya watu hupambana sio tu kupata mapato au pesa, bali kuongeza kiasi wanachopata. Na kupambana kupata kipato au pesa nyingi zaidi zaidi ya unachopata kwenye unachokifanya, sio jambo baya ila inaweza kuwa sio rahisi.

Ukitupa macho au kufanya utafiti katika biashara flani, utagundua watu hupata faida au kipato tofauti. Yani inaweza kuwa ni Huduma au Biashara moja lakini Baadhi ya Watu wakawa wanaoingiza pesa nyingi kuliko wengine. Hii ni hali ambayo ipo na itaendelea kuwepo maana waswalihi wanasema “Kila mtu na ridhiki yake”. Lakini kama hauridhika, kunauwezekano wa kupambana na kuongeza kiasi unachoingiza. Tumeona hii kwenye simulizi za watu mbalimbali wenye mafanikio makubwa ulimwenguni.

Kama ni mmoja ya watu wanaohitaji kutengeneza Pesa zaidi kwenye biashara au Huduma, hapa chini kuna mambo yanayoweza kusaidia kufanikisha hilo.

Ujuzi utakao kuwezesha kuingiza pesa mtandaoni BONYEZA HAPA>>>

Mambo ya kuzingatia ili kutengeneza Pesa zaidi kwenye unachokifanya (Biashara au Huduma)

Kujichanganya na waliofanikiwa.



Ukitaka kwa kama waliofanikiwa kwenye mambo yako, jaribu kujichanganga na watu waliofanikiwa kwenye mambo hayo. Watu wengi huwa wanajitenga na waliofanikiwa na kuanza kuwasema. Lakini wewe ili kufanikiwa kama wao, unatakiwa kuwa upande wao ili upate mitazamo kama yao. Kujichanga na walio fanikiwa kunaweza kukupatia mbinu mbalimbali za kufikia kwenye kipato unachohitaji. Mbali na mbinu, unaweza kupata hata fulsa toka kwao.

Utayari wa kujifunza na kubadilika.



Hiki kitu ni muhimu sana kwenye maisha ya mafanikio na kuongeza kipato. Ukiwa tayari kujifunza mambo na kubadilika, basi utakua na uwezo wa kujifunza mambo muhimu kwenye huduma au biashara yako. Alafu pia utakua na uwezo wa kuyafanyia kazi baadhi ya mambo ili kuongeza kipato.
Baadhi ya watu hauwana uwezo huo. Wanaweza ambiwa au kuona mbinu zote za kuongeza kipato lakini wasifanye chochote cha maana. Yani hufanya biashara au huduma kwa mazoea huku wakilalamika kuwa wanatamani kuongeza kipato. Na mbaya zaidi ni hawataki kubadilika.

Kuelewa Soko au wateja.


Chunguza mahitaji ya wateja na matatizo yao. Elewa tabia, wanachopenda, na uwezo wa kifedha wa wateja wako. Fikilia ni jinsi gani unaweza wasaidia kwenye mambo yao na ukapata pesa. Jaribu kutafuta pengo na litumie kama fursa kwenye kwenye biashara au huduma yako.


Usipoelewa vizuri unao wahudumia, utakua haujaielewa vizuri huduma yako pia. Na usipoielewa biashara au huduma yako, unaweza usipate hata faida ya unachofanya.

Kutambulisha kwa watu (Itangaze)



Ukiwa na Biashara au Huduma ambayo haitambuliki na wengi, inawezakua ni ngumu kupata watu wengi wanataokufanya upate hata faida. Lakini ikiwa inatambulika na unaitangaza, watu wataona unachofanya na kujihusisha nacho.

Hii itakusaidia kupata faida kuwa kwenye kitu unachofanya. Kwa sasa mtu unaweza tumia hata mitandao ya kijamii (kama Instagram, Facebook na TikTok) kutangaza bidhaa/huduma.

Jinsi ya kutangaza biashara yako Mtandaoni BONYEZA HAPA>>>

Usifanye mambo haya ukiwa Dubai

Dubai ni mji maarufu duniani unaovutia watalii kutoka kila pembe ya dunia. Una mandhari za kuvutia, teknolojia ya kisasa, utajiri na ni mahali panapopendwa sana na watu. Lakini, kama ilivyo kwa miji mingine mikubwa, kuna sheria, desturi, na kanuni za kipekee ambazo wageni wanapaswa kuziheshimu. Kutozingatia mambo kama hayo ukiwa Dubai, kunaweza kusababisha usumbufu au matatizo makubwa hatakama ni mgeni.

Kama mgeni unayeitembelea Dubai kwa mara ya kwanza, ni muhimu kujua mambo unayotakiwa kujiepusha nayo ili kuhakikisha safari yako ni ya kufurahisha na sio matatizo. Mji huu una mchanganyiko wa mila za Kiislamu na tamaduni za kisasa, ambazo zote zinahitaji heshima kutoka kwa wageni wake. Kutokujua sheria za msingi kunaweza kusababishia migogoro isiyo ya lazima.

Katika makala hii, tutakupa mwongozo wa mambo unayopaswa kuepuka unapokuwa Dubai. Kwa kuzingatia mwongozo huu, utakuwa na fursa ya kufurahia safari yako bila wasiwasi na kuonyesha heshima kwa wenyeji wa mji huu wa kuvutia.

Jinsi ya kupata Ticket za ndege za bei rahisi BONYEZA HAPA>>>

Mambo Usiotakiwa Kufanya Ukiwa Dubai

Usile hadharani kipindi cha Ramadan


Kipindi cha Ramadan ni takatifu kwa Waislamu, na kula, kunywa, au kuvuta sigara hadharani wakati wa mchana ni marufuku kwa wote, wakiwemo wageni. Ni muhimu kujizuia na kuheshimu ibada ya kufunga kwa wenyeji. Kama ukiwa katika mji huo kipindi cha Ramadan, basi kuwa mtulivu na ufuate utaratibu wao.

Usilale na mpenzi wako chumba kimoja kwenye baadhi ya hoteli

Hoteli nyingi katika Dubai zina sera zinazofuata sheria za Kiislamu, na wanandoa wasiooana hawaruhusiwi kulala chumba kimoja. Hakikisha unafahamu sera za hoteli kabla ya kufanya malipo. Kuna hotel nyingine huruhusu wageni kulala pamoja hatakama hawajaoana na ndio unapaswa kuzitumia ili kuepuka usumbufu.

Kunywa pombe hadharani

Ingawa pombe inaruhusiwa lakini ni kwenye maeneo maalum kama baa na hoteli zinazoiruhusu. Kujiachia na kunywa au kuionyesha hadharani kunaweza kusababisha matatizo makubwa, ikiwa ni pamoja na faini au kifungo. Swala hili linatakiwa kuzingatiwa kila siku na sio siku za Ramadan tu kama ilivyokua kwenye kula.

Kusalimia kwa kutumia mkono wa kushoto

Katika tamaduni za Kiarabu, mkono wa kushoto unachukuliwa kama mchafu, na hivyo ni vyema kutumia mkono wa kulia unapotoa au kupokea kitu, au hata kusalimiana. Fanya havyo maana Dubai ina utamaduni wa kiarabu na nivema ukauheshimu unapokuna wenyeji.

Hatumaini hayo wamekupa mwanga na mwongozo juu ya jinsi gani unatakiwa kuwa au kufanya huko Dubai. Mbali na kuyajua hayo, ni vema ukawa chini ya mtu mwenyeji atakea kusaidia kujua zaidi mambo ya kufanya katika mji huo ili kuhakikisha haukosei.

Huu ni ushauri kwa mtu anaesema “Naipata pesa lakini siioni” katika Maisha

Ikiwa unapambana kupata pesa na unapata lakini hauioni, hii makala ni ya kwako.


Kwanza unatakiwa kujua kuwa watu wengi wapo kwenye hali hiyo kwa sasa. Yani unaweza kuwa na pesa ndogo au nyingi zinazoingia lakini zinapita mkononi mwako tu na hazituli.

Pamoja na kwamba watu husema “Pesa sio Kila kitu” lakini unatakiwa kuelewa kuwa maisha ya sasa yanahitaji pesa. Hii ni kwasababu asilimia kubwa ya vitu vilivyopo kwenye maisha yetu, vinatumia pesa na vinadai pesa kabisa Yani.

Mfano; ukiwa umepanga nyumba unayolipa elufu 50 kwa mwezi inamaana katika Maisha yako Kila baada ya siku 30 unalipia elufu 50. Sasa hapo Ukijumlasha na mambo ya chakula, umeme na mambo mengine yanayojitokeza kwenye mwezi unaweza jikuta Kila mwezi unatakiwa kwenye mikono yako utoe pesa nyingi sana. Na hizo pesa zote unazotumia kwa ujumla wanaita “Gharama za maisha”. Hii inamaana maisha yana “Gharama”.

Mbinu za kutimiza malengo yako ya Mwaka BONYEZA HAPA>>>

Gharama za maisha na kiasi cha pesa unachoingiza

Gharama za maisha yako zikiwa ni kubwa kuliko kiasi cha pesa unachoingiza, unawezakuwa ni mtu unaeshika pesa lakini huzioni na unaangukia kwenye madeni. Yani unakua ni mtu unaetumia pesa nyingi kuliko unazoingiza.

Kujitoa kwenye hali hiyo unatakiwa kwanza kumuomba mungu akusaidie badala ya kukimbilia kwenye vitu kama pombe ili kumpunguza Mawazo.


Hatua ya pili, unatakiwa kutulia na kuiweka akili yako kwenye matumizi yako ili kuelewa kiasi gani unatumia kwa siku, mwezi na hata mwaka. Hapa utatakiwa kujua pesa kiasi gani unatakiwa kuwa nayo kwa mwezi ili uwe na mahitaji muhumu yote(Kodi, chakula n.k). Na pia unatakiwa kujua pesa kiasi gani huwa zinatoka mikononi mwako na kwenda kwenye vitu visivyo vya muhimu. Kiufupi unatakiwa kuzingatia pesa zinatokaje mikononi mwako.

Baada kujua pesa zinatokaje mikononi mwako, utatakiwa kuanza kuzizuia baadhi ya pesa zinazokwenda kwenye mambo yasio ya muhimu. Ni ngumu sana maana pesa nyingine unaweza gundua zinatoka mikononi mwako ili kuifurahisha Roho na imekua ni kama Tabia tayari kufanya hivyo. Lakini pambana sana kuzuia kwa kubadilisha tabia na kuepuka utoaji wa pesa usio wa muhimu sana.

Wakati ukiendelea kupambana kuzuia pesa zisitoke mikononi mwako kizembe, unaweza kuwa na hasira sana kuhusu pesa maana utakua unaona baadhi ya pesa zinaendelea kutoka mikononi mwako bila umuhimu na unashindwa kuzizuia. Lakini usikate tamaa maana jambo hili litakukumbusha kujiuliza “Nitarudisha vipi pesa zilizotoka mikononi mwangu bila umuhimu?”, Pia utajiuliza “Nifanye nini ili hizi pesa zinazokuja zisiwe zinatoka mikononi mwangu?”.

Unarudisha vipi pesa zilizotoka mikononi mwako?

Ni ngumu kurudisha pesa zinazotoka mikononi mwako ila unaweza anza kuzingatia utengenezaji wa pesa nyingi nyingine zitakazokuja mikononi. Yani hapa naongelea kuongeza kipato chako.

Mfano: kama ni mfanya biashara, basi unatakiwa kufanya bashara yako ikuingizie pesa nyingi zaidi. Na njia rahisi ya kufungua ubongo wako kwenye upande wakuongeza kipato ni kujifunza toka kwenye vitabu au watu wengine wanaoingiza pesa zaidi. Au unaweza anza kujaribu vitu mbalimbali ili kuitanua biashara yako iweze kuingizia pesa zaidi.

Kiufupi ni unatakiwa kutafuta njia za kuongeza kipato au pesa zinazokuja mikononi mwako huku ukiendelea kuzuia matumizi yasio na maana. Na ukifanikiwa kuingiza pesa nyingi kuliko unazotumia, utakua ni kama umefanikiwa kuzirudisha pesa zinazotoka mikononi mwako huku ukipata na nyingine za juu kwaajili ya mambo mengine.

Nini cha kufanya ili pesa zisiwe zinatoka mikononi mwako?

Kufanikisha hilo unatakiwa uwe unaweka pesa yako kwenye sehemu isiopungua thamani yake au uwe unaiweka pesa yako kwenye sehemu inayofanya pesa yako izalishe pesa nyingine.

Kiufupi ni utanatakiwa uwe unatuza pesa yako kwa kuweka kwenye akaunti au michezo ya kutuziana pesa. Wengine huwa wananunua mpaka viwanja ili kuitunza pesa tu isishuke thamani. Na pia unaweza iweka pesa yako kwenye biashara inayozalisha pesa zaidi ya ulioiweka.

Katika safari ya kuelekea mafanikio. Usisahau kuwa mungu atakusaidia ukijituma, na pia karamu na daftari ni muhumu kuvitumia kwenye mahebu yako ya kimaisha.

Mbali na hayo; kujiweka katikati ya watu wanapenda mafanikio ni muhimu. Hakikisha unakua na watu wanaopenda mafanikio kwenye maisha na sio waliokata tamaa. Ukishindwa kabisa kupata watu, wafuate wanao hamasisha kujituma na mafanikio kwenye maisha waliopo mtandaoni. Kama wewe ni kijana wa kiume unapenda kutiwa hasira sana za kutoka ulipo, unaweza wafuata hata wakina Chiefgodlove au Chimakeke. Pamoja na mabaya yao, hiyo ni moja ya kazi yao.

Endelea kuwa karibu na The bestgalaxy!

Wanasema “Ukitaka Kufanikiwa, Kuwa Kama Tai” kwasababu hizi

Tai au Eagle ni ndege maarufu kwa uwezo wake kwenye mambo mbalimbali na amekua akiongelewa sana. Baadhi ya watu hutumia ndege huyu kama alama za kuonesha ujasiri, nguvu na ubora. Lakini pia kunawatu humtumia ndege huyu kama mfano katika Maisha na mafanikio.


Kutumia mfano wa tai kama alama ya mafanikio ni njia bora ya kuelewa mambo muhimu yanayoweza kutusaidia kufikia sehemu flani maishani. Ili kufanikiwa, Kuna muda ni kweli tunahitaji kuiga tabia na sifa fulani za tai ambazo ni zenye thamani na zinazoweza kutupeleka mbali. Kati ya sifa hizo ni hizi hapa chini.

Jinsi ya kulinda ndoto zako zisife maishani BONYEZA HAPA>>>

Sifa za kumuiga Tai ili kufanikiwa kwenye maisha

Kuwa na Maono na Mtazamo wa Mbali

Tai ana uwezo wa kuona mbali sana, hadi kilomita 5! Hii inampa nafasi ya kuona mlo wake au adui akiwa mbali. Ili kufanikiwa, ni muhimu kuwa na maono ya mbali na kutazama mambo kwa upana. Jiulize: unataka kufikia nini maishani, na ni vikwazo gani vinaweza kujitokeza? Kama tai, kila mara angalia mbali zaidi ya hali ya sasa, na ujipange kulingana na unachokiona mbele.

Kuanza upya

Kuna wakati Tai hutenga muda kujibadilisha kwa kung’oa manyoya yake ili kufanya manyoya mengine mapya yaote. Hii ni muhimu kwetu pia; wakati mwingine ni lazima tuondoe tabia, mahusiano, au mawazo ambayo yanatuzuia kusonga mbele. Wakati mwingine, uamuzi wa kuacha kile kinachoturudisha nyuma, ndicho kinachoweza kutupeleka mbali zaidi. Hivyo tunapaswa kuishi kwa mfano huu katika mambo yetu ya kila siku.

Kukabiliana na Changamoto

Tai huwinda nyoka kwa kuruka chini na kuwashika kwa makucha yao, kisha kuruka juu huku nyoka akihangaika. Kisha tai wanaweza kuponda au kung’oa kichwa cha nyoka huyo na kukimeza kizima wakiwa bado wanaruka.

Tai huenda juu kwasababu ndio sehemu ambayo anaijua vizuri lakini nyoka hawezi kuhimiri. Tunawezasema Tai huwa anampeleka nyoka sehemu ambayo anaijua vizuri na ile inaruhusu yeye kushinda vita kirahisi.

Hii katika maisha inatukumbusha kuwa bora katika upande wetu na kutumia tulichonacho kuzishinda changamoto zinazokuja bila kuogopa. Tumia ulichonacho kuwa unapohitaji kuwa, au nenda katika sehemu inayoruhusu kupata unachohitaji. Na pia ondoka sehemu inayosababisha ushindwe.

Kwahivyo, ukitaka kufanikiwa, kuwa kama tai: mtazamaji wa mbali, mwenye moyo usiotetereka, na mwepesi wa kubadilika.