Category Archives: Mahusiano

Maneno matamu ya kumwambia mpenzi wako kwa SMS

Maneno matamu yana nguvu ya kipekee ya kugusa moyo wa mtu. Unaweza muumiza mtu kwa maneno au kumfurahisha. Kwenye mapenzi, unaweza tumia maneno kumfurahisha mpenzi wako na kuimarisha uhusiano wenu. Hata ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) unaweza kuwa njia rahisi na ya haraka ya kuonyesha hisia zako za dhati na kumfurahisha mpenzi wako. Unaweza usiwe naye kwa muda wote, lakini maneno yako yanaweza kuunganisha mioyo yenu hata mkiwa mbali.

Mapenzi si tu kumfanyia mpenzi wako matendo makubwa, bali pia ni kuhusu kufanya mambo madogo madogo kila siku. Mambo kama kumtumia ujumbe mzuri uliojaa upendo unaweza kuwa ni kuonesha mapenzi pia. Kumwambia mpenzi wako neno “Ninakufikiria,” au “Unanifanya nijisikie furaha.” Kupitia sms kunaweza fanya some huo ujumbe na kufikilia mambo mengi chanya juu ya upendo wenu. Yani kuna ujumbe hata ukimfikia mpenzi akiwa anawasiwasi au ameweka jambo baya moyoni, akiusoma moyo wake unakua vizuri ghafla na kusahau yote.

Hapa sisi kama kawaida, tumekuandalia maneno ya mapenzi unayoweza tumia. Haya ni yale maneno matamu ambayo unaweza kumwambia mpenzi wako kwa njia ya SMS. Maneno haya yamebeba hisia, yanayowaweka wapenzi karibu, na kufurahisha.

Mpenzi anaekupenda sana anaweza kukuacha kwasababu hizi BONYEZA HAPA>>>

Maneno matamu ya kumwambia mpenzi wako kwa sms

  • Walimwengu bhana… Watakuja kukudanganya, watajifanya hawajui kuwa tunapendana, wanajifanya wanakupenda sana ila nia yao waharibu penzi letu alafu wapate cha kusema. Najua kupendana kwetu ni huzuni kwao, ila sitaacha kukupenda.
  • Huenda kiumbe unaye muogopa hapa Duniani ni mwanaume ila naomba usiniogope mimi. Nakupenda sana na nipo kufuta maumivu yote umepitia malkia wangu.

  • Wakiniambia niwaweke moyoni, nitawambia moyoni upo wewe na funguo za moyo nimepoteza.. siwezi kukutoa na wala siwezi waingiza

  • Na jua kuna nyakati tunaweza pita zikawa ngumu kidogo kuamini kuwa tunapendana. Ila usisahau kuwa nakupenda hata kwenye nyakati hizo wangu.

  • Siku njema kwangu ni ile ninayojua upo salama na bado unanipenda. Ukiwa salama nakua na Amani, ukiwa unanipenda nakua nina furaha mpenzi.

  • Tuhesabu 1 mpka 5 alafu ntakwambia kitu. Haya tuanze sasa. Moja, Mbili, tatu, nne, tano, Anaesoma ujumbe huu ndie ameuteka moyo wangu. Nampenda sana.

  • Umewahi jaribu kuhesabu nyota? Ukiwa unahesabu nyota angani, unaweza anza kwa kuziona chache mwanzoni lakini ukizingatia, nyingine hua kama zinaibuka na kuwa nyingi kiasi cha kutohesabika. Ninasababu nyingi za kukupenda ila ni ngumu kuhesabu kama ilivyo kwenye nyota. Kila muda unavyoenda, nazidi kupata sababu nyingi za kukupenda.

  • Moyo wangu unanisukuma nikwambie nipo tayari kufanya chochote hapa Duniani kwaajili yako. Yote ni sababu unaupa furaha mpaka siku hizi unadunda sana likitajwa jina lako.

  • Mbali na uhai nilionao, penzi lako ndio kitu cha thamani maishani mwangu. Naweza potezea chochote ila nikabaki na furaha sababu wewe unanipenda.
  • Nakupenda sana mpenzi. Moyo wangu Nimekupa mazima kama zawadi ya upendo. Na ikitokea siku nikakwambia unauumiza, Sina maana unirudishie, ninamaana uubembeleze.
  • Maana sahihi ya mapenzi nimeijua nilipokupata wewe. Penzi lako limenipeleka ulimwengu uliojaa Raha, kwenye Giza umekua ni taa mpaka najivunia kuwa na wewe.
  • Unataka kujua wewe ni nani kwangu? Wewe ni yule ambae tukikosana nakua sina furaha. Yule ambae nikifikilia anavyonipenda huwa natabasamu. Yule alienionesha kuwa Asali ladha yake halisi ni utamu. Yule natamani niwe nae hilele maishani mwangu.
  • Nakupenda sana na natamani ujue kuwa walimwengu wanataka tuachane wakati sisi tunataka tuwe wote milele. Tukiyasikiliza ya walimwengu tutafika wanapotaka tufike na tukisikilizana, tufika tunapotaka kufika.
  • Umejaa kwenye kila sehemu ya moyo wangu. Unaweza kuwa Sababu ya huzuni au furaha yangu.
  • Unaweza kaa bila kuvuta pumzi ila sio kwa muda mrefu. Na ndivyo naweza kaa bila ukaribu na wewe ila sio kwa muda mrefu. We ni mtu muhimu kwangu, nakupenda.

Ni hayo tu katika ukurasa huu, unaweza tembelea ukurasa mwingine na kusoma sms za mapenzi nyingine kama hizi zitakua sio chaguo zuri kwako. Endelea kuwa karibu na The bestgalaxy kwa mambo mengine zaidi.

Movie gani ni nzuri kuiangalia ukiwa na Mpenzi wako?

Katika vitu hufurahisha zaidi, kutazama filamu/movie nzuri ukiwa na mpenzi ni moja wapo. Unakua ni wakati mzuri wa kujenga uhusiano wenu kwa pamoja huku mkifurahia hadithi zinazovutia na kugusa nyoyo. Kuangalia movie pamoja kunawapa wapenzi nafasi ya kufurahia na kutathimini mahusiano au maisha kutokana na wahusika wa movie na kujifunza mengi kupitia wahusika hao.

Movie nzuri za kutazama na mpenzi wako hazihitajika kuwa na hadithi za kuvutia. Lakini pia zinapaswa kuwa zinakugusa hisia na zenye maudhui ambayo yanawaweka nyinyi wawili kwenye safari nzuri ya mahusiano. Unapo chagua movie za kuangalia pamoja unatakiwa kuwa makini sana kwa sasa maana sio kila movie unapaswa kuangalia mukiwa pamoja. Mnachokiangalia pamoja ni vema kikawa kinaziweka hisia zenu pamoja, kuwajenga kwenye mahusiano na kuwaburudisha.

Katika makala hii, tunaangalia orodha ya filamu/ movie ambazo ni bora kutazama ukiwa na mpenzi wako Mwanamke au Mwanaume. Movie hizi zitaamsha hisia, kuleta furaha, na kufanya mufurahie muda wenu wa pamoja.

Unaweza angalia movie itakayo kifaa zaidi alafu akaitafuta, kuiangalia kwenye platform mbalimbali za movie mtandaoni.

Jinsi ya kuangalia movie Bure mtandaoni BONYEZA HAPA>>>

Movie nzuri kutizama ukiwa na mpenzi

  1. Rapunzel (Katuni/Animation)

Hii ni movie/filamu ya Tangled (2010) ya Disney. Ni hadithi ya kifalme inayomuhusu muhusika Rapunzel mwenye nywele ndefu za kichawi, anayetoka kwenye mnara wake kwa msaada wa mwizi aitwaye Flynn Rider. Ni mchanganyiko wa vichekesho, mapenzi, na adventure.

  1. Titanic

Titanic (1997), iliyoongozwa na James Cameron, ni filamu ya mapenzi na drama ya kihistoria. Inahusu kuzama kwa meli ya Titanic mwaka 1912. Wanaigiza Leonardo DiCaprio (Jack) na Kate Winslet (Rose), kama wapenzi kutoka tabaka tofauti wanaokutana na kupendana kwenye meli hiyo.

  1. No Hard Feelings

Filamu hii ya vichekesho ya mwaka 2023 inamshirikisha Jennifer Lawrence. Inahusu Maddie, mwanamke anayekodiwa na wazazi matajiri kumfundisha kijana wao mwenye aibu (Percy) jinsi ya kuwa na ujasiri kabla ya kuanza chuo. Ni mchanganyiko wa vichekesho, mapenzi na mafunzo ya maisha.

  1. Subservience

Filamu hii ya kisayansi (sci-fi thriller) inahusu madhara ya teknolojia ya AI (akili bandia). Nyota wake ni Megan Fox na Michele Morrone. Hadithi inazungumzia AI ya nyumbani inayogeuka na kusababisha matatizo makubwa.

  1. What the Peeper Saw

Filamu hii pia inajulikana kama Night Child (1972). Ni thriller ya kisaikolojia kuhusu mvulana anayetuhumiwa kuhusika na kifo cha mama yake na uhusiano wake wa ajabu na mama wa kambo. Ni hadithi ya hofu na hila za akili.

Mbali na movie hizi, Kuna movie au filamu nyingine nyingi sana zinawoza kufa ukiwa na mpenzi wako. Kama una movie nyingine kichwani, unaweza andika hapo kwenye sehemu ya maoni ili kuwasaidia wengine.

Sms za kumwambia mpenzi wako kuwa unampenda BONYEZA HAPA>>>

UTAMU WA JUMLA 06 (Simulizi ya Maandishi)





Walivyoondoka tu nikajisemea “Bora wameniamsha maana simu nimeiweka pabaya kiasi kwamba mwizi angepita maeneo haya angechukua simu bila mimi kujua”. Baada ya hapo mawazo ya Salma yakaanza kuteka kichwa changu. Nikaanza kuwaza “Dah Salma nae sijui kaenda wapi?… Naanza mpaka kukosa raha yani. Na hii ndoto nilioiota hapa ni ukweli au imesababishwa na makelele ya waliokua wananiamsha tu? Itakua ni hawa mbwa wameniletea lindoto la ajabu… ila sasa mbona hayupo na hakuniambia jana kwamba hatokuepo leo?”Niliwaza mambo mengi sana hapo lakini kichwa kilikua hakinipi majibu ya moja kwa moja, nilikua najiuliza maswali yanayo zaa maswali tu.


Mida ya saa 7 mchana hivi nikiwa palepale mlangoni nilikuta Salma anarudi na anarudi na mzigo mkubwa kiasi kwenye pikipiki. Nilivyomuona Moyo ukadunda kwa furaha “Nduh” alafu nikaendelea kuwaangalia yeye na dereva wa pikipiki wakifika pale. Walipofika nikasalimiana na dereva wa pikipiki pamoja na Salma pia alafu nikasaidia kutua mzigo na kumuwekea mlangoni kwake maana alishakua malaika wangu muda huo, vitu vyake vigumu na vizito lazima nijihusishe navyo.

Baada ya hapo dereva wa pikipiki aliondoka na kutuacha pale na mimi hapo nilimuuliza alikua wapi akaniambia alikua kununua mzigo wa nguo za watoto anataka kuanza kuuza maana alikua hana kazi ya kufanya hapo mjini. Aliponijibu tu hivyo mimi sikumchimba sana kwenye mambo ya kazi huko, nikajikuta moyo umekua mwepesi alafu nikawa na furaha ya ajabu kumuona malaika wangu Salma amerudi.


Siku hiyo tukaendelea kuongea mambo ya mahusiano yetu na mambo mengine ya kijinga kijinga mpaka jua linazama.  Usiku uliingia na katika kutumiana nae ujumbe usiku huo nilimuomba aje tulale wote lakini alikataa, nikamuomba nimfuate nikalale kwake lakini bado alikataa. Nikajua huenda ni mwanamke muoga na anaogopa kukubari kirahisi kuwa na mwanaume, hivyo nikamuacha siku hiyo, sikumsumbua sana. Na hata kulivyokucha niliendelea kuwa nae vizuri tu kimaongezi ila sikuingizia swala la yeye kukataa kulala na mimi usiku. Sikwenda kwenye mafunzo siku hiyo ili tu nibaki na yeye nyumbani.



Siku ya pili usiku katika kuchati nikaamua kujaribu tena kumshawishi tulale wote usiku huo chumbani kwangu ili angalau nipate nafasi ya kumkamata na kumgusa panapotakiwa. Nakumbuka nilimwambia “Salma, njoo ulale kwangu leo… Natamani tulale wote” lakini hakukubari, akajibu “Ah hapana, huko siji hahaha”. Nilijaribu pia kumwambia anifungulie mlango wa chumba chake ili niende nikalalale kwenye chumba chake lakini hakuniruhusu kufanya hivyo, alikataa. Siku hiyo nilijisikia vibaya kidogo maana ilikua ni mara ya pili kunigomea lakini nikajitahidi kupuuza alafu tukaendelea kuongelea mambo mengine. Kulivyokucha, tulikua tunaongea mambo ya mapenzi na vitu vingine kama kawaida lakini sikua naingizia mambo ya yeye kukataa kulala na mimi usiku. Na kiukweli nilikua siwezi muuliza “Kwanini hutaki kulala na mimi?” akiwa mbele ya macho yangu kwakua nilikua kwa kiasi flani namuogopa na pia kichwani nilikua nawaza “Nisiwe na haraka, huenda usiku unaofuata atakubari”. Jambo hili lilinipa mawazo sana mpaka nikashindwa tena kwenda kusoma mafunzo, nikabakia tu nyumbani na yeye.


Siku ya tatu usiku pia alinigomea na siku hiyo niliumia sana maana ilikua ni mara ya tatu hiyo najaribu kumshawishi na hanikubalii. Lakini usiku huo nilijikaza tena nikaendelea kuongeanae mambo mengine tu. Na baada ya kukucha nikakutananae kama kawaida na tulikua kama wapenzi kabisa katika kusalimiana na kuongea. Siku hiyo nilibaki nyumbani ili niongee nae tena kama kawaida lakini sikupata nafasi ya kukaa nae muda mrefu maana mida ya saa 3 asubui alikua anaenda kuuza nguo za watoto na aliniaga na aliniambia anaweza kurudi jioni.
Hiyo siku Salma alivyoondoka na kuniacha pale nyumbani nilikumbwa na mawazo mengi sana juu yake kwakua nilikua simuelewi kabisa. Nakumbuka niliingia ndani ya chumba changu nikakaa nikawanawaza “Huyu dada mbona ananitesa hivi? Au ndo ameanza mambo aliokua ananifanyia Zuu kipindi nipo chuo?  yaani nashindwa kumuelewa maana mchana tukikutana anakua kama ni mpenzi wangu ambae anaweza kubali chochote ninachomwambia lakini nikimwambia usiku tulale wote anakataa… Inamaana na haelewi ninachomaanisha au? Mh itakua huyu Salma hanipendi ila ananiigizia… Itakua ananiigizia tu huyu maana pamoja nakwamba nashindwa kumwambia moja kwa moja ninachotaka lakini jinsi ninavyomwambia tulale wote, yeye ilibidi aelewe tu nataka nini. Au mimi ndio nakosea kumwambia? Mh labla ila bado nampenda acha anisumbue tu akili yangu… Kuna siku ataniruhusu tu kugusa mtunda wake ule… yani mdada mweupee, mzuri sura alafu kapewa umbo lenye mamizigo ya kutosha… mmh acha anitese tu ila nikikamata nitambana mpaka atafurahi”


Wakati nimo ndani mule naendela kuwaza nikasikia kama kunamtu nje anapiga hodi hivi, Nilipotoka nje nikakutana na  majamaa watatu. Mmoja kati yao niliposalimiana nae akajitambulisha kuwa yeye ndie mwenye kile chumba ambacho nilikikuta kwenye nyumba hiyo wakasema mwenye nacho amesafiri. Alisema amekuja hapo kuchukua vyombo vyake na ameishaongea na mwenye nyumba. Mimi nikamkubalia na baada ya dakika chache nikawa nawashuhudia wakifungua mlango na kuanza kutoa vitu kuvipeleka kwenye gari ambalo lilisimama mbali kidogo na kwenye nyumba.

Baadae na mimi nikaona nisiishie kuwaangalia tu, nikajumuika nao kuwasaidia kutoa vyombo na kupeleka kwenye gari. Basi tukaanza kupiga stori huku tukifanya kazi kama ilivyo kawaida kwa wanaume kupiga stori nyingi hatakama hatujajuana sana. Tulifanikiwa kupakia kila kitu kwenye gari na jamaa akaanza kuniaga. Nakumbuka yule jamaa alisema “Asante sana, mimi nimehamia mtaa wa mbele hapo kunajumba linawapangaji wengi, Hiyo nyumba ni ya mama mmoja tajiri sana anafahamika kama Mama Suzi anakaa kwenye jumba lake huko… Ukiwa na muda unaweza ukanitembelea mzee” basi mimi nikaitikia “Anh sawa, usiwaze”. Baada ya mimi kusema hivyo akasema “Poa bwana, utaniagia huyu Tausi maana naona hayupo sjui kaenda kujiuza huko hahaha”.

Mh mimi nikashtuka, nikamuuliza “Tausi yupi huyo?” akasema “huyo dada mweupe mwenye chumba hicho”. Mh nilishangaa nikajikuta naropoka “Anaitwa Tausi huyo?”. Huyo jamaa akajibu “Ndio.. kwani vipi? si ndio jina lake ilo au?” Muda huo niliona niseme tu “Ndio” ili tukaete maengezi. Nikamsikia jamaa akisema huku akiondoka “Nasikia huyo dada ni hela yako tu… ukimpa hela, anakupa chungawa. Kuna mitaa niliwahi muona wanamjua sana ila sijui mitaa ya huku kaamia kufanya nini… Kwaheri bwana”. Mimi sikua na maneno mengi hapo nikajibu “Sa.. sawa” alafu nikaenda haraka ndani kupumzisha akili maana hali yangu iliishaanza kuwa mbaya. Nilikaa kitandani nikaanza kuwaza “Yaani inamaana Tausi ndio huyu Salma?… Na inamaana wale madada ulioniamsha nikiwa nimelala walikua wanamtaka Salma ambae ndie huyo Tausi?… alafu huyo tausi anajiuza?… Ah hapana, Mpenzi wangu Salma sio huyo Tausi wao”…





INAENDELEA….   

UTAMU WA JUMLA 05 (Simulizi ya Maandishi)

Ila kama huyu ni mke wa mtu basi waliosema mke wa mtu mtamu hawajakosea kabisa… Ngoja nimuulize” nikaifuta ile SMS niliotaka kuituma. Nilivyofuta nikamwambia tu “Salma, nikuulize Swali?” alafu ikapita kama dakika moja nikakuta anajibu “Ah hapana usiniulize, nijibu kwanza swali langu”….

Basi mimi nikamwambia “Skia Salma, nijibu kwanza swali ntakalokuuliza alafu ndio nitakwambia” nikakuta tu kaniambia “Nina hamu” nilipo soma nikawa nawaza “Anamaanisha nini huyu? mbona kama ametangulia mbele sana huyu… Neno tata hili… Anamanisha nini kusema hivi usiku huu? Dah sijui nimjibu nini sasa hapa?” kabla sijapata cha kumjibu nikakuta ametuma SMS nyingine imeandikwa “Nina hamu ya kumjua huyo anaenipenda”. Nilipoona amesema hivyo, nikamuelewa alichokua akimaanisha ila alikua ameishaniingiza tamaa juu ya kumpata maana aliposema tu anahamu akili yangu ikawa inaniletea picha za jinsi alivyoumbika, Salma alikua ni dada flani mzuri wa sura na amebalikiwa umbo.

Nikajikuta nimetupia mbali wazo la kumuuliza mambo ya kuolewa, nikamwambia “Sawa, huyo mtu anaekupenda ni mimi”. Alikaa kama dakika 3 hivi bila kujibu mpaka nikaanza kuwaza “Au nimekosea kumwambia? Mbona hajibu? Au anaandika ujumbe mrefu huyu… Dah” lakini ghafla nikakuta kajibu “Mmh Haya, lakini samahani, sijakuelewa vizuri unanipenda kivipi yani?”. Mh alivyosema hivyo nikawanawaza mbona kama anataka kukataa huyu wakati alikua kama anaelewa ninachotaka kumwambia?… Kwamba hajaelewa kweli?… Dah liwalo na liwe, ngoja nimuelekeze tu”. Basi nikatulia nikaandika “Salma, nakupenda sana na upendo wangu kwako nashindwa hata niuelezee vipi kwako ila tambua tu nahitaji tuwe wapenzi. nimejikuta tu nakupenda Salma, nahitaji nafasi katika moyo wako maana moyo wangu umeishauteka.” alafu nikamtumia. Akatulia kama dakika 2 hivi bila kujibu na mimi nikawa nasubiri huku moyo wangu unadunda “Nduh Nduh Nduh”.

Nakumbuka baada ya ukimya wa dakika chache akasema “Kitu gani umependa kutoka kwangu?” nikafikilia ninavyompenda nikaona siwezi elezea kitu gani nampendea maana nimejikuta tu napenda jinsi alivyo hivyo nikamjibu “Nakupenda jinsi ulivyo tu”. Akakaa tena kama dakika 4 ivi alafu akasema “kwani nikoje?” mimi nikamwambia “Ni dada falni mzuri, msafi, unajielewa na mtulivu pia, nahisi ni mungu aliniumbia… Nimejikuta navutiwa kua na wewe ikiwezekana maishani Salma. Naona nakua na furaha nikiwa na wewe. Alafu sijaanza leo kukupenda, nakupenda tangu nakutia machoni siku ile tuliokutana hapo nje”. Nilivyo mwambia hivyo, akaniambia “Kwani siku ile tuliokutana hapo nje ilikua ndio siku yako ya kwanza kuniona?” nikamjibu “Ndio salma, nilipokuona nilihisi nimekutana na malaika”. Basi nikakuta kanijibu ujumbe wa kucheka “Hahahaha” mimi nikamwambia “Kweli tena, sitanii”

Akakaa tena kama dakika 4 hivi alafu akasema “Sawa, mimi mwenyewe nakupenda ila naogopa usijekua unanidanganya mwisho ukaniumiza” mimi kwa haraka haraka nikawa na furaha nikamwambia “Siwezi fanya huo ujinga, Nakupenda sana Salma”. Nikakuta kanijibu “Haya, Nakupenda pia” nilipata furaha ya ajabu mpaka nikataka nipige kelele usiku huo mule ndani. Niliona kama ni bahati kuwa na mahusiano na dada huyo maana alikua ni mzuri na anajipenda sana kiasi kwamba ukimuona barabarani huwezi zani anatokea kwenye nyumba za kupanga, unaweza hisi ni mke wa mtu mwenye pesa sana au ni wale wadada wazuri wa kwenye video.

Basi usiku huo ulikua wa furaha sana na nilikua na hamu tukutane pindi kutakapokucha maana muda huo mvua ilikua inanyesha sana na ulikua muda mbaya tayari. Na kweli kulikucha ila nilichelewa kidogo kuamka kutokana na kuchelewa kulala na kitu cha kwanza kukifanya kilikua ni kumtumia Salma SMS lakini ilionesha kuwa hapatikani kwa muda huo. Nilipotoka nje nikakuta mlango wa Salma unaonekana kama Salma hayupo ndani maana umefungwa kwa nje. Nilivyona hivyo nilikua na vimaswali kichwani mpaka nikaamua nisiende kwenye mafunzo ya kampuni siku hiyo. Nilikaa tu chumbani kwangu, ukafika muda wa kula chakula nikaenda kununua alafu nikarudi nikakaa mlangoni kwangu nikawa nacheza gemu kumsubiri. Kwenye mida ya kama saa 4 asubui hivi nilikua nimechoka kushika simu, niliegemea pembeni ya mlango pale nje, usingizi ukanichukua.

Huko usingizini nikaanza kuota nipo na Salma sehemu nisioijua hata vizuri napambana kumshika na kumkumbatia Salma lakini nashindwa sababu yeye ananisukuma huku akinifokea kama hanijui kwa kusema “Hebu niachie… Wewe Mkaka vipi!… We mkaka!”. Dah ndoto hiyo ilifanya nishtuke toka usingizini na nilipofungua macho mbele yangu nikakuta Madada wawili wamesimama mbele yangu pale mbele ya mlango wangu wananiangalia huku wakiniamsha kwa kusema “Wewe kaka… Wewe kaka”. Basi mimi nikasema “Naam” huku nikiwa najaribu kuyaweka macho vizuri ili niwaone vizuri maana macho yangu yalikua usingizini na hao madada sikujua watakuwepo mbele yangu. Nikawaangalia sura zao haraka haraka nikakuta sura zao ni ngeni.

Basi nikakuta wananisalimia na mimi nikaitikia alafu wakauliza “Samahani kaka, tulikua tunaulizia anapokaa dada mmoja hivi anaitwa Tausi… tunasikia anakaa mitaa hii”. Mimi kwakua nilikua mgeni kidogo kwenye maeneo hayo na nilikua sijafahamiana sana na watu wa mtaa huo, sikuweza mtambua mtu wanaemuulizia hivyo nikawaambia “Ah mimi sijui watu wengi mtaa huu ila hapa hakuna mtu anaitwa tausi” wakanishukuru alafu wakawa wanaondoka. Madada hao walikua wasafi na wamevaa vinguo vifupi vinavyotega macho ya wanaume. Mimi kwa haraka haraka nilivyoona muonekano wao nilihisi huenda wanafanya kazi ya kuuza miili yao maana walikua wameanika vitu nje nje alafu hawajiwazii.

Walivyoondoka tu nikajisemea “Bora wameniamsha maana simu nimeiweka pabaya kiasi kwamba mwizi angepita maeneo haya angechukua simu bila mimi kujua”. Baada ya hapo mawazo ya Salma yakaanza kuteka kichwa changu. Nikaanza kuwaza “Dah Salma nae sijui kaenda wapi?… Naanza mpaka kukosa raha yani. Na hii ndoto nilioiota hapa ni ukweli au imesababishwa na makelele ya waliokua wananiamsha tu? Itakua ni hawa mbwa wameniletea lindoto la ajabu… ila sasa mbona hayupo na hakuniambia jana kwamba hatakuepo leo?”

INAENDELEA….

Vitu vya kufuatilia ili kujenga Imani ya Mapenzi tena (Wengi wameipoteza)





Imani ya mapenzi ya kweli, tunaweza sema ni imani, uaminifu, na matumaini yaliyowekwa katika mahusiano ya mapenzi ya dhati kati ya watu wawili. Ni hali ya kuamini kwamba mapenzi yanaweza kustahimili changamoto, misukosuko, na majaribu ya maisha bila kuvunjika. Kwa upande mwingine inaweza kuwa ni imani inayofanya uamini kuwa mnapendana, mtapendana na mtaendelea kuwa pamoja.

Imani hii ya mapenzi watu huwa nayo mwanzoni katika maisha ikiwa iko vizuri tu. Lakini baada ya kukutana na maumivu ya mapenzi, wengi huipunguza au kuipoteza kabisa. Yani unaweza kuta mtu alikua na mpenzi wake wa kwanza akiamni watakua pamoja milele lakini jambo flani baya linatokea, wanaachana akiamini hakuna mwanamke au mwanaume yoyote mwenye mapenzi ya kweli. Maumivu ya mapenzi hufanya watu wafikilie tofauti kabisa kuhusu mahusiano ya mapenzi.

Kuondoa au kupunguza Imani katika mapenzi sio jambo baya maana husaidia kuwa makini kwenye mahusiano yajayo lakini kukizidi kunaweza kuwa kubaya. Mfano; kuna watu wanaimani ndogo sana juu ya mapenzi kasi kwamba hawawezi tulia kwenye mahusiano na hata wakiingia, hayadumu kwasababu hawayazingatii wala kuwa na malengo. Hapa ndio utasikia mtu anakwambia “Sina imani na Wanawake kwenye mapenzi” au “Siamini mwanaume yoyote mwenye mapenzi”. Na kunatabia nyingi mbaya zinaweza kuzaliwa baada ya Imani ya mapenzi ya kweli kupungua au kuondoka.

Baadhi ya watu huwa kwenye hali mbaya ya kutoamini katika mapenzi mpka hutamani hata kupata msaada utakaofanya wawe na imani tena. Yani wanatamani wampende mtu mmoja kwa dhati huku wakiwa na malengo yalionyooka.

Jambo la kurudisha Imani sio jepesi sana maana hutegemena na kilichoiondoa au kuipunguza. Lakini hapa chini The bestgalaxy tumejaribu kuweka vitu vya kufuatilia ili kuongea Imani ya mapenzi ya kweli. Ni vitu vidogo sana ila vinaweza kujenga imani ya mapenzi ya kweli kwa kiasi kikubwa.

Jinsi ya kupata Mpenzi mtandaoni BONYEZA HAPA>>>

Vitu vya kufuatilia ili kujenga imani ya mapenzi ya kweli tena

Simulizi za mapenzi



Baadhi ya simulizi za mapenzi huwa zinajenga Imani ya mapenzi ya kweli unapozifuatilia. Zinaweza kuwa za sauti, maandishi na hata video lakini unapozifuatilia zinakushawishi kuingia kwenye mahusiano na kuamini yatadumu.
Kupitia simulizi hizi, unaweza jifunza mambo mbalimbali ambayo yatakusaidia kuwa mvumilivu tena, mwenye mapenzi ya dhati na kuamini kuwa mahusiano yako yatadumu. Unaweza hata kufunguka ubongo na kujua mbinu mbalimbali za kutatua changamoto ili kudumu kwenye mahusiano yako.

Mfano wa simulizi nzuri za namna hii ni simulizi iitwayo SUKARI YA DADA na UTAMU WA JUMLA.

Nyimbo za mapenzi



Nyimbo huwa zinaimbwa na watu wengi sana hapa Duniani na katika mapenzi watu haimba mambo tofauti tofauti. Baadhi ya nyimbo za mapenzi hinaweza kukusaidia kuamini tena kwenye mahusiano ya mapenzi ya kweli. Sio kila nyimbo huwa zinakua hivyo ila Kuna nyimbo nyingi chanya za mapenzi zinazoweza kukujenga kiiimani kwenye mahusiano.

Mambo ya Dini



Dini za kikriso na kiislam huwa zinamuongonzo juu ya mapenzi na hakuna inayoelezea mambo ya muumizana au kutoaminiana. Dini zote nimewaka wazi nini cha kufanya mnapopendana ili kuwa pamoja na zinahitaji muwepamoja milele. Uvumilivu heshima na mambo yote ya msingi katika kuwa pamoja kwenye mahusiano ni mambo ambayo huelezwa wazi kwenye dini.

Kwaiyo kufuatilia dini yako kunaweza kuijenga Imani na hata kukusaidia kuishi maisha na mazuri na mpenzi wako.

Mwisho ningependa kukushauri kuwa katika kufuatilia mambo haya ili kujenga Imani, ni vema ukamuhusisha na mpenzi wako. Yani mshawishi na mpenzi wako kufuatilia mambo haya ili muijenge imani kwa Pamoja.

UTAMU WA JUMLA 04 (Simulizi ya Maandishi)





Mh alikua amejisogeza karibu yangu na tulikua tumegusana kabisa kiasi kwamba nilikua najikuta nahisi vitu tofauti na kitu ninachokifanya muda huo. Mwili wake mlaini ulileta joto la ajabu mwilini mwangu alipokua karibu yangu maaana alikua ni mwanamke mwenye kila sifa ya kuamsha hisia kwa mwanaume. Ukiachana na hayo yote, alikua ananukia vizuri.

Basi siku hiyo nilifanikiwa kumrushia nyimbo kwenye simu yake na tulipeana hata namba za simu ili tuweze kuwasiliana kwenye simu. Baada ya hapo tulikua tunaurafiki nae na  urafiki huo ulikua kama unaelekea kuwa wa kimapenzi hivi japo nilikua sijawahi mwambia nampenda wala yeye hajawahi niambia hivyo.

Kuna siku tulikua tumekaa sehemu moja tunaongea pale nje mlangoni kwangu mida ya jioni… Nakumbuka tulikua tunapiga stori za kawaida huku mimi nimeshika simu yangu naangalia video za vichekesho. Salma alikua pembeni yangu kidogo upande wa kulia. Niliona video moja ikanichekesha sana mpaka nikasema “Hahah angalia video hii” Salma akasogea zaidi kwangu ili aone lakini katika kusogea kwake aliingia mpaka mwilini kabisa, mimi nikawa namuonesha video huku akili ikiwa imehama kutokana na yeye kuja mwilini mwangu. Nakumbuka aliangalia video ile alafu nikamuona akicheka “Hahaha…. wasumbufu hawa” huku akiyatoa macho yake kwenye simu na akaniangalia usoni.



Kwakua mimi akili ilikua haipo tena kwenye video ipo kwake, tukajikuta tumekaa kimya kwa sekunde chache tunaangaliana alafu tunataka kama kusogezeana midomo yetu hivi. Ilikua kama tunataka kuikutanisha midomo hivi lakini ghafla Salma akazuga kwa kushtuka na kusema “Ivi mziki huo unalia wapi?” huku akitoka mwilini mwangu. Na mimi nikajiweka vizuri na kusema “Mh  Itakua huko nyuma” na baada ya hapo tukaendelea na stori nyingine ila kiukweli ilibaki kidogo sana kuanza kupimana joto la mwili.


Ukiachana na siku hiyo, kuna siku nyingine tulikaa pamoja sehemu na tulikua tumegusana miili yetu alafu alikua amevaa kinguo kilaini kifupi ambacho kinaonesha mpaka sehemu za juu ya magoti. Tulikua tunaongea mambo ya kawaida tu ila mimi mawazo yangu ya kahama kabisa maana alikua ananigusa gusa ila yeye yupo bize kuongea ongea.
Nilikua namuangalia anavyoongea alafu kichwani nawaza “mwanamke ananukia vizuri huyu… Midomo yake mizuriii… Dah… ananipa majaribu na mapaja yake… Sijui niyaguse? Mh ngoja nijifanye kama nayagusa bahati mbaya maana natamani balaa”. Uvumilivu ukanishinda, nikajikuta tu mkono wangu nimeuweka kwenye moja ya paja lake na lilikua limejaa  sana nikaanza kulipapasa kama natafuta vitu hivi. Nakumbuka muda huo alikua anataja nyimbo anazozipenda na kabla hajamaliza, nikauweka mkono wangu. Nilivyo fanya hivyo akaacha kuongea na alishtuka kidogo na akasema kwa kisauti cha chini “OOh.. iiii… Wewe… mkaka nini?… Mbona unafanya hivyo?” Mimi ujasiri ukanikimbia nikazuga nikasema “Ku… Kuna kitu nimeona kama kimedondokea hapa” huku nikiutoa mkono.

Basi aliniangalia usoni kidogo alafu akayatupa macho yake chini kwa aibu huku akiguna “MMh”. Mimi mwenyewe nilifanya kitendo hicho kwa msukumo wa hisia zangu juu yake tu hata sikujielewa, nilipoutoa tukakaa sekunde chache alafu tukaendelea kupiga stori kama kawaida. Salma alikua ni mwanamke mzuri na alikua ananivutia ila uzuri wake ulikua unaniogopesha mpaka kumwambia nakupenda maana alikua anateka hisia mpaka akili zangu zinahama, pia nilikua nahisi ni mke wa mtu na mme wake huenda amesafiri hivyo naweza kutwa nae muda wowote.


Nilikaa kama miezi miwili hivi nilikuwa naongea nae, ninamazoea nae lakini sijamwambia kama nampenda. Ila katika hiyo miezi miwili nilikua kunavitu sivielewi kabisa kwenye maisha yake. Nilikua namuona anaishi peke yake, Sijawahi muona na mwanaume na wala Hafanyi kazi yoyote inayoonekana na karibu kila siku anapika na kula. Nilikua najiuliza hela “Anatoa wapi?” maana hata kutoka nyumbani huwa hatoki mara kwa mara, anaweza kwa wiki akatoka mchana masaa mawili kwa siku moja au mbili tu akarudi nyumbani. Usiku pia huwa anatoka na anarudi asubuhi ila hii katika miezi hiyo miwili niliwahi muona akitoka usiku mara moja tu na alirudi na mchubuko kidogo kwenye paji lake la uso. Nikamuuliza aliniambia alikua kwenye sherehe na kuna mtu alimuumiza kwa bahati mbaya.

Siku moja katika mida ya saa 5 usiku hivi nilikua nikitumiana nae SMS kwenye simu yeye akiwa kwenye chumba chake alicho panga na mimi kwenye chumba changu. Kimvua kilikua kinanyesha siku hiyo nje na kilianza mida ya saa 4 usiku hivi. Nakumbuka katika kutumiana SMS Salma aliniambia “Yani mvua ya leo imeleta baridi hatari… yani nimejifunika shuka mbili nzito lakini bado nahisi baridi” mimi nikasema “Ah mimi huku nina shuka moja jepesiii, fikilia baridi ninayoihisi hapa ni kiasi gani” akasema “hahah wewe basi unatia huluma, Au nikupe shuka moja zito unipe lako jepesi?”. Basi mimi nikajibu “Njoo unipe utakua umenisaidia sana Salma” alafu nikawa nasubiri atakachojibu. Nikakuta anachelewa kujibu nikaanza kuwaza kichwani “Eh mbona anachelewa kujibu huyu, anakuja kweli nini?… Mh kwajinsi alivyoumbika sita mruhusu atoke… Mh na ile mizigo yake aliobeba nitakavyoifanya hata amini…. Mtoto msafi balaa”.




Wakati nikiwaza hayo nikakuta SMS toka kwa Salma imeingia, moyo wangu ukadunda pigo moja kubwa “Nduh” nilipoona SMS imeingia na nilipoifungua nikakuta amesema “Mh ningekuja kukupa ila naogopa”. Nikamjibu “Unaogopa nini sasa?” akajibu “nakuogopa wewe” mimi kama utani nikamwambia “Haha kwanini sasa unamuogopa anaekupenda?” akachelewa kidogo kunijibu alafu akaja kujibu “Mh wewe acha kunirusha roho bana… nani huyo ananipenda?”. Alivyosema hivyo mimi nikapumua kwa nguvu kama mara mbili hivi alafu nikatuliza kichwa nikaandika “Mimi hapa nakupenda. alafu nilitamani ujue hili toka nakuona kwa mara ya kwanza. Nakupenda sana Salma, umeukamata moyo wangu mpaka nashindwa elewa jinsi ya kuelezea upendo nilionao kwako, sitamani nikukose… Nataka uwe mpenzi wangu”. Baada ya kuiandika nikawa kama nimeituma hivi alafu nikaiweka simu pembeni ya kitanda changu kisha nikalala chali nikawanaangalia juu huku nikiwanawaza “Dah sijui atakubali huyu… Akikubali nitamfaidi kweli na ile mizigo ya nyuma alafu Kabinuka… Kifua chake tu kizuri sijui ndani atakuaje. Mtoto namuona mtamu kabla sijamla Dah… nilipanga kutokumpa moyo mwanamke ila huyu sjui kaniibia moyo?” alafu hapo hapo nikaanza kuwaza tena “Mh ila huyu mwanamke nikimtongoza na akikubali alafu baadae mtu akaja kusema natembea na mke wake si nitaharibu kilakitu nilichojia huku Dar?… Wazazi wangu wakisikia nimepata matatizo kwasababu ya kutembea na mke wa mtu watanionaje? wataendelea kutupa hela zao kwaajili yangu kweli? Mh sidhani”.

Nikakuta Ghafla SMS toka kwa Salma imeingia imeandikwa “Wewe, mbona kimya?” nikashtuka nikaangalia vizuri nikakuta SMS nilioiandika kumbe sikuituma, hivyo haikwenda. Nikajicheka kidogo huku nikijisemea “Bora hata haikwenda, ngoja nimuulize maswala ya kuolewa vizuri maana ananitamanisha lakini nikienda kichwa kichwa naweza umia mimi. Ila kama huyu ni mke wa mtu basi waliosema mke wa mtu mtamu hawajakosea kabisa… Ngoja nimuulize” nikaifuta ile SMS niliotaka kuituma. Nilivyofuta nikamwambia tu “Salma, nikuulize Swali?” alafu ikapita kama dakika moja nikakuta anajibu “Ah hapana usiniulize, nijibu kwanza swali langu”….




INAENDELEA….

Jinsi ya kurudiana na mpenzi wako wa zamani (Ex)

Kurudiana na mpenzi wako wa zamani inaweza kuwa hatua kubwa inayohitaji fikra za kina na maandalizi mazuri. Watu wengi hupitia hali ya kutaka kurudiana baada ya uhusiano kuvunjika. Lakini sio jambo la kukurupuka tu; kuna masuala mengi ya kuzingatia kabla ya kuchukua hatua yoyote.

Katika makala hii, tutajadili hatua muhimu unazoweza kufuata ili kurudiana na mpenzi wako wa zamani kwa njia yenye mafanikio. Kila hatua imeundwa kukusaidia kufikiria kwa kina na kuimarisha uhusiano wenu unapofanikiwa kuurudisha kwenye uhai. Lengo ni kuhakikisha kuwa kurudiana kwenu kunaleta furaha na uimara badala ya maumivu ya zamani. Endelea kusoma ili uione njia bora ya kurudisha mahusiano kwenye hali nzuri.

Mambo ya kufanya kwa Mpenzi asieonesha kukupenda BONYEZA HAPA>>>

Jinsi ya kurudiana na mpenzi wako wa zamani

Fikilia maamuzi yako kabla ya hatua

Kwanza kabisa; Fikilia maamuzi unayotaka kufanya kama ni sahihi au si sahihi. Na tena ufikilie kuwa kama maamuzi ni sahihi kwasasa ila yataonekana kawa mabaya baadae, hautajilaumu sana.
Kwenye mapenzi, kuna baadhi ya watu huachana na mtu alafu hupata mtu alie sahihi, na pia kuna watu hurudiana na mtu alie sahihi. Sasa unahisi utakua ni yupi kati ya hawa watu? Hebu fikilia vizuri kwanza maamuzi yako.

Angalia kama kuna upendo kati yenu

Upendo ni kitu kigumu kukificha kikiwepo kati yenu hatakama mumeachana. Na kama mumeachana ila kuna upendo kati yenu, kunakua na uwezekano wa kurudiana. Kwaiyo kama unataka kurudiana na mpenzi wako, angalia kwanza kama kuna upendo kati yenu.


Unaweza utambua upendo kirahisi kwa kujaribu kuwa karibu nae. Angalia kama anawivu na wewe, angalia kama anakuwekea milango ya mumuingia, angalia kama uwepo wako karibu nae anautambua au kuukupenda kabisa.

Mfano mzuri; kwenye simu unaweza kuta alikublock lakini baada ya muda kaondoa block. Au kama sio kwenye simu basi anaweza hata kuwa mara nyingi anakuja katika sehemu unazoweza kumuona kirahisi na kuanza kuongea nae.

Jenga uaminifu upya

Kama mlitengana kwasababu iliopelekea asikuamini, basi unatakiwa kufanya kazi kubwa sana ya kujenga uaminifu. Mfano; Ikiwa ulimsaliti ndio mkaachana, utakua na kazi ya kumfanya aamini kuwa unajutia kosa lako, hautamsaliti tena na hauhitaji kumpoteza kwenye maisha yako. Tena kwa vitendo zaidi na sio maneno tu.


Kujenga uaminifu kunaweza kuchukua muda sana ila hakikisha unazingatia sana swala hilo maana asipokuamini, kunakua na uwezekano mkubwa wa kuvutiwa na wengine anaohisi wanamapenzi ya dhati kulio wewe. Hii ni kwasababu kosa lako limekua kama ishara ya kuwa hauna mapenzi ya dhati kwake.

Anzisha mahusiano ya mapenzi rasimi kwa uangalifu

Mwisho, fanya kuanzisha mahusiano ya mapenzi rasimi. Unaweza anza kufanya hivi kwa kumwambia bado unampenda na kuomba nafasi ya kuwa nae. Akikubari, utakua tayari umeingia nae kwenye mahusiano. Lakini usiishie kujiachia tu, jaribu kuwa muangalifu kwenye mambo mbalimbali kati yenu. Zingatia kuendelea kujenga uaminifu na kufanya mahusiano yenu yawe imara zaidi.

Wakati ukifanya yote hayo, epuka kulazimisha mpenzi au mtu ulieachananae kurudiana tena. Yani ukiona dalili za yeye kutotaka murudiane kivyovyote, acha kumfuatilia kabisa maana hata baada ya kurudiana unaweza kuteswa kihisa.