Category Archives: Mahusiano

Jinsi ya kumueleza hisia zako Mwanaume bila kusema unampenda

Kuna mtaalam mmoja wa mambo haya alisema hivi…

Mara nyingi kuwa na aibu ndio chanzo cha wanawake wengi kushindwa kuwaeleza hisia zao kwa wanaume wanao wahitaji na kibaya zaidi wanawake tunaweza kutunza siri zetu kwa muda mrefu hivyo, hutunza pia hizo hisia kama siri nyingine japo hutuumiza sana pale wanaume tunaowapenda  wanapoenda kwa wanawake wengine.

Wapo baadhi ya wanawake ambao hawana uoga katika kueleza hisia zao kwa wanaume na pia huwa huru pindi wanapokuwa karibu na wanaume. Lakini wanawake wengi ni sisi ambao tunashindwa hata kuongea pindi tunapo wakaribia wanaume tunaowapenda.

Sio kwamba tunakosa ustadi wa kimapenzi wa kimapenzi au hatujui kutamka maneno ya kueleza hisia zetu ila ni tunasikia raha na furaha inayotuzidi mpaka tunaogopa maana mapigo ya moyo hupiga kwa kasi na maneno yote hupotea na hurejea baada ya mwanaume uondoka.

Kuwa na aibu hakupaswi kukuzuia kumueleza mwanaume unayempenda hisia zako. Kuna mambo madogo madogo ambayo unaweza kuyafanya na ukafanikiwa kufikisha ujumbe wa hisia zako kwa mwanaume unayempenda lakini kitu cha msingi inatakiwa kujiamini tu.

Badala ya kumfuata na kumwambia mwanaume vile unajiskia juu yake unaweza tumia njia ya vitendo itakayo mfanya kukuzingatia na kuelewa kuwa unamuhitaji na utamfanya akuhitaji pia.

1.Wasiliana nae kwa macho.

Kuwasiliana kwa macho ni moja wapo ya njia rahisi na ya hila zaidi ya kumruhusu mwanaume ajue kuwa unavutiwa naye. Wakati mwingine wazo la kuwasiliana na mtu usiempenda linaonekana kuwa la kichefuchefu, lakini ikiwa unafikiria ni mzuri, muangalie. Kama ni muoga sana basi jaribu kuangaliana na picha yake kwenye simu yako. Usimtazame kama wewe ni polisi na yuko kwenye orodha ya watu wanaotafutwa. Mtazamo mfupi ndio unahitajika yaani muangalia mpaka ugonganenae macho na agundue ulikua unamungalia kisha acha kumuangalia na uiangalie sehemu nyingine (ila usingalie chini kamwe) huku ukiendelea na shughuli zako. Kitendo hiki ukiwa unakifanya kitamfanya ahisi kitu juu yako na anaweza kuanza mawazo ya upendo juu yako.

Katika Matumizi yako ya simu usifanye vitu hivi (Unaweza juta!) GUSA HAPA>>>

2. Weka tabasamu.

Pindi unapomuangalia hakikisha anakukuta na tabasamu zuri la kupendeza. Sio anakukuta unamuangalia huku umeweka sura ya kawaida tu utamfanya asihisi chochote juu yako na akakuona ni mtu unaemfuatilia mambo yake hivyo hakikisha unaweka tabasamu zuri litalomuonesha kufurahishwa na yeye. Akikukuta katika hali hii moja kwa moja atagundua umevutiwa nae.

3. Muulize swali kuhusu jambo flani.

Hii ni njia nzuri sana kwaajili ya kuanzisha mahusiano kati yenu.

Kuuliza swali kuhusu jambo flani au kuomba usaidizi juu ya jambo flani. Unaweza muuliza mwaswali ambayo yatamfanta ajibu kwa urefu au atumie muda wake kukuelekeza.

Mfano: Eliy, nimependa wallpaper ya simu yako, naomba nielekeze jinsi ya kuweka wallpaper kama yako?

Naomba nielekeze jinsi ya kufanya kitu hiki?

Njia hii pia utakusaidia kuanzisha mazungumzo nae yaani pale unapokosa neno la kuongea au kuanza mazungumzo basi unaweza uuliza kuhusu kitu flani.

Mbinu 6 zitakazo kusaidia katika mapishi yako GUSA HAPA>>

4. Mtege kwa kujichezesha.

Kila mwanamke anavitu ambavyo anajua vinamshawishi zaidi mwanaume katika mwili wake. Vitu hivi vinaweza kuwa ni lips nzuri, macho na vinginevyo. Vitu hivi unaweza vitumia pale ambapo unakuambele ya macho yake au unapogundua anakuangalia. Kuvitumia vitu hivi kunaweza kumchanganya mwanaume kisawa sawa mpaka akashindwa kuongea na kumfanya avutiwe na wewe zaidi.

 Mfano, unaweza zichezesha lips zako pindi anapokuangalia na kukuelekeza kitu fulani ulicho omba akuelekeze.

Kwakufanya vitendo Kama hivi kutachochea hisia zake kwako.

5. Toa maoni juu ya kile unachokiona kwake na pia usisahau kumsifia na kusifu anavyovipenda.

Kila mtu anapenda kusifiwa na  sikuzote watu huwapenda watu wanaowasifu pia unachotakiwa kujua ni kwamba  wanaume wengi huongeza juhudi katika jambo fulani pale wanaposifiwa yaani kama ni mchezaji mpira alafu ukawa unamwabia kuhusu uchezaji wake mzuri wa mpira basi utamfanya ajiskie vizuri mpaka ataanza kukualika mazoezini ili tu umuone anachokifanya na umsifie tena. Hivyo basi kumsifu inaweza kuwa njia nzuri ya kufanya avutiwe na wewe.

6. Usichukue vitu kibinafsi.

Ikiwa umemfanyia yote hayo na bado haoneshi matokeo mazuri juu yako, Usihisi kuwa wewe ni mbaya au hunamvuto. Huenda haoneshi dalili nzuri juu yako kwasababu hataki kukuchezea hivyo unapaswa kuheshimu pia mawazo yake na kuendelea na maisha yako huku ukimtafauta anaekupenda kwa dhati. 

”kwanini wanawake wazuri/warembo hawaolewi?” sababu zinaweza kuwa hizi

Mara nyingi wanawake warembo na wenye mvuto wa kumvutia kila mwanaume huishia kuzisikia ndoa kwa wenzao tu kutokana na sababu mbalimbali.

Wengi huwa na tabia ambazo huudhi na huwaogopesha wanaume wanaowahitaji bila wao wenyewe kujijua.

Ivi unaweza kuchagua kuwa na kitu chenye muonekano mzuri maishani mwako kitakachokupa shida na maumivu milele?

Ikiwa watu hushindwa kuvumilia kuishi na vidonda vinavyowapatia nyumba, magari na pesa, unafikiri urembo/uzuri unaweza kuwa na nini cha ajabu kwenye maisha?

Wanaume huwa sio wajinga na katika asilimia kubwa ya wanawake wanaoolewa huwa ni wanawake wa kawaida sana ukiwaangalia kwa macho jinsi walivyo, mpaka unakuta wengine wanajiuliza “mbona kamchagua mwanamke wa kawaida sana pamoja na malizote zile?”

Ukiwa mrembo/mzuri utapendwa na wanaume wengi ila watakupenda kwa lengo la kupata Penzi tu, baada ya hapo utakuwa wa kuchezewa na baadhi ya sababu zinazopelekea wanaume kufanya hivyo ni zifuatazo;

Tabia

Wanawake kama hao huwa na tabia mbaya na nikiongelea tabia mbaya basi najumuisha uvaaji, ukaaji, viwanja vya starehe, lugha zisizo nzuri na marafiki pia. Vitu hivyo humtenganisha mwanamke mzuri na wanaume wa oaji. Labla akutane na mtu wa tabia yake lakini asilimia kubwa ya wanaume wenye tabia hizo huwa wanatafuta wanawake waliotulia huku wakiendelea wanawake warembo wasio tulia. Wanaume wengi huwa hawapendezwi na tabia za aina hiyo hata mwanamke awemrembo kiasi gani.

Kuwa na maringo sana

Unakuta mwanamke ameweka kucha ndefu, nzuri,za kuvutia na anamaringo kiasi kwamba mwanaume mwenye mpango wa kuoa akimuona anajiuliza 

“Sasa kwa hizi kucha atanifuliaje nguo?… Anamaringo sana sijui itakuaje tukipishana?… Anaanzaje kuosha vyombo?… Ivi atakubali kutulia na kulea mtoto?.. Inaonekana hata kupika hajui”

Mwisho mwanaume anaona hafai wala haoneshi tabia zozote za mwanamke ambae anatakiwa kukaa katika nyumba.

Katika Matumizi yako ya simu usifanye vitu hivi (Unaweza juta!) GUSA HAPA>>>

Ghali kuwatunza

Wanawake warembo huwa ghali kuwatunza kwa sababu wamejiwekea dhana kuwa wanafaa kupelekwa katika hoteli kubwa kubwa na maeneo yaliyo na bidhaa ghali. Huwa hawalegezi msimamo hasa kuhusu mahitaji yao na wanakotaka kwenda kununua bidhaa.

Mwanaume akipiga hesabu za haraka haraka kuhusu ghalama ambazo anatumia kipindi cha ambacho yupo na mwanamke mrembo anaependa kulidhishwa kwa kufanyiwa mambo makubwa huwa anagundua kumuoa ni sawa na kubeba mzigo mzito sana kichwani.

Ni wabinafsi

Wanawake wa aina hiyo huishi wakifikiria dunia ni yao na kwamba wanafaa kuabudiwa na kila mwanamume. Wanaume wengi hupenda kuwa katika mahusiano nao na hii ndio sababu kubwa ya wanawake hawa kujiona wa hali ya juu sana.

Wasichojua ni kuwa wanaume huwatumia tu na kuwaacha kutokana na tabia zao ili kutafuta mwanamke mzuri wa kuoa. Kibaya zaidi ni kwamba, wanawake hawa huendelea kutiwa moyo na uzuri wao huku wakisahau kuwa umri walionao hauwasubiri.

Hawataki kuwa wazazi

Wanawake hao hupenda kusalia wakiwa wanapendeza, hivyo huwa wanaogopa kuzaa wasipate mikunjo, wasinenepe au kuwa na matiti kulegea. Kwa kawaida, hakuna mwanamume anayependa kuoa mwanamke ambaye hawezi kumzalia, hasa kwa sababu ya utamaduni wa Kiafrika. 

wavivu kutatua changamoto za mahusiano

Kuna wanawake ni warembo na wazuri sana kiasi ambacho wanaume huwafananisha au huwasifu kuwa ni kama malaika. Kutokana na kusifiwa sana hujiona wazuri sana na hupenda kuwa kama yai kwenye mahusiano. Ukweli ni kwamba hata uwe mzuri vipi, kuna changamoto utakutananazo kwenye mahusiano. Nikizungumzia changamoto inaweza kuwa umekuta mweza wako kabadilika ghafla au kunajambo limetokea katiyenu na linafanya musielewane. Wanawake wazuri wanapokutana changamoto hizi huwa hawajisumbui kutatua changamoto…. Wanaona bora kubadilisha mwanaume kuliko kutafuta njia inayoweza rekebisha mahusiano yao hatakama wao ndio chanzo cha kuyumbisha mahusiano. Hali hii inawafanya wawewanabadilisha tu wanaume na hawafikii hatua ya ndoa… Na hata wakiingia kwenye ndoa huwa sio wavumilivu maana ndoa inachangamoto nyingi zaidi.

Sasa kama una sifa za aina hiyo, huenda ni wakati wako kubadilika ikiwa unataka kupata mume. 

Fanya haya baada ya kondomu kupasuka katika tendo

Mpira wa kondomu hutumika katika tendo la kujamiiana ili kuzuia mimba na vile vile hutumika kwa lengo la kuzuia maambukizi ya virusi vya ukimwi na magonjwa mengine ya zinaa. 

Katika utumiaji wa mipira ya kondomu kupasuka kwa kondomu hutokea mara nyingi Sana bila kutarajiwa. Mara nyingi kitendo hiki husababisha mimba zisizotarajiwa na maambukizi ya magonjwa ya zinaa. Hapa kuna hatua nne unazoshauriwa kuzifuata iwapo kondomu imepasuka:

1. Kuwa mtulivu na tafuta kondomu hiyo iliopasuka.



Mara nyengine kwa mwanamke vipande vya mpira huo wa kondomu vinaweza kuingia ndani ya mwili.

Ingiza vidole vyako ndani ya mwili, vishike na kuvitoa nje.

Mipira ama vipande vya kondomu vinavyosalia ndani ya mwili wa binadamu vinaweza kusababisha hasara hivyobasi ni muhimu kuangalia na kuhakikisha kuwa umetoa kondomu yote.

2. Tumia dawa za kuzuia kushika mimba iwapo hamjakubaliana kupata mtoto(Kwa mwanamke)



Dawa hizi zinapaswa kutumiwa katika kipindi cha saa 72 tu. Zinauzwa madukani yaani zinapatikana katika maduka ya dawa.

Iwapo huna mpango mbadala unaweza kutumia dawa za kupanga uzazi.



3. Kupimwa magonjwa ya zinaa hususan HIV iwapo hujui hali ya mwenzako




Nenda katika kituo cha dharura karibu nawe na umwambie daktari yaliofanyika.

Pia unaweza kuchukua dawa aina ya Post Exposure Prophylaxis (PEP) katika kipindi cha saa 72.

PEP ni mchanganyiko wa dawa za kukabiliana dhidi ya virusi vya ukimwi ambazo zinakuzuiwa kutoambukizwa HIV iwapo mwenzako ni mwathiriwa.

Kumbuka kwamba kila ugonjwa wa zinaa una muda wake wakati unapoambukizwa na wakati utakapoonyesha unapopimwa.

Unashauriwa kufanyiwa vipimo zaidi vya vya magonjwa ya zinaa baada ya mwezi na baada ya miezi sita ili kujua hali yako.



4. Jiulize kuhusu kilichosababisha na usirudie kosa.





Wapenzi wengi huruka hatua hii bila kujua kuwa hayo ni makosa makubwa, kwa sababu utakapoelewa ni kwa nini mpira huo ulipasuka ndipo unaweza kujiweka vizuri katika mchezo mwingine. Hivyobasi jiulize kuhusu hilo.

SMS za mchana mwema kwa mpenzi wako

Ukiwa kwenye mahusiano Unaweza kufanyia vitu vingi kwema kwa mweza wako ili kuonesha unamjali. Kutumia ujumbe wa mapenzi mpenzi wako ni Moja ya Jambo linaloonesha kujali pia… Mukiwa ni wapenzi mulio mbali hii inaweza kuwa ni kitu muhimu kinachojenga mahusiano kuliko hata kutuma tuma pesa.

Zifuatazo ni SMS au meseji za kumtakia mchana mwema mpenzi wako. Kama unahitaji Unaweza chagua zinazoendana na mahusiano yako kwa sasa kisha ukazitumia kwa umpendae. Endelea kuwa karibu na The Bestgalaxy kwa mambo mengine mazuri zaidi.

SMS za mchana mwema kwa mpenzi wako

Upendo wangu kwako huongezeka kila wakati ninapokutazama. Hautafifia wala kuisha kwa sababu hauna mwisho. Kila mara kumbuka kuwa Nakupenda sana na kwa muda huu nakutakia mchana mwema kipenzi changu.



Mpenzi, muda huu nakukumbusha tu kuwa wewe ndio chaguo langu. Yaani naomba ujue kuwa wewe ni Mfalme wa kasri langu na kwamba moyo uliokaa kifuani mwangu utalidunda jina lako. Ninakupenda zaidi ya ninavyoweza kusema nakupenda. Mchana mwema mpenzi wangu.






Nakutakia mume/mke mtamu zaidi ulimwenguni siku njema. Hakuna mtu katika ulimwengu mzima anaweza kuwa mpenzi wa maisha yangu kwa sababu nafasi hiyo tayari imechukuliwa na wewe, mume/mke wangu mpendwa. Nakupenda Saana na napenda kukupenda.



Asante kwa kupenda kila kitu changu, pamoja na kutokamilika kwangu. Mungu alinipa zawadi isiyo na kifani maishani mwangu pale alipokuumba wewe mpenzi wangu. Nakupenda sana kuliko ujuavyo.




Tambua kuwa wewe ni mtu pekee katika ulimwengu wote ambaye hufanya maisha yangu kuwa kamili kabisa na maridadi. Mpendwa, asante kwa kuleta joto na mwangaza katika maisha yangu. Sijawahi jutia kukupenda.





Nina nafasi moyoni mwangu ambayo hakuna mtu anayeweza kuchukua kwa sababu hakuna mtu mwingine anayeweza kunifanya nifurahi kama unavyonifanya. Nakutakia mchana mwema.




Wewe ni damu ambayo hupitia mishipa yangu. Wewe ndiye kipande muhimu ambacho hufanya roho yangu ikamilike. Siwezi kamwe kuishi katika ulimwengu huu bila wewe, mpenzi wangu wa thamani. Kuwa na siku mchana mwema huko uliko!


SMS za kumtakia mpenzi wako usiku mwema GUSA HAPA>>>




Kuangalia machoni pako kunanipeleka kwenye ulimwengu wenye zaidi ya maelfu ya furaha. Penzi lako hufanya nijihisi Niko paradiso. Umeniweza sasa, naomba kokote uendako usisahau kuwa nakupenda mpenzi wangu. Mchana mwema kwako.

Kila nikiona simu au SMS toka kwako moyo wangu hudunda kwa furaha… Kiufupi nakupenda na natamani kuelezea upendo wangu zaidi ya kukuambia “nakupenda” ili tu utambue na usije kuniumiza. Tambua hilo kipenzi changu… Nakutakia mchana mwema.

Ukiona dalili hizi Jua Account yako ya Facebook  imedukuliwa na si salama GUSA HAPA>>>>

Maneno ambayo hautakiwi kusema kwa mwenza wako

Endapo umekwisha ingia katika mahusiano au unatarajia kuingia katika mahusiano ya kimapenzi, yapo mambo yanyofaa ambayo unaweza kumwambia mpenzi wako naye akafurahi, lakini yapo mambo ambayo kimsingi hupaswi kabisa kumwambia mpenzi wako. Kwani endapo utaamua kumwambia utatengeneza njia ambayo itawafanya mahusiono yenu yafe mara moja.
Maneno yafuatayo ni hatari kwa kuwa yanaleta madhara makubwa moyoni mwa mlengwa na ni vyema kuzuia kuyatamka kwa namna yoyote ile.

Jinsi ya kufanya mpenzi wako akuwaze Kila mara BONYEZA HAPA>>>

Maneno ambayo hutakiwi kuyasema kwa mwenza wako


1. Nakuchukia

Chuki ni kitu kikubwa sana, kwa kweli huwezi kuishi na mtu ambaye unamchukia. Hutakiwi kumtamkia mwenza wako neno hili. Unaweza kuchukia tabia yake lakini si yeye mwenyewe. Njia nzuri ni kusema kuwa โ€œNachukia au sipendi tabia yako ya kuchelewa kurudi nyumbaniโ€ au maneno yanayofanana na hayo.


2. Maneno ya matusi

Maneno kama โ€œmjingaโ€ au โ€œmpumbavuโ€ yasitumike kwa mwenza wako hata kama yana ukweli ndani yake. Japo ujinga ni kutofahamu kitu fulani lakini neno hili linaleta majeraha kama likitoka kwa mwenza. Hasa kama linatoka wakati wa ugomvi au kutofautiana.
Usiseme maneno mabaya yanayomshusha mweza wako mfano kuhusu mwonekano mbaya wa mwenza wako kama โ€œsura mbayaโ€,โ€Mnene kama nguruweโ€ na maneno mengine kama hayo.

Ukiona dalili hizi Jua Account yako ya Facebookย  imedukuliwa na si salama GUSA HAPA>>>>


3. Kumfananisha tabia mbaya mwezi wako na wazazi wake.

โ€œTabia zako kama mama yakoโ€, au โ€œ..kama baba yakoโ€ maneno yanayomfananisha mwenza wako na wazazi au familia anakotoka yanachokoza sana na huweka vidonga kwa muda mrefu moyoni na yaepukwe.


4. Acha! nitafanya mwenyewe

Katika mahusiano kusaidiana ni jambo la kawaida na muhimu, maneno mabaya ya namna hii yanamvunja moyo mweza wako kutaka kufanya jambo kwako siku nyingine na linaleta utengano na kuvunjika kwa upendo.


5. Maneno mabaya ya kukatisha tamaa

โ€œHutawezaโ€ ,โ€Hutafanikiwaโ€ n.k yanavunja moyo kwa mwenza wako na kurudisha nyuma maendeleo. Ni muhimu kwa wenza kupeana moyo na kusaidiana ili wote muende mbele kwa pamoja. Umoja ni nguvu.
Hivyo nikusihi ya kwamba kama kweli unataka kudumu katika mahusiano acha mara moja kumwambia maneno hayo, bali unatakiwa kumfariji kwa maneno mazuri yenye kuleta upendo wa kweli na kujenga hamasa ya kudumu

Magroup ya WhatsApp ya kujiunga bure GUSA HAPA>>>

Mazoezi ya mwili ambayo husaidia katika Mapenzi

Mazoezi ni kitu muhimu sana katika maisha ya mwanadamu kwa sababu huuweka mwili vizuri na huuepusha na baadhi ya magonjwa pia. Mazoezi pia yamethibitika kusaidia katika kuuweka mwili mwili vizuri katika upande wa tendo la kujamiiana/kufanya mapenzi kwa jinsia zote mbili. Lakini unatakiwa kujua kuwa si mazoezi yote huwa na faida katika upende wa kufanya mapenzi bali ni mazoezi ya Kigel ndio huwa na faida katika upande huu.


Kigel ni aina ya mazoezi rasmi yalioandaliwa kwaajili ya kuimarisha misuli ya nyonga na viungo vilivyopo chini kwa mwanaume na mwanamke. Mazoezi haya husaidia viungo vilivyopo chini ya nyonga kuboresha mawalisiliano, kuboresha udhibiti wa kibofu cha mkojo na pia huimarisha uwezo wa kufanya tendo/mapenzi

Ukiona dalili hizi Jua Account yako ya Facebook  imedukuliwa na si salama GUSA HAPA>>>>

Jinsi ya kufanya mazoezi ya kigel
Kitu kizuri kuhusu mazoezi haya ni hayahitaji gharama zaidi ya muda wako maana unaweza yafanya hata ukiwa nyumbani. Mazoezi haya hufanywa na wanaume au wanawake. Tafuta sehemu yenye hewa safi na nafasi ya kutosha pia iweinaruhusu wewe kulala chini (chini pawe pasafi au weka kitambaa), inaweza kuwa ni chumbani, sebleni na ikiwezekena nenda katika vyumba maalumu vya kufanyia mazoezi. Baada ya hapo unaweza fanya mazoezi yafuatayo;

Zoezi la kwanza;

Lala chali katika sakafu ilionyooka, kunja magoti kisha pandisha kiuno juu kabisa kama picha iliopo juu inavyoonesha. Baada ya kufanya hayo anza kupandisha kiuno hicho na kukishusha. Endelea kufanya hivyo kwa muda usiopungua dakika tano.

Zoezi la pili;



Jilaze katika sakafu ukiwa umenyooka na umeangalia chini, kisha unyanyue mwili wako kwa kutumia miguu yako na mikono yako kama jinsi picha inavyoonesha. Kaa kwa kuganda kama ulivyo na hakikisha wiliwako unanyooka kama rula kutoka miguuni hadi kichwani. Endelea kukaa kwa muda usiopungua dakika tano.

Zoezi la tatu;

Lala chali ukiwa umeinyoosha miguu alafu nyanyua mikono na miguu juu kisha kunja magoti miguu ikiwa bado ipo hewani. Anza kuushusha mguu wa upande mmoja wakati huohuo hukishusha mkono wa upende tofauti na uliopo mguu kisha rudisha tena mguu na mkono juu. Rudia kitendo hicho kwa mguu na mkono mwingine. Endelea kurudia rudia tena tendo hilo kama picha inavyooneshwa katika picha inavyooneshwa hapo juu kwa muda usiopungua dakika tano.

Maneno ambayo hutakiwi kuyasema kwa mwenza wako GUSA HAPA>>>

Hayo ni baadhi tu ya mazoezi ya kigel ambayo unaweza fanya kila siku ili kuuweka mwili wako uwe vizuri katika tendo la kujamiiana. Sasa tuangalie baadhi ya faida ambazo mtu anaefanya mazoezi haya huzipata.


Faida kwa mwanaume

  • Huongeza uwezo wa kujizui kumaliza tendo kwa haraka
  • Huimarisha misuli katika sehemu zake
  • Huongeza uwezo wa kubana mkojo

Faida kwa mwanamke

  • Huimarisha misuri ya nyonga na kuifanya iwe fanisi
  • Huongeza hamu ya kufanya mapenzi
  • Hufanya mzunguko wa damu ufanyike vizuri katika sehemu zake.

Natumaini mpaka hapa umejifunza kitu na nakusihi endelea kuwa na The Bestgalaxy hakikisha upo na sisi kila wakati ili uendele kupata vitu vizuri.

Ujumbe mzuri kwa mpenzi wako katika kipindi cha Krismasi

Kipindi cha mwisho wa mwaka ni kipindi kizuri sana cha wapenzi kutumia muda wao pamoja. Sasa kama unampenzi basi katika ukaribu wenu wa kipindi hiki unaweza kumtumia mpenzi wako ujumbe mzuri utakao mfurahisha na kujiona wa peke katika maisha yake. Hapa tume kuandalia jumbe nzuri unazoweza mtumia mpenzi wako katika kipindi cha Krismasi. jumbe hizo ni zifuatazo;


~~~~Tulikutana, tukapambana ili tubaki pamoja, tukashinda na tulikua na nguvu katika changamoto zote tulizokabiliana nazo mpaka kufika hapa. Nafikili penzi letu litazidi kuwa imara zaidi. Nimependa kutumia Christmas hii kukukumbusha kuwa, nakupenda sana mpenzi wangu.~~~~

~~~~~~Penzi lako ni zawadi bora ambayo ninaweza kuifurahia zaidi! Krismasi njema, mpenzi!~~~~

~~~~Siku zinakwenda, masaa yana kwenda mimi bado nipo na wewe. Unaona naishi kwa furaha, naona kuishi ni raha lakini tambua sababubu kubwa ni wewe. Tafadhari usije sahau kuwa nakupenda na moyo wangu umetekwa na wewe.~~~~~~

~~~~~Krismasi inakuja mara moja kwa mwaka, lakini tafadhali jua kwamba ninakuenzi kila siku, bila kujali umbali kati yetu. Christmas njema mapenzi wangu.~~~~~

~~~~Nakutakia Christmas njema mme/mke wangu… Nakupenda Sana na ningependa popote ulipo utambue una nusu ya moyo wangu na nusu niliobakinayo yote inakupenda wewe.~~~~

~~~~Penzi letu ni changa bado lakini upendo wangu kwako upo zaidi ya unavyoweza kufikilika, nakupenda Sana na nafurahi kila nikikuona mbele ya macho yangu hakika umeteka hisia zangu. Nakutakia furaha msimu huu wa sikukuu na nitafurahi zaidi tukitumia wote siku ya Christmas.~~~

~~~~~Wewe ni ua zuuri lililoota katika bustani ya moyo wangu, tena ni ua pekee la thamani, linalonipa furaha katika maisha yangu. Nakupenda Sana na najivunia kuwa na wewe malaika wangu. Kuwa na furaha tele katika msimu huu wa sikukuu, kipenzi changu!~~~~~~

~~~~~Hakuna raha kama kupendwa na wewe na sijawahiona karaha kuwa na we. Kama moyo wangu ungekuwa wazi, ungejiona ukiwa peke yako na ukobusy kunipa furaha. Nakupenda Sana na nakutakia furaha katika msimu huu!~~~~~

~~~~Katika Christmas hii nitapenda niwe na furaha, na nikae na mtu ninaempenda na anipae furaha. Vyote hivyo vitakamilika endapo tutatumia siku hiyo pamoja maana utanipa furaha na vile vile nitakuwa na wewe nikupendae na unapae furaha. Mpenzi, tutakua wote si ndio?~~~~

~~~~~Wanasema furaha haiwezi kupimwa kwa maneno halisi, Ni kweli. Tambua kuwa Krismasi hii inatukumbusha kwamba upendo, furaha, na nia njema ndio vitu halisi vinavyoinua maisha yetu. Asante kwa furaha unayoniletea tangu nilipokutana na wewe, mpenzi wangu.~~~~~

SMS za kumtakia mpenzi wako usiku mwema

Kutuma sms au ujumbe wenye maneno mazuri kwa mpenzi wako, ni kitu muhimu sana katika mapenzi. Unapotuma ujumbe/message moja kwa moja unakua umeonesha kumjali na pia kumkumbusha kuwa yeye ni wamuhimu kwako. Leo nakupa sms ambazo unaweza zituma kwa mpenzi wako kwaajili ya kumtakia usiku mwema na akajisikia vizuri. Chagua ujumbe unaoendana na hali ya mahusiano yako Kwa sasa hapa chini na umtumie. Lakini kumbuka kuwa sio pazima umtumie ujume kama ulivyo andikwa hapa. Unaweza ubadilisha badilisha.

Ukiona dalili hizi Jua Account yako ya Facebook  imedukuliwa na si salama GUSA HAPA>>>>

SMS za mapenzi za kumtakia usiku mwema mpenzi wako

# 1: Natamani usiku wa kwanza ambao tutakua pamoja. Natumai unafikiria juu yetu kama mimi. Daima kumbuka kuwa nakupenda mpaka mwisho wa wakati. Ulale vizuri mpenzi.

# 2: Mpenzi wangu mtamu, nadhani siku yako imekuwa nzuri kama wewe. Lala na upumzike vizuri, ili uweze kuamka mchanga na mwenye nguvu kwa siku ya kesho. Usiku mwema.

# 3: Maneno hayawezi kuelezea jinsi ninavyokupenda na kukuthamini. Tumekuwa na moja ya siku bora za maisha yetu na ni maombi yangu tutakuwa na siku kama hizo kwa maisha yetu yote. Usiku mwema, mwanamke mzuri

# 4:Natumai leo imekuwa nzuri kwako. Nimekuwa nikifikia niwezaje pata furaha usiku huu. Nikakumbuka kuwa kumtakia usiku mwema mpenzi aliekatika moyo wangu hunipa kutanipa furaha. Usiku mwema.

Maneno ambayo hutakiwi kuyasema kwa mwenza wako GUSA HAPA>>>

# 5: Usiku mwema, mpenzi wangu. Natumai umelala vizuri na una ndoto bora. Nakupenda sana. Siwezi kusubiri kukuona asubuhi.

# 6: Hello, sweetie. Nilitaka kukujulisha kuwa nimekuwa nikifikiria juu yako siku nzima. Kuwa na usiku mzuri na ndoto za kupendeza. Nakupenda.

# 7: Ni ngumu sana kuwa mbali na wewe. Nimekukumbuka sana. Napatashida kusubiri siku nikakayokuwa nawe nyumbani na kukuona tena. Usiku mwema.

# 8: Usiku Mwema, mpenzi. Lala vizuri na ndoto zako zote ziwe nzuri. Kumbuka jinsi ninavyokupenda. Natarajia kukuona kesho.

Mambo ya kushangaza usioyajua kuhusu Wanawake na Wanaume BONYEZA HAPA>>>

# 9: Pole na kazi… Usiku wa leo natamani ningekuwa nawe. Lala vizuri mpenzi wangu na uwe na ndoto tamu, Nakupenda.

SUKARI YA DADA (mwanzo-mwisho)

SIMULIZI YA SUKARI YA DADA

SUKARI YA DADA ni simulizi inayomuhusu Kijana ambae alienda Dar es salaam kwaajili ya kufanya kazi za ndani baada kutofanya vizuri kidato cha nne. Kwenda huko ilikua ni njia pekee alioiona itamsaidia maishani kwa wakati huo lakini katika kuelekea anapohitaji, anakutana na changamoto nyingi sana kutokana na ujana. Imesomwa na maelufu ya watu mpaka sasa.

Inavipande 17 vinavyo burudisha na kuelimisha unaposoma mwanzo hadi mwisho. Lakini  unapomaliza kuisoma simulizi hii mpaka mwisho, unaweza soma simulizi nyingine mbili ambazo ni UTAMU WA JUMLA na MZIGO WA WAKUBWA.

Kiufupi SUKARI YA DADA, UTAMU WA JUMLA na MZIGO WA WAKUBWA ni Simulizi tofauti ila zinauhusiano unaokupa picha moja nzuri sana ukiwa kama msomaji. Yani ukisoma zote 3 unapata picha ya simulizi moja kubwa sana yenye vipande 41.

Baadhi ya watu husema ni simulizi zilizoandikwa kiufundi na maajabu. Sijui wewe ukizisoma utazipa jina gani ila Ukihitaji kupata simulizi hizi, unaweza kuwasiliana nasi tukakutumia kwa njia ya WhatsApp. Gusa kitufe hapa chini kuwasiliana na sisi kwa njia ya WhatsApp. Au piga 0715233405 muda wowote kwa mahitaji ya simulizi au maelezo.

Unapata zote kwa Tsh 2500 TU!

Unaweza pata ukiwa Tanzania na hata nje ya Tanzania. Haziruhusiwi kusomwa na watu wenye umri chani ya miaka 18. Hii ni kwasababu  zimekusanya lugha na mafundisho kwaajili ya walio kwenye kigezo cha umri huo.

Simulizi Bora za kusoma katika The Bestgalaxy BONYEZA HAPA>>>

Unataka kuzijua simulizi hizi zaidi?

Miongoni mwa simulizi zinazopendwa kusomwa kwa sasa ni Sukari Ya Dada, Utamu Wa Jumla, na Mzigo Wa Wakubwa. Hadithi hizi tatu, zilizochapishwa kupitia The Bestgalaxy, zinafuatilia maisha ya vijana waliokumbwa na changamoto mbalimbali za maisha na mapenzi.

Kilicho cha kipekee kuhusu simulizi hizi ni kwamba zinahusiana. Wahusika wanaweza kuonekana zaidi ya mara moja katika hadithi tofauti. Kwa mfano, mhusika mmoja katika Sukari Ya Dada anaweza kutajwa au kuhusika pia katika Utamu Wa Jumla au Mzigo Wa Wakubwa. Hadithi moja inaendelea pale nyingine ilipoishia, au huonyesha upande mwingine wa maisha ya baadhi ya wahusika wale wale.

Kwa hiyo, hizi si hadithi tatu tofauti tu โ€“ ni sehemu za simulizi moja kubwa inayoonyesha maisha ya vijana wa sasa kwenye mazingira yenye changamoto nyingi.

1. Sukari Ya Dada: Ndoto za Mjini na Maisha Halisi

Simulizi ya Sukari Ya Dada inamfuata kijana aliyehamia Dar es Salaam baada ya kushindwa mitihani ya kidato cha nne. Akiwa hana elimu ya kutosha wala msaada wa kifamilia, anajikuta akifanya kazi za ndani. Hapo ndipo anapoanza kukumbana na vishawishi na maisha ya mapenzi ambayo hatimaye yanamfanya kutambua mambo mengi kuhusu dunia na watu. Hadithi hii inaangazia namna vijana wengi wa kike na kiume wanavyoingia mijini wakiwa na matumaini makubwa lakini wakikumbana na uhalisia wenye changamoto nyingi.

2. Utamu Wa Jumla: Mapenzi, maisha na  Mafanikio

Hadithi hii ni mwendelezo wa maisha ya baadhi ya wahusika kutoka Sukari Ya Dada. Inamfuatilia kijana kutoka Tabora anayejiunga na chuo jijini Dar es Salaam kusoma biashara. Urafiki wake na Jimmy, mwanafunzi mwenza, aliefungua mlango wa maisha ya starehe, wanawake, na biashara zisizo rasmi wakiwa chuo. Hii ni simulizi inayoangazia mambo mbalimbali ambayo kijana ambae ni msomi wa kisasa ameyapitia katika kujitambua kwakeupande wa mahusiano na maisha.

3. Mzigo Wa Wakubwa: Majukumu

Mzigo Wa Wakubwa inahusiana moja kwa moja na simulizi za awali, Sukari Ya Dada na Utamu Wa Jumla. Hadithi hii inamuhusu kijana mwinginetoka Tanga anaeinjia mjini na kufunzwa mengi kuhusu maisha na mahusiano. Inatoa pia sehemu za maisha ya wahusika kutoka simulizi hizo nyingine, inapitia mambo mbali mbali kuhusu maisha yao, hatua zao na changamoto wanazokutana nazo katika upande wa mahusiano na mapenzi.


Hitimisho:


Kwa mashabiki wa fasihi simulizi, Sukari Ya Dada, Utamu Wa Jumla, na Mzigo Wa Wakubwa ni kazi ambazo hazifai kupuuzwa. Zinabeba burudani na mwanga juu maisha ya kweli ya vijana wa leo. Ni hadithi za kujifunza, kufikiria, na kuburudika.


Fanya haya ili kuchelewa kupiga bao

Kuwahi kumaliza katika tendo huweza kusababishwa au kuchochewa nqa vitu vingi sana. Wengi huusisha swala hili na magonjwa lakini kiukweli watu wengi huwa wanawahi kumaliza mchezo kutokana na mazingira au mawazo aliojiwekea mwenywe katika vichwa vyao. Kuna baadhi ya vitu ambavyo vinaweza kumsaidia mwanaume asiwahi kumaliza mchezo katika tendo.

Fanya mazoezi ya mwili

Kama tunavyo fahamu kuwa mwili wenye afya nzuri daima hufanya kazi vizuri, kwahiyo kitu rahisi cha kufanya ni kujenga tabia ya kufanya mazoezi ambayo husaidia kujenga afya njema na kukufanya uwe na mzunguko mzuri wa damu. Kama una mwili wenye afya basi inaweza kukusaidia kwa namna ya kifikra ambazo huchangia kuepukana na swala la kumaliza mchezo kwa haraka.

Pumua vizuri

Kiungo chochote cha mwili huhitaji nguvu kamili ili kufanya kazi vizuri. Unapo pumua vizuri na kwa ukamilifu, viungo hupata nguvu za ziada. Baada ya kuinza tu (wakati wa tendo), jaribu kupumua kwa ufasaha ili mwili uweze kupata hisia kabla ya kuanza kulisakata rumba.
Mshirikishe mwenzako

Kuridhika kimapenzi ni tukio ambalo wote wawili mnaridhika. Ili kujifunza kujizuia kumaliza mchezo kwa haraka, ni vizuri kuwasiliana na mwenzi wako wa kimapenzi. Anaweza akakusaidia kushinda tatizo hili, kila unapohisi unataka kumaliza mapema, sema ‘subiri’ na usitishe kwanza shughuli zote kwa muda kidogo ili kwenda sawa nae.

Usiliwaze sana tendo

Pia kabla ya kwenda kuanza tendo kwa mfano upo ofisini na unajua jioni unakwenda kucheza mchezo basi jitahidi usiwaze hayo mambo chukulia kama ni kitu cha kawaida. Hii ni kwasababu kuongeza concentration ya kuwaza inaongeza stimulation kiasi kwamba ukimgusa mpenzi wako tayari umekwishaachia hata kabla ya kuanza mchezo.

Chagua style

Pia angalia angalia style zenye kuchochea kumaliza kwa haraka kwa mfano mbuzi kagoma…. etc hii ni ngumu kujizuia kumaliza hasa kwa bao la kwanza maana panakuwepo na constriction ya hali ya juu very tighten kiasi kwamba ukigusa tu tayari ..so ni vizuri style kama hizi zikafuata baada ya bao la kwanza ili uweze ku-enjoy vizuri zaidi.