Category Archives: Games

App ya Gamehub imerahisisha kucheza game za Xbox katika simu

Wachezaji wa games kwenye simu wanazidi kupewa njia rahisi na za kisasa za kufurahia games wanazozipenda kwenye simu. App ya Gamehub ni moja ya suluhisho jipya ambalo limeleta mabadiliko makubwa kwa wapenzi wa games. Kupitia app hii, sasa inawezekana kucheza game za Xbox moja kwa moja kwenye simu yako ya mkononi bila haja ya kuwa na console ya Xbox.

Kama bado haujajua ni kwamba unaweza cheza game za Xbox kwenye simu  lakini hii itakuhitaji utumie huduma ya xcloud. Xcloud ni huduma inayokuwezesha mtu kucheza game za Xbox na nyingine nyingi katika mtandao (Online). Kupitia huduma hii, unaweza cheza game nyingi kubwa kwenye simu yako bila kuwa na simu yenye uwezo sana maana. Kikubwa utakachotakiwa kuwa nacho ni internet yenye kasi tu na tulisha zungumzia juaa ya hilo kwenye makala nyingine hivyo hatauta zungumzia sana hapa.

Game la Fortnite katika Xcloud

Hapa tunakujuza tu kuwa kuna app inaitwa Gamehub imerahisisha zaidi mchakato wa kucheza game za Xbox kupitia hiyo hiyo xcloud.

Kitu kizuri ilicho rahisisha ni kuondoa uhitaji kwa kutumia VPN ikiwa upo nje ya nchi zenye huduma (kama vile US). Yani kupitia app ya Gamehub utaweza kucheza game za Xbox kupitia xcloud popote bila kutumia VPN. Utafanikisha jambo kilo kupitia kipengele cha kuchagua unataka kucheza kama upo sehemu (location). Unaweza fanya yafuatayo kujaribu hiya.

Jinsi ya kucheza game za Xbox kwenye simu kwa app ya Gamehub

Unachohitaji ni kuwa na akaunti ya Xbox, simu yenye uwezo wa kuunganisha intaneti, na app ya Gamehub yenyewe.

  • Fungua app na ujisajiri
  • Baada ya kujisajili, nenda kwenye upande Xbox kwa kubonyeza alama ya Xbox
  • Ukiwa hapo, palasa sehemu ya pembeni katika upande wa kulia, kwenda kushoto kuelekea kulia.
  • Ukifanya hivyo utaletewa sehemu ambayo utachagua location (mahali). Wewe unaweza chagua USA au UK.
  • Baada ya hayo, Chagua game unalotaka kucheza alafu ujisajiri kwa akaunti yako ya Microsoft kama kawaida kwaajili ya kuanza kucheza.

Nakukumbusha tu kuwa kama haujalipia Xbox game pass ultimate, hautaweza kucheza game zaidi ya Fortnite.

Hii ni habari njema kwa watu ambao hawana nafasi au uwezo wa kununua vifaa vya Xbox lakini bado wanatamani kufurahia michezo hiyo.

Umecheza game la Delta Force Mobile kwenye simu yako?

Game la Delta Force Mobile ni game la first- person shooter lililotengenezwa na NOVA logic kwaajili ya simu za mkononi. Limekua likiangaliwa na watu wengi sana wanaotumia simu za mkononi kucheza game za online zinazohusisha kucheza pamoja na wengine. Hapa nazunguzia watu wanaocheza game la Warzone mobile, Blood strike na hata Arena breakout mobile au game nyingine kama hizo.

Kwenye kulicheza game la Delta force mobile, mtu unahitajika kutumia internet maana ni game la online. Lina Mode zaidi ya moja unawezoweza kucheza ukiwa na watu wengine kutoka pande mbalimbali Duniani. Mode zake zote ni nzuri ila inategemeana na umeipenda mode gani. Unaweza cheza mode ya Operations, Warfare au Black Hawk Down Kisha unachagua mode ambayo ni nzuri zaidi kwako. Watu wengi hupenda Warfare maana ni mode ya haraka inayofurahisha.

Katika muonekano, game la Delta Force Mobile Lina graphics nzuri sana zinazofanya uone picha nzuri zinazofanana na uhalisia unapolicheza. Na uzuri ni kwamba unaweza kupunguza ubora wa picha au kuongeza.

Chaguo la kuweka picha yenye ubora wa kawaida au ubora wa hali ya juu ni wako. Kama simu yako inaweza kuhimili game katika picha zenye ubora wa juu, basi unaweza kuongeza ili iwe na picha kali zaidi.


Hasara ya kucheza game zikiwa kwenye picha za ubora wa hali ya juu ni kupata moto kwa simu au kukumbana na lags. Kwaiyo ukitaka kuongeza ubora hakikisha simu yako inaowezo wa kuhimili pia.


Kulicheza game la Delta Force Mobile




Ili simu yako iweze kulicheza game la Delta Force Mobile inatakiwa iwe na vigezo vifuatavyo:
Kwa Android simu itatakiwa kuwa na angalau, Snapdragon 865, 8GB za RAM na Android 10 au zaidi. Kwa simu za iOS iphone itatakiwa kuwa na angalau A13 chip, 4GB za RAM na iOS 14+ (Ambayo ni iPhone 11)


Unapoliingiza game kwenye simu, unatakiwa pia kuwa na nafasi ya 12GB katika Storage. Hii iwe ni unatumia Android au iOS.

Kwasasa game la Delta Force Mobile limetoka rasimi na unaweza cheza kwa kutumia simu yako ya Android au iOS (iPhone). Limeachiliwa rasimi 22 Apr 2025 kwa watu wote ulimwenguni.

Kama unataka kujaribu kwasasa, pakua hapa chini.

Download Delta Force Mobile Android>>>

Download Delta Force Mobile iOS (iPhone)>>>

Jinsi ya kuondoa Lag unapocheza game la Warzone Mobile

Warzone Mobile ni game lililolalamikiwa sana na wachezaji wake wingi toka siku ya kwanza linatolewa rasimi. Wachezaji wake wamekua wakikumbana na changamoto nyingi sana na kupitia mitandao wamekua wakieleza matatizo yanayowakatua. Watengenezaji(Developers) wa game wamekua wakijaribu kutatua baadhi ya matatizo lakini kuna baadhi ya matatizo yanaweza kutatuliwa na wachezaji wenyewe tu. Moja ya matatizo yanayoweza tatutuliwa na mchezaji wa game mwenyewe ni hili la “Lag”.

Lag katika upande wa game, tunaweza sema ni uchelewaji au kusitasita kwa game wakati wa unacheza. Mara nyingi tatizo hili huonekana sana likiwa kwenye game za Online (zinazotumika internet) lakini hata game za Offline hukubwa na tatizo hili.
Haijalishi Lag zipo kwenye game la Offline au Online, huwa zinakera na kumuondoa mchezaji katika hali ya kufurahia kucheza game.

Katika Warzone Mobile unaweza kumbana na Lag mara nyingi sana usipozingatia baadhi ya mambo. Ikiwa unapata Lag unapolicheza unatakiwa kuzingatia mambo ya fuatayo ili kufurahia game lako bila tatizo hilo.

Magemu yenye muonekano mzuri ya battle Royale BONYEZA HAPA>>>

Zingatia haya kuondoa Lag unapocheza game la Warzone Mobile

Tumia kifaa au simu yenye uwezo mkubwa


Kuna vigezo rasmi vinavyoeleza ni kifaa au simu gani inauwezo wa kutumika kucheza game la Warzone Mobile. Lakini hii haina maana kila simu au kifaa kilicho kidhi vigezo kitaweza kucheza game hilo vizuri. Baadhi ya vifaa vinaweza tumika kucheza lakini katika kucheza, unakutana na tatizo la Lag. Hii inawezatokea kwasababu simu au kifaa hicho hakina uwezo ila sio wa kutosha kucheza bila matatizo. Kwaiyo unatakiwa kupata kifaa kizuri kwaajili Warzone Mobile hatakufanya utafiti kabla haujanunua.

Jiunge na internet nzuri yenye kasi


Warzone Mobile ni game la online. Hivyo unapolicheza, jambo la misngi kulizingatia ni mtandao/internet. Ukiwa unacheza game hili katika mtandao usio na kasi au ambao haujatulia, itakua ni ngumu kuondokana na Lag. Kwaiyo hakikisha unatumia internet ilio vizuri ili kufurahia game bila Lag.

Punguza ubora wa picha ikiwezekana

Wakati mwingine Lag hutokana na ubora wa hali ya juu wa picha unaosababisha kifaa chako kushindwa kuchakata vizuri. Unashauriwa unapokua unakumbana na Lag, upunguze ubora wa picha wa game lako katika kipengele cha “Graphics” kwenye “Settings”. Kufanya a hivyo kunaweza ondoa Lag katika uchezaji wako wa game.

Usicheza kifaa au simu ikiwa ya moto

Simu au kifaa unachotumia kucheza game, kinaweza kuwa kina pata moto unapocheza. Hali hii ya kifaa hicho kupata moto, inaweza pelekea game kuwa na Lag unapocheza.

Kwaiyo unapogundua simu yako ni yamoto na game lako lina Lag, basi huo ni muda wa kuliacha game hilo ili kifaa chako kupunguze joto.

Mwisho; Kuzima Voice chat ni kitu kidogo ambacho kinaweza kukupunguzia Lag lakini kwa kiasi kidogo sana. Pamoja na mambo yote hayo, Game la Warzone Mobile huwa linakua na matatizo yanayojitokeza mara kwenye updates zake. Hivyo kuna muda Lag zinaweza kutokea na tatizo likawa nje ya uwezo wako.

Kati ya game za Online na game za Offline zipi ni Bora kwako?

Games za kucheza kwenye simu ni moja ya mambo muhimu sana kwa watu wengi. Watu hupenda sana kucheza game mbalimbali kupitia simu zao na jambo hili huwaburudisha. Katika games ambazo watu hupenda kucheza kwenye simu, kuna makundi mawili ambayo tunaweza gawanya kwasasa.

Kundi la kwanza ni games zinazohitaji muunganiko wa internet ili kuchezwa. Hizi huitwa “Online games” kwasababu humuitaji mtumiaji kuwa mtandaoni ili kucheza. Mfano mzuri wa game hizi ni game liitwalo “Call of Duty Warzone Mobile”. Hauwezi fanya chochote katika game la Call of Duty Warzone Mobile bila kuwa na muunganiko wa internet.

Mbali na kundi hilo, kuna games nyingine huwekwa katika kundi liitwalo “Offline games” ambalo linamaanisha games zisizohitaji internet. Unaweza zicheza games hizi bila kutumia mtandao wa internet. Subway Suffer ni mfano mzuri wa games hizi.

Makundi yote mawilli ni mazuri lakini uzuri hutegemena na mtu unaeyacheza unataka nini, kwa wakati gani na katika mazingira gani. Hapa chini tumejaribu kuelezea mambo machache kuhusu makundi haya na kukupa maelezo yatakayo kufanya uelewe kati ya game za Online na Offline, zipi ni chaguo bora kwako.

Magame ya mpira ya kucheza kwenye simu BONYEZA HAPA>>>

Kati ya game za Online na za Offline zipi ni Bora kwako?

Ubora wa muonekano (Nazungumzia Graphics)

Sio game zote za online ni zina ubora wa hali ya juu kwenye muonekano lakini nyingi walizozingatia graphics katika utengenezaji, huwa zinakua na muonekano mzuri sana. Ili game liwe na muonekano wa hali ya juu, watengenezaji mara nyingi hufanya kazi kubwa.


Kwa kipindi hiki watengenezaji wa games huwa wanaona game za online zinaeweka urahisi kwa wao kuweka njia mbalimbali za kujiiingizia kipato kwa kazi wanayofanya. Kwaiyo wakiweka nguvu yao kwenye kuboresha maonekano wa game za online, huwa wanatengeneza vizuri sana wakiamini kazi yao itawalipa.

Kutokana na Hilo, mara nyingi ukitaka game zenye muonekano wa hali ya juu sana, upande wa Online games unaweza kukupatia unachotaka.

Game zenye muonekano mzuri za Online battle Royale BONYEZA HAPA>>>

Kucheza na marafiki

Kama unapenda game za kucheza na marafiki ambazo hujulikana kama (Multiplayer games) basi tambua Kuna game za online na game za offline zipo hivyo. Lakini game za online za mtindo huu kwa sasa ndio hupendwa zaidi maana huruhusu watu kucheza pamoja hata wakiwa mbali.


Ikiwa marafiki unaocheza nao game wapo karibu na wewe basi game za offline za mtindo huu zitakufaa lakini kama wapo mbali, game za online za mtindo huu ndio chaguo sahihi kwako.

Update za lazima

Watengenezaji wa games mara nyingi huboresha game zao na kuwataka wenye game hizo ku-Update. Game za online ndio mara nyingi hufanyiwa marekebisho ya mara kwa mara na kuwataka Watumiaji ku-Update. Na mchezaji usipo fanya hivyo kwa wakati, unaweza zuiwa kulicheza game mpaka utakapo update.


Hali hiyo haipo sana kwenye game za offline. Game nyingi za offline huwa hazilazimishi mtu ku-Update.
ku-Update game ni jambo zuri lakini linaweza kuwa usumbufu kwa baadhi ya watu kama litafanywa kuwa la lazima. Ikiwa utaona hili jambo ni usumbufu, basi game za offline ni chaguo zuri kwako.

Kucheza popote

Game za online ni game zinazohitaji internet kuzicheza, na game za offline huwa haziitaji internet. Ikiwa hautakua kwenye mazingira yenye internet au ukakosa internet, hauwezi cheza game za online. Lakini game za offline huwa zinachezwa mahali popote. Ni wewe tu na simu yako yenye chaji ya kutosha ndio vinahitajika.


Kwaiyo game za offline ni chaguo zuri sana na Bora kama unahitaji kucheza game ukiwa popote pale ulimwenguni.

Kwa kuangalia mambo tulioyagusia hapo juu, unaweza pata picha ya nini unahitaji kati ya game za online na game za offline. Endelea kuwa karibu na The bestgalaxy kwa mambo mengine kuhusu games na zaidi.

Warzone Mobile: Tatizo la kukwama katika “CONNECTING TO ONLINE SERVICES”

Call of Duty Warzone Mobile ni game maarufu la vita unaloweza cheza kwenye simu. Ni moja ya game za “shooting” zinazo ruhusu mchezaji kupambana au kushirikiana na watu wengine katika vita. Wachezaji wengi kutoka pande mbalimbali hapa ulimwenguni wanaweza kuungana kama Team ili kupambana pamoja katika vita ndani ya game hili.

Kitu kingine kizuri kuhusu game la Call of Duty Warzone Mobile ni kwamba linachezwa bure. Lakini kuna vipengele vya ziada ambavyo unaweza kununua kwa kuhushisha pesa halisi. Unaweza kununua mavazi maalum, vifaa vya kipekee na mambo mengine yanayokusaidia kuwa na nguvu zaidi katika mapambano.


Kiufupi, Warzone Mobile ni game zuri ingawa kunabaadhi ya Wachezaji wake hukumbana na changamoto au matatizo mbalimbali toka lilipotolewa. Moja ya matatizo ni kukwama katika “CONNECTING TO ONLINE SERVICES” unapolifungua game na kutaka kulicheza. Hapa chini, Kuna njia ambazo ukitumia, unaweza fanikiwa kujitoa katika kukwama huko.

Jinsi ya kucheza game za Xbox katika Simu BONYEZA HAPA>>>

Njia za kuondoka katika “CONNECTING TO ONLINE SERVICES” kwenye Warzone Mobile

Kuwa katika Internet yenye kasi

Kuna muda game la Warzone Mobile linaweza kwama unapolifungua Kwasababu haupo kwenye mtandao wa internet mzuri. Hili ni game la Online na huitaji internet yenye kasi ili uweze cheza bila matatizo. Internet yenye kasi ni jambo la msingi katika kufurahia kucheza Call of Duty Warzone Mobile maana game hu-stream Online baadhi ya vitu kuhusu game.


Kwaiyo kama utakumbana na tatizo la “CONNECTING TO ONLINE SERVICES” kwasababu hii, jaribu kuwa katika mtandao wa internet wowote wenye kasi zaidi ya unaotumia.

Tumia Data badala ya Wifi

Ikiwa umepata tatizo la kukwama katika Warzone Mobile alafu unatumia internet kutoka kwenye Wifi, fanya kutumia Data. Hamisha simu yako kutoka kwenye Wifi uliojiunganisha kisha washa Data la simu yako.

Kwa kufanya hivyo, unaweza kuona game haligandi katika sehemu ya “CONNECTING TO ONLINE SERVICES”. Baadhi ya watu hutumia njia hii kucheza game pale linapokwama. Lakini sio kila mtu akifanya hivi, tatizo huondoka. Kwa watu wengine, njia hii hugoma na huwa wanatumia njia iliopo hapa chini.

Vuka tatizo kwa VPN

Unapokuwa na tatizo la kukwama katika Warzone Mobile, unaweza kutumia VPN kuvuka sehemu uliokwama. Yani washa VPN kisha fungua game. Baada ya kufungua game, halita kwama tena ila ukivuka sehemu ambayo huwa inakwama, utatakiwa kuzima VPN ndipo uendelee kulicheza. Usipo Zima VPN unaweza ukashindwa kuingia katika mode yoyote kucheza.

Unaweza tumia VPN yoyote kufanya hivi na asilimia kubwa ya watu hutumia njia hii wanapokwama.

Mwisho; Warzone Mobile ni game nzuri sana na huchukua nafasi kubwa katika simu pia. Swala hili linaweza kuleta ugumu wa kufanya maamuzi ya kulifuta katika simu na kuliingiza tena. Lakini kama mbinu zote zitashindikana, unaweza fanya maamuzi ya kufuta na kuliiingiza upya katika simu yako ili kutatua tatizo. Njia hii sio nzuri sana lakini inaweza kuweka mambo sawa pia.

Magame mazuri ya truck ya kucheza kwenye simu (Android)

Je, wewe ni mpenzi wa magari makubwa na unapenda kutumia simu yako ya Android kwa burudani ya games? Basi, hapa uko mahali sahihi. Katika dunia ya sasa, teknolojia imetupatia fursa ya kufurahia magame mengi ya truck moja kwa moja kwenye simu za smartphone. Muda huu, hapa The bestgalaxy wakati mzuri wa kuangalia game nzuri za truck zinazopatikana kwenye simu za Android.

Katika makala hii, tutaangalia game za truck ambazo yanakupa nafasi ya kuendesha magari haya makubwa katika mazingira tofauti na changamoto za kuvutia. Kuna game nyingi sana za mtindo huu lakini sio kila game la Truck ni zuri. Sisi hapa tutaangalia Magame machache mazuri tu. Ikiwa unatahitaji game zuri kutumia muda wako wa ziada kulicheza, unaweza changua kati ya yaliopo kwenye orodha yetu hapa bila kupoteza muda wako sana kutafuta.


Kabla ya kufika kwenye orodha yetu, ni muhimu kuelewa kwanini magame ya truck yamekuwa maarufu sana. Na pia haya magame sio tu yanakupa furaha, bali pia yanakusaidia kuboresha ustadi wako wa kuendesha na kushinda changamoto mbalimbali. Kwa hivyo, kaa mkao wa kula, tupo tayari kukuletea orodha ya magame bora zaidi ya truck kwa simu yako ya Android

Magame mazuri ya truck ya kucheza kwenye simu

Truck Simulator : Ultimate

Truck Simulator: Ultimate” ni game la simu ambalo linakupa fursa ya kusimamia biashara yako ya malori au truck. Katika game hili, wachezaji wanaweza kuendesha trucks tofauti ili kukamilisha misheni na katika mazingira tofauti tofauti. Muonekano wa mazingira na game kiujumla ni mzuri sana. Linaweza chezwa Online na offline pia.

Mbali na hayo, game la “Truck Simulator: Ultimate” lina kipengele cha multiplayer ambacho kinawaruhusu wachezaji kuungana na kushindana kutoka sehemu mbalimbali duniani. Jambo hii linafanya game kuwa na changamoto zaidi na kuongeza ushindani.

Truckers of Europe 3

Truckers of Europe 3” ni Offline game lililotengenezwa na Wanda Software, ambalo linakupa nafasi ya kuwa dereva wa lori katika bara la Ulaya(Europe). Mazingira yake ni mazuri na game pia limeundwa na picha nzuri sana ukilinganisha na baadhi ya magemu mengine.


Wachezaji wanaweza kuwa kwenye malori mbalimbali wakifanya kazi za usafirishaji na kupata pesa ambazo zinaweza kutumika kuboresha malori kwa ajili ya usafirishaji bora.
Wachezaji wanakutana na changamoto za kuendesha trucks barabarani kama vile hali mbaya ya hewa na barabara zenye vikwazo. Kiufupi, kama ni mpenzi wa game za malori au truck, hili game ni chaguo zuri pia.

Truck Simulator World

Truck Simulator: World” ni game la Truck la simu unalokuwezesha kuingia katika maisha ya udereva wa lori kwa kiwango cha kimataifa. Wachezaji wa game hili wanachukua kazi za usafirishaji, wanapata kupata mapesa au mapato na kutumia mapato hayo kuboresha malori yao.

Muonekano wa game upo vizuri pamoja na kuwa Offline game (haliitaji Data kucheza). Lakini unaweza cheza Online pia ili kufurahia kucheza game na marafiki au watu toka sehemu mbalimbali ulimwenguni.

European Truck Simulator

European Truck Simulator” ni game limetengenezwa na Ovidiu Pop na linakupa fursa ya kuendesha malori katika nchi mbalimbali za Europe. Wachezaji wanapata pesa kwa kukamilisha misheni za usafirishaji alafu wanazitumia pesa hizo kuboresha Trucks zao kama ilivyo kwenye game nyingine nyingi za Truck Simulator.


Ni moja ya magemu pendwa na tuck ambayo Mamilioni ya watu wanaotumia simu wanayapenda. Moja ya sababu game hili kuwa moja na magame pendwa ni uwezo wa kuchezwa bila Data. Sio lazima uwe na muunganiko wa internet ili kucheza game hili, unaweza cheza Offline na Online ukihitaji.

Mbali na games hizo, za truck, Kuna game nyingi sana unaweza jaribu na ukazipenda. Tumeziweka game hizi hapa ili kukurahisishia utafutaji wako tu. Endelea kuwa karibu na The bestgalaxy kwa mambo mengine kuhusu games.

Jinsi ya kutengeneza pesa kwa kucheza games mtandaoni

Kucheza games sio tu burudani ya kupoteza muda, bali pia inaweza kuwa chanzo cha mapato kwa wachezaji wanaojua mbinu sahihi. Katika makala hii, tutaangazia njia mbalimbali ambazo unaweza kutumia kutengeneza pesa kwa kucheza magame mtandaoni.

Sekta ya magame ya imekua kwa kasi, ikileta mapinduzi katika jinsi tunavyotumia teknolojia kwa burudani na hata ajira. Hii imeleta mabadiliko makubwa, hasa kwa vijana ambao wanapenda magame na teknolojia. Kutokana na maendeleo ya Teknolojia, wachezaji wengi wameweza kubadilisha ujuzi wao wa magame kuwa vyanzo vya mapato vya kudumu, wakitumia njia tofauti mtandaoni.

Kutengeneza pesa kwa kucheza ukiwa kama mcheza games mtandaoni, inawezekana. Unaweza tengeneza mamilioni ya pesa ukiwa kama mcheza games kwenye mtandao. Lakini kama ilivyo katika pande nyingine yoyote, kufanikiwa kutengeneza pesa kwa kucheza games mtandaoni sio rahisi. Kiufupi sio kila mtu anayeweza kufanikiwa bila kuweka juhudi na kujua njia bora za kufuata. Unaweza kuwa mtu mwenye ujuzi wa hali ya juu kuhusu Games na bado kutengeneza pesa mtandaoni kwa njia hii kukawa ni kitu kigumu kwako.

Kwa hiyo, ni muhimu kufahamu mbinu mbalimbali ambazo zitakusaidia kufanikisha lengo hili. Katika makala hii, tutakupa mwanga juu ya njia hizo ili uweze kuanza safari yako ya kutengeneza pesa kupitia magame mtandaoni.

Jinsi ya kucheza game za Xbox kwenye simu BONYEZA HAPA>>>

Jinsi ya kutengeneza pesa kwa kucheza games mtandaoni

Kuwa LIVE streamer wa games

Kwenye platform za video kama vile TikTok, YouTube na Twitch kunakupa uwezo mtu kuwa live mtandaoni ukicheza games. Katika kucheza games unaweza ingiza pesa kama utatimiza au kufuata utaratibu wa kuanza kulipwa pesa kwenye platform.


Kila platform huwa na utaratibu wake katika kuanza kutengeza pesa ukiwa LIVE lakini kitu kikubwa kinachozingatiwa ni watu wanaofuatilia na kuangalia LIVE zako. Kama utakua na uwezo wa kupata watu wengi wanaopenda kufuatilia unapokuwa LIVE, basi unakua na nafasi kubwa ya kuingia pesa pia.


Kuwa LIVE streamer wa games anaeingiza pesa inaweza kukuchukua muda mrefu na mara nyingi unashauriwa kuwa mtu unaependa unachokifanya kwanza kabla ya kufikilia pesa. Ila ukifanikiwa kutoboa kwa kutengeneza jina na kushughalikia pande zote za pesa, unaweza ingiza zaidi ya $4000 kwa mwezi ambayo ni mamilioni ya pesa.

Kuonesha ujuzi kupitia video za YouTube

Kama katika games unaujuzi ambao unaweza kuwa msaada kwa watu wengine, unaweza ingiza pesa kwa kugawa ujuzi huo kupitia YouTube. YouTube hulipa watu wanaotengeneza video na kuweka YouTube. Ili kuanza kulipwa, unahitajika kutimiza vigezo vyao ambayo huusisha watu kukufuata na kuangalia video zako.


Ukianza kutengeneza video zinazowapa ujuzi watu wengine na kuziweka YouTube, unaweza pata watu wanaoungana na wewe alafu ukaanza kulipwa. Kwa mfano; kuna watu hutengeneza video zinazoelekeza kutatua matatizo ya games mbalimbali na watu humpenda.

Kuuza bidhaa kuhusu games mtandaoni

Mtu unaependa kucheza games inaweza kuwa rahisi kwako kutambua vitu ambayo wachezaji games wanaweza penda na kununua. Uwezo huu unaweza kuutumia kuanza kuuza bidhaa ambazo wacheza games wenzako watanunua. Unaweza kufanya hivyo mtandaoni na ukajiingizia pesa za kutosha. Sio jambo rahisi kulifanikisha ila kunawatu hufanya na kuingiza pesa kwa njia hii imekua sehemu ya maisha yao. Mfano wa bidhaa mtu anaweza kuuza ni Game pads, Games, gaming T-shirts na hata gaming consoles.

Kuwa mtengeneza games (Game developer)

Unaweza kuengeza pesa kwa kuwa mtengeneza video games ambae unaweza muita “Game developer”. Uwezo wako wa kuyajua magame kiundani, unaweza kukusaidia kuwa mtu unaetengeneza game nzuri zinazopendwa na watu. Ukifanikiwa kutengeneza game zuri, ukalitoa alafu watu wakapenda, utaingiza pesa nyingi kwa namna mbalimbali.


Mbali na kutengeneza pesa kupitia kutengeneza game lako mwenyewe, unaweza pia kuajiliwa kwenye kampuni za games lakini ajira kwenye upande huu ni chache sana.
Hili sio chaguo rahisi ila ni chaguo linaloweza kufanya mtu utengeneze pesa kama mcheza games.


Kutokana na ukuaji wa Teknolojia, mtu anaweza tengeneza game na kuanza kuingiza pesa bila kuwa na ujuzi sana kuhusu kutengeneza games. Lakini njia ilionyooka ya kufanya hivi itakuitaji usome na kupata uzoefu wa mambo mengi kuhusu utengenezaji wa games. Inaweza kukuchukua miaka kuwa vizuri katika upande huu.

Unapotaka kutumia njia hizi kutengeneza pesa na kupata matokeo mazuri, ni vema ukafanya kwa kiwango cha kimataifa. Yani lenga maeneno au nchi ambazo zimeweka mbele uchezaji wa games kwa kiasi kikubwa.

Ni hayo tu katika upande huu wa kutengeneza pesa ukiwa mchezaji wa games. Isiwe mwisho kuwa karibu na The bestgalaxy, kuna mambo mengi kwaajili yako. Endelea kuwa karibu na sisi kwa mengine zaidi.

Game za simu ndogo za batani (Java games)

Pamoja na uwepo wa Smartphone zinazoweza kumuwezesha mtu kucheza games nyingi nzuri lakini watu bado hutumia simu ndogo za batani kucheza games. Kufanya hivi sio jambo baya maana kuna game nzuri sana unaweza furahia kwenye simu ndogo za batani kuliko simu nyingine. Kwa mtu ambae umeanza kucheza game kipindi cha Smartphone unaweza usione ulimwengu wa game za simu ndogo za batani vizuri lakini ni ulimwengu mpana sana.

Hapa The bestgalaxy Leo tunaenda kuangalia upande wa game za simu ndogo za batani za java. Kuna simu za batani ambazo zinakuwezesha kucheza game zinazofahamika kama “Java games” au “Magame ya java” kwa waswahili. Simu hizi zinakua na program ya java ambayo huwakilishwa kwa alama ya kikombe kinachotoa moshi.


Ukitaka kujua kama kwenye simu yako ya batani kuna “Java”, ingia kwenye orodha ya program au app zinazotokea ukibonyeza kwenye “Menu”. Baada ya hapo, angalia kama kuna app au program iliowakilishwa na kikombe alafu imeandikwa “java”.

Jinsi ya kupata simu Janja/Smartphone bila kutumia Pesa nyingi BONYEZA HAPA>>>


Simu yako ikiwa na java utakua na uwezo wa kucheza game nyingi sana. Kuna game nyingi unaweza download na kuziingiza kwenye simu yako uzifurahie bure kabisa. Kama una simu ndogo za muundo huu huu, zifuatazo ni kati ya game nzuri sana za java unazoweza furahia.

Magame za simu ndogo za batani

Midnight pool 3

Midnight Pool 3 ni game la mchezo wa pool uliotengenezwa kwa simu ndogo za Java. Game hili ni toleo la tatu katika mfululizo wa game za Midnight Pool. Ni game zuri sana lililotengenezwa na kampuni ya Gameloft, inayojulikana kwa game nyingi bora katika ulimwengu wa game za simu za Java na hata platform nyingine. Katika “Midnight Pool 3,” wachezaji wana nafasi ya kucheza pool katika mazingira mbalimbali ya kuvutia, kama vile mabaa na vilabu vya usiku. Unaweza cheza hata na rafiki kwa kupokezana simu mukiwa wawili.

Download

Real Football 2012

Ni game maarufu la mpira wa miguu kwa simu ndogo za Java na lilitengenezwa na Gameloft pia. Game hii lilikuwa na sifa kadhaa ambazo zilifanya kuwa kivutio kwa wapenzi wa soka na wachezaji wa game za simu ndogo kipindi cha nyuma. Game hii limejumuisha ligi mbalimbali na timu nyingi maarufu kutoka kote ulimwenguni katika miaka ya 2012. Wachezaji wanaweza wekwa tatika timu tofauti kwa kufuata taratibu za mchezo.

Download

God of War

Hili ni game maalufu mno na katika Ulimwengu wa game za simu ndogo za java unauwezo wa kulifurahia pia. Ni game linalohotaji kutumia akili sana na limeundwa kwa kuzingatia miundo ya game za God of War nyingine. Yaani japo ni game la simu ndogo ya batani lakini kunajinsi limeundwa kukufanya uhisi ulimwengu wa game nyingine za kisasa za God of War.

Download

Gangstar 2

Gangstar 2 ni game muundo wa game za GTA japo sio moja ya game za GTA lakini muundo umefanana. Watu wengi waliokua wakitamani kucheza game la GTA kwenye simu walikua wanacheza game hili kama badala. Sio kwamba game la GTA la java halikuepo ila ni kwasababu lilikua ni game Bora kuliko GTA katika Ulimwengu wa game za java za simu ndogo. Unaweza kuendesha gari, kutumia siraha na kufuata mission katika miji mbalimbali kama game za GTA.

Download

Counter Terrorism 3D

Counter Terrorism 3D ni moja ya game za Java zilizotengenezwa kwa ajili ya simu ndogo. Hii ni game ya aina ya FPS (First Person Shooter) ambalo mchezaji anachukua jukumu la kuwa mwanajeshi anayepambana na magaidi katika mazingira ya kivita. Muonekano wa Game hili ni wakuvutia ukilinganisha baadhi ya game za java za simu ndogo. Ni muonekano wa 3D na unatosha kabisa kuwa muonekano Bora kwa simu ndogo za java.

Download

Magemu ya java ya simu ndogo yanaweza kuchezwa mpaka sasa lakini ni magemu ya zamani ndogo yenye historia kubwa katika ulimwenguni. Kuna kipindi yalikua yanaonekana magame ya maana kuliko sasa.

Magame mazuri na rahisi kwa kila mtu unayoweza kucheza kwenye simu (Android)

Katika ulimwengu wa sasa wa teknolojia, simu za mkononi zimekuwa sehemu muhimu ya maisha yetu ya kila siku. Tunazitumia kwa mawasiliano, kuperuzi mitandao ya kijamii, na kwa burudani. Moja ya njia maarufu zaidi za kuburudika kwenye simu zetu ni kucheza magame mbalimbali. Magame kwa wengi ni njia ya kupumzika, kujifurahisha, na hata kujifunza mambo mapya maana kuna game zinazofunsha pia.

Ingawa kuna maelfu ya magame yanayopatikana kwenye internet, si magame yote yanakua yanaonekana mazuri kwa kila mtu. Kuna watu hawajajikita sana kwenye games na kama wakicheza game huwa wanapenda games zisizo na mambo mengi sana. Kwa bahati nzuri, kuna magame mazuri mengi rahisi ambayo yanaweza kuchezwa na watu wanamna hii, bila kujali umri au ujuzi wa teknolojia.

Magame ya mpira ya kucheza kwenye simu BONYEZA HAPA>>>

Katika makala hii, tutakuletea orodha ya magame mazuri na rahisi ambayo unaweza kucheza kwenye simu yako kama ni mtu wa namna hii. Kabla hatujaenda katika kuangalia games hizi, fahamu kuwa game zinaweza kusaidia kupunguza msongo wa mawazo na kuongeza furaha katika maisha yako ya kila siku.

Magame mazuri na rahisi kwa kila mtu unayoweza kucheza kwenye simu (Android)

Classic block falling

Hili game ni moja ya magame yenye muundo ambao baadhi watu husema ni “magame ya kupanga tofali”. Katika game hili unadondoshewa vitu kama tofali ambavyo huwa katika maumbo tofauti na utatakiwa kuyapanga vizuri. Unakua unapata score baada ya kufanikiwa kupanda vizuri tofari bila kuacha nafasi. Game kama hizi zipo nyingi na zinafahamika mno. Kucheza game la Classic block falling inaweza kuwa sio jambo gumu kulifanya kwa watu wengi.

Water color sort

Water color sort ni gemu lingine rahisi linaloweza kuchezwa na kila mtu. Kwenye game hili unapewa maji yenye rangi nyingi yaliowekwa kwenye chupa 2 au zaidi alafu utatakiwa kukusanya maji yenye rangi sawa na kuyaweka kwenye chupa zake. Water color sort linahitaji mchezaji atumie akili sana kabla ya kufanya maamuzi unapocheza. Kadri unavyoendelea kucheza na kushindwa ndivyo unaendelea kukutana na mafumbo yanayohitaji utumie akili zaidi. Ni game lisilo na mambo mengi kabisa na hufurahisha pia.

Bubble Shooter

Ukiwa umetulia na unahitaji game lisilo na mambo mengi kulicheza basi kumbuka kuna hili huitwa Bubble shooter. Hili game mchezaji unakua unatumia vimipira vyenye rangi kuvilenga vimipira vingine vinavyoning’inia juu. Ili kufanikiwa, unatakiwa kulenga vimipira vinavyo fanana rangi na ya mpira unaorengea. Yani kama umepewa mpira mwekundu wa kurengea basi utatakiwa kuulenga mpira wa rangi nyekundu pia.

Subway suffer

Subway suffer ni game maalufu sana ulimwenguni katika ulimwengu wa game ya simu za smartphone. Katika gemu hii, unacheza kama kijana anaekimbia ili kukwepa polisi anaemkimbiza baada ya kumkuta akichora maeneno ya treni. Unatakiwa kukimbia kwenye Barabara ya treni ili askari huyo asikukute. Katika kukimbia unakua unakutana na vitu mbalimbali unavyotakiwa kukwepa. Unakua unakimbia na kukwepa vitu kama ilivyo kwenye game kingine maalufu liitwalo Tempo run japo hayelekeani sana.

Racing in Car 2


Racing in Car 2 ni game la simu ambalo linakuweka kwenye ulimwengu wa kuendesha magari uwe kama Dereva. Game hili mchezaji anakua Dereva na anacheza kwa kuyumbisha simu ili kulielekeza gari upande wa kwenda pindi linapotembea barabarani. Katika barabara mchezaji anatakiwa kufanya vizuri kwa kupishana na magari mengine vizuri huku kuepuka ajali.

Huu ni mwisho wa orodha yetu lakini kuna game nyingine zaidi ya hizi tungeweza weka hapa. Lakini hatuwezi weka zote hivyo hizi zikikufaa, zijaribu na ufurahie.

Game zenye muonekano mzuri za Online battle Royale (simu)

Unatafuta magame mazuri ya kucheza? Hii ni moja ya makala usizotakiwa kukosa unapotaka magame ya kucheza kwenye simu. Kabla ya yote ningependa kukufahamisha hapa tunaenda kuangalia game nzuri zenye muonekano mzuri lakini game hizi ni game za Online battle loyale. Duniani kwasasa watu wengi hupenda kucheza game hizi kwa sasababu ni games zinazo jumuisha kushindana au kushirikiana na watu toka sehemu mbalimbali ulimwenguni.


Magame ya muundo huu husaidia watu kufahamiana au kupata marafiki. Kuna game za battle royal ukizicheza kwa muda wa saa moja unaweza kuwa umekutana na watu zaidi ya ishirini toka sehemu mbali za Dunia. Watu hao unaokutanana nao wanaweza kuwa marafiki zako japo haushauriwi sana kujenga urafiki na watu usio wajua tabia zao. Kuna watu huwa na tabia mbaya ambazo zinaweza kuwa ni wizi au utapeli mtandaoni, hivyo unatakiwa kuwa makini na watu unaokutana nao kwenye online games.

Game za mpira za kucheza kwenye simu BONYEZA HAPA>>>

Magame mazuri ya Battle Royale ya kucheza kwenye simu (Android na iOS)

Call of duty Warzone Mobile

Warzone Mobile ni moja games maarufu katika upande wa games za “Battle royale”. Game hili ni game la kivita ambalo ni FPS, yaani ni first person shooter ambalo lipo chini ya Activation kama games nyingine za Call of duty. Call of Duty: Warzone, ulioundwa kwa ajili ya vifaa vya simu na kutolewa mwaka 2024. Kabla ya hapo lilikua lipo lakini halikutolewa kwaajili ya simu.
Kwenye battle royal ya call of duty warzone Mobile mtu kwanza unafurahia graphics au muonekano mzuri. Mbali na Hilo Kuna mode zaidi ya moja unazoweza kuzifurahia.

Mambo ya kujua kuhusu game la Call of Duty warzone mobile BONYEZA HAPA>>>

PUBG mobile

PUBG mobile ni game lingine zuri katika upande wa battle royal. PUBG ni Third person shooter na vile vile ni First-Person Shooter. Ukitaka muonekano mzuri PUBG mobile ni chaguo sahihi lakini utatakiwa kujua kuwa Kuna “PUBG lite” ambayo hua ni game la PUBG lililopunguzwa ubora kwaajili ya simu zenye uwezo mdogo na kupunguza matumizi ya data. Ukitaka kufurahia ubora wa game la PUBG kwa asilimia 100, tumia PUBG mobile na sio PUBG lite.

Call of duty Mobile

Call of duty Mobile ni game lingine la Call of Duty lililoundwa kwaajili ya simu. Game hili lilikuepo kabla ya game la “Call of Duty warzone Mobile” halijatolewa kwaajili ya simu. Linawachezaji wengi na kitu kizuri ni kwamba linaweza chezwa kwenye simu zenye uwezo mdogo kidogo ukilinganisha ya Call of Duty warzone. Muonekano wake upo vizuri na katika modes lina mpaka mode ya zombies unayoweza furahia kucheza na marafiki.

Fortnite

Fortnite Mobile ni toleo la game maarufu la ” Fortnite battle royale” lililoundwa na Epic Games kwajili ya watu wanaotumia simu kucheza games. Game hili lilipititia matatizo ambayo huenda yangefanya game hili liwe limesahulika kwasasa lakini kutokana na ubora na kuwa game zuri mpaka Leo hawazisahau. Tatizo ambalo game la Fortnite battle royal mobile lilipitia ni kuondolewa kwenye platform kubwa ya Playstore. Jambo hili lilileta ugumu kwenye upatikanaji wa game hili kwenye simu.

Jinsi ya kucheza game la Fortnite kwenye simu bila kudownload BONYEZA HAPA>>>

Free Fire


Free Fire ni game la simu la aina ya “battle royale” lililotengenezwa na Garena. Katika game hili, wachezaji wanarushwa kwenye kisiwa ambapo wanapaswa kupambana na wachezaji wengine hadi awepo mshindi atakae simama hai. Hii ni kama battle royal za game nyingine ila lina mazuri yake tofauti. Free Fire ni game maalufu ulimwenguni na hukubali kuchezwa kwenye simu zenye uwezo mdogo kidogo ukilinganisha na baadhi ya game nyingine kubwa za battle royal.

Huo ndio mwisho wa orodha yetu katika ukurasa huu. Kama imekua msaada kwako, unaweza wajuza na rafiki zako juu game hizi. Endelea kuwa karibu na The bestgalaxy.