Category Archives: Funny stories

SOMA STORI HIZI UVUNJE MBAVU

Dogo kakamatwa na polisi akiwa na
bangi mfukoni;
POLISI: Kijana unatembea na bangi
hili ni kosa la jinai
DOGO: Afande mi naona kama nimelogwa
hiyo bangi kila nikiitupa chooni unakuta imerudi mfukoni mwangu
POLISI: Acha kunifanya mie fala
twende kituoni
DOGO: Kama huniamini afande na wewe tumbukiza chooni utaona imerudi
mfukoni mwangu toka jana inanisumbua sana ….
POLISI: Natumbukiza tuone na
ukinidanganya ndipo utakapojua
Dola maana yake nini ……afande
akatumbukiza bangi chooni
POLISI: Haya hebu toa hiyo bangi sasa mfukoni mwako
DOGO: Bangi bangi gani?
POLISI: Si ile uliyosema inarudi
mfukoni mwako
DOGO: Afande mi sikuelewi kabisaa,
mi na wewe tulizungumza wapi kuhusu bangi Mimi hiyo bangi naijua wapi
bangi hata kuishika sijawahi Au unataka kunibambikizia
kesi ya bangi afande?

πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Gusa hapa>> USOME JAMBO ZURI ZAIDI KWAAJILI YAKO

Dah soma hiiπŸ‘‡πŸ‘‡

Ni majira ya saa 11 jioni nikitoka zangu Morogoro kwenye usaili narudi zangu Dar ninapoishi.. Kutokana na ugumu wa maisha, nimebakiwa na shilingi 3000 tu mfukoni hapo nikiwaza chakula cha jioni pamoja na nauli ya daladala..tena ukizingatia Mbagala ilivyo mbali.. Nikajipa moyo siku itapita.
Tulipofika Chalinze, basi lilisimama na akapanda mrembo mmoja matata sana, umri kati ya miaka 24 hadi 26, mwenye urefu wa wastani, mweupe, mwembamba kiasi huku akiwa ametupia suruali ya jinsi pamoja na t shirt iliyomkaa vizuri na kuonesha umbo lake maridhawa la namba nane. Akaja akaketi kwenye siti iliyopo pembeni mwangu kwa kuwa kabla ya kufika chalinze, abiria aliyekuwa amekaa jirani yangu alishuka.. Basi tukasalimiana na safari ikaendelea.
Akajitambulisha anaitwa Karishma.. Na Mimi nikamwambia naitwa Abdulghan nilichukua jina la mdogo wangu abdulghanim ilimradi tu nikaeka zile za kihindi fulani ilimladi mambo yaende sawa. Basi tukapiga stori nyingi sana.. Tulipokaribia kufika Mbezi akaniaga akasema atashuka kituo cha mbezi mwisho kwani ndipo anapoishi. Basi nikamuaga..tukabadilishana namba za simu.. Kwa kweli alikuwa mcheshi sana na nilifurahi mno kupata namba zake nikijua nishapata bint mrembo mwenye asili ya kihindi.. Basi baada ya kufika Ubungo wakati natoa mizigo yangu sehemu ya kuhifadhia, nikaona pochi ya kike.
Nikakumbuka karishma nae aliweka mizigo yake pale..nikasema hebu nifungue niangalie ndani.. Heeeeh nikakuta pesa nyingi sana za kitanzania pamoja na Dola za marekani nyingi sana pamoja na vitambulisho vya karishma. Nikajiuliza, je nimpigie au nipotezee niondoke na pesa?? Wakati nawaza hayo ghafla nikaona simu inaita..Jina ni karishma. Dah..nikawazaaa nikiwazu huku simu inaita..nikaamua tu kupokea,
“Hallo, samahani Abdulghan eti umeona pochi yangu hapo hata sijui nimeipoteza wapi”
Nikamjibu ” Yah karishma ndio nimeiona sasa hivi nashuka Ubungo hapa nikawa nataka nikupigie simu”
“Ooooh thanks God! Yaan you can keep hizo hela but please naomba unisubiri nijekuchukua passport na visa yangu vitambulisho hivyo ni muhimu mno yani”
“Whaaat?? Mbona usiku sana! Are you serious?”
Ilikuwa inakaribia saa 6 usiku.
“Yah, why not? Sawa Nakusubiri Karishma.”
“ahsantee akasema Karishma”
“Usijali.. Nikiwa nafijiria sasa akifika usiku huu atarudi kweli kwao ama itakuwaje”.
Mawazo yakanijia nitaenda kulala nae kama atakubali.
Dah, ni kama nilichanganyikiwa ghafla.. Nikaona gari aina ya BMW X6 ikiingia langoni Mara nikamuona Karishma akishuka akiwa peke yake.
Nikawa nawaza, sijui itakuwaje huko ndani kama akikubali kwenda kulala na mimi ? Wakati nawaza hayo, mara nasikia Abdulghan nashukuru kwa kunihifadhia vitu vyangu mi siwezi kurudi nyumbani mana nimewaaga nitalala kwa rafiki yangu.
Sasa unaonaje tuende Landmark hotel tukalale pale mpaka asubuhi.
Mimi tena bila ya hiyana nikakubali kinyonge huku nikijua ataingia tu kwenye mtego.
Abdulghan mbona umeitikia kiunyonge au mi stahili kulala na wewe?.
Uzalengo ukanishinda usiseme hivyo Karishma kwanini usistahili?.
Nikapanda kwenye gari mpaka Landmark Hotel tukachukua chumba kimoja nikamuliza Mimi nitalala wapi choon au? Akanijibu utalala kitandani na Mimi.
Hivi naota ama kweli nikasema kimoyoni.
Abdulghan naenda kuoga nawe pia ujiadae nikirudi uende.
Mara akatoka choon akiwa na nightdress hee! Mtoto kajazia nyuma utasema body ya Nissan morano.
Salale! Anakuja kitandani nilipo.
“Unajua nini kilichotoea”
“We Abdulaziz Umejilaza tu hapo kwenye mkeka mbona hao samaki hivi umeongeza mkaa kweli? Na wakiungua hawo utakula wali na chumvi…”
Dah, mama yangu kaniamsha nilikuwa ndotoni, tena usingizi wa mchana..Duuh!!!
Dah! Hizi ndoto nyengine

Gusa hapa>> USOME JAMBO ZURI ZAIDI KWAAJILI YAKO

VICHEKESHO VYA KUVUNJA MBAVU ZAKO

Kuna vichaa walitolewa hospitali moja kwenda nyingne asa wakiwa njiani wakaambiwa wakachimbe dawa(wajisaidie) alafu safari iendelee waliposhuka kila mtu na njia yake wakakimbia dereva kuona hivyo akamwambia konda tutafanyaje sasa? Konda akajibu niachie mimi nitaliweka sawa hilo wakaondoka wakafika stend wakakuta abiria kibao wakashusha nauli watu wakajazana konda akasema dereva haina kituo hiyo mojakwa moja mpaka hospital,.

Gusa hapa ujiunge>> VICHEKESHO KUMU VYA KUVUNJAMBAVU 2022


MKE: vipi leo mbona mapema na mpole?
MUME: ofisi yetu imeungua na watu wote wamekufa,
MKE: ilikuwaje wewe ukapona?
MUME: nilikuwa chooni, jirani na ofisi najisaidia.
MKE: Loh masikini familia zao itakuwaje?
MUME: watalipwa milioni 100 kila mfiwa.
MKE KWA HASIRA: ona sasa na wewe kunya kunya kwako umetukosesha mihela..ungeenda kunya akhera……
Ungekuwa Mwanaume Ungejibu Vip


Mlevi kakutwa akikojoa eneo la
shule, Mwalimu mkuu akamuuliza,
hilo bango hapo limeandikwaje?
Mlevi akajibu ‘USIKOJOE HAPA’.
Mwl: Kwahiyo unafanya nini
hapo?
Mlevi kwa makini na upole
akajibu: HAKI YA MUNGU NILIJUA
NDIO JINA LA SHULE!!


STORI ZA VICHEKESHO VYA KUVUNJA MBAVU

mke; mme wangu ungekuwa tajiri ningefurahi
mimi; kwa nini?
mke; ungekuta na sisi tuna gari nzuri hatutembeu kwa mguu
mimi; ah wap,unadhani ningekuwa tajiri ningekuwa na wewe?ungekuta natoka na kina wema,zari…

Gusa hapa jiunge>> VICHEKESHO YA MWEZI HUU TAFUTA HAPA (MPYA)

Mlevi katuma meseji kwa mke wake; “Darling nipo bar napata mbili tatu,nitaludi nyumbani ndani ya dakika hamsini zijazo,ukiona kimya tafadhari soma tena hii meseji”. mke wake akakaa dakika hamsini kimya,kaisoma tena meseji inamwambia Nitarudi nyumbani ndani ya dakika hamsini zijazo ukiona kimya tafadhari soma tena hii meseji.
hahahahaaaa…………kumbe kila akirudia mesejiinamwambia vilevile ila inamuongezea dakika hamsini..jamaa akarudi kesho yake asubuhi mkewe alichoka ile mbaya…

Magemu mazuri ya kucheza kwenye Simu


Mwalimu aliingia darasani na kuwauliza wanafunzi juu ya ndoto zao za baadae.
MWAL: John we unataka ukiwa mkubwa uwe nani?
JOHN: Nataka niwe daktari wa moyo niwasaidie watanzania wanaougua magonjwa ya moyo.
MWAL: vizuri. Na wewe Rose unataka kuwa nani?
ROSE: Nataka kuwa rubani, niweze kusaidia watu wanapenda kusafiri kw anga.
MWAL: Safi sana Rose. Utakua utakua mfano kwa wasichana wenzio kuwa na bidii kwenye masomo ya sayansi.
MWAL: Na wewe James??
JAMES: mimi nataka kuwa tajiri mkubwa sana. Niwe na nyumba Tanzania, S.Africa, Marekani na Dubai. Niwe na gari 7 za kutembelea. Kila siku nabadilisha. Leo nikipanda hii, siirudii hadi week iishe. Nataka niwe namiliki viwanda, Makampuni, ndege binafsi na mashamba makubwa. Nataka niwe na nguvu serikalini ya kuamua nani awe Rais na nani asiwe……”
Akameza mate kisha akaendelea….
“Nataka kuwa na walinzi 20 wenye silaha nzito wakinizunguka, na watumishi wakininyenyekea. Nataka kuwa bilionea ninayeogopwa. Lakini pia nataka kuwa na mke mzuuuri sana ambaye nitakuwa natembea nae kila mahali.”
MWAL: ndoto nzuri sn lakini unahitaji bidii sana kutimiza. Haya na wewe Jenny tueleze unataka kuwa nani??
JENNY: Nataka kuwa mke wa James.!!

Gusa hapa>> USOME JAMBO ZURI ZAIDI KWAAJILI YAKO


WALEVI WAWILI KATIKA MAZUNGUMZO YAO
MLEVI 1 hivi rafiki yangu china ni mbali kweli
MLEVI 2 sidhani mbona pale kazin kuna mchina anakuja na baiskeli
πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†

πŸ˜‚πŸ˜‚ πŸ˜‚