All posts by Admin
Vichekesho vya Maandishi unavyoweza kusoma
Kucheka ni njia bora ya kupunguza mawazo yanayotukumba kila siku. Katika maisha haya yenye changamoto nyingi, kila mtu anahitaji muda wa kupumzika na kufurahia vitu vidogo vinavyoweza kuleta tabasamu. Hakuna njia bora ya kufurahia muda wako wa kupumzika kama kuangalia video au kusoma vichekesho vya maandishi, vinavyoweza kukuchekesha na kukufanya usahau magumu ya maisha kwa muda.
Utafiti unaonyesha kwamba kucheka kuna faida kubwa kiafya, kama vile kupunguza msongo wa mawazo, kuongeza kinga ya mwili, na kuboresha hali ya moyo. Kicheko pia huimarisha mahusiano ya kijamii kwa sababu huleta furaha na mshikamano miongoni mwa watu unaocheka nao. Kwa hivyo, kama unatafuta kitu cha kukuchekesha na kukupa muda wa kuburudika, basi uko mahali sahihi.
Katika makala hii, tumekusanya orodha ya vichekesho vya maandishi vinavyovutia na kuchekesha, ambavyo unaweza kusoma popote ulipo. Jiandae kwa kucheka kupitia vichekesho hivi vya maandishi!
Soma Vunjambavu za vichekesho BONYEZA HAPA>>>
Vichekesho vya Maandishi vya kuvunja mbavu
- Mtoto katika maombi
Kila mara mtoto alikua akiambiwa kuwa anaeleta au kuwapa chakula ni Mungu. Siku moja, Mama yake alimwambia huyo mtoto aombee chakula kabla ya kula. Mtoto akaanza:
“Mungu, tunashukuru kwa chakula hiki. Naomba pia ulete chips na soda kesho maana ugali na mboga za majani kila siku zinachosha!”
Watu wote mezani walicheka sana.
- Mtoto na Mwalimu
Mwalimu alianza kuuliza kila mwanafuzi darasani “Kwa nini unahitaji kujifunza hesabu?”
Mtoto mmoja akajibu “Ili mama yangu asitumie hela zangu vibaya nikimpa anishikie”
Darasa zima likacheka
- Bibi na TikTok
Bibi Fatuma alikuwa sio mjanja na hakuielewa teknolojia ya TikTok. Wajukuu wake walimshawishi ajaribu. Alianza na video kutaka kutengeneza video akiwa anacheza live. Badala ya kubonyeza kitufe cha kuanza kurekodi, aliweka simu mfukoni na kuanza kucheza peke yake huku akipiga makelele ya nyimbo za zamani.
Baada ya muda mrefu, aliwauliza wajukuu:
“Mbona hakuna mtu ana-like video yangu?”
Wajukuu alipo fikilia kuwa bibi yake alichofanya, alicheka sana.
- Mtu na mpenzi wake wanaoongea kwenye simu
MKAKA: Hi uwapi swity?
MDADA: Niko home
MKAKA: Unafanya nini?
MDADA: Nakula
MKAKA: Unakula nini?
MDADA: Mama katengeneza macaroni, ambayo kanyunyizia chiizi na sausage fulani imported ambazo baba amenunua supermaketi Masaki, na saladi, kisha ntateremsha na Epo juisi…
Mara ghafla ikasikika sauti ya mama yake “Hivi we Gulo kaka yako atakula nini na we umemaliza ugali na maharage yote?”
- Ndoa nyingine
Mtaani kwetu kuna jamaa mmoja anaitwa chogo, ana mtoto mmoja anaitwa “emma” pamoja na mke wake.. leo bwana katoa kali; Alikua amekaa nje ya nyumba yake kwenye kibalaza, alikua ameshikilia cheti cha ndoa yake.. akanza kukitazama sana, ikafika kipindi mke wake ikabidi avunje ukimya na kumuuliza “Baba emma, mbona unakitazama sana hicho cheti..?” bwana chogo akajibu huku akilia, akitoa sauti ya upole “NATAFUTA EXPIRE DATE YA HIKI CHETI CHETU..” Mke wake hoi akazimia…!
Jinsi ya kutengeneza Pesa zaidi kwenye unachokifanya (Biashara au Huduma)
Tunafanya mambo mbalimbali ili kuingiza pesa kwenye maisha yetu. Karibu kila mtu ana Kazi, Biashara au Huduma ambayo humuwezesha kupata kipato cha kuendesha maisha yake. Kipato kinaweza kuwa kikubwa au kidogo lakini maisha huitaji pesa, hivyo watu hupambana sana katika vyanzo vya mapato yao ili kuishi. Katika kupambana huko, baadhi ya watu hupambana sio tu kupata mapato au pesa, bali kuongeza kiasi wanachopata. Na kupambana kupata kipato au pesa nyingi zaidi zaidi ya unachopata kwenye unachokifanya, sio jambo baya ila inaweza kuwa sio rahisi.
Ukitupa macho au kufanya utafiti katika biashara flani, utagundua watu hupata faida au kipato tofauti. Yani inaweza kuwa ni Huduma au Biashara moja lakini Baadhi ya Watu wakawa wanaoingiza pesa nyingi kuliko wengine. Hii ni hali ambayo ipo na itaendelea kuwepo maana waswalihi wanasema “Kila mtu na ridhiki yake”. Lakini kama hauridhika, kunauwezekano wa kupambana na kuongeza kiasi unachoingiza. Tumeona hii kwenye simulizi za watu mbalimbali wenye mafanikio makubwa ulimwenguni.
Kama ni mmoja ya watu wanaohitaji kutengeneza Pesa zaidi kwenye biashara au Huduma, hapa chini kuna mambo yanayoweza kusaidia kufanikisha hilo.
Ujuzi utakao kuwezesha kuingiza pesa mtandaoni BONYEZA HAPA>>>
Mambo ya kuzingatia ili kutengeneza Pesa zaidi kwenye unachokifanya (Biashara au Huduma)
Kujichanganya na waliofanikiwa.
Ukitaka kwa kama waliofanikiwa kwenye mambo yako, jaribu kujichanganga na watu waliofanikiwa kwenye mambo hayo. Watu wengi huwa wanajitenga na waliofanikiwa na kuanza kuwasema. Lakini wewe ili kufanikiwa kama wao, unatakiwa kuwa upande wao ili upate mitazamo kama yao. Kujichanga na walio fanikiwa kunaweza kukupatia mbinu mbalimbali za kufikia kwenye kipato unachohitaji. Mbali na mbinu, unaweza kupata hata fulsa toka kwao.
Utayari wa kujifunza na kubadilika.
Hiki kitu ni muhimu sana kwenye maisha ya mafanikio na kuongeza kipato. Ukiwa tayari kujifunza mambo na kubadilika, basi utakua na uwezo wa kujifunza mambo muhimu kwenye huduma au biashara yako. Alafu pia utakua na uwezo wa kuyafanyia kazi baadhi ya mambo ili kuongeza kipato.
Baadhi ya watu hauwana uwezo huo. Wanaweza ambiwa au kuona mbinu zote za kuongeza kipato lakini wasifanye chochote cha maana. Yani hufanya biashara au huduma kwa mazoea huku wakilalamika kuwa wanatamani kuongeza kipato. Na mbaya zaidi ni hawataki kubadilika.
Kuelewa Soko au wateja.
Chunguza mahitaji ya wateja na matatizo yao. Elewa tabia, wanachopenda, na uwezo wa kifedha wa wateja wako. Fikilia ni jinsi gani unaweza wasaidia kwenye mambo yao na ukapata pesa. Jaribu kutafuta pengo na litumie kama fursa kwenye kwenye biashara au huduma yako.
Usipoelewa vizuri unao wahudumia, utakua haujaielewa vizuri huduma yako pia. Na usipoielewa biashara au huduma yako, unaweza usipate hata faida ya unachofanya.
Kutambulisha kwa watu (Itangaze)
Ukiwa na Biashara au Huduma ambayo haitambuliki na wengi, inawezakua ni ngumu kupata watu wengi wanataokufanya upate hata faida. Lakini ikiwa inatambulika na unaitangaza, watu wataona unachofanya na kujihusisha nacho.
Hii itakusaidia kupata faida kuwa kwenye kitu unachofanya. Kwa sasa mtu unaweza tumia hata mitandao ya kijamii (kama Instagram, Facebook na TikTok) kutangaza bidhaa/huduma.
Protected: UTAMU WA JUMLA 08 (Simulizi ya Maandishi)
Jinsi ya kushinda Aviator (Zingatia mambo haya)
Katika michezo ya kubahatisha inayoweza chezwa mtandaoni, Aviator ni moja ya michezo maalufu sana. Mchezo huu wa kubahatisha unapatikana katika tuvuti nyingi zinazohusisha na kubeti hapa nchini. Mfano wa tuvuti unazoweza kutembea ili kucheza Aviator ni Parimatch, Wasafi bet na hata Sportybet.
Unaweza weka dau au pesa kwenye mchezo wa Aviator na ukashinda hata mara 4000 ya pesa yako. Mfano; unaweza Tsh 200 kwenye mchozo huu na ukabahatika kupata hasi Tsh 800,000. Lakini sio rahisi kufikilia ushindi wa kiasi hicho maana mchezo wa Aviator ni mchezo wa kubahatisha. Hivyo ushindi wa kiasi hicho unaweza kukudondokea ukiwa na bahati. Wengi hubahatika kupata mara mbili mpaka mara kumi ya pesa zao.
Hapa The bestgalaxy, leo tumekuja na Mambo kadhaa ambayo ukiyazingatia yanaweza kufanya uwemshindi mara kwa mara katika kucheza Aviator. Tumia muda wako kuyasoma ili kujiweka sawa katika mchezo huu kushinda Aviator.
Jinsi ya kubeti Bure BONYEZA HAPA>>>
Mambo ya kuzingatia ili kushinda Aviator
Usisahau kuwa Aviator ni mchezo wa kubahatisha
Pamoja na kwamba mchezo wa Aviator unaweza kuifanya pesa yako iwe mara mbili au zaidi lakini usisahau kuwa ni mchezo wa kubahatisha(Sio kazi au Ajira). Yani unaweza bahatika kupata faida ya pesa yako au ukapata hasara kabisa kwa kuipoteza hela yako. Hii isikutishe ila ikuweke vizuri kisakiolojia pale unapopata hasara.
Hakikisha pesa unayotumia kuchezea mchezo huu ni pesa ulioitenga kwaajili ya kuchezea mchezo wa kubahatisha ili usipate mawenge katika mchezo.
Usiweke pesa kwenye kila mzunguko
Kwenye Aviator, ndege huwa inazunguka mizunguko mingi sana ila ukitaka kushinda mara nyingi, unatakiwa kuwa muangalifu unapoweka pesa yako kwenye mzunguko. Usiweke pesa kwenye kila mzunguko. Baadhi ya mizunguko iache ipite bila kuweka pesa na usijilaumu pindi mzunguko uliouacha, ukifanya vizuri kuliko ulivyotarajia. Kuiacha baadhi ya mizunguko izunguke bila kuweka pesa, kunaweza kuokoa pesa zako kwenye mizunguo mibaya.
Usisubiri pesa ijizidishe mara nyingi
Ni kweli Aviator inaweza kuifanya pesa izidishwe hata mara 4000 lakini usisubiri pesa yako izidishwe kiasi hicho ndio Ucashout(utoe). Watu wengi wanaotaka kuzizidisha pesa zao mara nyingi huishia kuzipoteza kabisa. Usiwe mmoja wao, hakikisha unakua makini katika kucashout na utosheke mapema ili kuioka pesa yako. Akili yako ikiwa na matarajio madogo unaweza pata faida zaidi kuliko mwenye kuwinda pesa kubwa. Tosheka kabla ya moyo wako kutosheka. Sehemu salama zaidi kutoa pesa ni 1.50x mpaka 2.00x.
Cheza mchezo kwenye utulivu huku ukiisikiliza sauti
Unapocheza mchezo huu, huwa kuna sauti inatoka katika mchezo. Ile sauti inaweza kuwa kama kelele zisizo na maana lakini inamsaada mkubwa kwenye kutuliza akili. Kusikiliza sauti ile kwenye utulivu huku unacheza, kutakufanya uzingatie mchezo na kufanya maamuzi ya kuweka au kutoa pesa kwa uangalifu.
Kama umeingia kwenye tuvuti yoyote yenye Aviator lakini haupati sauti unapocheza, fanya kugusa sehemu inayoonesha kile kindege alafu utaanza kusikia sauti.
Mwisho, ningependa kuifunga makala hii kwa kukumbusha kucheza michezo ya kubahatisha kistaabu. Yani hakikisha unakua mchezaji wa kawaida tu na sio mrahibu.

Maneno matamu ya kumwambia mpenzi wako kwa SMS
Maneno matamu yana nguvu ya kipekee ya kugusa moyo wa mtu. Unaweza muumiza mtu kwa maneno au kumfurahisha. Kwenye mapenzi, unaweza tumia maneno kumfurahisha mpenzi wako na kuimarisha uhusiano wenu. Hata ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) unaweza kuwa njia rahisi na ya haraka ya kuonyesha hisia zako za dhati na kumfurahisha mpenzi wako. Unaweza usiwe naye kwa muda wote, lakini maneno yako yanaweza kuunganisha mioyo yenu hata mkiwa mbali.
Mapenzi si tu kumfanyia mpenzi wako matendo makubwa, bali pia ni kuhusu kufanya mambo madogo madogo kila siku. Mambo kama kumtumia ujumbe mzuri uliojaa upendo unaweza kuwa ni kuonesha mapenzi pia. Kumwambia mpenzi wako neno “Ninakufikiria,” au “Unanifanya nijisikie furaha.” Kupitia sms kunaweza fanya some huo ujumbe na kufikilia mambo mengi chanya juu ya upendo wenu. Yani kuna ujumbe hata ukimfikia mpenzi akiwa anawasiwasi au ameweka jambo baya moyoni, akiusoma moyo wake unakua vizuri ghafla na kusahau yote.
Hapa sisi kama kawaida, tumekuandalia maneno ya mapenzi unayoweza tumia. Haya ni yale maneno matamu ambayo unaweza kumwambia mpenzi wako kwa njia ya SMS. Maneno haya yamebeba hisia, yanayowaweka wapenzi karibu, na kufurahisha.
Mpenzi anaekupenda sana anaweza kukuacha kwasababu hizi BONYEZA HAPA>>>
Maneno matamu ya kumwambia mpenzi wako kwa sms
- Walimwengu bhana… Watakuja kukudanganya, watajifanya hawajui kuwa tunapendana, wanajifanya wanakupenda sana ila nia yao waharibu penzi letu alafu wapate cha kusema. Najua kupendana kwetu ni huzuni kwao, ila sitaacha kukupenda.
- Huenda kiumbe unaye muogopa hapa Duniani ni mwanaume ila naomba usiniogope mimi. Nakupenda sana na nipo kufuta maumivu yote umepitia malkia wangu.
- Wakiniambia niwaweke moyoni, nitawambia moyoni upo wewe na funguo za moyo nimepoteza.. siwezi kukutoa na wala siwezi waingiza
- Na jua kuna nyakati tunaweza pita zikawa ngumu kidogo kuamini kuwa tunapendana. Ila usisahau kuwa nakupenda hata kwenye nyakati hizo wangu.
- Siku njema kwangu ni ile ninayojua upo salama na bado unanipenda. Ukiwa salama nakua na Amani, ukiwa unanipenda nakua nina furaha mpenzi.
- Tuhesabu 1 mpka 5 alafu ntakwambia kitu. Haya tuanze sasa. Moja, Mbili, tatu, nne, tano, Anaesoma ujumbe huu ndie ameuteka moyo wangu. Nampenda sana.
- Umewahi jaribu kuhesabu nyota? Ukiwa unahesabu nyota angani, unaweza anza kwa kuziona chache mwanzoni lakini ukizingatia, nyingine hua kama zinaibuka na kuwa nyingi kiasi cha kutohesabika. Ninasababu nyingi za kukupenda ila ni ngumu kuhesabu kama ilivyo kwenye nyota. Kila muda unavyoenda, nazidi kupata sababu nyingi za kukupenda.
- Moyo wangu unanisukuma nikwambie nipo tayari kufanya chochote hapa Duniani kwaajili yako. Yote ni sababu unaupa furaha mpaka siku hizi unadunda sana likitajwa jina lako.
- Mbali na uhai nilionao, penzi lako ndio kitu cha thamani maishani mwangu. Naweza potezea chochote ila nikabaki na furaha sababu wewe unanipenda.
- Nakupenda sana mpenzi. Moyo wangu Nimekupa mazima kama zawadi ya upendo. Na ikitokea siku nikakwambia unauumiza, Sina maana unirudishie, ninamaana uubembeleze.
- Maana sahihi ya mapenzi nimeijua nilipokupata wewe. Penzi lako limenipeleka ulimwengu uliojaa Raha, kwenye Giza umekua ni taa mpaka najivunia kuwa na wewe.
- Unataka kujua wewe ni nani kwangu? Wewe ni yule ambae tukikosana nakua sina furaha. Yule ambae nikifikilia anavyonipenda huwa natabasamu. Yule alienionesha kuwa Asali ladha yake halisi ni utamu. Yule natamani niwe nae hilele maishani mwangu.
- Nakupenda sana na natamani ujue kuwa walimwengu wanataka tuachane wakati sisi tunataka tuwe wote milele. Tukiyasikiliza ya walimwengu tutafika wanapotaka tufike na tukisikilizana, tufika tunapotaka kufika.
- Umejaa kwenye kila sehemu ya moyo wangu. Unaweza kuwa Sababu ya huzuni au furaha yangu.
- Unaweza kaa bila kuvuta pumzi ila sio kwa muda mrefu. Na ndivyo naweza kaa bila ukaribu na wewe ila sio kwa muda mrefu. We ni mtu muhimu kwangu, nakupenda.
Ni hayo tu katika ukurasa huu, unaweza tembelea ukurasa mwingine na kusoma sms za mapenzi nyingine kama hizi zitakua sio chaguo zuri kwako. Endelea kuwa karibu na The bestgalaxy kwa mambo mengine zaidi.
Protected: UTAMU WA JUMLA 07 (Simulizi ya Maandishi)
Usifanye mambo haya ukiwa Dubai
Dubai ni mji maarufu duniani unaovutia watalii kutoka kila pembe ya dunia. Una mandhari za kuvutia, teknolojia ya kisasa, utajiri na ni mahali panapopendwa sana na watu. Lakini, kama ilivyo kwa miji mingine mikubwa, kuna sheria, desturi, na kanuni za kipekee ambazo wageni wanapaswa kuziheshimu. Kutozingatia mambo kama hayo ukiwa Dubai, kunaweza kusababisha usumbufu au matatizo makubwa hatakama ni mgeni.
Kama mgeni unayeitembelea Dubai kwa mara ya kwanza, ni muhimu kujua mambo unayotakiwa kujiepusha nayo ili kuhakikisha safari yako ni ya kufurahisha na sio matatizo. Mji huu una mchanganyiko wa mila za Kiislamu na tamaduni za kisasa, ambazo zote zinahitaji heshima kutoka kwa wageni wake. Kutokujua sheria za msingi kunaweza kusababishia migogoro isiyo ya lazima.
Katika makala hii, tutakupa mwongozo wa mambo unayopaswa kuepuka unapokuwa Dubai. Kwa kuzingatia mwongozo huu, utakuwa na fursa ya kufurahia safari yako bila wasiwasi na kuonyesha heshima kwa wenyeji wa mji huu wa kuvutia.
Jinsi ya kupata Ticket za ndege za bei rahisi BONYEZA HAPA>>>
Mambo Usiotakiwa Kufanya Ukiwa Dubai
Usile hadharani kipindi cha Ramadan
Kipindi cha Ramadan ni takatifu kwa Waislamu, na kula, kunywa, au kuvuta sigara hadharani wakati wa mchana ni marufuku kwa wote, wakiwemo wageni. Ni muhimu kujizuia na kuheshimu ibada ya kufunga kwa wenyeji. Kama ukiwa katika mji huo kipindi cha Ramadan, basi kuwa mtulivu na ufuate utaratibu wao.
Usilale na mpenzi wako chumba kimoja kwenye baadhi ya hoteli
Hoteli nyingi katika Dubai zina sera zinazofuata sheria za Kiislamu, na wanandoa wasiooana hawaruhusiwi kulala chumba kimoja. Hakikisha unafahamu sera za hoteli kabla ya kufanya malipo. Kuna hotel nyingine huruhusu wageni kulala pamoja hatakama hawajaoana na ndio unapaswa kuzitumia ili kuepuka usumbufu.
Kunywa pombe hadharani
Ingawa pombe inaruhusiwa lakini ni kwenye maeneo maalum kama baa na hoteli zinazoiruhusu. Kujiachia na kunywa au kuionyesha hadharani kunaweza kusababisha matatizo makubwa, ikiwa ni pamoja na faini au kifungo. Swala hili linatakiwa kuzingatiwa kila siku na sio siku za Ramadan tu kama ilivyokua kwenye kula.
Kusalimia kwa kutumia mkono wa kushoto
Katika tamaduni za Kiarabu, mkono wa kushoto unachukuliwa kama mchafu, na hivyo ni vyema kutumia mkono wa kulia unapotoa au kupokea kitu, au hata kusalimiana. Fanya havyo maana Dubai ina utamaduni wa kiarabu na nivema ukauheshimu unapokuna wenyeji.
Hatumaini hayo wamekupa mwanga na mwongozo juu ya jinsi gani unatakiwa kuwa au kufanya huko Dubai. Mbali na kuyajua hayo, ni vema ukawa chini ya mtu mwenyeji atakea kusaidia kujua zaidi mambo ya kufanya katika mji huo ili kuhakikisha haukosei.
Movie gani ni nzuri kuiangalia ukiwa na Mpenzi wako?
Katika vitu hufurahisha zaidi, kutazama filamu/movie nzuri ukiwa na mpenzi ni moja wapo. Unakua ni wakati mzuri wa kujenga uhusiano wenu kwa pamoja huku mkifurahia hadithi zinazovutia na kugusa nyoyo. Kuangalia movie pamoja kunawapa wapenzi nafasi ya kufurahia na kutathimini mahusiano au maisha kutokana na wahusika wa movie na kujifunza mengi kupitia wahusika hao.
Movie nzuri za kutazama na mpenzi wako hazihitajika kuwa na hadithi za kuvutia. Lakini pia zinapaswa kuwa zinakugusa hisia na zenye maudhui ambayo yanawaweka nyinyi wawili kwenye safari nzuri ya mahusiano. Unapo chagua movie za kuangalia pamoja unatakiwa kuwa makini sana kwa sasa maana sio kila movie unapaswa kuangalia mukiwa pamoja. Mnachokiangalia pamoja ni vema kikawa kinaziweka hisia zenu pamoja, kuwajenga kwenye mahusiano na kuwaburudisha.
Katika makala hii, tunaangalia orodha ya filamu/ movie ambazo ni bora kutazama ukiwa na mpenzi wako Mwanamke au Mwanaume. Movie hizi zitaamsha hisia, kuleta furaha, na kufanya mufurahie muda wenu wa pamoja.
Unaweza angalia movie itakayo kifaa zaidi alafu akaitafuta, kuiangalia kwenye platform mbalimbali za movie mtandaoni.
Jinsi ya kuangalia movie Bure mtandaoni BONYEZA HAPA>>>
Movie nzuri kutizama ukiwa na mpenzi
- Rapunzel (Katuni/Animation)
Hii ni movie/filamu ya Tangled (2010) ya Disney. Ni hadithi ya kifalme inayomuhusu muhusika Rapunzel mwenye nywele ndefu za kichawi, anayetoka kwenye mnara wake kwa msaada wa mwizi aitwaye Flynn Rider. Ni mchanganyiko wa vichekesho, mapenzi, na adventure.
- Titanic
Titanic (1997), iliyoongozwa na James Cameron, ni filamu ya mapenzi na drama ya kihistoria. Inahusu kuzama kwa meli ya Titanic mwaka 1912. Wanaigiza Leonardo DiCaprio (Jack) na Kate Winslet (Rose), kama wapenzi kutoka tabaka tofauti wanaokutana na kupendana kwenye meli hiyo.
- No Hard Feelings
Filamu hii ya vichekesho ya mwaka 2023 inamshirikisha Jennifer Lawrence. Inahusu Maddie, mwanamke anayekodiwa na wazazi matajiri kumfundisha kijana wao mwenye aibu (Percy) jinsi ya kuwa na ujasiri kabla ya kuanza chuo. Ni mchanganyiko wa vichekesho, mapenzi na mafunzo ya maisha.
- Subservience
Filamu hii ya kisayansi (sci-fi thriller) inahusu madhara ya teknolojia ya AI (akili bandia). Nyota wake ni Megan Fox na Michele Morrone. Hadithi inazungumzia AI ya nyumbani inayogeuka na kusababisha matatizo makubwa.
- What the Peeper Saw
Filamu hii pia inajulikana kama Night Child (1972). Ni thriller ya kisaikolojia kuhusu mvulana anayetuhumiwa kuhusika na kifo cha mama yake na uhusiano wake wa ajabu na mama wa kambo. Ni hadithi ya hofu na hila za akili.
Mbali na movie hizi, Kuna movie au filamu nyingine nyingi sana zinawoza kufa ukiwa na mpenzi wako. Kama una movie nyingine kichwani, unaweza andika hapo kwenye sehemu ya maoni ili kuwasaidia wengine.
UTAMU WA JUMLA 06 (Simulizi ya Maandishi)
Walivyoondoka tu nikajisemea “Bora wameniamsha maana simu nimeiweka pabaya kiasi kwamba mwizi angepita maeneo haya angechukua simu bila mimi kujua”. Baada ya hapo mawazo ya Salma yakaanza kuteka kichwa changu. Nikaanza kuwaza “Dah Salma nae sijui kaenda wapi?… Naanza mpaka kukosa raha yani. Na hii ndoto nilioiota hapa ni ukweli au imesababishwa na makelele ya waliokua wananiamsha tu? Itakua ni hawa mbwa wameniletea lindoto la ajabu… ila sasa mbona hayupo na hakuniambia jana kwamba hatokuepo leo?”Niliwaza mambo mengi sana hapo lakini kichwa kilikua hakinipi majibu ya moja kwa moja, nilikua najiuliza maswali yanayo zaa maswali tu.
Mida ya saa 7 mchana hivi nikiwa palepale mlangoni nilikuta Salma anarudi na anarudi na mzigo mkubwa kiasi kwenye pikipiki. Nilivyomuona Moyo ukadunda kwa furaha “Nduh” alafu nikaendelea kuwaangalia yeye na dereva wa pikipiki wakifika pale. Walipofika nikasalimiana na dereva wa pikipiki pamoja na Salma pia alafu nikasaidia kutua mzigo na kumuwekea mlangoni kwake maana alishakua malaika wangu muda huo, vitu vyake vigumu na vizito lazima nijihusishe navyo.
Baada ya hapo dereva wa pikipiki aliondoka na kutuacha pale na mimi hapo nilimuuliza alikua wapi akaniambia alikua kununua mzigo wa nguo za watoto anataka kuanza kuuza maana alikua hana kazi ya kufanya hapo mjini. Aliponijibu tu hivyo mimi sikumchimba sana kwenye mambo ya kazi huko, nikajikuta moyo umekua mwepesi alafu nikawa na furaha ya ajabu kumuona malaika wangu Salma amerudi.
Siku hiyo tukaendelea kuongea mambo ya mahusiano yetu na mambo mengine ya kijinga kijinga mpaka jua linazama. Usiku uliingia na katika kutumiana nae ujumbe usiku huo nilimuomba aje tulale wote lakini alikataa, nikamuomba nimfuate nikalale kwake lakini bado alikataa. Nikajua huenda ni mwanamke muoga na anaogopa kukubari kirahisi kuwa na mwanaume, hivyo nikamuacha siku hiyo, sikumsumbua sana. Na hata kulivyokucha niliendelea kuwa nae vizuri tu kimaongezi ila sikuingizia swala la yeye kukataa kulala na mimi usiku. Sikwenda kwenye mafunzo siku hiyo ili tu nibaki na yeye nyumbani.

Siku ya pili usiku katika kuchati nikaamua kujaribu tena kumshawishi tulale wote usiku huo chumbani kwangu ili angalau nipate nafasi ya kumkamata na kumgusa panapotakiwa. Nakumbuka nilimwambia “Salma, njoo ulale kwangu leo… Natamani tulale wote” lakini hakukubari, akajibu “Ah hapana, huko siji hahaha”. Nilijaribu pia kumwambia anifungulie mlango wa chumba chake ili niende nikalalale kwenye chumba chake lakini hakuniruhusu kufanya hivyo, alikataa. Siku hiyo nilijisikia vibaya kidogo maana ilikua ni mara ya pili kunigomea lakini nikajitahidi kupuuza alafu tukaendelea kuongelea mambo mengine. Kulivyokucha, tulikua tunaongea mambo ya mapenzi na vitu vingine kama kawaida lakini sikua naingizia mambo ya yeye kukataa kulala na mimi usiku. Na kiukweli nilikua siwezi muuliza “Kwanini hutaki kulala na mimi?” akiwa mbele ya macho yangu kwakua nilikua kwa kiasi flani namuogopa na pia kichwani nilikua nawaza “Nisiwe na haraka, huenda usiku unaofuata atakubari”. Jambo hili lilinipa mawazo sana mpaka nikashindwa tena kwenda kusoma mafunzo, nikabakia tu nyumbani na yeye.
Siku ya tatu usiku pia alinigomea na siku hiyo niliumia sana maana ilikua ni mara ya tatu hiyo najaribu kumshawishi na hanikubalii. Lakini usiku huo nilijikaza tena nikaendelea kuongeanae mambo mengine tu. Na baada ya kukucha nikakutananae kama kawaida na tulikua kama wapenzi kabisa katika kusalimiana na kuongea. Siku hiyo nilibaki nyumbani ili niongee nae tena kama kawaida lakini sikupata nafasi ya kukaa nae muda mrefu maana mida ya saa 3 asubui alikua anaenda kuuza nguo za watoto na aliniaga na aliniambia anaweza kurudi jioni.
Hiyo siku Salma alivyoondoka na kuniacha pale nyumbani nilikumbwa na mawazo mengi sana juu yake kwakua nilikua simuelewi kabisa. Nakumbuka niliingia ndani ya chumba changu nikakaa nikawanawaza “Huyu dada mbona ananitesa hivi? Au ndo ameanza mambo aliokua ananifanyia Zuu kipindi nipo chuo? yaani nashindwa kumuelewa maana mchana tukikutana anakua kama ni mpenzi wangu ambae anaweza kubali chochote ninachomwambia lakini nikimwambia usiku tulale wote anakataa… Inamaana na haelewi ninachomaanisha au? Mh itakua huyu Salma hanipendi ila ananiigizia… Itakua ananiigizia tu huyu maana pamoja nakwamba nashindwa kumwambia moja kwa moja ninachotaka lakini jinsi ninavyomwambia tulale wote, yeye ilibidi aelewe tu nataka nini. Au mimi ndio nakosea kumwambia? Mh labla ila bado nampenda acha anisumbue tu akili yangu… Kuna siku ataniruhusu tu kugusa mtunda wake ule… yani mdada mweupee, mzuri sura alafu kapewa umbo lenye mamizigo ya kutosha… mmh acha anitese tu ila nikikamata nitambana mpaka atafurahi”
Wakati nimo ndani mule naendela kuwaza nikasikia kama kunamtu nje anapiga hodi hivi, Nilipotoka nje nikakutana na majamaa watatu. Mmoja kati yao niliposalimiana nae akajitambulisha kuwa yeye ndie mwenye kile chumba ambacho nilikikuta kwenye nyumba hiyo wakasema mwenye nacho amesafiri. Alisema amekuja hapo kuchukua vyombo vyake na ameishaongea na mwenye nyumba. Mimi nikamkubalia na baada ya dakika chache nikawa nawashuhudia wakifungua mlango na kuanza kutoa vitu kuvipeleka kwenye gari ambalo lilisimama mbali kidogo na kwenye nyumba.
Baadae na mimi nikaona nisiishie kuwaangalia tu, nikajumuika nao kuwasaidia kutoa vyombo na kupeleka kwenye gari. Basi tukaanza kupiga stori huku tukifanya kazi kama ilivyo kawaida kwa wanaume kupiga stori nyingi hatakama hatujajuana sana. Tulifanikiwa kupakia kila kitu kwenye gari na jamaa akaanza kuniaga. Nakumbuka yule jamaa alisema “Asante sana, mimi nimehamia mtaa wa mbele hapo kunajumba linawapangaji wengi, Hiyo nyumba ni ya mama mmoja tajiri sana anafahamika kama Mama Suzi anakaa kwenye jumba lake huko… Ukiwa na muda unaweza ukanitembelea mzee” basi mimi nikaitikia “Anh sawa, usiwaze”. Baada ya mimi kusema hivyo akasema “Poa bwana, utaniagia huyu Tausi maana naona hayupo sjui kaenda kujiuza huko hahaha”.
Mh mimi nikashtuka, nikamuuliza “Tausi yupi huyo?” akasema “huyo dada mweupe mwenye chumba hicho”. Mh nilishangaa nikajikuta naropoka “Anaitwa Tausi huyo?”. Huyo jamaa akajibu “Ndio.. kwani vipi? si ndio jina lake ilo au?” Muda huo niliona niseme tu “Ndio” ili tukaete maengezi. Nikamsikia jamaa akisema huku akiondoka “Nasikia huyo dada ni hela yako tu… ukimpa hela, anakupa chungawa. Kuna mitaa niliwahi muona wanamjua sana ila sijui mitaa ya huku kaamia kufanya nini… Kwaheri bwana”. Mimi sikua na maneno mengi hapo nikajibu “Sa.. sawa” alafu nikaenda haraka ndani kupumzisha akili maana hali yangu iliishaanza kuwa mbaya. Nilikaa kitandani nikaanza kuwaza “Yaani inamaana Tausi ndio huyu Salma?… Na inamaana wale madada ulioniamsha nikiwa nimelala walikua wanamtaka Salma ambae ndie huyo Tausi?… alafu huyo tausi anajiuza?… Ah hapana, Mpenzi wangu Salma sio huyo Tausi wao”…
INAENDELEA….