All posts by Admin

Jinsi ya kutafuta Jina la movie kupitia kipande cha video

Kwasasa ukizunguka katika mitandao ya kijamii, unaweza pata video fupi ambazo ni vipande vya movie. Video hizi fupi zinaweza kuonesha sehemu nzuri ya movie flani lakini kupata jina la movie hiyo inaweza kuwa changamoto. Mfano; Kuna siku nimewahi kutana na video katika Mtandao Facebook. Hiyo video ilikua inaonesha sehemu ya kusisimua ya movie. Sehemu hiyo ya movie ilinifanya nitamani kutafuta na kuangalia movie hiyo mwanzo mpaka mwisho. Lakini nilishindwa kufanya hivyo kutokana na kutojua jina la movie yenye kipande hicho.
Sawa hili huwa linapitiwa na watu wengi sana katika kipindi hiki. Watu huona vipande vya movie kwenye TikTok, Facebook na WhatsApp lakini wanashindwa kujua majina ya movie zenye vipande hivyo. Baadhi ya watu huwa wanabahatika kupata Jina la movie kwenye sehemu ya maoni (Comment) japo sio mara zote utapata watu waliotaja jina kwenye sehemu hiyo. Lakini hayo yasikutie shaka maana kuna njia Bora ya kutafuta Jina la movie kupitia kipande kifupi cha video ulichokiona sehemu yoyote. Ukihitaji kujua juu ya hili? soma yafuatayo hapoa chini.

Jinsi ya kutafuta Jina la Movie kwa kipande cha kifupi cha Video

  1. Piga Screenshot sehemu nzuri ya video.

Kitu Cha kwanza unatakiwa kufanya ni kuplay kipande cha video fupi ulionayo alafu upige screenshot sehemu nzuri. Ninapozungumzia sehemu nzuri, ninamaana sehemu ambayo inawaonesha waingizaji na mazingira yao vizuri.
Unaweza piga Screenshot mbili au zaidi ili upate screenshot moja itakayokua vizuri kuliko zote.

  1. Ingiza Screenshot katika Google Lens.

Baada ya kupata screenshot moja nzuri sana, utatakiwa uiingiza Katika Google Lens. Hii Google Lens inakuwezesha kutafuta taalifa za vitu kupitia picha. Mfano; ukiipatia Google Lens Screenshot (picha), itakupa taalifa mbalimbali kuhusu hiyo screenshot. Na kama utaipatia Screenshot ulioipiga katika kipande cha movie, unapata taalifa zinazojumuisha Jina la movie.

App ya Google Lens inapatikana Playstore kwa watu wanaotumia simu za Android(Ina alama ya kamera. Lakini kwa iPhone unaweza tumia Google chrome. Inapatikana kama kipengele kidogo katika Google. Kama unatumia Google kupitia Chrome, utakiona kipengele cha Google Lens kikiwakilishwa na alama ya kamera.
Kutumia Google Lens ni rahisi tu; unaifungua, unachagua picha au screenshot iliopo kwenye simu yako alafu unaiacha ikupe taalifa Toka Google kuhusu hiyo screenshot.

  1. Kupata jina, angalia kwa umakini matokeo ya Google.

Google itakupa matokeo mengi kuhusu hiyo screenshot lakini kwakua unataka jina la movie, utatakiwa kuwa makini kuchambua. Umakini unahitajika maana kama screenshot yako haikua vizuri, unaweza pata taalifa tofauti na unazotafuta.
Lakini kama utajiridhisha kuwa majibu ni sahihi, utakua umefanikiwa kupata jina la movie kama ulivyohitaji.

Jinsi ya Kuangalia movie Bure mtandaoni BONYEZA HAPA>>>

Ujumbe mzuri kwa Mke au Mume aliye mbali na wewe

Katika maisha ya ndoa, kuna nyakati ambazo wanandoa wanalazimika kuwa mbali kwa sababu mbalimbali kama vile kazi, masomo, au majukumu mengine ya maisha. Ingawa umbali unaweza kuwa changamoto, ni muhimu kuendelea kudumisha mawasiliano na kuonyesha upendo na kujaliana hata mkiwa mbali. Kwa bahati nzuri, ujumbe wa maandishi ni njia rahisi na ya haraka ya kufikisha hisia kwa mke au Mume, huku ukimpa moyo na kumhakikishia kuwa yupo akilini kila wakati.

The Bestgalaxy, katika makala hii tumekusudia kutoa mifano ya ujumbe mzuri kwa mke au mume aliye mbali. Ujumbe huu unaweza kumtia moyo, kumfariji, au hata kumpongeza kwa kukuweka moyoni, bila kujali umbali uliowatenganisha. Maandishi haya madogo lakini yenye maana kubwa yanaweza kuimarisha uhusiano wenu na kumfanya mwenzako ajisikie kupendwa na kuthaminiwa hata akiwa maili nyingi kutoka kwako.

Mambo ya kuzingatia katika kuwasiliana na mpenzi aliye mbali BONYEZA HAPA>>>

Ujumbe mzuri kwa Mke au Mume aliye mbali na wewe

  • Tupo mbali ila unavyonionesha upendo ni kama nipo karibu na wewe. Nakupenda na sitoacha kukupenda maana nililiandika Jina lako kwenye moyo wangu kwa wino usiofutika milele.


  • Kwenye familia yangu wewe ni malkia, mama watoto wangu na ndio familia yangu kiufupi. Kila nikikumbuka unavyonipenda, kunipa furaha, kunisaidia na kusimama nami, najiona nimekupata kama bahati. Ni maisha tu yananiweka mbali nawe ila nakupenda na natamani nirudi.

  • Nipo mbali kwasasa ila tambua Moyo na Mawazo yangu vipo kwako. Kila siku yangu ya huku haiwezi kuwa sawa bila kajua hali yako. Nakupenda sana na nakuahaidi kutunza penzi letu mpaka tutakapo onana.


  • Wanasema “Umbali si kitu kwenye mapenzi ya kweli”. Umenifanya niamini hivyo kwasababu haujapunguza penzi lako kwangu. Umekua na mimi kwa simu kila moyo unapohitaji, tumekua wanandoa ambayo ni marafiki kwenye kila hali. Nakupenda sana na asante kwa kuwa nami.
  • Huwa nakuona kwenye ndoto zangu. Na hata nikifumbwa macho kwenye maisha siku hizi sioni giza, nakuona wewe mwanga wangu. Asante kwa kuwa rafiki na mshauri na mzuri kwangu. Usijesahau kuwa nipo mbali ila nakupenda sana.

  • Ni wanawake wengi huitaji mahusiano ila wachache hukubali kuwa Mama. Asante kwa kukubari kuwa mama watoto wangu. Pia ni wanawake wechache huvumilia mume anapokua mbali lakini wewe unafanya hivyo. Asante kwa kuniheshimisha na sichoke kuniheshimisha. Nakupenda sana mke wangu.


  • Mungu akulinde huko uliko mume wangu. Unapambana sana juu ya maisha yetu. Naweza kuwa sipo vizuri katika kukushukuru kwa kila jambo ila tambua nakupenda na kukuombea kwenye kila unalofanya. Nakupenda sana mme wangu.

  • Nakukumbuka kila mara Mme wangu. Siku ya kuonana na wewe naiona kama ipo mbali sana ila kamwe siwezi punguza upendo wako. Naomba kwa mungu nafasi zetu ziwe pamoja milele, na akusaide kwenye kila jambo lako kipenzi.

Unapomtumia ujumbe mzuri mke au mume wako aliye mbali unamkumbusha kuwa unampenda, unamjali na haujamsahau. Kwaiyo jambo hili ni muhimu sana katika Mahusiano.

Mambo mazuri unayoweza kufanya kwa App ya Mtandao wako wa Mawasiliano



Kutokana na ukuaji wa Teknolojia, mitandao ya mawasiliano imekua na app za pesa ambazo tunazitumia kwenye simu za smartphone. App ninazozingumia hapa ni app ya Mpesa, My Halo, Mixx by yas, My Airtel na nyingine kama hizo.
Watu wengi wenye smartphone hutumia app hizi na zimekua zikirahisisha sana mchakato wa kutuma pesa kwa ndugu na marafiki zao. Uzuri wa app hizi katika kutuma pesa ni huwa zinarahisisha mchakato mzima wa kutuma pesa. Zinapunguza na changamoto ambazo hujitokeza mara nyingi mtu anapotuma pesa.


Mfano wa changamoto hizo ni kukosea na namba ya mtumiajia na kupata lile tatizo la “Invalid MMI code.” Unapochelewa kufanya uchaguzi katika Menu za kawaida.

Ukiwa unatumia app, kunakuwa na uwezekano mdogo wa kukosea namba ya mtu maana unaweza ichukua moja kwa moja kwenye majina uliotunza.



Sasa mbali na mambo ya kutuma pesa kwa ndugu na marafiki, app hizi Kuna mambo zimeyarahisisha sana. Kama unatumia moja ya app hizi, basi angalia orodha ya mambo mazuri unayoweza fanya kwa urahisi kupitia app hizi za pesa.

Jinsi ya kutafuta simu iliopotea au kuibiwa BONYEZA HAPA>>>

Mambo mazuri unayoweza fanya kwa app ya mtandao wako wa Mawasiliano

Kutafuta wakala waliokaribu na wewe


Kama unatumia app za pesa za Makampuni ya mawasiliano, kwasasa unaweza tafuta Mawaka waliokaribu na wewe kwenye eneo ulilopo. Yani hatakama umefika kwenye eneo geni kwako, unaweza fungua app na kuangalia mawakala waliopo kwenye eneo lako na unaweza hata kuwapigia. Kipengele hiki ni kizuri zaidi kwa watu wanaosafiri kwenda sehemu mbalimbali wasizozijua vizuri.

Kubook ndege



Ukitaka kupata ticket za ndege kwa haraka na urahisi, unaweza tumia app hizi pia. Tumewahi zungumzia jinsi ya kubook ndege kwa app ya Mpesa, hivyo jambo hili linaweza kuwa sio jambo geni. Ila kama haujasoma makala iliozungumzia hayo, basi fahamu kuwa unaweza kubook na kupata Tiketi za ndege kupitia app ya Mpesa na app nyingine zenye kipengele cha kulipia ticket za ndege kwasasa.

Kulipia kwenye tuvuti za mtandaoni



Katika tuvuti nyingi ulimwengu huwa zinaweka mfumo wa kulipia kwa kutumia Visa au Mastercard. Mfano; ukihitaji kulipia bidhaa katika tuvuti ya Amazon au AliExpress kwasasa, utahitajika kuwa na Visa au Mastercard. Jambo la kupata Visa au Mastercard limerahisishwa sana kwenye app za pesa za mitandao ya mawasiliano tunayotumia. Unaweza zitengeneza kwa urahisi kupitia App ya Mpesa, Mixx by yas na app nyingine ndani ya dakika 5 tu. Jifunza za zaidi swala hili hapa.

Kusimamia, kuwekeza pesa au Kukopa pesa


Ukitaka kusimamia vizuri pesa zako unazotunza kwenye simu, ni vema ukawa unatumia app maana zimeweka urahisi. Unaangalia Salio la akaunti yako kirahisi na hata kufanya miamla ukiwa nje nchi. Kiufupi usimamizi wa pesa yako unakua ni rahisi zaidi.


Mbali na usimamizi, app hizi kwasasa zinakupa uwezo wa kuwekeza pesa kwa urahisi ili kuizalisha. Ukiachana na kuwekeza, unaweza hata kukopa pia.


Ni hayo tu tuliokuandalia katika makala hii, Endelea kuwa karibu na The bestgalaxy kwa mengine zaidi.

Simulizi ya “Punda” ni mfano mzuri wa kutosikiliza watu katika Maisha

Moja kati ya simulizi ambayo huongelewa sana katika mifano ya maisha ni hii simulizi ya Mume, Mke, na Punda. Kama uijui vizuri simulizi hii, tulia uisome hapa chini;

Kulikuwa na mume na mke waliokuwa wakisafiri kijijini kwao wakiwa na punda. Njiani, walikutana na watu wa aina mbalimbali waliokuwa na maoni yao kuhusu safari yao.

Mume na mke walitembea kwa mguu huku wakiwa wamechukua punda wao akiwa amefungwa kwa kamba shingoni. Walionekana wamechoka, lakini walikuwa wakifurahia mazungumzo yao. Walipokutana na kundi la watu wa kijiji flani, walihisi macho yakiwatazama sana.

“Mna akili kweli? Mna punda lakini mnatembea kwa miguu! Kwa nini msimpande?” mmoja wa watu akasema huku akicheka.

Mume akatazama mke wake na akasema, “Labda wana ongea cha maana hawa. Hebu tubadilike.”

Mume alipanda punda huku mke akitembea pembeni. Baada ya muda, wakakutana na kundi jingine la watu.

“Angalia huyu mwanaume! Anawezaje kumpanda punda huku mke wake maskini anatembea? Hana hata huruma!” mmoja wa wanawake akasema kwa sauti ya lawama.

Mume aliona haya na kushuka. “Basi wewe panda sasa,” alimwambia mkewe.

Mke akapanda punda, alafu mume akaanza kutembea kwa miguu. Njiani, wakakutana na kundi jingine la watu waliokuwa wakifanya kazi shambani.

“Jamani! Angalia huyu mwanamke hana hata aibu. Anampanda punda huku mume wake mzee anatoka jasho akitembea!” mmoja wa wanaume akasema kwa dhihaka.

Mume na mke walitazamana na kuamua wote wapande punda.

Wote wawili walipanda punda na kuendelea na safari yao. Hawakufika mbali, wakaanza kusikia watu wakiwazungumzia tena.

“Hawa watu hawana huruma! Wote wawili wanampanda punda huyu mdogo. Wanataka kumuua kwa uzito wao?” mmoja wa wazee akasema huku akitikisa kichwa chake.

Mume na mke vichwa kikawaka moto, waliona bora wambebe huyo punda mgongoni ili wasisemewe tena. Wakafunga miguu ya punda kwa kamba vizuri na kumbeba kama mzingo. Walipokuwa wakivuka daraja, watu waliwaangalia kwa mshangao na kucheka sana.

“Jamani, angalia hawa wajinga! Wamegeuza mambo. Badala ya punda kuwabeba wao, wao ndio wanambeba punda!”

Kwa aibu, waliishiwa nguvu, punda akaanguka mtoni. Mume na mke wakakaa kimya huku wakitazama punda akizama majini…

Simulizi hii inamaana gani kwenye Maisha?

Simulizi hii inakumbusha kuwa katika Maisha, Haijalishi unafanya nini, watu watasema tu. Unaweza kufanya jambo kwasababu zako nzuri tu lakini wakaangaliwa kwa ubaya. Kiufupi, unapokua na ndoto au mambo mbalimbali unayotaka maishani, maneno ya watu usiruhusu yakuyumbishe au kukupoteza kama ilivyokua kwa wenye Punda.

Ushauri kwa aliesema pesa zake hazioni BONYEZA HAPA>>>

Zingatia haya ili usichokwe na Mpenzi wako

Kuchokwa na mpenzi wako ni mojawapo ya changamoto kubwa ambazo watu wengi hukutana nazo katika mahusiano ya kimapenzi. Wakati mwingine, bila hata kugundua nini sababu ya kuchokwa, mtu anajikuta tu amechokwa. Hili si jambo la kushangaza, kwani mahusiano yanahitaji juhudi, uelewa, na ubunifu ili yaendelee kuwa yenye afya nzuri kwa pande zote mbili(Upande wa Mwanamke na Mwanaume).

Ni kawaida kwa watu kupuuza umuhimu wa mambo madogo yanayochangia uimara wa mahusiano alafu mahusiano yanayumba. Muda mwengine, mambo hayo tukiyafanya kwa kuzidi, yanafanya watu wachokwe kwenye mahusiano.
Kwa bahati nzuri, kuna mambo muhimu ya kuzingatia ili kufanya usichokwe kirahisi kwenye mahusiano. Baadhi ya mambo hayo ni yafuatayo;

Ujumbe wa mapenzi kwa umpendae BONYEZA HAPA>>>

Mambo ya kuzingatia ili usichokwe na mpenzi wako

Kuwa chanzo cha furaha na Amani kwake

Hapa Duniani tukiwa binadamu huwa tunapenda sana kuwa kwenye nyakati za Amani na furaha. Mara nyingi huwa tunapenda na kuwakumbuka sana watu wanaotupa Amani na furaha maishani. Na ni ngumu sana kumchoka mtu anaekupa furaha na Amani maishani, hivyo kuwa mtu huyo kwake. Kuwa mtu ambae anajua kabisa akiwa na wewe anapata amani na furaha.
Hakikisha kunamuda ukiwa nae unaweka lawama, kesi na matatizo pembeni alafu mnafanya mazungumzo ya furaha na Amani.

Mfanye akukose kwa muda flani (Akumiss)


Ni sawa kwa na mpenzi wako pamoja kwa muda mrefu lakini isiwe ni kila mara. Kuna muda inabidi ujiweke mbali nae kidogo ili akukumbuke na kujua umuhimu wako. Wataalam huwa wanasema kitu ambacho huonekana au kupatikana kirahisi hupunguza thamani. Na kwenye mahusiano hii inawezatokea pia.

Kuna muda jiweke busy na mambo yako, usipatikane kirahisi mpaka akutafute. Hii isiwe ni ugomvi, fanya kama kumkumbusha umuhimu wako kidogo kwa kuwa mbali nae alafu jirudi tena kwake kama kawaida. Kwa lugha nyingine tunaweza sema mfanye “Akumiss” kidogo kwa muda alafu kuwa nae karibu tena. Ukiwa unafanya hivi inaweza kuwa ngumu kwa mpenzi wako kukuchoka.

Kuwa na tabia ya kumfanyia asivyotarajia

Kama upo kwenye mahusiano alafu mambo yote unayomfanyia mpenzi wako ni yanayojirudia au yamezoeleka, basi kuna siku unaweza chokwa.
Ni vema ukawa na tabia ya kufanya baadhi ya vitu bila yeye kutarajia.

Usitabilike kwenye baadhi ya mambo katika Tendo au katika Maisha ya kuishi nae kawaida.

Kutengeneza nae mambo yajayo(future)

Mahusiano ya mapenzi bila future, yanawezekana ila huwa yanafika sehemu mnachokana. Yani kama ni Tendo tu ndio huwakutanisha pamoja na mpenzi wako, basi tambua tu kuna siku unaweza chokwa au wewe mwenyewe ukamchoka mwenzako.


Mahusiano ya mapenzi ni pamoja na kuwa pamoja au kushirikiana katika mambo mbalimbali ya kimaisha. Na ili usichokwe, ni vema ukawa na tabia ya kupanga mambo mtayofanya pamoja mbali na tendo. Mfano, naweza panga na mpenzi wako kwenda kwenye sharehe pamoja, kuishi nyumba moja, kununua kitu flani pamoja na hata kukutana tu mupige stori.

Ukizingatia hayo yote, unaweza fanya iwe kungumu kwa mpenzi wako mwanamke au mwanaume kukuchoka. Anaweza kuwa anatamani kila siku uzidi kwa nae kwenye maisha yake.

Hizi ni Website nzuri kwa watumiaji wa iPhone

Ukiangalia ulimwengu wa teknolojia ya sasa, unaona iPhone inabaki kuwa moja ya vifaa maarufu na vyenye ushawishi mkubwa. Kutokana na muundo wake wa kifahari na uwezo wake, iPhone imekuwa chaguo la kwanza kwa mamilioni ya watu duniani kote. Kwa baadhi ya watu iPhone si kifaa cha mawasiliano, ni sehemu ya mtindo wa maisha.

Kila matoleo au kizazi kipya cha iPhone kinaleta ubunifu ambao si tu unarahisisha maisha, bali pia unafanya matumizi ya simu kuwa ya kuvutia zaidi. Kwa kutumia iPhone, unapata fursa ya kufurahia maelfu ya apps kwaajili ya mahitaji tofauti yanayoweza kuwa katika upande wa mawasiliano, burudani na hata uzalishaji/biashara.

Kwa upande wa kupiga picha nzuri; Kamera za hali ya juu za iPhone zinakupa uwezo wa kupiga picha nzuri sana na wengi hupenda iPhone kwaajili ya jambo hilo.

Mbali na Kamera mtumiaji hufurahia huduma za kipekee kama Siri, iCloud, na FaceTime ambazo hufanya utumiaji wa iPhone kuwa wa tofauti na simu nyingine.

Katika makala hii, tutaangazia website au tovuti chache ambazo ni kwaajili ya watumiaji wa iPhone. Hizi ni zile tuvuti ambazo zinaweza rahisisha zaidi baadhi ya mambo kwa mtumiaji wa iPhone.

YouTube channel za kuangalia Movies Bure BONYEZA HAPA>>>

Website/Tuvuti nzuri kwa watumiaji wa iPhone

Apple Support

Apple ni mahali ambapo mtumiaji wa iPhone anaweza kupata suluhu za matatizo mbalimbali ya kifaa cha iPhone. Kupitia Apple support, mtu unaweza badili password ya akaunti ya Apple, kuupdate kifaa chako ili kupata maboresho na mambo mengine.
Apple Support imeletwa na kampuni ya Apple ili kusaidia watumiaji wa bidhaa za Apple kama iPhone na hata bidhaa mbali na iPhone.

Tubi TV

Kwa wapenzi wa movie wanaonatumia iPhone, hii inaweza kuwafaa zaidi. Tubi TV ni tuvunti ambayo inawezesha watu kuangalia Movie bure katika Internet. Kupitia iPhone yako, unaweza itumia tuvuti ya Tubi TV kuangalia maelufu ya movie bila kulipia chochote(Bure).
Huduma hii ya movie inapatikana USA hivyo ukiwa nje ya sehemu husika, hautaweza ipata bila kutumia VPN.

Kwaiyo utatakiwa kupata VPN hata ya Bure kwenye iPhone yako alafu utaunganisha kwenye server za USA kisha ndio utaingia kwenye Tuvuti ya Tubi TV.com
Ukishaingia katika tuvuti, utatakiwa kuifungua tena tuvuti hiyo katika “Desktop view mode”(Washa kipengele cha “Request Desktop view”) ili isikulazimishe kudownload app ya Tubi TV. Usipofanya hivyo, hautafanikiwa kuangalia Movie hata moja.

MacRumors

Hii tuvuti ya MacRumors, inajihusisha na taalifa mbalimbali zinazohusu bidhaa za Apple. Kwakua iPhone ni bidhaa ya kampuni ya Apple, basi habari zake mpya huwa zinapatikana katika MacRumors. Mfano wa taalifa unazoweza kupata kupitia MacRumors ukiwa kama mtumiaji wa iPhone ni mabadiliko yaliofanywa katika iOS, Ujio wa iPhone mpya na mengineyo.
MacRumors sio sehemu pekee unayoweza kupata habari za simu za iPhone lakini ni moja ya sehemu bora za kupata habari muhumu kuhusu simu za iPhone na vifaa vingine vya kampuni ya Apple.

iPhone Photography School

Website ya iPhone Photography School inakuwezesha kunielewa zaidi Kamera ya iPhone. Kwenye tuvuti hii, unaweza pata masomo ya kuitumia kamera ya iPhone kwa ustadi mkubwa.


Wengi huwa tunatumia kamera za simu zetu bila kuzingatia vipengele vya upigaji mzuri wa picha. Katika iPhone, watu wanaweza piga picha nzuri sana lakini wengi kati yao hawajui kwa upana kamera ya iPhone. Kiufupi watu hutumia Kamera ya iPhone kwa mazoea lakini inamambo mengi sana na yanahitaji mtu utenge muda wa kuelewa kila kipengele na kukitumia.

Ni hayo tu katika orodha hii. Unadhani ni tuvuti gani nyingine nzuri kwa watumiaji wa iPhone? Tuandikie kwenye sehemu ya maoni ili kusaidia wengine.

Utataka Tena Au (Simulizi ya Maandishi)

Nilihamia Dar es Salaam kutafuta maisha, nikitegemea msaada wa kaka yangu ambaye hakuwa ameoa. Nilipokaa kwake, sikutilia sana mkazo kujenga maisha yangu. Badala yake, niliweka nguvu kwenye starehe za usiku, yani nikifanya kumbi za burudani kuwa sehemu yangu ya nisioweza kukoswa.

Huko kwenye kumbi, nilikutana na Merry. Mwanamke wa kuvutia, mwenye mwili wa mzuri sana. Uhusiano wetu ulianza kama biashara. Yani nilimpa pesa, naye alinipa penzi. Lakini kadri tulivyozidi kuzoeana, pesa zikawa si muhimu tena. Tulianza kufurahia penzi letu bila malipo, lakini tulikua tunakutana tu katika kumbi za starehe. Hakukuwa na mipango ya zaidi ya starehe.

Baada ya muda, niliona kuwa maisha yangu hayakuwa na mwelekeo ninao uelewa. Nilirudi kijijini kujaribu kujijenga upya. Nilijihusisha na kilimo na nikapata pesa za kutosha. Nikiwa kijijini, nilisikia kwamba kaka yangu ameoa na sasa anaishi na mkewe. Habari hizo zilinipa furaha na msukumo wa kurudi mjini ili kuanza maisha yangu binafsi.

Nilipofika mjini, nilipanga nyumba yangu na kuanza kujitegemea. Kabla ya kumtembelea kaka, niliendelea na starehe zangu maana ndio kitu nilichukua nakupenda sana hapo mjini. Nakumbuka nilipofika tu, Nikawasiliana na Merry ili tukutane kwe starehe tufanye mambo yetu. Lakini Merry aliniambia kuwa ameacha mambo ya zamani na hafiki tena kwenye kumbi za starehe kwakua ameolewa. Nilisikitika, lakini nikajitahidi sana mkushawi ili nipate tu penzi lake mara moja au turudi kwenye penzi letu kabisa. Baada ya mazungumzo marefu, alikubali na akasema atanifuata nyumbani kwangu tu na sio kwenye kumbi za starare tena.
Nilimuelekeza sehemu ambayo anatakiwa aje alafu alipokuaja, nikachukua hapo na kumpeleka ndani kwangu. Alikua ameva nguo nyeusi alafu fupi kiasi cha kuonesha sehemu za juu kidogo ya miguu. Muonekano wake ulikua unavutia sana na mapigo yangu ya moyo yalikua yanaongezeka kwa tamaa tulipoingia ndani. Ni kawaida yake kunichemsha Damu kiivyo maana ni mwanamke mwenye umbo zuri la kuvutia Kila mwanaume.

Nakumbuka tulikaa dakika chache tukiongea mule ndani mwangu kisha tukaanza kufanya kilichotukutanisha. Sauti za Merry za kuimba “Aahh mmh aissh aishii” ndizo zilitawala humo ndani huku tukiwa tunacheza hiyo nyimbo kwa kunesanesa.
Alilala na mimi usiku mzima ili kunifurahisha. Raha za kucheza mziki zilizidi mpaka alipokua anaondoka asubuhi, nilimshawishi aje tena akipata muda na akakubari.

Uhusiano wetu wa kimapenzi uliendelea kwa siku kadhaa tukiwa tunafurahia sana. Lakini moja, niliona ni vyema kumtembelea kaka yangu baada ya kukaa bila kuonana toka niingie hapo mjini. Nilipofika kwake, nilipigwa na mshangao wa ghafla kwasababu nilimkuta Merry akiwa ndiye mke wa kaka yangu!

Macho yetu yalikutana kwa sekunde chache tukaona aibu, lakini tuliweka sura za kutojali kama hatujawahi kuonana. Aibu ilitawala mioyo yetu, lakini hakuna aliyeweza kusema neno. Kila mmoja wetu alijua kwamba siri hiyo haikustahili kufichuliwa. Tangu siku hiyo, ni kama tulikubaliana kuwa kimya na kuacha kila kitu kilichotokea nyuma yetu.
Kuna muda nilikua nawaza “Huyu mke wa kaka huenda sio mtu mzuri… Alikua anawezaje kulala na mimi usiku wakati kaolewa?” Lakini nilikua nikifikilia tena kwa Mimi ndio niliepambana sana kumshawishi aje kunipa penzi wakati ananiambia ameolewa, naamua kuendelea kuwa kimya tu.
Mwisho nilianza maisha mapya, nikijifunza kuwa baadhi ya siri ni lazima zibaki kuwa siri, hasa zinapogusa heshima na furaha ya wengine.

MWISHO

SMS za kumiss Mpenzi wako (Mwanamke au Mwanaume)

Katika maisha ya mahusiano ya kimapenzi, kuna nyakati ambapo hisia za kumkumbuka mpenzi wako zinakuwa nyingi sana. Hali hii hutokea pale mnapokuwa mbali au hata wakati mnakuwa karibu lakini shughuli za kila siku zinawazuia kuwa pamoja. Kumkosa mtu unayempenda kwa muda ni huleta hali ngumu sana hata mnapokua na mapenzi ya dhati. Lakini ni jambo zuri ni kwamba, kuieleza hali hiyo kwa mpenzi wako hufanya ajue umuhimu wake kwako na hata kukupenda zaidi. Yani unaweza kumtumia hata ujumbe wa sms mzuri wa kumueleza jinsi gani umemiss na akafurahi na kujua unamuhitaji.

Mfano; Ujumbe mdogo wa “Nimekukumbuka mpenzi wangu, natamani niwe karibu na wewe” unaweza kubeba uzito wa hisia zako zote na kuonyesha jinsi gani unamuhitaji mpenzi wako. Wakati mwingine, huenda mpenzi wako anajihisi mpweke au hana uhakika wa hisia zako ila akiwa anapata ujumbe wako wa kummiss, anaweza kuwa ni faraja anayoihitaji. Ni jambo dogo kulifanya lakini lenye nguvu ya kuimarisha uhusiano na kuonyesha kwamba unamjali.

Mambo yasiofaa kuwambia marafiki kuhusu Mpenzi wako BONYEZA HAPA>>>

Katika makala hii, tumekusanya orodha ya SMS bora ambazo unaweza kumtumia mpenzi wako kumjulisha jinsi unavyomkumbuka. Unaweza zitumia bura kuleta furaha kwenye mahusiano wako.

SMS za kumiss mpenzi wako

  • Nipo hapa nimetulia ila kila nikifikilia jinsi nafurahia nikiwa karibu yako, natamani nikufuate ulipo. Nakumiss sana mpenzi, natamani niwepo ulipo.
  • We ni ile tamu waliosema “haionjwi” kwasababu mtu akionja hunogewa. Tangu nilipo onja ukaribu wako, nautamani kila mara. Nakumiss sana.
  • Upo mbali mpenzi wangu, lakini moyo haujawahi punguza upendo wako. Bado nahitaji wewe uwe wangu, na Bado nahitaji niendelee kuwa wako.
  • Unauzuri wa kushangaza kama nyota angani. Nikiangalia nyota na vitu vingine vyenye uzuri wa kushangaza, huwa nakukumbuka sana wewe.
  • Kuna muda unaweza waza eti nitakuacha na maumivu niende mbali. Huko mbali nafika vipi bila wewe? Moyo unakuhitaji kila dakika. Hata sasa nimekumiss nakuwaza wewe…
  • Nakupenda sana. Tafadhali njoo unijaze furaha ya uwepo wako Kipenzi. Moyo wangu umemiss zile hisia za kuwa karibu yako.
  • Huku Moyo uliokupenda unanisumbua kuhusu wewe. Umekukumbuka sana mpenzi wangu, natamani uje useme nao kwa ukaribu. Umechoka, uhitaji kukuona wewe Tabibu.
  • Njoo niyaone yale macho yako mazuri Mpenzi. Njoo unilishe kile chakula mimi hupenda. Nimekumiss mpaka onaona giza, siioni furaha bila ya wewe ninaekupenda.
  • Kile na hitaji nikiwa na huzuni, ni wewe. Na hata kile nile nahitaji nikiwa na furaha, ni wewe. Kiufupi, maisha yangu nayaona ni mzuri nikiwa na wewe. Nimekumiss mpenzi wangu.
  • Nakupenda na ninakutaka karibu nami zaidi ya kitu chochote ulimwenguni. Nakuhitaji zaidi ya chupa ya maji jangwani. Uko wapi mpenzi?

Sms hizi za kumiss ni nzuri kwa walio kwenye ndoa (Mume au mke) na hata kwa wasio kwenye ndoa (Wapenzi). Kikubwa unatakiwa kuchagua sms au ujumbe unapenda na hali yenu. Na pia ni muhimu kujua ni wakati gani wa kumtumia sms huyo umpendae.

Earphone za Bluetooth na Earphone za waya: zipi Bora kwako?

Ukiwa unapenda kusikiliza muziki mzuri kwenye simu yako, Earphone zinaweza kukufanya ufurahie mziki zaidi. Earphone zinaweza kukufanya uzingatie unachokisikiliza na pia zinaweza kukusaidia katika kusikiliza vitu usivyotaka wengine wasikie. Ni vifaa vizuri kwa maisha ya sasa na watu wengi wanatumia Duniani.

Katika kutumia Earphone katika kipindi hiki, unakua na machaguo mawili ya Earphone ambazo utazitumia. Chaguo la kwanza ni Earphone za Bluetooth (wireless) na chaguo la pili ni Earphone zilizo na waya. Katika machaguo haya mawilli, wengi hukimbilia katika hizi Earphone za Bluetooth kwa kuona ni zakisasa kwasasa lakini uhalisia ni kwamba Earphone zote ni nzuri ila inategemeana na mahitaji au matumizi yako. Yani kuna namna Earphone za Bluetooth zikawa mbaya au nzuri kwao na pia Kuna namna Earphone za waya zinaweza kuwa mbaya au nzuri kwako.

Hapa chini, tunajaribu kukufungua ili uweze kujua namna ambavyo Earphone za Bluetooth na za waya zinaweza kuwa nzuri au mbaya kwako.

Kutengeneza au kurekodi nyimbo kwa kutumia simu BONYEZA HAPA>>>

Kati ya Earphone za Bluetooth na Earphone za waya, zipi ni Bora kwako

Katika chaji


Earphone za waya hazimalizi chaji kwenye simu. Unaweza tumia earphone za waya hata kama betri ya simu ina asilimia 3% na kusiwepo na ongezeko kubwa la kasi ya betri kuisha chaji. Unashauriwa kutumia Earphone kusikiliza music pale unapohitaji betri ya simu yako isipungu sana.

Earphone za Bluetooth huwa zinamaliza chaji maana hutumia Bluetooth kama muunganiko. Ingawa simu za kisasa nyingi kwa sasa huwa jitahidi kutunza chaji unapomtumia Bluetooth, lakini Bado hauwezi fananisha na Earphone za waya. Earphone za waya ni Bora kwenye upande wa kutunza chaji ya simu yako na wala hazihitaji kuzichaji ili kuzitumia.

Kubebeka na kutunza


Earphone za Bluetooth ni rahisi kutunza au kubebeka. Kama unatumia hizi Earphone, utakuwa na uwezo wa kuzitunza sehemu mbalimbali kwa urahisi na hata unapozitumia, hukaa kwenye masikio vizuri bila kusumbuliwa na mawaya. Hazikuzuii kufanya mambo yako; Unaweza weka simu mbali huku ukiendelea kusikiliza mziki kwa uhuru sehemu nyingine.

Earphone za waya, haziwezi kukuweka huru kwenye mambo yako. Kutokana na waya, mtumiaji unatakiwa kuwa na mipaka ili usikate waya. Hautatakiwa kwenda mbali sana na simu alafu pia hautatakiwa kufanya mambo yatayokaya hiyo waya.

Ubora wa Sauti


Earphone za Waya hazina tatizo la kuchelewa kwa sauti. Ukihitaji mziki mzuri zaidi na wenye ubora toka kwenye simu yako, unashauriwa kutumia Earphone za waya. Ila hakikisha zipo kwenye bora pia ili kupata matokeo mazuri. Na kwa watu wanaojihusisha na utengenezaji wa Madhuri yanayohusisha Muziki, wanashauriwa zaidi kutumia Earphone kwenye kazi zao.

Earphone za Bluetooth huwa zinatatizo la kuchelewa kwa Muziki unaposikiliza. Mbali na hiyo, mziki wake sio halisi, hupitia kwenye mchakato unaoweza ondoa uhalisia wa Muziki (Mfano: kuongeza Bass).

Mpaka hapo, unaweza kuwa unahisi Earphone Bora kwako ni zipi? Endelea kuwa karibu na The bestgalaxy kwa Mambo mengine. Usisahau kuwa karibu na sisi pia kwenye mitandao ya kijamii.