YouTube ni Moja ya app maharufu sana Duniani. Inatumiwa na ma billion ya watu toka nchi mbalimbali hapa ulimwenguni. Hapa Tanzania kunabaadhi ya watu huisi YouTube inajihusisha na videos lakini sio “Movies”. Ukweli ni kwamba YouTube ni moja ya app ambazo zinajihusisha na movies kama app nyingine maharufu katika upande wa Movies.
YouTube inakipendele cha movies kiitwacho “Movies & Shows” kinachokuruhusu wewe kama mtumiaji wake kuangalia movies zozote unazozitaji. Lakini unachotakiwa kujua kuhusu kipengele hiki cha movies ni kwamba, zipo movie za bure na pia movie ambazo lazima ulipie au ununue ndio uziangalie.
Kwa bahati mbaya, ukiwa Tanzania uweza kunagalia movies za kulipia tu katika kipengele hiki. YouTube bado haijaruhusu kipengele hiki kitoe movie za bure kwenye baadhi ya nchi, ikiwemo Tanzania. Kwaiyo ukiwa Tanzania huwezi kuangalia movies za bure kwenye kipengele Cha movie YouTube.
Lakini hii haiwezi kukuzuia kabisa kukiona kipengele hiki na movies zake za bure. Unaweza Tumia VPN kukiona na kuangalia movies zake za bure bila tatizo. Unachotakiwa kufanya ni kufuata hatua zifuatazo:
Download VPN kwenye simu yako.
Ifungue VPN, chagua Server yoyote ya “USA” kisha iconnnet
Ingia YouTube Kisha gusa “Library” alafu chagua “Your Movies and Shows“
Baada ya hapo gusa “Free with Ads“
Ukishafanya hivyo utakua tayari upo kwenye movies za bure za kipengele Cha movies Cha YouTube. Itakua ni juu yako kuchagua ipi uiangalie.
Mpira wa miguu ni mchezo maarufu zaidi duniani. Hapa tutajadili kuhusu magemu ya mchezo huu maarufu. Katika ulimwengu huu, mbali na kutazama mechi ya moja kwa moja za mpira wa miguu, kuna watu wengi wanaopenda kucheza magemu ya mpira au Kandanda. Kuna ambao wanapenda kucheza magemu kupitia vifaa vya kucheza magemu kama vile, Playstation . Na watu wengine hutumia simu kucheza magemu ya mpira wa miguu.
Unaweza pia kuwa mmoja wa watu wanaotumia simu kwenye michezo ya mpira wa miguu ndio maana uko hapa. Ikiwa wewe ni mmoja wao basi hapa ni sahemu nzuri kwako. Tunakupa orodha ya gemu 5 bora za Mpira unazoweza kucheza kwenye simu (Android) Bila kupoteza muda wako, sasa twende moja kwa moja kwenye orodha ya magemu bora ya mpira au soka kwa simu ya Android.
FIFA Mobile ni mojawapo ya magemu bora ya Soka ya Android kwa mashabiki wa soka. Gemu hili limetolewa na EA. Huchezwa Kwa kutumia Data, yaani huitaji internet. Katika gemu hili unaweza kujenga timu yako ya ndoto na kuanza safari ya soka. Na unaweza kuijenga kwa kusajili superstars unaopenda katika soka. Linakuruhusu kucheza au kushindana na watu wengine mtandaoni.
Gemu hili hapo awali ulilitwa “PES” lakini sasa ni “eFootball“. Kwa hivyo, ikiwa wewe ni moja ya watu ambao tayari umecheza magemu ya PES, basi hii pia ni PES lakini PES imebadilishwa jina kuwa eFootball. Kwenye orodha hii ya mgemu bora ya mpira ya simu za Android, tunaongeza gemu hili kwasababu ni gemu nzuri. Muonekano kwenye gemu hili ni mzuri. Ili kucheza gemu la eFootball kwenye simu ya Android unahitaji kutumia intaneti. Kwa maneno mengine tunaweza kusema gemu hili hutumika Data japo ni bure kupakua na kucheza. Simu yako lazima iwe na zaidi ya 2G RAM, Android 7 na 3.3GB ya nafasi ili kuwa na gemu la eFootball bila matatizo. Pia ikiwa na CPU 1.5 GHz au zaidi itaifanya ifanye kazi vizuri zaidi.
3. Dream league Soccer.
Dream league Soccer (DLS) ni gemu lingine la mpira au soka linaliweza kucheza kwenye simu simu. Gemu hili lilitolewa na First Touch games limited. Katika gemu hili unaweza kuunda timu yako ya ndoto na kusaini wachezaji wako unaowakubali wa mpira wa miguu kwenye timu yako. Internet huitajika ili kucheza gemu hili kwa sababu ni DSL ni gemu linalihitaji data kulicheza. Lakini kulipakua na kuicheza ni bure ingawa ukihitaji, unaweza kununua baadhi ya vitu ndani ya gemu kwa pesa halisi.
Total Football ni gemu lililotolewa mwaka 2022 (Beta). Gemu hili huchezwa Kwa kutumia Data/internet japo ukiwa Haina data unaweza kunavitu unaweza kuvifanya kwenye gemu na vikakufurahisha. Studio Vega Private Limited ndio wamelitoa gemu hili. Kwenye gemu hili unaweza kuunda timu yako, kusaini wanasoka mashuhuri kisha kuipeleka timu yako kileleni. Jumla ya mchezo wa Kandanda ni mzuri sana na ni bure kuucheza na Kupakua kwenye simu ya Android.
5. Pro League Soccer.
Ikiwa unataka gemu zuri la Android ambao haliwezi hata kuchukua nafasi kubwa ya simu, gemu hili ni kwa ajili yako. Pro League Soccer ni gemu la simu la mpira was miguu ambalo ni dogo kuliko tulioyataja juu. Unaweza kuona gemu hili ni tofauti na magemu kama vile FIFA au eFootball lakini inafurahisha sana kulicheza. Linakuruhusu kuandika majina ya wachezaji na hata kutengeneza Jezi unavyotaka. Mojawapo ya jambo zuri ni kwamba, gemu la hili linaweza kuchezwa bila internet.
Hivi ndivyo tunamaliza orodha hii. Lakini kumbuka kuwa kuna zaidi ya magemu ma 5 bora ya mpira kwa simu za Android ingawa tume orodhesha magemu matano pekee.
Ikiwa unataka kujua zaidi kuhusu magemu ya simu na vitu vingine basi usisahau kutembelea tovuti hii kila siku. Daima tuko hapa kukufahamisha mambo mengi.
Kama umekua ni mtu unaesumbuliwa na simu katika masuala ya chaji, hasa kwenye upande wa simu kuchelewa kujaa pale unapoichomeka chaji basi nakujuza ni vitu gani ambayo unaweza kufanya ili kuifanya simu yako ijae kwa muda mfupi sana.
Lakini kabla ya yote ningependa kukukumbusha kuwa endapo utakua na maswali kuhusu jambo lolote linalokutatiza kuhusu simu yako, hakikisha unawasiliana na sisi. Pia usiache kufuatilia Kila post mpya ili kujifunza maana vitu vingi zaidi vipo mbeleni. Zifuatazo ni njia ambazo ukizifanya unaweza ifanya simu yako ijae chaji kwa haraka sana.
Kuizima simu wakati wa kuichaji kunaweza ifanya simu ijae haraka sana kuliko ikiwa imewashwa. Ni vema sana kuitumia njia hii wakati ambao unahitaji simu ijae haraka na pia hufanya betri kujaa kwa utumivu na hii huimarisha hata betri lako. Lakini tatizo la njia hii ni kwamba husababisha mtu usiwe hewani hivyo basi ni vema kuitumia pale unapokua unajua kutokuwa hewani kwako hakutokupunguzia chochote.
Airplane mode hupatikana sehemu ile ya juu inayoshushwa pindi tunapowasha Data. Huwakilishwa na alama ya ndege za usafiri. Ili kuiwasha utatakiwa kuishusha sehemu ya juu ya simu yako kisha gusa alama yake kama unavyogusa pindi unapowasha Data. Njia hii hufanya simu ijae haraka mno lakini tatizo ni hautaweza kupokea wala kupiga simu maana Airplane mode ikiwashwa huvifunga vitu hivyo.
3. Washa power saving mode
Hii inaweza kuwa ni app ambayo huzizima baadhi ya app ili kupunguza matumizi ya chaji. Hupatikana kwenye arodha ya app ulizonazo au katika sehemu ya juu ya simu (Mara nyingi huwakilishwa na alama ya betri ilioambatana na alama ya jumlisha). Uzuri wa kutumia njia hii ni kwamba, utaweza kupiga au kupokea simu bila tatizo huku simu yako ikiendelea kujaa kwa kasi. Lakini simu nyingi za kisasa haziruhusu kuwasha power saving mode wakati simu ikiendelea kuchaji. Sio tatizo, unaweza pakua power saving mode app itakayofanya kazi hii kutoka Playstore. Natumani unaelewa jinsi ya kufanya simu ijae chaji haraka. Endelea kuwa nasi kujifunza vitu vingi zaidi.
Kama ni mtumiaji wa simu za smartphone unatakiwa kuwa makini sana katika matumizi yako ya smartphone maana ukiitumia smartphone yako vibaya unaweza kujikuta jela au unaweza kuwa kwenye wakati mgumu kwa kupoteza vitu vyako vya msingi na heshima kwa jamii. Leo nimekuandalia baadhi ya vitu ambavyo unapaswa kuvizingalia katika kutumia smartphone yako. Tutazungumzia vitu vichacheche tu, vingine tutaangalia katika makala nyingine. Lakini Kabla ya yote ningependa kukushukuru Kwa kufuatilia “The Bestgalaxy” na nakusihi usiache kufuatilia ili kujifunza vitu vingi zaidi.
Bila kupoteza muda hebu tuangalie ni vitu gani usifanye katika matumizi ya simu yako…
1. Usijichukue picha za utupu na kutunza kwenye simu yako.
Kama ni mtu unaependelea kujichukua picha za utupu kwa makusudi na kuzitunza basi hakikisha unajiweka tayari kiakili kuwa hata zikivuja hazita kushtua wala kukuumiza. Kumekua na uvujaji mkubwa wa picha/video za utupu na ukweli ni kwamba asilimia kubwa ya watu wenye picha au video hizo hawajui ni kwanini picha hizo zimetoka nje ya simu zao. Kitu muhimu kukijua ni kwamba si vizuri kuweka picha au video hizo kwenye simu maana kunavitu vingi sana ambavyo vinaweza pelekea kuvuja kwa vitu vyako.
2. Usiingize app nje playstore hovyo hovyo.
Wengi tumezoea kuingiza app tunazozipenda kupitia playstore lakini kuna baadhi huwa tunaingiza tu yaani mtu katuma kwenye group la WhatsApp, basi unajaribu kuiingiza au umesearch Google bila kuangalia ata site inaaminika vipi, unaiingiza kwenye simu yako. Kitu muhimu cha kujua ni kwamba kuna app ambazo ukiingiza kwenye simu yako tu huwa zinabeba taarifa zako kwenye simu na kuzituma kwa huyo mtaka taharifa za watu tena kwa kutumia bando lako bila wewe kujua. App hizi hupatikana nje ya Playstore hivyo basi katika kuingiza app nje ya Playstore hakikisha sehemu unayotoa app unaiamini na inaaminika pia.
3. Usisambaze taarifa au link usizozijua kiundani. Kama ni mtumiaji mzuri wa simu na mitandao nadhani umewahi fanya kitendo cha kusambaza link au ujumbe flani ili upata kituflani lakini mwisho ukagundua ni uongo. Sasa unadhani uliowasambazia walikuchukuliaje? na ulichokisambaza kingekua kinahusisha utapeli, unadhani tapeli wa hao uliowasambazia angekua ni nani kama si wewe? Usipendelee kusambaza ujumbe au tahalifa usizo na uhakikanazo na wala usiwe na tamaa na vitu vya bure mitandaoni, utaibiwa alafu unaonekana wewe ndio mwizi.
4. Usisahau taarifa za Email yako wala kuzigawa.
Wewe ni mmoja kati ya watu wasio jua Email zao au password zakuingilia katika email zao? Naweza kusema, kwasasa Email ni kitu cha msingi kuliko simu unayotumia. Email yako ni utambulisho wako katika sehemu mbalimbali pia email husaidia kupata vitu vyako vya msingi vilivyopo kwenye simu endapo simu yako itaibiwa au kuhalibika ghafla. Kwakutumia email yako utaweza itafuta simu yako ikipotea na kutambua mahali ilipo. Email hurahisisha sana mambo maana unaweza ukawa umeibiwa simu au imezimwa ghafla lakini ukawa unavitu vyote muhimu kama picha zako,video na majina ya simu kwa kushika Email yako na password yake kichwani mwako (Kama uliseti hivyo).
Tambua kuwa ni muhimu kujua Email yako na password yake na kamwe usimpatie mtu password maana utakua umempa tahalifa zako na akiwa mjanja atakupekua mpaka vitu unavyo search Google na kujua uwezo wako unaishia wapi.
Simu kuingia maji Ni moja ya mambo ambayo hutokea katika shughuli zetu za Kila siku. Jambo hili huogopesha sana maana husababisha mpaka baadhi ya simu kupata matazizo au kutowaka kabisa. Hatuwezi zuia simu zetu kuingia katika maji maana hutokea Kama ajali, lakini tunaweza zuia simu zibaki salama yaani zisiwe na matatizo yoyote baada ya kuingia kwenye maji.Kama simu yako imeingia maji na unahitaji iwesalama basi fanya mambo yafuatayo;
Baada ya simu kuingia maji unatakiwa kuhakikisha aiendelei kuwaka. Izime bila kupoteza muda maana ikiendelea kuwaka maji yalioingia yatasababisha vitu vya ndani ya simu hiyo kuharibika.
2. Chomoa betri
Kama simu yako inachomoka betri hakikisha unachomoa betri na kuliweka pembeni ya simu ila kama simu yako si ya kuchomoka betri, Fanya kuichoma line au memory Kisha kimbia moja kwa moja kwa fundi ili aifungue na kutenganisha vitu ili ikauke Kwa uhakika.
Chomoa line ya simu,Memoy na ikiwezekana nenda kwa fundi aliopo karibu na wewe ili aifungue ibaki wazi na kukauka kirahisi. Baada ya kuiweka wazi unatakiwa kuiweka sehemu kavu kwa muda mrefu mpaka itakapokauka kabisa.
Zingatia: usijaribu kuiwasha simu kwa kuijaribu kabla ya kufuata hatua hizi!
Ukweli kuhusu mchele: Watu wengi huweka simu zao katika mchele wakiamini simu zao zitapona lakini kitu cha muhimu kukijua ni kwamba, mchele ni unaweza kukausha maji lakini Kuna uwekano wa asilimia 4 hadi 1 ya maji yalioingia kubaki ndani ya simu na kuleta matatizo ambayo yatakuja kuonekana mbeleni. hivyo kabala ya kuweka huko unatakiwa kufuata hatua hizi pia.
Kama itakua si maji ila vimiminika vingine: kama simu itangia katika pombe,Maji ya chumvi na vimiminika vingine, utatakiwa kuzima na kutoa betri kisha Kifungua nakuisafisha au kuifuta na kitambaa maana usipofanya hivyo baadhi ya vimiminika vikikaukia ndani ya simu, huozesha baadhi ya vitu vilivyo ndani ya simu (ukishindwa ni bora upeleke kwa fundi).
Nyongeza: Kuna baadhi ya simu zimeundwa kutoathiliwa na maji kabisa(Water proof). Yani hata ikidumbukia kwenye maji huwa maji hayaingii ndani ya simu. Lakini pia kunasimu ambazo zimeundwa kuzuia maji Kwa muda flani au maji ya joto flani(water resistant) lakini hazuii Kwa asilimia 100%. Simu hizi unaweza zidumbukiza kwenye maji dakika Moja au mbili na kuzitoa bila tatizo. Mara nyingi masharti yake ni maji yasiwe joto na usizidishe muda.
Pengine tayari uweishaona baadhi ya watu wakiwa wanatumia Katuni zilizofanana na wao katika kukomenti na hata kwenye profile picha zao za Facebook. Hao Katuni wanaowatumia huitwa “Avatar”. Avatar wapo mpaka katika mitando kama Instagram na Snapchat pia. Avatar katika Facebook in Katuni ambae hutumika kama muwakilishi wako. Yani kwamfano unataka kutuma picha kwenye komenti inayoonesha unacheka, unweza tu Kutuma picha au stika ya Avatar akiwa anacheka.
Ili kuwa na avatar katika Facebook ni lazima umtengeneze. Tena Avatar utakemtengeza anatakwa afanane na wewe maana ni muwakilishi wako katika Facebook.
Jinsi ya kutengeneza Avatar kwenywe Facebook
Kutengeneza Avatar ni rahisi tu, hauitaji ujuzi sanaaa. Kwanza Facebook wenyewe wanataka Kila mtu awe na avatar wake kwaiyo wamekaka urahisi katika kutengeneza Avatar. Kama unahitaji kutengeneza Avatar basi unaeza fuata hatua zituatazo:
Fungua app yako ya Facebook
Gusa vimistari vitatu kisha gusa jina lako utakaloliona juu baada ya kugusa vimistari.
Abaada ya kufanya hivyo utatua katika Ukurasa wa profile yako. Achana na vitu vyote hapo, tafuta kisehemu kilichoandikwa “Avatars” na uguse.
Ukishagusa unapelekwa sehemu ya kumtengeneza Avatar wako sasa.
Kumtengeneza Avatar ni rahisi tu, utakua unachangua rangi rake,macho,nguo na muonekano Kwa ujumla.
Ukisha maliza kumtengeneza utagusa batani ya blue ilioandikwa “Done“.
Kwa kufanya hivyo utakua tayari una Avatar wako katika Facebook. Lakini unachotakiwa kujua ni kwamba Avatar ni kitu kidogo lakini kikubwa sana. watakua wanatumiaka sana na binadamu katika miaka ijayo kuliko sasa. Tutakuja kuzungunzia kuhusu hili siku za mbele.
Rolf Bochholz ni mjerumani alieingizwa katika kitabu cha rekodi za dunia (Guinness World Record ) Kama mtu aliefanya mabadiliko mengi zaidi kwenye mwili wake. Mjerumani huyu anatumia jina la @robuchholz katika Instagram.
Rolf amefanya zaidi ya mabadiliko 516 katika mwili wake ikiwemo kuutoboa mwili wake,kuchora tattoo na pandikiza nyama katika paji lake la uso zinaonekana kama mapembe. Ametoboa vitobo vingi sana kuzunguka mdomo wake, katika pua na pajilake la uso ambayo huvimia kuweka vipuri. Anatattoo nyingi sana katika mwili wake na pia amepandikiza nyama upande wa kulia na wakushoto wa paji lake la uso zinazomfanya aonekane kama ni mtu mwenye mapembe.
Rolf Buchholz alianza safari yake ya kufanya mabadiliko ya mwili wake akiwa na umri wa miaka 40 ambapo alianza kwa kuchora tattoo na kujitoboa vitobo kwaajili ya kuingiza vipuri. Rolf anaamini kuwa mabadiliko anayoyafanya katika mwili wake hayambadilishi yeye kwa chochote maana unaobadilika ni mwili tu na si yeye. Pamoja na kufanya mabadiliko zaidi ya 516 katika mwili wake lakini hajatosheka hata kidogo.
SUKARI YA DADA ni simulizi inayomuhusu Kijana ambae alienda Dar es salaam kwaajili ya kufanya kazi za ndani baada kutofanya vizuri kidato cha nne. Kwenda huko ilikua ni njia pekee alioiona itamsaidia maishani kwa wakati huo lakini katika kuelekea anapohitaji, anakutana na changamoto nyingi sana kutokana na ujana. Imesomwa na maelufu ya watu mpaka sasa.
Inavipande 17 vinavyo burudisha na kuelimisha unaposoma mwanzo hadi mwisho. Lakini unapomaliza kuisoma simulizi hii mpaka mwisho, unaweza soma simulizi nyingine mbili ambazo ni UTAMU WA JUMLA na MZIGO WA WAKUBWA.
Kiufupi SUKARI YA DADA, UTAMU WA JUMLA na MZIGO WA WAKUBWA ni Simulizi tofauti ila zinauhusiano unaokupa picha moja nzuri sana ukiwa kama msomaji. Yani ukisoma zote 3 unapata picha ya simulizi moja kubwa sana yenye vipande 41.
Baadhi ya watu husema ni simulizi zilizoandikwa kiufundi na maajabu. Sijui wewe ukizisoma utazipa jina gani ila Ukihitaji kupata simulizi hizi, unaweza kuwasiliana nasi tukakutumia kwa njia ya WhatsApp. Gusa kitufe hapa chini kuwasiliana na sisi kwa njia ya WhatsApp. Au piga 0715233405 muda wowote kwa mahitaji ya simulizi au maelezo.
Unaweza pata ukiwa Tanzania na hata nje ya Tanzania. Haziruhusiwi kusomwa na watu wenye umri chani ya miaka 18. Hii ni kwasababu zimekusanya lugha na mafundisho kwaajili ya walio kwenye kigezo cha umri huo.
Miongoni mwa simulizi zinazopendwa kusomwa kwa sasa ni Sukari Ya Dada, Utamu Wa Jumla, na Mzigo Wa Wakubwa. Hadithi hizi tatu, zilizochapishwa kupitia The Bestgalaxy, zinafuatilia maisha ya vijana waliokumbwa na changamoto mbalimbali za maisha na mapenzi.
Kilicho cha kipekee kuhusu simulizi hizi ni kwamba zinahusiana. Wahusika wanaweza kuonekana zaidi ya mara moja katika hadithi tofauti. Kwa mfano, mhusika mmoja katika Sukari Ya Dada anaweza kutajwa au kuhusika pia katika Utamu Wa Jumla au Mzigo Wa Wakubwa. Hadithi moja inaendelea pale nyingine ilipoishia, au huonyesha upande mwingine wa maisha ya baadhi ya wahusika wale wale.
Kwa hiyo, hizi si hadithi tatu tofauti tu โ ni sehemu za simulizi moja kubwa inayoonyesha maisha ya vijana wa sasa kwenye mazingira yenye changamoto nyingi.
1. Sukari Ya Dada: Ndoto za Mjini na Maisha Halisi
Simulizi ya Sukari Ya Dada inamfuata kijana aliyehamia Dar es Salaam baada ya kushindwa mitihani ya kidato cha nne. Akiwa hana elimu ya kutosha wala msaada wa kifamilia, anajikuta akifanya kazi za ndani. Hapo ndipo anapoanza kukumbana na vishawishi na maisha ya mapenzi ambayo hatimaye yanamfanya kutambua mambo mengi kuhusu dunia na watu. Hadithi hii inaangazia namna vijana wengi wa kike na kiume wanavyoingia mijini wakiwa na matumaini makubwa lakini wakikumbana na uhalisia wenye changamoto nyingi.
2. Utamu Wa Jumla: Mapenzi, maisha na Mafanikio
Hadithi hii ni mwendelezo wa maisha ya baadhi ya wahusika kutoka Sukari Ya Dada. Inamfuatilia kijana kutoka Tabora anayejiunga na chuo jijini Dar es Salaam kusoma biashara. Urafiki wake na Jimmy, mwanafunzi mwenza, aliefungua mlango wa maisha ya starehe, wanawake, na biashara zisizo rasmi wakiwa chuo. Hii ni simulizi inayoangazia mambo mbalimbali ambayo kijana ambae ni msomi wa kisasa ameyapitia katika kujitambua kwakeupande wa mahusiano na maisha.
3. Mzigo Wa Wakubwa: Majukumu
Mzigo Wa Wakubwa inahusiana moja kwa moja na simulizi za awali, Sukari Ya Dada na Utamu Wa Jumla. Hadithi hii inamuhusu kijana mwinginetoka Tanga anaeinjia mjini na kufunzwa mengi kuhusu maisha na mahusiano. Inatoa pia sehemu za maisha ya wahusika kutoka simulizi hizo nyingine, inapitia mambo mbali mbali kuhusu maisha yao, hatua zao na changamoto wanazokutana nazo katika upande wa mahusiano na mapenzi.
Hitimisho:
Kwa mashabiki wa fasihi simulizi, Sukari Ya Dada, Utamu Wa Jumla, na Mzigo Wa Wakubwa ni kazi ambazo hazifai kupuuzwa. Zinabeba burudani na mwanga juu maisha ya kweli ya vijana wa leo. Ni hadithi za kujifunza, kufikiria, na kuburudika.
Kama una YouTube channel na unabambana jinsi ya kuikuza na kuanza kulipwa basi hii ni kwaajili yako. Ili mtu aanze kulipwa YouTube inabidi awena vigezo vya kuanza kulipwa. Vigezo viwili muhimu na vigumu kwa baadhi ya watu ni:
Video zako ziwe zimeangaliwa kwa masaa 4000.
Uwe na Subscribers 1000 au zaidi.
Ukiachilia mbali vigezo hivyo unatakiwa pia kuwa na video ulisotengeneza mwenye. Ukiwa na vigezo hivyo unaweza kuomba YouTube na waanze kukulipa.
Sasa wewe kwenye YouTube channel yako unavigezo hivyo?
Kama vigezo vya Subscribers 1000 na Masaa vimekua ni vigumu kwako basi sisi tutakusaidia kupata vigezo hivyo kirahisi bila kupoteza muda. Tunaweza kuoneza Subscribers 1000 na Masaa 4000 ndani ya siku tatu TU kwenye Channel yako ya YouTube. Na tukikuongezea utakua na uwezo wa kuomba YouTube wakulipe bila Tatizo.
Tumeleta njia hii kama bure tu Kwa watu wanao pambana kwenye YouTube. Ila itabidi ulipie ghalama ambazo tutatumia kukutimizia hivyo viwango.
Kama unataka subscribers 1000 ni Tsh 150,000 tu. Masaa wanayotaka YouTube ni 4000. Sisi tunafanya kuongeza masaa 1000 Kwa Tsh 37,000 tu. Yani kutaka yote 4000 utagalamia Tsh 148,000 tu.
Unaweza kuwa unaineza masaa 1000 Kila mwezi,. Yani Kila mwezi Tsh 37,000…
Kwaiyo hapo ni wewe tu nakuanza kulipwa. Na ukumbuke kua baada ya kuanza kulipwa utakua unaendelea kuongeza Subscribers huku ukiwa unakua Hela ya kazi unayoifanya. Na YouTube channel yako inapanda thamani kwani hata ukitaka kuiuza utauza bei kubwa maana inalipwa na YouTube.
Kama unahitaji kufanyiwa wepesi huu basi tucheki WhatsApp Kwa kugusa kitufe hapa chini. Tutakushauri pia.
Mahali hapa watu wajanja hujifunza vitu mbali mbali kuhusu teknolojia, mapezi na maisha kiujumla. Nikukumbushe tu kuwa unaweza swali, maoni au ujumbe wako kwenye WhatsApp Kwa kugusa HAPA>>>
Mbali hayo pia unaweza jiunga nasi kwenye WhatsApp tukawa tunataalifu kwa njia ya WhatsApp kuhusu vitu vitu vipya tunavyovitoa kwaajili yako. Ukitaka kujiunga na huduma hii, save Namba hii: 0622 586 399 Kwenye simu yako Kisha itumie ujumbe “Niunge na The Bestgalaxy kwenye Whatsapp”
Njia rahisi ya kuipata website hii ni kuiweka kama app kwenye simu yako. Unaiweka vipi? Fuata maelekezo yafuatayo:
Nenda kwenye Ukurasa wetu wa kwanza kabisa Kwa kugusa HAPA>>> Kisha kutakua kama picha inavyoonekana hapa chini๐
Gusa vidoti vitatu vilipo upande wa juu wa app yako. Kama jinsi inavyoonesha picha hii๐
Baada ya kugusa zitakuja chaguzi nyingiii. We gusa sehemu ilioandikwa “Add to home screen” kama inavyoonesha picha hii ๐
Baada ya kufanya hivyo, gusa Nemo “Add” kama picha inavyoonekana hapa chini ๐
Ukisha gusa add app yetu itakua katika simu yako kama unavyoona hapa chini ๐
Kwa kufanya hivyo utakua unauwezo wa kutembelea mahali hapa kirahisi kabisa. Usisahau kuwasiliana nasi na kutujuza mambo gani unahitaji zaidi toka kwetu.
Unaweza soma maelezo zaidi kuhusu the bestgalaxy hapa>>>>