All posts by Admin

Fanya haya kabla simu yako haijaibiwa ili kuipata ikiibiwa

Kuibiwa simu(Smartphone) ni Jambo ambalo karibia kila mtu hapendi limtoke lakini huwa linamtokea tu pasipo kutarajia. Ukiwa bado upo na simu yako unatakiwa kuandaa mazingira ya kuipata kirahisi pindi itakapoibiwa. Ili kuipata simu iliobiwa unatakiwa kuwa na taalifa ambazo zitatumika katika kufanikisha zoezi la kuitafuta simu yako. Taalifa hizo ni pamoja na namba za IMEI za simu.

Jinsi ya kufanya simu isiishe chaji haraka GUSA HAPA>>>


Kila simu huwa na namba zake za IMEI na endapo utaenda polisi ili wakusaidie kutafuta simu yako basi utahitajika kuwapa namba za IMEI za simu ilioibiwa ili kufanikisha upatikanaji wake. Hivyo ni muhimu kuwa na namba za IMEI za simu zetu ili tukipoteza tuzipate kirahisi. 


Sasa unachotakiwa kufanya kabla simu yako haijaibiwa ni kwenda katika sehemu ya kupiga simu alafu piga namba  *#06#  Kisha zinakili katika karatasi namba(IMEI) utakazoletewa na utunze karatasi hilo kwenye vitu vya muhimu ili lisipotee kirahisi.

Kama utakuja kupapoteza simu yako, namba hizo zitatumika kuipata simu yako pindi utakapo peleka swala lako polisi. Pia kumbuka kutunza na lisiti ya ununuzi wa simu.

Ukiona dalili hizi Jua Account yako ya Facebook  imedukuliwa na si salama GUSA HAPA>>>>

Jinsi ya kufanya simu ijinunulie bando la internet (usichome pesa zako kununua bando)

Watu wanaotumia smartphone mara nyingi hutumia pesa nyingi sana kwenye bando la internet. Kama nawe ni mmoja wa watu wanaotumia sana internet na unatumia pesa nyingi kwenye kipengele hiki cha simu yako basi Huenda kwenye makala hiii unaweza fungua ubongo na kujua cha kufanya ili simu isizichome sana pesa zako. Lakini Kabla ya yote ningependa kukushukuru Kwa kufuatilia The Bestgalaxy na kama ndio mala ya kwanza kuingia hapa, ni vema kama utaanza kufuatilia mahali hapa ili ujifunze vitu vingi.

Jinsi ya kubet bure (bila kuweka pesa) GUSA HAPA>>>

Unawezaje kuifanya simu isizichome pesa zako katika suala la bando?

Kwa jibu la halaka halaka tunaweza sema kupunguza manunuzi ya bando na kulitumia bando lako Vizuri kunaweza okoa pesa za Kwa kiasi flani. Lakini njia nzuri ya kufanya simu yako isichome pesa zako kwenye suala la bando ni kuitumia simu yako kutengeneza pesa ambazo utakua ukizitumia kununua bando. Kwakufanya hivyo utakua umeifanya simu ijinunulie bando. Nimeandaa makala ya sauti inayokupa mwanga wa vitu unavyoweza kufanya kwenye simu yako na vikakupa pesa kwanzia Tsh 10000 Hadi 100,000. Vitu ambavyo baadhi ya wajanja hufanya na kama hulijui hili na upo hapa basi upo mahali sahihi pakufungua ubongo wako.

Ukiona dalili hizi Jua Account yako ya Facebook imedukuliwa na si salama GUSA HAPA>>>>

Ukijifunza vitu hivi vitakusaidia kutengeneza pesa utakazokua unazitumia kununua bando bila kuumiza pesa yako. Ukitaka kuifungua makala hii unaweza bofya kitufe ilichopo hapa chini lakini Kabla haijafunguka utadaiwa password… Password hii mimi ntakupatia Kwa Tsh 10,000 tu. Kwaiyo kama unahitaji kujifunza basi unaweza nipigia au kutuma ujumbe kwenye 0715233405, utalipia Kisha nitakupa password itakayokuwezesha kufungua na kujifunza mbinu za uhakika za kupata pesa kwenye simu yako. Na pia unaweza chati nasi kwenye whatsApp kwa kugusa HAPA>>>

Katika Matumizi yako ya simu usifanye vitu hivi (Unaweza juta!) GUSA HAPA>>>

Njia za kupunguza au kutumia data kidogo kwenye TikTok (oka bando lako la internet)

Tiktok ni moja ya mitandao ya kijamii iliyo na watu wengi wanaotumia kushiriki/kushare video. Ni wazi kuwa watu wengi ambao wana app ya Tiktok, hutumia muda mwingi kwenye TikTok . Kuna watumiaji wengine wa Tiktok wanaweza kutumia zaidi ya saa moja au mbili kutazama video kwenye Tiktok. Hii kwa sababu Tiktok ina video fupi zinazowafanya wafurahie. Lakini Tiktok hutumia kiasi kikubwa cha data kutokana na video tunazoangalia. Hii inamaanisha jinsi video utazama video zaidi, ndivyo data inavyotumika.

Hii sio kesi ikiwa kununua vifurushi vya internet sio kazi kubwa kwako na unahitaji kufurahiya au kuburudisha akili na Tiktok katika video zenye bora. Lakini inakuja shida wakati inaumiza mfuko wako au kukugharimu kwa njia yoyote.

Katika nakala hii tutajadili jinsi ya kupunguza au kutumia data kidogo kwenye TikTok. Kwa hivyo ikiwa wewe ni mmoja wa watumiaji wa Tiktok ambao wanataka kupunguza au kutumia data kidogo kwenye TikTok, uko kwenye nakala inayofaa.

Jinsi ya kufanya simu ijinunulie bando la internet (usichome pesa zako kununua bando) GUSA HAPA>>>

Njia 3 za kupunguza au kutumia data kidogo kwenye TikTok.

1. Tumia app ya “Tiktok lite”


Kuna programu mbili za Tiktok ambazo unaweza kutumia na app hizi ni tofauti. Kuna app yakawaida ya Tiktok na Kuna app inayoitwa “Tiktok lite”. App ya Tiktok lite ni programu inayotumia data kidogo kuliko app ya kawaida ya Tiktok. Kwa hivyo ikiwa unahitaji kutumia data kidogo kwenye TikTok, unaweza kuanza kutumia app ya Tiktok lite badala ya kutumia ya kawaida ya Tiktok.

2. Usiangalie video nyingi.

Ni wazi kuwa mara nyingi kutumia kiwango cha juu cha data ni matokeo ya kiasi cha video ulizotazama. Kwaiyo kupunguza kiwango cha video unazotazama kwenye TikTok pia kutapunguza utumiaji wa data yako unavyotaka. Jipe kiwango cha video unazotaka kutazama kwa siku bila kuharibu bajeti yako ya data.

Jinsi ya kufanya simu isiishe chaji haraka GUSA HAPA>>>

3. Washa Kiokoa Data.

Tiktok wana kipengele cha “Data saver” ambacho kinapunguza matumizi ya data ya simu za mkononi. Kipengele hiki hakiwezi kufanya kazi kama upo kwenye wifi. Unaweza kuwasha kipengele hiki kwa urahisi kwa kwenda kwenye “Me” na Gonga vidoti Tatu kisha uchague “Data Saver” baada ya hapo Kiwashe kipengele hicho. Baada ya kufanaya hivyo, utaanza kutumia data kidogo kuliko hapo awali.

Fanya haya kabla simu yako haijaibiwa ili kuipata ikiibiwa GUSA HAPA>>>

SMS za kumtakia mpenzi wako usiku mwema

Kutuma sms au ujumbe wenye maneno mazuri kwa mpenzi wako, ni kitu muhimu sana katika mapenzi. Unapotuma ujumbe/message moja kwa moja unakua umeonesha kumjali na pia kumkumbusha kuwa yeye ni wamuhimu kwako. Leo nakupa sms ambazo unaweza zituma kwa mpenzi wako kwaajili ya kumtakia usiku mwema na akajisikia vizuri. Chagua ujumbe unaoendana na hali ya mahusiano yako Kwa sasa hapa chini na umtumie. Lakini kumbuka kuwa sio pazima umtumie ujume kama ulivyo andikwa hapa. Unaweza ubadilisha badilisha.

Ukiona dalili hizi Jua Account yako ya Facebook  imedukuliwa na si salama GUSA HAPA>>>>

SMS za mapenzi za kumtakia usiku mwema mpenzi wako

# 1: Natamani usiku wa kwanza ambao tutakua pamoja. Natumai unafikiria juu yetu kama mimi. Daima kumbuka kuwa nakupenda mpaka mwisho wa wakati. Ulale vizuri mpenzi.

# 2: Mpenzi wangu mtamu, nadhani siku yako imekuwa nzuri kama wewe. Lala na upumzike vizuri, ili uweze kuamka mchanga na mwenye nguvu kwa siku ya kesho. Usiku mwema.

# 3: Maneno hayawezi kuelezea jinsi ninavyokupenda na kukuthamini. Tumekuwa na moja ya siku bora za maisha yetu na ni maombi yangu tutakuwa na siku kama hizo kwa maisha yetu yote. Usiku mwema, mwanamke mzuri

# 4:Natumai leo imekuwa nzuri kwako. Nimekuwa nikifikia niwezaje pata furaha usiku huu. Nikakumbuka kuwa kumtakia usiku mwema mpenzi aliekatika moyo wangu hunipa kutanipa furaha. Usiku mwema.

Maneno ambayo hutakiwi kuyasema kwa mwenza wako GUSA HAPA>>>

# 5: Usiku mwema, mpenzi wangu. Natumai umelala vizuri na una ndoto bora. Nakupenda sana. Siwezi kusubiri kukuona asubuhi.

# 6: Hello, sweetie. Nilitaka kukujulisha kuwa nimekuwa nikifikiria juu yako siku nzima. Kuwa na usiku mzuri na ndoto za kupendeza. Nakupenda.

# 7: Ni ngumu sana kuwa mbali na wewe. Nimekukumbuka sana. Napatashida kusubiri siku nikakayokuwa nawe nyumbani na kukuona tena. Usiku mwema.

# 8: Usiku Mwema, mpenzi. Lala vizuri na ndoto zako zote ziwe nzuri. Kumbuka jinsi ninavyokupenda. Natarajia kukuona kesho.

Mambo ya kushangaza usioyajua kuhusu Wanawake na Wanaume BONYEZA HAPA>>>

# 9: Pole na kazi… Usiku wa leo natamani ningekuwa nawe. Lala vizuri mpenzi wangu na uwe na ndoto tamu, Nakupenda.

Jinsi ya kubet bure (bila kuweka pesa)

Kubet ni mchezo maharufu sana ulimwenguni wa kubahatisha. Kuna kama watu bilioni 1 au zaidi hujihusisha na maswala ya kubet. Yawezekana na wewe ni moja ya watu wanaojihusisha na kubet ndio maana upo hapa.

Ikiwa wewe ni mdau wa kubet au sio mdau was kubet basi ningepeda kukushukuru Kwa kusoma post za The Bestgalaxy na usiache kutembelea sehemu hii. Katika makala hii fupi nakujuza jinsi unavyoweza kubeti bure kabisa yaani bila kuiumiza pesa yako.

Wapi unapata Odds za bure au Mikeka ya uhakika? BONYEZA HAPA>>>

Njia 3 za kubet bure

Kutumia Ofa za kubeti Bure kwa Watumiaji

Kama unataka kubet bure kunanjia nyingi unaweza kufakisha hilo. Kuna makampuni mengi sana ya kubet kwa sasa huwa yana taratibu za kuwapa watu nafasi au ofa za kubet bure wakati wakiendelea kutumia huduma zao. Hizi ofa hutofautiana na kila kampuni hutoa kwa utaratibu wake ila kwakua ni bure inakua sio mbaya sana. Moja ya makampuni haya ni Gwalabet.

Hawa kwa taalifa tulizojichukua Tarehe 5 mwezi wa 10 mwaka 2024, wanasema kwamba “Kila akaunti ya mteja wa GwalaBet itapata bet ya bure ‘FREEBET’ ya Tsh 500 kila Ijumaa kama itakuwa imetumia kiasi cha kuanzia Tsh 2,000 ndani ya wiki husika.” Sijajua wewe unasoma makala hii kwa muda gani ila fahamu kuwa huwa wanatoa kweli japo utaratibu wa kupata, huwa unabadilishwa badilishwa baada ya muda. Pesa hii unaweza iona kwenye kipengele cha “FREE BET”. Kama utahitaji maelezo zaidi, unaweza kupata maelezo yote katika website yao.

Kupata zawadi ya kualika Marafiki

Njia nyingine ya kubeti bure ni kupata zawadi ya kualika Marafiki. Mitandao mingi ya kubeti huwa Ina kipengele ambacho kina kuruhusu kualika Marafiki na ukifanikiwa kualika, unapata pesa ya kubeti Bure. Katika kualika huwa wanaweka utaratibu ambao utaufuata kumualika rafiki au marafiki zako ili upate zawadi itayakuwezesha kubeti Bure.

Mfano mzuri ni kampuni ya Wasafi bet; inakupa nafasi ya kupata zaidi ya Tsh 2000 kwa kualika Marafiki. Unachotakiwa kufanya ni kwenda kwenye kipengele chao kiitwacho “Referral” au “Mchizi bonus” alafu tumia Link au Code utakazopewa kuwaalika marafiki katika Facebook, WhatsApp na sehemu nyingine. Katika kipengele hicho kuna maelezo mengine unayoweza kusoma ili kuelewa zaidi.

Kujiunga na Makampuni mapya

Makampuni mengi huwa yanahitaji watuaji wapya na hutoa bonus kwa Watumiaji huo wapya pindi wanapo deposit. Yani unapoingiza pesa kwa mara ya kwaza, unapata na pesa nyingine ya bure kwaajili ya kubetia. Pesa hii inafahamika kama “Welcome bonus”. Na kiasi cha pesa hutofautiana maana kila kampuni ina utaratibu wake.

Mfano, Kampuni ya Parimatch huwa inakupa hadi asilimia 100% ya pesa yako. Yani ukiingiza kiasi ya Tsh 2000 baada ya kujiunga, unapata Tsh 2000 nyingine kama zawadi. Mbali na kampuni hii, Kuna kampuni nyingine nyingi hutoa zaidi kwa mtindo huu japo hutofautiana kwenye kiasi.

Watu wengi hutumia njia hizi kupata nafasi za kubeti bila kumiza pesa zao moja kwa moja. Na njia rahisi hapa huwa ni ile ya kwanza na hii ya mwisho.

Katika matumizi yako ya simu usifanye vitu hivi (Unaweza juta!) GUSA HAPA>>>>

Kwanini bando lako la wiki la internet huisha ndani ya siku Moja/mbili?

Kwasasa katika dunia matumizi ya internet yameongezeka. Na inaonesha yatazidikuongezeka zaidi ya hapa maana baadhi ya huduma na vitu vilivyokua havihusiani na internet vimekua vinategema internet Kwa sasa. Mfano mzuri ni magari ya kisasa yanayotoka kipindi hiki. Mengine yanatumia internet kukupa huduma ya redio na vitu vingine. Yani huwezi sikiliza redio ya gari bila internet. Hebu tuachane na ulimwengu na tuingie Tanzania Sasa.

Ni wazi kuwa Kuna watu wanatumia sana internet na vifurushi vya internet Kwa hapa Tanzania vinaweza kukughalimu hata za zaidi ya 2000 Kwa GB 1(inategemea na kifurushi). Katika kununua vifurushi na kutumia internet, Kuna baadhi ya watu hununua vifurushi vya internet vya wiki lakini huvimaliza kabla ya wiki na hawajui ni Kwanini. Hiki sio kitu kukubwa kama hakikuumizi kwenye sawala la pesa lakini kama kinakuumiza basi hapa ntakujuza ni kwanini ipo hivyo na hatua gani unaweza kuchukua.

Jinsi ya kufanya simu isiishe chaji haraka GUSA HAPA>>>

Pata bando za internet Kwa Bei rahisi (Tigo & Halotel) GUSA HAPA>>>>

Kwanini bando la wiki la internet linawahi kuisha kabla ya wiki?

Kiufupi ni kwamba kitu kinacho maliza bando mara nyingi ni “matumizi”. Ukiwa na Mb 50 ikiingia kwenye internet na kutumia au zikatumika Mb 50, utabakiwa na Mb 0 hata kama ulipewa zikae mwezi. Ni mahesabu tu.

Ukiwa unamatuzi ya internet yanayotumia Mb nyingi basi utahitaji Mb nyingi ili uzitumie sio sinazokaa sana. Hata ununue bando la mwaka mzima, kama matumizi yako ni makubwa kuliko hilo bando au Mbs ulizonazo, utamaliza kabla ya huo mwaka kuisha.

Jinsi ya kufanya simu ijinunulie bando la internet (usichome pesa zako kununua bando) GUSA HAPA>>>

Kwani watu hutumia bando kiasi gani?

Kwa watumiaji wa Smartphone (Tz) wengine wanaweza kutumia Mb 200 kwa siku na kunawatu hufia hadi Gb 1, G 2 au zaidi. Hii hii pia hutegeana na “matumizi” ya mtu.
Kuna watu ambao hutumia internet kuangalia movies, kucheza magemu (cloud games) au wapo internet kikazi. Watu hawa hata GB 2 mbili zinaweza kuwa ndogo kwao Kwa siku.
Mbali na watu hao kunawatu wanamatumizi ya kawaida tu. Inawezakua wanatumia kupata nyimbo mpya, habari, matokeo ya michezo na vitu vingine kama hivyo. Watu wanye matumizi haya wanaweza kutumia chini ya Mb 500 japo wanaweza vuka hapo pia.

Nifanye nini ili kutomaliza bando la internet Kwa haraka?


Kama unataka usimalize bando lako la internet Kwa haraka basi inabidi uanze kujichunga kwenye matumizi maana maranyingi matumizi ndio hulimaliza bando.
Kama ni mtu wa movies basi punguza kuangalia movies au videos unazoangalia kwa siku.
Jizuie kutumia internet sana kama bando linaumiza pesa yako.
Ingiza vitu kama offline games au vichekesho na vitu vingine ambayo vitakua vinakufurahisha kwenye simu yako bila kuwasha data. Mfano wa vitu vingine ni Simulizi. Unaweza ukawa unanunua simulizi za kusoma kwenye simu yako alafu unakua unasoma kidogo kidogo ukiwa na muda.
Hayo ni machache niliokuandalia kwenye makala hii inayohusu internet. Tutakutana kwenye makala nyingine Lakini usiache kufuatilia The Bestgalaxy ili kujifunza mengi zaidi.

Magemu mawili mazuri ya mapigano ya ndege (Android)

Watu wengi huwa wanapenda kucheza magemu ya ndege kwenye simu zao kwakua huwafurahisha. Ni wazi kuwa magemu ya ndege huwa ni mazuri na ya kuvutia ndio maana hufurahisha lakini si magemu yote huwa ni mazuri, mengine hukera kutoka na sababu mbalimbali kama vile muonekano mbaya na sauti za ndege zisizo na uhalisia.

Katika post hii nakupa gemu 2 za ndege ambazo ni nzuri,ndogo na watu wengi hupendelea kuzicheza katika simu zao za Android ulimwenguni.
Kabla ya kuendelea ningependa kukujuza kuwa magemu haya mara nyingi huchezwa kwa kuyumbisha simu yako.

Simu ikiingia maji unatakiwa kufanya nini? GUSA HAPA>>>

Zifuatazo ni gemu 2 za ndege ambazo ziko vizuri na pia hupendwa na watu.

1. Wings Of Still


Wings Of Still ni gemu la mapigano ya ndege ambalo mpaka Sasa limechezwa na watu zaidi ya milioni 10 na wamelipenda. Gemu hili linamuonekano mzuri na mazingira yenye uhalisia. Linakupa nafasi ya kuchagua aina ya ndege uitakayo kutokana na Score ulizojizolea.

Kama utahitaji gemu hili utalipata kirahisi sana kupitia playstore na ni kwa Mb chache. Unaweza rahisisha upatikanaji wa gemu hili kwa kugusa  INSTALL

2. Modern Warplanes

Ni moja kati ya magame mzuri sana ya ndege yanayo pendwa zaidi na watu. Linahusisha mapigano ya ndege angani na linakupa uhuru wa kuchagua ndege ipi ya kivita unayohitaji kuwanayo kwenye vita hivyo. Watu hulisifu sana muonekano wake kwa ufupi modern warplanes ni gemu zuri sana.

Mbali na gemu hili kuwa na muonekano mzuri, pia hupatikana kirahisi sana kwa Mb chache. Linapatikana playstore bure na unawezalipata kirahisi kwa kugusa  INSTALL

Download na kuangalia movie zote bure kwenye simu GUSA HAPA>>>

Jinsi ya kufanya simu isiishe chaji haraka GUSA HAPA>>>

Jinsi ya kuangalia mechi za Tanzania kwenye simu

Kama ni shabiki mzuri wa soka la ndani basi bilashaka ninahakika unijiskia Vizuri sana pale unapotazama mechi zinazohusishia timu za bongo kama vile Azam fc, Simba, yanga na nyinginezo.


Tulishazungunzia katika makala iliopita jinsi unavyoweza cheki ama kuangalia mpira wa nje kwenye simu. Kama ni mfuatiliaji wetu mzuri utakua tayari umelijua hilo. Kwenye makala hii tunakujuza jinsi ya kuangalia mechi za Tanzania kwenye simu(online). Yaani namba unavyoweza kuangalia mechi zote zinazohusishia soka la bongo/Tanzania.

Magemu ya mpira ya kucheza kwenye simu GUSA HAPA>>>

jinsi ya kuangalia mechi za Tanzania kwenye simu

Njia rahisi ya kuangalia mechi za Tanzania kwenye simu yako ni kutumia app iitwayo AzamTv Max. Unaweza gusa HAPA>>> kuipakua.

App hii imejaa channel ambazo huusika na mechi saka za Tanzania. Lakini app hiii sio ya bure. Utahijika kulipia ili kufurahia unachokipenda kiganjani kwako.


Mbali na app Azam Max, Kuna baadhi ya app pia huwa zinakupa uwezo wa kuangalia mechi za soka la bongo Kwa Bei nafuu ila huwezi fananisha huduma zake na huduma za Azam Max. AzamTv Max ni Moja ya app bora.

Jinsi ya kupata mkopo kwenye simu GUSA HAPA>>>>

Magroup ya WhatsApp ya kujiunga bure GUSA HAPA>>>

Unapotaka kuangalia soka kwenye simu inatakiwa kuwa na internet yenye kasi na iliotulia ili kufurahia zaidi kuangalia soka kiganjani mwako. Kama unajua kabisa internet yako haipo sawa, ni vema ukaangalia tu kwenye TV maana utainjoi zaidi kuliko kwenye simu. Mara nyingi Sana unapokua unatuzama soka kwenye simu ilio na muunganiko wa internet unaosumbua kunakua na matatizo ya kuganda ganda kwa video.

Mtu akiku “Block” WhatsApp unaweza fanya hivi kuchati nae

Je, ungependa kujua mbinu za kuchati na mtu aliyekuzuia (Block) kwenye WhatsApp? Usijali, katika makala hii tutazungumzia kuhusu hilo.
Watu huzuiwa kwenye WhatsApp kwa sababu tofauti kama vile migogoro ya uhusiano na vitu vingine. Na hakuna njia ya kujitoa block mtu akiku block kwenye WhatsApp. Lakini hapo tutakupa njia za kuchati tu na mtu aliyekuzuia kwenye WhatsApp.
Kabla ya kwenda moja kwa moja kwa uhakika wa makala hii, hebu tuangalie vitu vinavyoashiria kwamba mtu amekublock kwenye WhatsApp.

Ni nini kinaonyesha kuwa mtu amekublock kwenye WhatsApp?

Huwezi kumuona yupo Online, muda wote unaoneshwa mara yake ya mwisho kuonekana Online/mtandaoni. Na pia huwezi ona profile picha.
Si hivyo tu, bali hata jumbe unazotuma kwake zinaonesha alama ya tiki moja tu wakati wote.
Ukiachana na hiyo, huwezi kufanikiwa kupiga simu ya sauti au ya video (voice call & video call) mtu aliekublock kwenye WhatsApp alafu akapokea.

Katika Matumizi yako ya simu usifanye vitu hivi (Unaweza juta!) GUSA HAPA>>>

Jinsi ya kuzungumza na mtu aliyekuzuia kwenye WhatsApp

1. Chati naye kupitia group la WhatsApp.

Kama alie kubook ni mpenzi wako au marafiki, basi mwambie rafiki yako mwingine atengeneze group la WhatsApp kisha akuweke wewe na mtu aliekublock kwenye hilo group. Baada ya rafiki yako kukuweka kwenye kikundi/group hilo, utaweza kuchati nea ndani ya hilo group.
Rafiki aliyeunda group anaweza kuondoka kwenye hilo group na kuwaacha nyie.
Baada ya hapo, utakua Ukituma meseji zako kwenye group kisha rafiki au mpenzi wako aliekublock atapokea ujumbe wako kupitia group hilo. Pia atakuwa na uwezo wa kujibu ujumbe wako.

Tumia hii kama nafasi ya kutatua migogoro kati yako na mpenzi wako au rafiki aliyekuzuia/kublock.

2. Tumia app nyingine anazotumia kuchati.

Ikiwa hutafaulu kuzungumza nae kupitia group la WhatsApp, jaribu kuzungumza na mtu huyo kupitia app nyingine za kuchati ambazo yeye hutumia. Unaweza kumpata kwenye Facebook messenger, Telegram, Signal na app nyingine zingine unazofikiri mtu huyo anatumia. Lakini unapaswa kukumbuka kuwa anaweza kublock pia kwenye app hizo, kwa hivyo ukipata nafasi ya kuchati na mtu huyo, itumie vizuri.

3. Tumia app za nambari ya pili (Vitural number apps)

Movies za kutafsiliwa GUSA HAPA>>>>

Hizi ni app zinazokupa nambari ya pili na unaweza kuitumia kutuma ujumbe mfupi au kumpigia mtu yeyote kama nambari yako ya kawaida ya simu. Mfano wa app hizi ni app iiitwayo “TextMe
Ikiwa haukufanikiwa kwa njia zilizo hapo juu, unaweza kupagua app moja ya nambari ya pili. Kisha chagua nambari na uitumie kutuma ujumbe au kumpigia simu aliyekuzuia. Tumia hii kama nafasi ya kutatua tatizo lililo kati ya wewe na aliyekuzuia.

Huu ndio mwisho wa makala hii Lakini ningepeda kukujuza kuwa hapa ndipo maunja yote ya teknolojia unaweza kuyapata. Kikubwa ni usisahau kutembelea mahali hapa Kila mara ili usikose vitu vipya.