All posts by Admin

Jinsi ya kutunza mahusiano ya mbali

Kuwa na mahusiano ya mbali ni jambo la kawaida kipindi hiki. Kuna mambo mengi katika maisha yanaweza fanya ukaanzisha mahusiano na mtu aliembali na wewe au ukaenda mbali na mtu ulie na mahusiano nae. Umbali katika mahusiano unaweza sababisha mahusiano kuwa katika hali ya kuvunjika kwa urahisi endapo hakutakua na mambo ambayo husaidia kutunza mahusiano. Unataka kujua mambo haya ni mambo gani? Sawa, hebu soma hapa chini.

Mambo ambayo hutunza mahusiano ya mbali (Mwanaume na Mwanamke)

Mawasiliano ni muhimu.

Mawasiliano ni jambo muhuimu lisilotakiwa kukosekana kwenye mahusiano ya mbali. Mawasiliano huwaunganisha wapenzi hata mukiwa mbali. Ni vema kufanya mawasiliano mara kwa mara na mtu ulienae kwenye mahusiano ili kulinda mahusiano yenu. Jisukume kumjulia hali mapenzi wako na kuzungumzane karibu kila siku mpaka mufikie ile hali ya kuhisi muko pamoja japo mupo mbali.

Uaminifu na uvumilivu

Katika mahusiano ya mbali, kupoteza uaminifu na uvumilivu ni rahisi sana. Uaminifu na uvumilivu ukipotea kwenye mahusiano ya mbali unaweza pelekea mahusiano kuvunjika. Ni vema kila mtu kwenye mahusiano hayo ya mbali akawa mvumilivu na kuonesha uaminifu kwa kuwa muaminifu kwa mwenzake. Mara nyingi mtu ukishaanza kutokua muaminifu kwa mwenzako aliembali, utaanza kubadili tabia zako kwake bila wewe kujijua. Hii inaweza pelekea mpenzi wako wa mbali kuanza kutokukuamini, kuumia na kushindwa kuvumilia au kukusaliti.  

Kuongea kuhusu mambo yajayo na mipango ya mbele bila kujali umbali.

Unapokua unawasiliama na mtu ulienae kwenye mahusiano na mnaongelea kuhusu mambo yajayo au mipango ya mbele mnajenga picha ya Future ya mahusiano yenu pamoja na kwamba muko mbali. Ongeanae kuhusu kesho, wiki ijayo, mwezi ujao, mwaka ujao na maisha yenu ya mbele kiujumla. Weka nae mipango, ongelea matukio yanu yanayokuja, wekeaneni ahadi ndogo na kubwa mtazo mtazokua mkiishi kuzitimiza, Ulizaneni kususu vitu mtavyo fanya kesho au mwisho wa wiki.

SMS nzuri kwa Mpenzi aliembali BONYEZA HAPA>>>

Kuonesha kuwa unampenda, unamjali na unatamani muwe karibu.

Muoneshe kuwa unampenda kwa kumwambia vitu vizuri, kumfanyia vitu vizuri vitakavyoonesha unamjali hata kama upo mbali. Kama amekwambia hayuko vizuri, usipuuze kisa muko mbali. Jaribu kuwa msaada kwake kwa njia itakayowezekana. Jali maneno yake na hisia zake pia alafu usisahau kuonesha kuwa unatamani muepamoja. Mwambie vitu vizuri unavyotamani toka kwake ukiwa huko mbali, muoneshe kua yeye ndie alieuteka moyo wako huko uliko na utamani awekaribu yako hata sasaivi.

Ni hayo tu tumekuandalia katika mengi unayoweza Fanya kutunza mahusiano ya mbali. Endelea kuwa karibu na The bestgalaxy na usinchukie kutembelea Kila mara.

Jinsi ya kucheza game la Fortnite online kwenye simu (bila kudownload)

Fortnite ni game lililotolewa na Epic Games katika  mwaka 2017. Epic games ni kampuni inayojihusisha na Games na imetengeneza magemu mengi tu, ikiwemo hili game linaloitwa Fortnite. Tangu game hili limetoka mpaka sasa kuna mamilioni ya watu wanalicheza na baadhi ya watu wanaotumia simu za Android ni miongoni mwa watu hao.

Hapa chini The bestgalaxy tunatoa maelezo juu ya jinsi ya kulicheza gemu kwenye simu za Android online bila kudownload. Game la Fortnite halipatikani katika Playstore hii ni baada ya kuondolewa kwa kutofuata sheria za Google Play store. Liliondolewa mwisho wa mwaka 2020 na game nyingi zikikiondelewa katika Playstore huwa zinakufa lakini Fortnite ni game ambalo lipo hai mpaka leo na unaweza cheza kwenye simu yako ya Android kwa kudownload nje ya Playstore na hata kujeza bila kudownlod pia.

Magemu ya mpira ya kucheza kwenye simu GUSA HAPA>>>

Jinsi ya kucheza game la Fortnite online kwenye simu (bila kudownload)

Kucheza gemu hili kwenye simu bila kulidownload ni rahisi tu japo utakitaji kuwa na internet yenye kasi, VPN pamoja na Accounti ya Microsoft. Kama hauna akaunti ya microsoft usihofu maana unaweza tengeneza  katika ya safari ya kulicheza gemu hili. Fuata hatua zifuatazo kucheza game la fortnite online kwenye simu bila kudownload.

  • Unganisha VPN na iwe kwenye server ya USA
  • Tumia web browser yako kuingia katika Xbox.com/play
  • Bonyeza kiduara cha upande wa kulia juu ya ukurasa wa kwanza wa Xbox.com/play
  • Bonyeza batani ya kijani ilioandikwa “SIGN IN” alafu jaza taharifa za akaunti ya Microsoft. Kama hauna akaunti utabonyeza neno “Create One” utakaloliona baada ya bonyeza hiyo batani ya kijani.
  • Baada ya kuweka sawa akaunti ya Microsoft utarudishwa kwenye ukurasa wa Xbox
  • Utatakiwa kutumia kisehemu ya tafuta cha ukurasa huo kutafuta game la “fortnite” alafu kuliona utalichagua na kubonyeza “Play” ili kuanza kulicheza.

Unapocheza gemu hili, hakikisha internet yako iko vizuri maana ikiwa iko vibaya unaweza kutofurahia kucheza gemu la fortnite kwa njia hii. Njia hii ya kucheza gemu huwa inaitwa “Cloud gaming” na huduma ya” Xbox cloud gaming” ndio inayotumika maana inaruhusu kucheza gemu hili bure.

Kama wewe ni mtu uliekua USA na upo kwenye sehemu ambayo game hili halikupi nafasi ya kucheza basi hizo hatua juu ukizifuata utaweza kucheza gemu lako pendwa ukiwa nje ya USA.

Jinsi ya kumfurahisha mwanamke katika mahusiano

Ili Kumfurahisha mwanamke kwenye mahusiano ni vema  ukajenga mazingira ya heshima, upendo, na yakueleweka. Mnaweza kuwa kwenye mahusiano na mwanamke lakini kama katika mahusiano hujajenga mazingira mazuri, Mwanamke anaweza kuwa hayafurahii.  Hapa The bestgalaxy tumekuandalia baadhi ya vitu unavyoweza kuanza kufanya kwenye mahusiano ili kumfurahisha  mwanamke katika mahusiano.

kumfurahisha mwanamke katika mahusiano

Muoneshe upendo na kumthamini

Muoneshe kuwa unampenda maana kama anakupenda kweli basi jambo kubwa analolitaka toka kwako ni kujua kama na wewe unampenda kwa dhati. Muoneshe kuwa unampenda kwa kumwambia au kufanya vitendo vinavyo ashilia unampenda na kumthamini katika maisha yako. Muombe msamaha unapomkosea, mbembeleze, kuwa msaada kwake na ukipata nafasi usisahau kumwambia kuwa yeye ni mtu muhimu maishani mwako au kumsifia pia.

Mtu akikublock WhatsApp Fanya hivi kuchati nae BONYEZA HAPA>>>

Msikilize na kumpa muda pia

Kati ya vitu ambavyo ukifanya, mwanamke hufurahi ni pamoja na kumpa muda na kumsikiliza. Mwanamke anafurahi sana pale mwanaume wake anapo mpa muda wake. Hivyo kama uko kwenye mahusiano, ni muhimu kutumia muda wako pamoja nae ili kumfurahsha. Mbali na kumpa muda , kumsikiliza hisia, mawazo, na maoni yake humfanya afurahi katika mahusiano.

Mpe nafasi huru na kumuheshimu

Kuwa nae kwenye mahusiano lakini lakini usimfunge kwenye vitu vyake binafsi ambavyo havina  athiri katika mahusiano yenu. Mpe huru wa kuchagua vitu anavyovipenda au kukataa vitu asivyopenda alafu heshimu maamuzi yake. Muache afanye mambo yeke binafsi kama mwanamke na usimlazimishe afuate mawazo yako kila mara katika vitu vyake visivyo hata kuhusu. Japo mupo kwenywe mahusiano lakini kunavitu inabidi uishie kuwa mshauri tu. Kwa kufanya hivyo, utamfanya mwanamke afurahi.

Kuwa muaminifu na muwazi

Ukimuonesha mwanamke kuwa wewe ni mwaminifu katika mahusiano yenu anaweza kuwa na furaha sana. Ukiwa sio mwaminifu katika mahusiano yenu mwanamke kama anakupenda anakua na roho juu muda wote kutokana mashaka kiasi kwamba anakua hafurahii mahusiano. Ni vema kuwa muwazi ili kumuondoa mashaka alafu jenga picha ya uaminifu kwenye mahusiano yako kwa kuwa mwaminifu kwake.

Kumuahidi na kumshtukiza mambo mazuri

Unapo muahidi mwanamke mambo mazuri kwenye mahusiano huwa anafurahi na ukitimiza ndio hufurahi zaidi. Ukiachana na kumuahidi, pia kumwambia au kumfanyia mwanamke mambo mazuri kwa kumshtukiza huwa kunamletea furaha kwenye mahusiano. Mambo haya mara nyingi humpasua mwanamke moyo kwa furaha na kujemga kumbukumbu nzuri za furaha katika mahusiano yenu.

Mlidhishe katika mchezo

Hakikisha unafanya vizuri katika michezo munayocheza ili afurahie. Kama utakua haumidhishi ni wazi kuwa anaweza kuwa hanafuraha ya ukweli na kupelekea kuitafura furaha sehemu nyingine. Kama unamatatizo katika kushiriki mchezo hakikisha unawafuata wataalam/madaktari ili kupata ufumbuzi wa tatizo ulilonalo kwenye machezo.  Hakikisha unakijali sana kifaa chako kikiwa na matatizo maana hicho kifaa sio chako, ni chake yeye. Anakipenda hicho kifaa na awezakuwa anakiota kabisa kwaiyo usikichukulie kirahisi.

Unaweza book ndege kwa app ya MPesa?

Moja ya app zinazotupa uwezo wa kufanya miamala ya kifedha katika viganja vyetu ni app ya Mpesa. App hii ni kwaajili ya watumiaji wa Vodacom. Moja ya faida za kutumia app ya Mpesa kwa mtumiaji wa Vodacom ni kwamba hata laini voda ikiwa haipo hewani au imepotea, unakua umebaki na uwezo wa kufanya miamala kwenye app hiyo kwa kutumia internet ambayo haihusiani na laini yako ya voda.  

Kuna baadhi ya watu wamekua wakiuliza juu ya kubook ndege za usafiri kwenye app ya Mpesa na hapa tunaenda kuangalia kuhusu hilo. Kama na wewe unahitaji kujua juu ya hili basi hapa unaweza pata mwanga.

Kubook ndege kwa app ya MPesa

Unaweza book ndege kwa app ya MPesa?

Ndio, inawezekana. Precision Air na Vodacom waliungana na kukuletea uwezo wa kubook ndege kwenye simu yako kupitia app ya Mpesa. Kwa sasa app ya Mpesa inavipengele vingi ikiwemo kipengele cha kubook ndege za usafiri. Precision Air wamekiri kuwa huduma ya kubook ndege kwa app ya Mpesa ni huduma rahisi na haraka kwa watumiaji. Na pia moja ya kitu kizuri kuhusu kubook ndege kupitia app ya Mpesa ni kwamba unapata punguzo la asilimia 20  ambayo inaokoa karibu robo ya pesa yako. Kwaiyo tunaweza sema pia hii ni njia ya kupata tiketi za ndege kwa bei rahisi.

Kipengele cha kubook ndege kwenye app ya MPesa

Ukifungua app ya Mpesa unaweza kiona kipengele cha kubook ndege maeneo ya chini kikiwa kimeandikwa “Book Flights”. Kama umeangalia chini na haujakiona, mbonyeza sehemu ilioandikwa “Services” alafu ukisha fanya hivyo utapelekwa kwenye orodha ya huduma na utaona kipengele kinachoitwa Book Flights kwenye orodha hiyo. Ukifungua kipengele hicho utakutana na ukurasa huu chini kwaajili ya kutafuta na kubook ndege itakayofanikisha safari yako.

Asante kwa muda wako, Endelea kuwa karibu na The bestgalaxy na usisahau kutembelea kila mara kupata vitu vipya.

sms za mahaba kwa mume au mke

Kuitwa Mume au mke haimaanishi hauitaji kumwambia mwenza wako unampenda au maneno mazuri ya upendo na mahaba.Watu wengi huisha ingia kwenye hatua ya kuitana mume au mke huwa wanasahau kuambiana maneno mazuri kiasi kwamba wanaweza kuyumbishwa kwenye mahusiano kwa kuanguka kimapenzi na mtu wa nje kisa anawaambia maneno mazuri na kuwasifia.

Kumwambia mke au mume wako maneno ya upendo ni jambo linaoweza mpa furaha na kuona unamjali haijalshi unatumia sms au unaongea moja kwa moja. Kama unataka kumtumia mke au mume wako sms za mahaba,hapa chini kuna orodha ya sms za mahaba kwa mume au mke ambazo unaweza tumia bure kabisa. Chagua zinazoendana na hali yako ya mahusiano ndio utumie.

Maneno ambayo hautakiwi kusema kwa mwenza wako BONYEZA HAPA>>>

sms za mahaba kwa mume au mke 

Umeuweza moyo wangu mpaka nahisi umeniloga. Unaupa raha moyo wangu nikikukosa pembeni yangu napata homa. Pezi lako ni tamu na kila siku linazidi kunoga. Kwako nimefika vya wengine siwezi onja.

Salamu yako ni nusu ya uhai wangu na kuikosa nisawa na kuidhulumu nafsi. Ukweli ni kwamba nikipata salamu yako huwa najisikia faraja moyoni mwangu, Nakupenda sana wangu.

Kuishi na wewe  ni raha sana. Penzi lako ni zawadi niliopewa na mungu katika maisha maana linanifanya nione thamani ya kuishi dear. Nitakupenda milele bila kujutia.

Mazoezi ya mwili ambayo husaidia katika tendo BONYEZA HAPA>>>

Umenifanya nijione wa thamani toka pale uliponichagua kuwa wako maishani. Kwenye milima na mabonde umepambana mpaka sasa umekuwa na mimi. Asante kwa upendo huu honey, nitakupenda milele maishani.

Wewe ndie mfalme wangu, Mwanaume ninaekupenda kwenye dunia hii, Mtu ninaejivunia kuwa nae maishani na natamani popote alipo ajue kuwa pamoja na yote tunayopitia kwenye maisha, bado ameteka hisia zangu.

Acha leo nikwambie ukweli. Thamani ya penzi unalonipa ni kubwa kwangu na siwezi fananisha na chochote kwenye hii dunia. Namshukuru mungu kwa kunikutanisha mpenzi mwema unaejali hisia za moyo wangu, Nakupenda sana mpenzi, usichoke kunipenda.

Wewe ndie malaika wangu, Fundi wa raha zangu, Msaidizi niliepewa na mungu, Mwanamke mzuri ninaempenda kwenye ulimwengu mpaka nikaamua kumchagua yeye tu maishani mwangu na sasa natamani ajue kuwa sijawahi jutia kuwa nae maishani, upendo wake unanipa furaha isio na kifani.

Penzi letu haliwezi kuvutia kuila mtu hapa duniani. Natamani uzibe sikio la kusiliza wengine na unisikilize mimi tu. Ninaposema nakupenda nasema toka moyoni. Usisikilize ya watu mpenzi mimi nakupenda wewe tu hapa duniani.

App zinazo kupa pesa kwa kufanya kitu kidogo kwako (Unazitumia Kila siku)

Hapa chini The bestgalaxy nimekuandalia orodha ya app chache ambazo zinaweza kupa zawadi ya pesa kwa kufanya jambo flani dogo linaloweza kuwa jepesi kwako.  Lakini kabla ya yote ufahamu kuwa pesa hizi ni ndogo sana na haziwezi kukufanya upate utajiri. Pia fahamu kuwa hizi app ni app ambazo hutoa pesa kama zawadi lakini sio app rasim kwenye upande huo. Hizi ni app rasmi katika upande wa kurahisisha upatikanaji wa huduma au mahitaji kirahisi. Yawezekana unazitumia kila siku. Kuna wakati tutazungumzia kuhusu platform rasimi kwa kutengeneza pesa nyingi.

Tunaweka app kwenye simu zetu kwasababu mbalimbali na moja kati ya sababu ya kuweka baadhi ya app ni kupata huduma au amahitaji kirahisi kwa kutumia simu. Mfano, kuna app ambazo tunaweka kwenye simu ili tuweze kupata huduma za kifedha kihisi kwenye simu zetu na pia  kuna app hurahisisha manunuzi ya vitu kwa kutusogezea bidhaa tunazoweza nunua kwenye simu zetu.

App zinazo kupa pesa kwa kufanya kitu kidogo kwako (Android)

Farasi

Farasi ni moja ya app ambazo zinajihusisha na maswala ya usafili. Kwakutumia app hii unaweza pata usafiri wa kukutoa ulipo mpaka mahali unapotaka kwenda kirahisi. App hii inakutumika na watu wengi tu katika maswala ya usafiri. App hii hua inatoa zawadi kwa watumiaji wake pale wanapoitumia kupata usafiri. Kwasasa unapoanza kuitumia unapata Tsh 3000 mbali na zawadi nyingine utazopata unapotumia. Angalia app kwa KUBONEZA HAPA alafu kama utakua unajiunga usisahau kujaza namba 715233405 kwenye kibox cha referral code.

Branch app

App ya Branch ni app ya mikopo. Ni moja kati ya app nzuri sana katika upande wa app zinazokuwezesha kupata mikopo kwenye simu Tanzania. App hii inaweza kukupa zawadi ya pesa pele unaporudisha pesa kwa mara ya kwanza baada ya kuazima ila kupata zawadi hii ni lazimu uwe umealikwa. BONYEZA HAPA kupata maelezo zaidi ya app hii na zawadi zake

Tigo pesa app

App ya Tigo pesa ni app ambayo hurahisisha zaidi maswala ya kufanya miamala kwa watumiaji wa Tigo. App  hii huwa anatoa kiasi kido cha pesa kama zawadi pale unapomualika rafiki yako. Kama unarafiki ambae anatumia mtandapo wa Tigo lakini ana app, unaweza mualika huyo rafiki alafu akapatiwa zawadi ya pesa kwenye akaunti yako ya Tigo pesa. Kama hauna app ya Tigo pesa, INGIA HAPA kuipakua.

Mwisho ningependa kukukumbusa tu kuwa app hizi sio app rasimi kwa kutengeneza pesa, zinatoa pesa kama zawadi TU.

jinsi ya kuwa romantic kwa mpenzi wako

Kumwambia mpenzi wako nakupenda na kuchezanae mchezo inaweza kuwa ni jambo zuri lakini tambua kuwa bado unaweza onekana sio romanic. Kuwa romantic kumekusanya mambo mengi sana katika mahusiano. Kiufupi kuwa romantic ni kuonyesha mapenzi kwa mpenzi wako, kumuonesha kuwa unamthamini na kumjali kwa kusema na kufanya matendo yanayogusa hisia zake. Hapa The Bestgalaxy tunafungua ubongo kwa kuelezea mambo machache ya kufanya ili kuwa romantic kwa mpenzi.

SMS za kumbembeleza mpenzi wako BONYEZA HAPA>>>

jinsi ya kuwa romantic kwa mpenzi wako (Mwanaume au mwanamke)

Mwambie maneno matamu na yakuvutia

Kama uko pamoja nae mnaongea au unazungumza nae kupitia simu, hakikisha unamwambia maneno matamu na yakuvutia. Ongea na mpenzi wako kwa hali ya utulivu alafu mwambie maneno ya upendo toka moyoni yatakayo ugusa moyo wake na kumfanya ajue jinsi gani unampenda. Funguka mwambie moyo wako unahisi vipi juu yake au msifu kwa maneo matamu.

Mzawadie zawadi zitakazo mfurahisha

Mpe zawadi ambazo unahisi atazipenda. Zawadi sio lazima iwekubwa au sio lazima iwe pesa. Unaweza mzawadia mpenzi wako vitu vidogo sana na akafurahi mpaka ndani ya moyo wake. Unaweza mzawadia mpenzi wako hata pipi ya kijiti tu na akafurahi ila inategemeana na namna ulivyomzawadia au muko katika hali gani. Mbali ya vitu kama pipi unaweza mzawadia vitu vingine unavyoona anapenda au anahitaji ila hajakwambia.

Mpe muda wako muwe pamoja

Ni wazi kuwa kama unampenda mwanamke, unatamani akupe muda wa kuwa nea na hivyo hivyo hata mwanamke akimpenda mwanaume anatamani apate muda wa kuwa na mpenzi wake. Kutumia muda wako kuwa na mwenzako ni jambo linaloweza kufanya uwe romantic. Unaweza kutumia muda na mpenzi wako mukiwa mnaogea, mnacheza michezo ya upendo, kutembea, kuangalia vitu, kusikiliza  au kusoma vitu.

Mtu akikublock WhatsApp Fanya hivi kuchati nae BONYEZA HAPA>>>

Mshawishi mwili

Kumbusu mpenzi wako, Kumshika mikono na kumkumbatia au kumgusa kwa ujumla ni mambo muhimu sana katika mahusiano maana ni vitu ambavyo vinaweza kukufanya uonekane romantic kwa mpenzi wako. Mchokoze kimwili mpezi wako na kama atakua na mahitaji ya kimwili ni vema ukaheshimu hisia zake. Siku hizi unaweza mchokoza hata kwenye simu kwakuongelea vitu vitakavyo msisimua kidogo.

Msikilize, thamini mawazo yake na tatua migogoro kwa upendo na amani

Msikilizea anachokwambia na uoneshe kuyathamini mawazo yake. Usipuuze mawazo yake anayoyasema maana atakuona humueshimu au kumjali. Kama kuna mgogoro umejitokeza kati yenu usiwe mwepesi wa kumjia juu kumfokea au kumtukana. Tafuta njia ya amani na upendo ya kutatua mgogoro huo. Sehemu ya kuomba msamaha muombe msamaha, Sehemu ya kubembeleza mbembeleze na sehemu ya kumsamehe msamehe.

Mambo humfanya mwanaume akupende sana na kukuchagua maishani BONYEZA HAPA>>>

Aibu yako isikuzuie kuonyesha mapenzi, kumuonesha kuwa unamthamini na kumjali kwa kusema na kufanya matendo yanayogusa hisia zake. Pia majukumu au kazi isiwe sababu ya kushindwa  kuonyesha mapenzi kwa umpendae, kumuonesha kuwa unamthamini na kumjali kwa kusema na kufanya matendo yanayogusa hisia. Ukishindwa kufanya hivyo mpenzi wako anaweza kuona sio romantic na wengine wanaweza wakakuacha kabisa maana hawafurahii mahusianio.

MIAKA IJAYO (Simulizi ya sauti)

Teknolojia imekua na msaada mkubwa sana katika maisha ya binadamu na imemuwezesha kufanya vitu vingi sana.

Wananadamu wamekua wakiiendeleza Teknolojia Kila siku kiasi kwamba inasemekana inaweza fikia wakati maisha ya binadamu yanaweza kuwa ya ajabu kuliko hivi sasa.

Sikiliza makala hii sehemu ya kwanza mpaka ya mwisho kupata picha ya maisha ya binadamu yanavyoweza kuwa kutokana na technology.

Miaka Ijayo: Sehemu Ya 1
Miaka Ijayo: Sehemu Ya 2
Ifahamu zaidi Simulizi ya MIAKA IJAYO

INAENDELEA…



Simulizi ya “MIAKA IJAYO” kutoka The Bestgalaxy ni simulizi ya sauti inayochunguza jinsi teknolojia inavyoendelea kubadilisha maisha ya binadamu na matarajio ya maisha ya baadaye. Unaposikiliza Simulizi hii, unapelekwa moja kwa moja katika ulimwengu wa baadae kwakua inatoa taswira ya dunia itakavyokua maendeleo ya kiteknolojia yatakapofika mbali. Inahimiza wasikilizaji kufikiria jinsi maisha yatakavyokuwa kutokana na maendeleo haya ya teknolojia.

Simulizi hii ilichapishwa kwa mara ya kwanza katika 2024 na inapatikana kwa mfululizo (series). Unaweza kuisikiliza bure katika tuvuti hii ya The Bestgalaxy.

Unataka kumuumiza mwanaume anae kutesa unampenda? Soma hapa

Kuna mwanaume ambae uponae kwenye mahusiano na unampenda lakini anakutesa? Unataka kufanya kitu kitakacho muumiza? Ni kitu gani unahisi ukikifanya kitamuumiza? Mh sawa ila kabla haujafanya maamuzi yoyote, hapa The bestgalaxy tunakujuza vitu vichache kuhusu hili.

Ni mara nyingi watu huangukia kwenye mahusiano ambayo huanza kwa kuwapa furaha lakini baadae hubadilika na kupoteza furaha kutokana na wenza wao kubadilika na kuanza kutojali hisia zao.Hali hii katika mahusiano inaweza kubadilika na kuwa nzuri au inaweza kuendelea kuwa mbaya zaidi na kupelekea kuvunjika kwa mahusiano kabisa.

Unapokua kwenye mahusiano alafu mwenza wako akabadilika ghafla na kuanza kukutesa au kutojali hisia zako ni vema ukajaribu kwanza njia mbali mbali kubaini nini tatizo na kurekebisha mahusiano yenu. Jaribu kuvumilia huku ukiongea na mpenzi kwa uwazi kabisa nakumuuliza  nini shida na mutafanya nini ili muwe sawa.

Uvumilivu ni jambo zuri sana pale mahusiano yanapoyumba ila kama mahusiano yanayumba na kugeuka mateso yasioisha mtu anaweza shindwa kuvumilia na kuanza kutafuta njia za kumuumiza anaemuumiza na hata kuondoka kwenye mahusiano kabisa. Kumuumiza mtu anaekuumiza kwenye mahusiano ni jambo baya sana maana linaweza pelekea ukajiumiza mwenyewe. Mfano; kuna dada moja alikua akiteswa kimapenzi na mwanaume wake. Akaamua kumuumiza mwanaume wake kwa kujiingiza kwenye mapenzi na rafiki wa mwanaume wake. Baade alipewa mimba na huyo rafiki alafu akapata na magonjwa pia kisha akatelekezwa. Unafikili uamuzi wa huyo dada ulimuumiza nani?

Ukiwa kama mwanamke, kuliko kufanya maamuzi yatakayo kuathiri hata wewe ni unaweza ukafanya yafuatayo.

Mambo muhimu kufanya kwa mpenzi mwenye hasira au ukorofI BONYEZA HAPA>>>

Mambo unayoweza fanya badala ya kufanya maamuzi mabaya

Jipende kuliko alivyokuzoea.

Kuna muda unaweza mzingatia sana mtu anaekutesa kiasi kwamba unasahau hata kujipenda. Unasahau thamani ulionayo na kujiweka hovyo hovyo. Ukiwa kwenye hali hii ni vema kuikumbuka thamani yako na kuanza kujipenda. Jipende bila hata kuambiwa unapendwa alafu jijali kwenye kila kitu. Vaa vizuri, pendeza, uwe msafi na ujiamini katika uwanamke wako ila usiwe na kiburi au dharau. Tambua kwamba wewe ni wa thamani na hata ukiambiwa “Sikupendi” bado thamani yako iko pale pale.

Usiingie kwenye mahusiano mengine kwa msukumo wa kuumiza mtu.

Ukiwa kwenye mahusiano ambayo mwenza wako anakutesa, kuna muda unaweza waza kutafuta mpenzi mwingine wa haraka haraka ili tu kumuumiza mweza wako. Wazo hili ni wazo baya sana maana linaweza kukufanya usiwe makini katika kuingia kwenye mahusiano. Jambo hili linaweza pelekea uingie kwenye mahusiano yatakayokupa shida na hata kukuacha katika hali mbaya zaidi.  

Usioneshe tena kuwa unaumizwa na mambo yake.

Kama kuna vitu mweza wako huwa anafanya kwa dharau ili kukuumiza na umejaribu kila mbinu kumzuia au kumwambia aache lakini anaendelea kufanya, acha kuonesha kuwa unaumia alafu kuwa kimya. Pengine anahitaji kukuumiza ndio maana anaendelea kufanya. Acha kumuonesha kuwa unaumia ili ajue amekuumiza mpaka umechoka. Kama atakua ni mtu anaejari, ataanza kuwaza mabadiliko yako.

Kubaliana hali halisi na ujipumzishe.

Ikiwa umevumilia na kujaribu kila njia ya kuokoa mahusiano yako lakini imeshindikana, kubaliana na hali halisi. Usilazimishe sana huwa kwenye mahusiano ambayo yanahatalisha mpaka maisha yako. Jaribu kurekebisha na ikishindikana kabisa, futa machozi alafu jipumzishe kwenye mahusiano hayo. Usifanye maamuzi yoyote mabaya.

Sms za mapenzi motomoto (Mahaba niue)

Kuna muda ukiwa kwenye mahusiano, unaweza tamani kumwambia maneneo ya mahaba moto moto mpenzi/mme/mchumba wako kwa njia ya ujumbe. Hili ni jambo hufanyiana wapenzi hasa mukiwa na upendo wa kweli kati yenu alafu munatumia sana simu kuwasiliana. Watu wengi wanapopokea jumbe au sms za mahaba toka kwa wawapendao, hufurahi.

Kama unataka kumtumia mpenzi wako sms za mapenzi motomoto basi hapa The bestgalaxy tunakupa sms za mapenzi motomoto ambazo unaweza mtumia mpenzi wako bila kuumiza kichwa sana. Kama utaona ni nzuri na zinaendana na mahusiano yako ya mapenzi, uaweza zitumia.

Maneno ambayo hautakiwi kusema kwa mwenza wako BONYEZA HAPA>>>

Sms za mapenzi motomoto (Mwanaume na Mwanamke)

  1. Siku hizi nanenepa kutokana na matunda unayo nipatia. Kila nikila nazidi kukung’ang’ania. Nafikiri wewe ndie mungu alinishushia maana umenipatia dear.
  2. Napenda kugusa ngozi yako laini kila nikiwa karibu yako. Kila ninapoigusa nahisi raha na msisimko. Hakika umeumbwa vizuri wewe mtoto, hahaha.
  3. Natamani unikumbatie nipate joto hapa nilipo. Natamani vitu vingi toka kwako japo siwezi sema. Nimekukumbuka sana mpaka nahisi siwezi hema.
  4. Natamani kusikia sauti yako mpenzi wangu. Unasauti nzuri inayougusa moyo wangu na kuulipua kwa furaha. Natamani tuishi pamoja ili niwe naisikia kila mara. Wewe ni tulizo la moyo wangu nakupenda sana.
  5. Natamani niwe na wewe kila siku,kila saa na kila dakika. Penzi lako moto naliitaji mpaka mwisho wa maisha. Nilikua naona mapenzi mabaya ila wewe kunakitu umenifundisha. Nakupenda zaidi ya sana.
  6. Ningerudi nyuma na kupewa nafasi ya kuchagua tena mtu ninaempenda, anaenifanya niwe na furaha na kunipa penzi linalo gusa moyo wangu bado ningekuchagua wewe. Nakupenda sana mpenzi wangu.
  7. Kukupata wewe kunanifanya nijione mwenye bahati sana katika dunia. Sijui sana kuhusu moyo wako ila tambua moyo wangu umeishazama katika penzi mpaka naogopa. Umeishaniteka sijiwezi mpenzi.
  8. Kuna watu niliwakaribisha kwenye maisha yangu wakanifanya nione mapenzi mabaya. Penzi lako nimefanya nione mapenzi matamu na sitamani niamshwe kwenye hii ndoto. Nakupenda sana.
  9. Nimeacha vitu vingi sana kwaajili yako na siwezi jutia maana unanipa furaha mpenzi wangu. Atuwezi kuwa sawa kila siku ila tambua nazidi kukupenda kila siku. Wewe ndie nimekuchagua moyoni na ndie daktari unaeweza tibu maradhi yangu. Wewe ni mtu wa thamani maishani mwangu.
  10. Penzi lako tamu, haliishi hamu. Upendo wangu kwako ni moto usiozima. Moyo wangu unalidunda jina lako na kila mara natamani kuwa karibu yako. Sijawahi penda kama hivi.

Mambo ya kushangaza usioyajua kuhusu Wanawake na Wanaume BONYEZA HAPA>>>