All posts by Admin

SMS za kumfanya mpenzi wako afurahi

Hapa kwenye ukurasa huu tunaenda tena kuangalia za sms za mapenzi unazoweza tumia kwa mpenzi wako. SMS tunazozingatia hapa ni kama ilivyoelezwa kwenye kichwa cha makala hii, yani tunaenda kuangalia sms zile zinazoweza mfurahisha mpenzi. Sio kila sms tutazoangalia hapa zinaweza mfurahisha mapenzi wako lakini kupitia orodha ya sms za mapenzi tulizoweka hapa chini unaweza pata sms nzuri inayoweza kumfurahisha mpenzi wako.

Usimtumie sms bila kufikilia kama ataipenda kwa jinsi unavyo mjua mweza wako. Kiufupi unatakiwa kuchagua sms kulingana na hali ya mahusiano yenu au hali ya mpenzi wako wakati unamtumia.

Mazoezi ya mwili ambayo husaidia katika tendo BONYEZA HAPA>>>

Sms za kufanya mpenzi wako afurahi

  • Asubuhi njema mpenzi wa moyo wangu! Kila siku ninapoanza na wewe, moyo wangu hujaa furaha na upendo siku nzima. Nakutakia siku yenye neema na mafanikio.
  • Leo ni siku ya kipekee kwa sababu nakupenda zaidi ya jana. Na usiwaze kuhusu kesho maana uko moyoni mwangu milele na kesho ntakupenda zaidi ya leo.
  • Ninapopitia picha zetu za pamoja, nakumbuka jinsi kila wakati tunavyopendana na kusaidiana. Kiukweli wewe ni nguzo yangu, na nakushukuru kwa kunifanya niwe na wewe maishani, Nakupenda sana.
  • Nakupenda sana Mpenzi wangu. Unanifanya nihisi nipo kwenye bahari ya mapenzi ambayo kuzama kwenye maji ni Raha na kuibuka raha. Unajua kunisafisha nakuwa mweupe, stamani kwenda kwengine nikachafuke.
  • Ningependa kushare nawe furaha yangu, maumivu yangu, na kila wakati wa maisha yangu. Kila ujumbe toka kwako hunijaza nguvu na matumaini. Nakupenda sana.
  • Hakuna neno la kutosha kueleza jinsi unavyonifanya nijisikie. Kila wakati ninaiona picha yako mbele yangu, moyo wangu unagonga kwa furaha kiwaza kuhusu wewe. Nakupenda sana mpenzi wangu, usije niacha mwenyewe.
  • Nashukuru kwa uwepo wako katika ulimwengu yangu. Umejaza moyo wangu furaha, upendo, na kufanya nitambue maana mapenzi ni nini. Kwangu maana ya mapenzi ni wewe. Nimeridhika kuwa nawe, Nakupenda.
  • Unaponikumbatia, nahisi niko salama na nina amani. Hakuna mahali pengine napendelea kuwa zaidi ya mikononi mwako. Nakupenda na nipo tayari kula kiapo.
  • Nimefurahi sana kuwa nawe katika kila hatua ninayoipiga maishani mwangu. Najua kwamba si kila changamoto tutayokutananayo maishani ni rahisi lakini siwezi yumba nikiwa na wewe kipenzi wangu.
  • Nakupenda sana na napenda vile umejua kunipa ninachotaka na naridhika nikikipata. Nitataka nini tena wakati penzi lako tamu nimenikamata? penzi lako ni hadimu, mbali na wewe siwezi pata.

Ni hayo tu, tuliokuandalia hapa Kwenye ukurasa huu. Usiache kufuatilia The bestgalaxy ili kujifunza mambo mengine yanayoweza kuwa muhimu kwako.

Kuwa mjanja! Tufuate kwenye akaunti zetu mpya za kijamii ; Instagram na Facebook

Jinsi ya kuongeza ubora wa picha zako za zamani kwenye simu

Unaweza piga picha yenye ubora kwenye simu yenye kamera nzuri lakini baada ya muda au kipindi flani ukawa na picha hiyo uliopiga ikiwa inaonekana haina ubora. Picha hiyo ya zamani unawezaona haina ubora baada ya kupitia kwenye mitandao ya kijamii na michakato mingine inayopunguza ubora wa picha. Mbali na hayo, baada ya kupata simu yenye kamera inayotoa picha zenye ubora zaidi, unaweza anza kuona picha ya zamani haina ubora.

Nikawaida watu kuwa na picha zao wanazoziona hazina ubora na kama ni mmoja watu hawa, hapa The bestgalaxy tunakupa mwanga kuhusu kuziongeza ubora. Unapokua na picha zisizo na ubora, kumbuka kuna huduma zinazokuwezesha kuongeza ubora wa picha. Huduma hizi ni software ambazo nyingi huiongezea picha ubora bila kukuhitaji ufanye vitu vingi. Zimewezeshwa na AI hivyo ni rahisi kutumia kiasi ambacho mtu yoyote anaweza tumia kuongeza ubora wa picha zake.

AI ni nini na inaleta matokeo gani katika Ulimwengu? BONYEZA HAPA>>>>

Jinsi ya kuongeza ubora wa picha zako za zamani kwenye simu za Android

Kwenye simu za Andoid kupata huduma ya kuongeza ubora wa picha, unaweza tumia app iitwayo UpFoto. App hii inatumia internet ila inaweza pandisha ubora wa picha yako bure na rahisi sana kuitumia. Ukihitaji kujaribu kwenye picha zako zilizopoteza ubora, fuata maelezo yafuatayo;

 

  • Nenda katika Playstore na uipakue app iitwayo UpFoto kwenye simu yako.
  • Fungua, chagua Lugha ya “English” alafu bonyeza “Start” kwenye ukurasa utaopelekwa.
  • Baada ya hapo bonyeza kitufe cha “Try now” kwenye sehemu ilioandikwa “Enhance” kisha uchague picha unayotaka kuiboresha.
  • Baada ya kuchagua, Bonyeza kitufe kilicho andikwa “Enhance” ili kuanzisha mchakato wa kuboresha hiyo picha.  
  • App ikimaliza mchakato, utaletewa picha ilioboreshwa alafu utatakiwa kubonyeza kitufe kilichoandikwa “Save” ili kuiweka picha hiyo kwenye simu yako.

Kwa kufanya hayo utakua umefanikiwa. Lakini unapaswa kujua kwamba app ya UpFoto inamatangazo ambayo utakua unakutana nayo katika kufuata hatua hizo. Mbali na matangazo, app hii itakuomba access chache kwenye simu yako na utakua unabonyeza “Allow” kuiruhusu.

Kama ubora utakua haujakulidhisha unaweza chukua picha iliotoka kwenye app hiyo, alafu ukairudisha kwenye app kuiongeza ubora kwa mara ya pili.

Dalili za kuwa mpenzi wako anakupendea pesa tu




Hapa tunaenda kuangalia viashiria au dalili za kuwa mpenzi wako anakupendea pesa. Kuna jinsi pesa inaumuhimu kwenye mahusiano ya mapenzi ya sasa na hii sio kwenye mahusiano, ni maisha kiujumla. Hata watu wa jinsia tofauti mukiamua kuwa pamoja tu kwa kushirikiana bila kuwa wapenzi bado kuna jinsi maisha yatahitaji pesa kutokana na mahitaji mulionayo kama binadamu wa dunia hii ya sasa. Hivyo pesa sio kitu kibaya au kitu cha ajambu kwenye mahusianio ya mapenzi. Lakini kitu hatari kwenye mahusiano ni kuwa kwenye mahusiano na mtu asiekupenda wewe ila anaigiza kukupenda ili apate au kufurahia pesa zako tu. Hii ni hatari maana baada ya muda au baada ya pesa kuyumba, mtu aliependa kweli anaweza anza kuumizwa.

Mazoezi ya mwili ambayo husaidia katika tendo BONYEZA HAPA>>>

Dalili za kuwa mpenzi wako anakupendea pesa tu

Kila nyuma ya jambo la upendo ni pesa




Mtu asiekupenda wewe lakini anapenda pesa zako anaweza kuwa anatumia upendo wa kuigiza kupata pesa. Unaweza tanguliza kitu kinachoonesha anakupenda lakini hapo hapo unagundua lengo la yote ni kupata pesa toka kwako. Anaweza kuwa mgomvi na hakupigii simu wala kukutafuta lakini siku akitulia na akikutafuta ni siku ambayo anashida au anahitaji pesa toka kwako.

Vitu vya kushangaza ambavyo hutokea ukimpenda mpenzi wako sana BONYEZA HAPA>>>

Usipo husisha pesa hakuzingatii kwa chochote




Pia mtu asiekupenda anaweza kuwa na tabia ya kukupuuza unaposema hauna pesa . Yani mahusiano yako na yeye yanaweza fikia wakati unaona kabisa unapotoa pesa, anakuonesha upendo lakini usipotoa anakasirika na kukupuuza kabisa kiasi ambacho upendo wake kwako unakua haupo. Kiufupi pesa ndio inakua kitu pekee kinachofanya akuzingatie na kukwambia anakupenda. Usipompatia anatafuta kila sababu ya kukasirika, kutokukutafuta na kukufanya ujione umemkosea sana.

Hatoi au kutumia pesa zake kwenye matatizo yako



Yani hata iwe unaumwa au umepata tazizo linalomuhitaji yeye aje kwa nauli au anunue kitu kawaajili yako bado atakuhusisha kwenye pesa atazotumia. Kiufupi anataka ulipie kila kitu anachokifanya kwaajili yako. Unaweza pata shida inayohitaji aje kwako au aende sehemu lakini akiambiwa anaweza kujibu “Sina nauli, nitumie”. Hawezi tumia pesa yake kwenye jambo lako hata iweje, atakuomba pesa tu.

Hajali kuhusu muelekeo wako au mahusiano yenu


Unaweza fanya maamuzi mabaya kuhusu pesa mbele yake na asikwambie kitu kuhusu maamuzi hayo. Hana wivu na wewe kwenye mahusiano unapoonekana na watu wengine, kikubwa kwake ni kumpa pesa tu. Mipango ya mbele ya pamoja kuhusu mahusiano huwa haileti na hata ukiileta haonekani kuona inamaana sana kwake. Anaweza kuwa na matumizi ya pesa mengi sana yasio husisha kujenga familia au maisha ya pamoja.



Pamoja na kuyaona mambo hayo yote kwa mwanaume au mwanaumke unaehisi anakupendea pesa inaweza kuwa haimaanishi kwa asilimia 100 yupo hivyo. Hivyo ni viashiria tu ambavyo ukiviona, itabidi uchanganye na mawazo yako kuchanganua kuwa mwanamke au mwanaume ulienae anakupendea pesa au upendo wake ni wakweli.

Game nzuri za PSP za kucheza kwenye Simu na PC

Kampuni ya Sony ni kampuni kubwa sana katika upande wa games kutokana na sababu nyingi ikiwemo kuleta vifaa vya games vyenye mafanikio makubwa ulimwenguni. Katika Miaka ya nyuma Sony ilitengeneza kifaa kidogo cha mkononi kiitwacho PSP (PlayStation Portable) kama moja ya vifaa vya games ambacho kinamuwezesha mtu kucheza games popote kama vile inavyotumika simu siku hizi. Hii PSP ilitolewa rasmi na Sony mwaka 2005 na ilikua ni bidhaa iliopokelewa vizuri sana na watu.

Kulikua kuna magemu/gemes kama 1900 hivi na zaidi ambayo mtu ukinunua PSP, unaweza kuyacheza. Lakini Baada ya muda Sony walitangaza kusitisha projekti yao ya PSP. Baada ya Sony kufanya hivyo Games za PSP na vifaa vya PSP vikaacha kuzalishwa mpaka leo. Lakini kutokana na ubora wa vifaa vya PSP na game zake kwa kipindi kile, watu mpaka sasa hawajaisahau PSP. Kuna watu mpaka sasa wana vifaa vya PSP, wengine wanaiga kutengeneza vifaa vya PSP na wengine wametafuta njia ya kuyacheza magemu ya PSP kwenye PC na Simu.

Ukitaka kucheza magame ya PSP kwenye simu au PC, utahitajika kutumia app au software ziitwazo Emulators. Moja ya Emulators za magame ya psp zinazotumika sana inaitwa “PPSPPP PSP Emulator“. Hii inafanya mpaka baadhi ya watu kuyafahamu magame ya PSP kama “Magame ya PPSPP”.

Magame ya mpira ya kucheza kwenye simu BONYEZA HAPA>>>

Game nzuri za psp za kucheza kwenye simu au PC

GTA Liberty City Stories

GTA Liberty City Stories psp

Liberty City Stories ni sehemu ya mfululizo maarufu wa magame ya Grand Theft Auto ambayo yapo chini ya Rockstar. Game hili katika upande wa PSP, ni kati ya game zuri sana kucheza katika PC na Simu pia. Unapo cheza game hili unacheza kama jamaa mmoja muhuni au muhalifu aitwae Toni Cipriani, ambaye anarudi mjini baada ya kukaa mbali kwa muda. Unaingia katika ulimwengu wa uhalifu wa Liberty City na kupambana kuwa juu katika mji huo.

God of War chain of Olympus

God of War chain of Olympus PSP

Game hili pia ni mfululizo wa magame ya God of War ambayo ni maarufu pia kwenye ulimwengu wa games. Humu unacheza kama Kratos ukipigana na miungu pamoja kutatua changamoto mbali kwa mtiririko wa simulizi ya God of War. Liliundwa SCE Santa Monica Studio na kuchapishwa na Sony Computer Entertainment kwaajili ya vifaa vya PSP. Ni game la PSP zuri kulicheza mpaka sasa.

Assassin’s Creed bloodlines

Assassin’s Creed bloodlines

Assassin’s Creed: Bloodlines katika psp ni game ambalo ambao lilitoka mwaka 2009. Magemu ya Assassin’s Creed yapo mengi katika ulimwengu wa games na hili ni moja kati ya hayo. Katika Assassin’s Creed bloodlines hili unacheza kama mtu aitwae Altair Ibn-La’Ahad. Huyo ni muhusika mkuu katika game na yupo katika miji ya Kilatini wakati wa karne ya 12(Zamani). Game la Assassin’s Creed bloodlines bado linaweza kuwa chaguo zuri mpaka sasa unahitaji kucheza game za psp maana sina stori nzuri na muonekano mzuri pia.

NFS most wanted

Need For Speed Most wanted

Ukiwa unapenda magame ya magari na unataka kufurahia game hizi upande wa PSP, game NFS most wanted linaweza kuwa zuri kwako. Game hili linaitwa “Need For Speed Most” wanted lakini unaweza liita “NFS most wanted” kwa ufupi. Need For Speed ni moja majina makubwa kwenye video games na hili game tunaloliongelea hapa, lina jina hili Kwasababu ni sehemu ya game za Need For Speed. Lilichapishwa na Electronic Arts Katika PSP na unaweza furahia mpaka sasa maana bado lipo vizuri.

Spider man 3

Spider man 3 PSP

Hili game la Spider man 3 la PSP la Spider-Man 3 ni sehemu ya mfululizo wa magame ya Spider-Man. Kuna magemu mengi ya spider man na hili ni moja ya magemu hayo lilichapichwa kwaajili ya PSP ambalo linafurahisha mpaka sasa. Humu ndani ukiwa kama spider man utapambana na maadui kama Sandman, Venom, na New Goblin.

Hapo juu tumeweka games chache TU lakini games za psp zipo nyingi sana nzuri mbali na hizo. Lakini unapaswa kujua games za psp zilisimama kutolewa hivyo hakuna games mpya za psp ambazo ni rasmi. Ila u aweza kutana na game za zamani za psp zilizo boreshwa lakini sio rasmi. Endelea kuwa karibu na The bestgalaxy kwa mambo kuhusu games na mengine.

Jinsi ya kuachana na mtu asiyekupenda

Mapenzi au mahusiano yana mambo mengi sana ya kufurahisha na kuumiza pia. Kupenda usipo pendwa ni moja ya jambo la maumivu sana katika mapenzi. Jambo hili kama haujawahi pitia, basi unaweza kuwa umewahi ona kwenye filamu au kwa mtu mwingine wa karibu yako. Ni jambo linaloumiza sana na huwa linamuumiza aliependa tu, asiependa huwa haumii maana moyo yake unakua hauhisi au kujali chochote.

Ikiwa upo kwenye hali ya kumpenda mtu asiekupenda inaweza fikia wakati akakuelewa na kuanza kukupenda pia. Hivyo usiwe mwepesi sana wa kukata tamaa.
Ila ukiona hakuna dalili nzuri za kukugeukia na kukupenda, kuachana nae ni uamuzi mzuri pia maana maumivu ya mapenzi yakizidi sio mazuri. Ni rahisi sana kumfanya mtu anaekupenda, akuchukie kuliko kumfanya mtu asiyekupenda, akupende. Kuna watu hupata magonjwa na hata kupoteza maisha kutokana na maumivu wanayopata katika kulazimisha kupendwa wasipopedwa. Kama utapenda, unaweza fuata hatua zifuatazo katika kuachana na mtu asiyekupenda kabisa.

Mambo ya kuepuka baada ya kuachana na Mpenzi wako BONYEZA HAPA>>>

Hatua za kuachana na mtu asiyekupenda

Kuwa muwazi kwake

Moyo wako unaweza kuwa unakusukuma kusema Mambo mengi sana kuhusu pendo wako kwake. Unapotaka kuachana nae, ni vema ukaufungua moyo wako kwake kwa kusema Mambo yote unayotamani ajue. Tua Kila kitu kilichokua moyoni mwako ili moyo wako na akili yako iwe huru pindi utakapokua umemgeuzia mgongo. Unaweza fanya hivi kwenye simu lakini itakua vizuri zaidi kama mtaonana kabisa na kufanya mazungumzo. Kama ni mwanaume au mwanamke, kuwa huru kumwambia vitu ambavyo badae havita uvuta moyo na kukusumbua kuwa huku mwambia. Mwambie jinsi gani unapenda, unatamani aweje kwako na ikiwezekana mwambie na anakupa shida kiasi gani.

Kumbuka thamani yako

Kumpenda mtu kunaweza kusahaulisha thamani yako. Ukiwa unalazimisha sana kupendwa usipopendwa, kunajinsi unaweza jihisi hauna thamani. Lakini ukweli ni kwamba, thamani hua inakua pale pale. kila mtu ana thamani hapa Duniani haijalishi unapendwa au haupendwi. Kikubwa ukumbuke au utambue thamani yako tu alafu baada ya hapo unaweza anza kujiamini kwenye mambo yako na maamuzi yako.

Zingatia vitu vingine na kujiweka mbali nae

Kumzingatia mwanamke au mwanaume alietambua upendo wako kunaweza kukuyumbisha hata kimaisha au kiuchumi bila kukuletea faida yoyote mwishoni. Ni vema ukaanza kuzingatia vitu vingine vinavyoweza rahisiha maisha yako au kukuletea faida mwishoni. Wekeza muda wako kwenye kujifunza vitu vipya, kufanya mazoezi au kazi. Wakati ukifanya hayo hakikisha unajiweka mbali na mtu asiyekupenda.

Jipe muda wa kusahau

Tambua kuwa maumivu ya kumuacha mtu unaempenda hayawezi kuisha katika siku moja au mbili. Yanaweza kuchukua muda mrefu kidogo na ili uweze kufikia hatua ya kuto kuumia. Unapaswa kukubaliana na kila kitu alafu ujipe muda wa kusahau. Pamoja na maumivu unavyoweza pitia unapaswa pia kujikumbusha kuwa “Maumivu yote yataisha,utakua vizuri na utapenda mtu mwingine”. Kunasiku unaweza fanikiwa kumtoa moyoni au kupunguza maumivu aliokupatia.

Wakati unajipa muda wa kusahau usisahau kufuahi, fanya vitu salama vinavyokupa furaha huku ukipanga mipango mipya ya siku zijazo.

Jinsi ya kutengeneza au kurekodi Nyimbo kwa kutumia Simu

Kutengeneza nyimbo kwa kutumia simu inawezekana? Ndio, inawezekana na nyimbo unayotengeneza kwa kutumia simu inaweza kuwa na mafanikio makubwa tu kama nyimbo za Studio rasmi. Kipindi cha nyuma, ukiwa kama msanii wa Muziki ilikua ni lazima uhusishe vyumba vya Studio rasmi vinavyomilikiwa na maproduser ili kufanya mazoezi ya nyimbo na kurekodi nyimbo zako. Lakini kwa sasa, hakuna ulazima sana wa kwenda huko kama hauna uwezo. Unaweza tumia simu yako ya mkononi kufanya mazoezi ya kurekodi nyimbo zako na hata kurekodi kabisa ukiwa nyumbani tu.

Jinsi ya kutengeneza au kurekodi nyimbo kwa kutumia simu

Unaweza tengeneza au kurekodi nyimbo iliokamilika kwenye simu ila utatakiwa kuwa na app maalumu kwa kazi hiyo. App zipo nyingi na kati ya app hizo kuna app ngumu kutumia, pia kuna app rahisi kidogo zisizo hitaji mambo mengi kwenye kuzitumia. Moja ya app ambazo ni rahisi kutumia ni app iitwayo “Voloco”. Inapatikana katika Playstore kwa simu za Android na hata Appstore kwaajili ya watu wa iPhone au vifaa vya iOS kwa ujumla.

App ya Voloco inahusiana zaidi na kuweka Voco kwenye Beat. Unaweza ingiza Beat lako mwenyewe au ukadownload humo humo ndani Beat zilizotengenezwa na watu wengine. Ni ngumu kukuelezea kila kipengele cha app hii kwa maandishi ili uweze kuitumia ila tumejaribu kukuelezea hapa chini kwa msaada wa picha vitu vya muhimu kuvijua utakapo fungua app hii.

Kutengeneza nyimbo ni project na kwenye app hii kitu cha kwanza utakachotakiwa kukifanya ni kutengeneza au kufungua project mpya. Ukisha fungua project mpya unaweza weka Beat unalotaka kuliimbia kwenye project hiyo alafu ukaanza kurekodi sauti au voco zako. Uzuri ni kwamba Ina Autotune hivyo kunajinsi sauti au voco zako zinaboreshwa.

Unashauriwa kuvaa Earphone unaporekodi voco zako. Baada ya kumaliza kila kitu kwenye project hiyo, unaweza itunza project yako kwenye app hiyo.


Ukihitaji kuitoka kama audio za kawaida unaweza ingia kwenye project ulizo tunza alafu ukabonyeza vidoti vitatu vilivyo kwenye project yoyote unayoyahitaji alafu ukaugusa “Download” ili kuidownload nyimbo uliotengeneza iwe kwenye simu yako. Utakua na chaguo la kutunza iyo nyimbo kama Audio au video. Nyimbo yoko itakua tayari lkuisikiliza japo unaweza pia kuipitisha kwenye software nyingine ili kuiweka kwenye ubora zaidi au kuibadilisha kuwa mp3 kama utahitaji.

Ujumbe wa siku ya kuzaliwa kwa Mpenzi au Rafiki

Moja ya siku au tarehe ambazo watu wanaweza ya ona zina umuhimu sana kuzijua kwenye maisha yao ni siku ya kuzaliwa. Na ni kweli zina umuhimu maana katika mambo mengi huwa watu wanahitajika kutaja siku au tarehe ya kuzaliwa. Mara nyingi hii inaweza kuwa ni kwaajili ya kudhibitisha umri maana mtu anaweza kujua umri wako kwa kujua siku uliozaliwa(tarehe,mwezi au mwaka). Umri wa mtu ni tofauti kati ya siku mtu aliozaliwa na siku aliopo.
Katika jamii zetu siku ya kuzaliwa imewekwa mbele sana kwa baadhi ya watu kiasi kwamba inakua inakumbukwa kila mwaka na kusherehekewa. Sio jambo la ajabu na sio jambo la lazima pia.

Jinsi ya kufanya mpenzi wako akuwaze kila mara BONYEZA HAPA>>>

Kama unampenzi au rafiki anaejali siku yake ya kuzaliwa, unaweza mfanyia jambo lolote la furaha katika siku yake ya kuzaliwa na akafurahi. Na inasemekana hata ambao hawazisherehekei na kuzijali siku zao za kuzaliwa, wanajiskia vizuri sana wakifanyiwa jambo lolote la furaha kuhusu siku yao hiyo. Hivyo ukiwa na rafiki au mpenzi hata ambae hajali kuhusu siku yake ya kuzaliwa, unaweza mfurahisha kwa kuonesha unaijali siku yake.

Katika birthday au siku ya kuzaliwa ya mtu, unaweza fanya mambo mengi kumfurahisha ikiwemo kumpa zawadi au kumtumia ujumbe kwenye simu. Hapa chini tumeweka baadhi ya jumbe au sms za kumtumia mpenzi au rafiki katika siku ya kuzaliwa.

SMS za kumbembeleza mpenzi wako BONYEZA HAPA>>>

Sms au Ujumbe wa siku ya kuzaliwa kwa mpenzi na rafiki

  • Mtu ambea ni mwanga wa maisha kwangu ni wewe. Napenda kila wakati ukumbuke kuwa furaha ya moyo wangu ni wewe. Nakutakia siku ya kuzaliwa yenye baraka tele.
  • Happy birthday rafiki yangu. Nakutakia maisha marefu na yenye furaha. Baraka na mafanikio ziwe katika Maisha yako na kila jema lisiache kukufuata.
  • Heri ya siku ya kuzaliwa rafiki yangu kipenzi. Natumai siku yako itakua nzuri na furaha. Napenda kukuona na furaha hivyo napenda kuona ukifurahia siku hii muhimu kipenzi.
  • Mpenzi wangu, Kuzaliwa kwako ni siku muhimu kwangu. Maana huo ni wakati zawadi yangu nzuri ililetwa toka kwa mungu. Nakupenda sana zawadi yangu, pia nakutakia maisha marefu yenye afya njema na furaha.
  • Happy birthday rafiki mpendwa! Nakutakia kila wakati kupata nguvu na msukumo wa kutimiza matamanio yako hapa Dunia. Maisha ni safari na nakutakia kila jema kwenye safari yako rafiki yangu.
  • Ninafuraha sana Leo maana ni siku mbayo malaika wangu ulizaliwa ili uje kuangaza maisha yangu. Kuwa na wewe na Raha sikufichi. Happy birthday my queen.
  • Nakupenda sana. Napenda jinsi unavyonifanyia katika Upendo na maisha kiujumla. Nafurahi kuwa na wewe. Tunapitia mengi ila daima nitakupenda wewe. Hicho ndio kitu natamani ujue katika siku hii, happy birthday mpenzi!
  • Nakutakia siku njema ya kuzaliwa rafiki yangu. Wewe ni mtu ambaye anamaanisha mengi kwangu na ambaye ninathamini sana wepo wako. Uishi maisha marefu rafiki yangu.
  • Kila siku ninapokuwa nawe ni zawadi kubwa. Siku ya kuzaliwa yako ni fursa kwangu ya kusherehekea upendo wetu. Heri ya siku ya kuzaliwa, mpenzi!
  • Upendo wangu kwako hauwezi kuelezwa kwa maneno yakatosha. Lakini katika siku hii ya kuzaliwa nataka nijaribu tu kwa kumwambia Nakupenda sana na uishi maisha marefu kipenzi changu. Happy birthday!
  • Ningekua na uwezo ningeiweka siku yako ya leo iwe ni siku ya kitaifa my love. Natamani Kila mtu ajue siku ya leo ndio siku mtu alieuweza mayo wangu na kunipa furaha maishani amezaliwa. Nakutakia siku njema na maisha marefu.

Sms hizi au jumbe hizi zina maneno mazuri ya siku ya kuzaliwa kwa rafiki na hata mpenzi. Unaweza zitumia bure kwa mpenzi wako mwanaume au mwanamke au rafiki. Kikubwa uchague ipi ni sahihi kuitumia kwa upande wako.

Kuwa mjanja! Tufuate kwenye akaunti zetu mpya za kijamii ; Instagram na Facebook.

Mambo 5 ya kujua kuhusu Tattoo

Pamoja na kwamba watu wengi wanaonekana wanachora tottoo kipindi hiki, lakini mabaki ya binadamu walioishi miaka iliopita yanaonesha kwamba tattoo hazijaanza kuchorwa miaka hii. Totoo zilianza kuchorwa toka zamani na mpaka sasa binadamu wameendelea kuzichora.


Kwasasa tottoo huchorwa kwa kifaa maalumu kinacho tumia sindano kuingiza wino katika ngozi. Hii inaweza kuwa ni tofauti na zamani kutokana na utofauti wa kiteknolojia.
Watu ambao huusika na kuchora tatoo kwa kiingereza huitwa “tattoo artists, tattooer au tattooist”. Kuchora tattoo ni sanaa kama sanaa nyingine lakini kuchora tattoo kumekua na mitazamo mingi sana kwenye jamii.
Hapa The he bestgalaxy, tunakupa mambo machache kuhusu Tattoo au uchoraji wa tattoo. Tende pamoja kuangalia mambo haya pengine lakini utapenda kuyajua.

Mambo 5 ya kujua kuhusu Tattoo

Wino mweusi

Katika kuchora tattoo, wino wa rangi nyeusi ni wino ambao ukichorea tattoo kwenye mwili, unakua ni rahisi ukuuondoa unapoifuta. Tattoo zinaweza kufutika kwa kutumia kifaa kinachotumia mionzi kinachoitwa Laser. Lakini kufuta Tattoo huambatana na maumivu. Wino mweusi unaweza kufutika kirahisi zaidi kama itakua ni ya wino mweusi.

Sindano huchoma ngozi mara 50 hadi 3000 kwa dakika

Mashine ya kuchorea tattoo Ina sindano ambayo hutumia kuingiza wino katika ngozi. Sindano hii unapoiweka katika ngozi ili kuingiza wino, huichoma ngozi kwa haraka mara 50 hadi 3000 kwa dakika moja. Jambo hili ndio huleta maumivu flani mtu anapochora tattoo. Lakini sindano hii huishia kwenye ngozi tu, haitakiwi kuchoma zaidi mpaka ndani kabisa ya mwili.

Asilimia 23 ya watu hujutia kuchora tattoo na hujutia zaidi majina.

Katika tafiti inaonekana kuwa baadhi ya watu hujutia maamuzi yao ya kuchora tattoo. Asilimia 23 ya watu waliochora tattoo imeonekana kujutia maamuzi yao ya kuchora tattoo hasa tattoo za majina. Na hii, kama utakua ni mfuatiliaji wa watu maalufu mtandaoni, unaweza kuwa tayari umeisha kutana taharifa za wasanii au watu maharufu wakijutia maamuzi ya kuchora tattoo kama hizo.

Tattoo ya thamani kubwa kuwahi kuchorwa.

Katika historia ya kuchora tattoo, tattoo ya thamani kuwahi kuchorwa ni yenye thamani ya Dola 924,000 za kimarekani. Hii ilikua ni tattoo ya muda mfupi iliochorwa kwa kujumuisha vipande vya almasi. Lakini tattoo hii iliochorwa kwa lengo la kuwa kama tangazo. Kampuni ya Shimansky ndio ilihusika na jambo hilo na aliechorwa tattoo hii alikua ni mwanamke model aitwae Minki van der Westhuizen.

Kuchangia damu.

Kuchora Tattoo hakukuzuii kuchangia damu kama utakua umekidhi vigezo vya kuchangia damu. Kumekua na baadhi ya watu wamekua wakijua kuwa ukichora tattoo hautaweza changia damu maishani mwako. Jambo hilo sio kweli, unaweza kuchangia damu bila shida kama utakua umekidhi vigezo vya kiafya vinavyohitajika kuchangia damu. Ila ukichora tattoo unatakiwa kukaa kwa miezi 3 au 6 ndipo ufanyiwe vipimo, uchangie damu.

Kuchora Tattoo sio jambo lisilo hitaji utaalamu. Kama umefikia uamuzi wa kuchora tattoo, unashauriwa kuwatumia wataalamu wa jambo hilo na sio kuchora hovyo tu. Hii ni Kwasababu kunavitu muhimu visipo zingatiwa unaweza jiwekea kwenye hatari zaidi kiafya kuliko tattoo yenyewe. Usalama usipo zingatiwa kwenye sindano, unaweza ambukizwa magonjwa. Pia Kuna wino wa tattoo huwa unapigwa marufuku kwasababu za kiafya lakini mtu asie mtaalamu wa mambo ya tattoo anaweza tumia wino huo kisa sio gharama kwake. Ukiachana na uliopigwa marufuku, wino mwekundu wa tattoo sio mzuri sana maana unaweza sababisha upere japo sio kwa wote. Nafikili umefurahia kujua mambo haya, usiache kufuatilia The bestgalaxy.

Jinsi ya kujiondoa kwenye post mbaya ulizoshirikishwa Facebook

Facebook inaruhusu kushirikisha mtu kwenye picha au post yako na huwa tunaita ku “Tag”. Mtu unaemshirikisha kwenye post yako anatakiwa kuwa ni rafiki yako wa Facebook. Kumshirikisha mtu ambae hamna urafiki kwenye Facebook haiwezekani kwa kumtag ila unaweza tumia kipengele cha kutaja (mention) kama njia ya kumshirikisha mtu.


Mtu unapo shirikishwa kwenye post kwa kipengele cha “Tag” na rafiki yako mmoja, marafiki zako wengine wanaweza pata taharifa kuwa umeshirikishwa kwenye post hiyo. Na endapo picha ulioshirikishwa itakua ni picha mbaya au usio taka kushirikiswa, Bado unauwezo wa kujiondoa.

Jinsi ya kujua kama akaunti yako ya Facebook ni Salama BONYEZA HAPA>>>

Jinsi ya kujiondoa kwenye post mbaya ulizoshirikishwa Facebook

Hapa chini tunaenda kukuelekeza hatua kwa hatua jinsi ya kujiondoa kwenye post waliokutag katika Facebook lakini hautaki kuhusishwa. Jambo zuri ni kwamba ukijiondoa, aliekutag hawezi pokea taharifa kuwa umejiondoa.
Ili mtu kugundua kuwa umejiondoa kwenye post aliokushirikisha itambidi azingatie vitu viwili. Cha kwanza ni idadi ya watu aliowashirikisha na Cha pili ni kuzingatia uwepo wa jina lako kwenye orodha ya watu aliowashirikisha. Watu wengi hawazingati jambo hili wanapo post picha na kushirikisha wengine katika Facebook japo.
Unaweza fuata hatua hii kuondoa Tag

  • Ingia katika Facebook na uende Katika post waliokutag
  • Bonyeza vidoti vitatu vilivyo upande wa pembeni katika post hiyo.
  • Chagua “Remove Tag” kwenye orodha ya chaguzi utazoziona.
  • Bonyeza”CONFIRM” ili kuthibitisha maamuzi yako ya kujiondoa kwenye post hiyo.

Ukisha fanya hivyo tu, post itakua uhusiano na wewe tena. Utakua umefanikiwa kujiondoa kwenye post hiyo na kama ilikua inaonekana kwenye orodha ya post zako, itaondolewa. Lakini kama ikitokea watu wengine au post mpya unaweza shirikishwa tena kama kawaida.

Mambo ya kushangaza usioyajua kuhusu Wanawake na Wanaume

Kuna mambo ya kushangaza usioyajua kuhusu Wanawake na Wanaume ila hapa tunaenda kukujuza.
Ulimwengu una Mambo mengi sana na hakuna binadamu anaweza yajua yote ila huendelea kujifunza au kujua mambo hayo akiwa anaishi . Hii ndio maana hata kuna watu wanasema “kuishi ni kujifunza”. Ukiwa kama binadamu, unapo ishi unakua unajifunza vitu mbalimbali kwenye maisha yako kwa kuyapitia, kuyaona na hata kuambiwa. Inasemekana kuwamba watu wengi wanaopata mafanikio makubwa katika Maisha huwa wanauwezo wa kupokea na kujifunza vitu vipya. Na sisi The bestgalaxy tuliwahi toa maelezo ya kwamba kuwa tayari kujifunza vitu vipya ni moja ya mambo ya msingi sana ili kupata mafanikio.


Lakini hapa hebu tuachane na mambo ya mafanikio, tuongele Mambo ya kushangaza usioyajua kuhusu Wanawake na Wanaume kama tulivyo sema. Katika vitu ambavyo tunaenda kuzungumza hapa, kunauwezekano ukawa unavijua au hauvijui lakini unapaswa kufahamu kuwa inasemekana ni vya kweli kuhusu Wanawake na Wanaume.

Ukiona dalili hizi ujue akaunti yako ya Facebook si salama BONYEZA HAPA>>>

Mambo ya kushangaza usioyajua kuhusu Wanawake na Wanaume

Wanawake hufanya vitu vingi kwa wakati mmoja.

Hii inaweza kuwa imeshuhudiwa mara nyingi katika Maisha ya mwanamke. Mwanamke anauwezo wa kufanya kazi nyingi kwa wakati mmoja. Mfano mzuri unaweza kumuona mwanamke alieolewa yupo na watoto nyumbani. Akiwa hapo nyumbani anaweza kuwa anapika, anamuhudumia mtoto na kufanya usafi wa nyumba kwa muda huo huo. Kazi zote hizi ninamtegemea yeye wakati huo na zinaweza kuisha bila matatizo.

Nywele za wanaume kukua haraka.

Tafiti zinaonesha kuwa Kuna utofauti katika ukuaji wa nywele za wanaume na wanawake. Wanaume wameonekana kuwa na nywele zinazokua haraka kuliko nywele za wanawake. Lakini utofauti ni mdogo sana na sio kila kuchelewa au kuwahi kukua kwa nywele husababishwa na jinsia. Kuna mambo mengine kama umri, afya au asili yanaweza sababisha nywele ziwahi au kuchelewa kukua .

Wanawake huishi miaka mingi.

Pia kunatafiti ambazo zinaeleza kuwa wanawake wameonekana kuishi muda mrefu hapa Duniani kuliko wanaume. Mnamo mwaka 2021, tofauti kati ya wastani wa muda wa kuishi kati ya wanawake na wanaume ulitofautiana miaka 5. Wastani wa umri wa kuishi ulikuwa umeonekana ni miaka 73.8 kwa wanawake na miaka 68.4 kwa wanaume. Watani huu unaonesha ni jinsi gani wanawake mara nyingi huishi kwa muda mrefu ukilinganisha na Wanaume.

Mazoezi ya mwili ambayo husaidia katika tendo BONYEZA HAPA>>>

Wanaume huongea maneno machache.

Katika kuongea, wanaume wanaonekana kuwa na kiwango cha chini cha maneno kuliko wanawake. Tafiti zinaonesha kuwa wanawake huongea maneno mengi zaidi ukilinganisha na wanaume. Wakati wanaume wanakadiliwa kuwa na uwezo wa kuongea maneno 13,000 kwa siku, mwanamke anakadiliwa kuongea maneno zaidi ya 20,000. Hii inaonesha utofauti wa kuongea upo kwa kiwango kikubwa.

Wanawake wanawaza mbele kuhusu mahusiano na familia.

Mwanamke mara nyingi huwaza mbali au mbele sana kuhusu mahusiano na familia. Mwanaume anaweza kuwa kwenye mahusiano akawa anawaza zaidi mafanikio ya kazi anayoifanya au kutimiza malengo lakini asiwaze mbali kuhusu familia kama jinsi mwanamke anavyowaza. Mwanamke anaweza waza kuhusu mume, watoto na hata mtindo wa maisha ya familia kwenye kipindi ambacho mwanaume anaweza kuwa bado hajawaza kumuoa. Mwanamke kwenda mbele sana kwenye upande huu ni jambo zuri maana hutengeneza familia.

Hayo ni baadhi tu ya mambo ya kushangaza usioyajua kuhusu Wanawake na Wanaume. Nina Imani utakua umejifunza kitu katika muda uliotumia kusoma makala hii. Endelea kuwa karibu The bestgalaxy kwa mambo mengine mbali na haya.