Ukiangalia jatika maisha ya sasa, ugundua kuwa wanaume wengi hawaoi mapema kama zamani. Badala yake, wengi wanachagua kuzingalia mahusiano ya muda mfupi yasio husisha ndoa. Hii imesababisha hata wanawake kuona kutolewa sio jambo rahisi katika kipindi hiki.
Wengi kujiuliaza; kwanini wanaume wanachelewa kuoa siku hizi?
Hapa chini Kuna sababu tano zinazo changia hali hii katika ulimwengu wa sasa.
Sababu 5 za Wanaume Wengi Wanachelewa Kuoa
1. Ugumu wa maisha
Maisha yamekuwa na gharama kubwa kuliko zamani. Kodi ya nyumba, chakula na mahitaji mengine yamepanda sana. Wanaume wengi wanahisi ni muhimu kuwa na kipato kizuri kabla ya kuoa. Kwa sababu hiyo, wanachagua kusubiri hadi wajipange vizuri kimaisha kwenye upande wa kifedha.
2. Mabadiliko ya majukumu ya mwanaume na mwanamke
Zamani kulikuwa na majukumu yaliyoeleweka na kukubalika kwa kila upande wa jinsia. Wanaume alikua wanakaa upande wao wa majukumu na mwanawake pia hivyo hivyo.
Lakini hivi sasa mambo yamebadilika sana. Wanawake na wanaume wote wanapambana kujenga maisha tofauti wanayo yahitaji.
Hii wakati mwingine huleta mchanganyo kiasi cha wanaume na wanawake kushindwa kuwa pamoja.
3. Hofu ya matatizo ya ndoa
Wanaume wengi wanaona au kusikia kuhusu migogoro ya ndoa, talaka na changamoto za mahusiano. Kuna watu wapoteza Mali na kufilisiwa kabisa kupitia swali la ndoa.
Hali hii huwafanya wawe waangalifu zaidi. Wengine wanaamua kuchelewa kuoa ili kuepuka kuingia kwenye matatizo hayo mapema.
4. Maisha ya uhuru (Single life)
Maisha ya bila ndoa yanaonekana kuwa na uhuru zaidi. Mtu anaweza kufanya maamuzi yake mwenyewe bila kuhusisha familia. Kwaiyo wanaume wengi huona kama wakiingia kwenye ndoa, watahitajika kuacha vitu vingi na kuingia kwenye sehemu inayo wabana.
Hii huwafanya baadhi ya wanaume kuchelewa kuoa huku wakifurahia maisha ya kwa Single.
5. Mabadiliko ya mitazamo kuhusu ndoa
Siku hizi, ndoa si lazima kama ilivyokuwa zamani. Watu wengi wanaamini unaweza kuwa na furaha hata bila kuoa. Yani mtu huona kuna mambo mengi anaweza kufanya na akafuria maisha yake mbali na kuwa kwenye ndoa.
Hii inafanya ndoa kuonakana ni uamuzi usio wa lazima kwenye maisha.
Na hata mitandao ya kijamii imebadilisha jinsi watu wanavyoona mahusiano na ndoa. Imechangia sana watu kuzingatia zaidi “Mahusiano” na sio “Ndoa”.
Kwa kifupi, wanaume wengi wanachelewa kuoa si kwa sababu hawataki, bali kwa sababu wanataka kuwa “tayari” kwanza. Wengine wanajipanga, na wengine wapo kwenye hizo sababu nyingine.
Ndoa bado ina thamani ndio maana bado Kuna wanaume wengine wanawahi kuoa na wanafurahia zaidi maisha yao.