Ishara 5 za Mwanamke Anaekuchukia kwenye Mahusiano

Mwanamke anaweza kukupenda na mukaingia kwenye mahusiano ya furaha sana. Lakini katika mahusiano yoyote, mambo yanaweza kubadilika na akaanza kukuchukia au kutokukupenda tena. Hii hutokea pia kwa wanaume, lakini kwa sababu tunazungumzia mwanamke, hebu tuchimbe zaidi.

Mwanamke kukuchukia katika mahusiano huwa kunakuwa na sababu. Inaweza kuwa umemkosea, amepata mtu mwingine, au ameona mahusiano hayo hayamfaidi kutokana na matarajio yake. Mara nyingi ni vigumu kwa mwanamke kusema moja kwa moja kuwa hakupendi tena, lakini kuna ishara ambazo ukiziona, unajua kabisa kuna kitu kimebadilika.

Jinsi ya kupata Mpenzi mtandaoni BONYEZA HAPA>>>

Ishara 5 za mwanamke anaekuchukia kwenye mahusiano

1. Hajibu SMS wala kupokea simu zako

Kama mwanamke anakupenda, ni lazima azingatie mawasiliano. Atapokea simu zako na kujibu ujumbe wako hata akiwa busy.
Lakini akiwa anakuchukia, hupuuza sana simu na ujumbe wako. Simu zako huwa kama usumbufu kwake, ujumbe wako unaweza kusomwa lakini usijibiwe. Hii ni ishara kuwa upendo umepungua au haupo kabisa.

2. Anasema yupo busy kila mara

Ni kweli binadamu anaweza kuwa busy sana, lakini si kwenye vitu anavyovipenda. Mara nyingi tunapata muda kwa watu tunaowapenda hata tukiwa na shughuli nyingi kuliko muda. Ni ngumu mtu kuwa busy kiasi cha kukosa muda kabisa kwa mtu anayempenda, hasa kwa wanawake.

Lakini mwanamke akikuchukia, atakuwa busy kila mara. Hatakupa muda wake, wala hatataka umpe muda wako.

3. Hataki mkutane tena

Kama mwanamke mlikuwa mnapanga kukutana na mnatimiza, lakini ghafla hataki tena, hiyo ni ishara mbaya. Mwanamke asiyekupenda anaweza kuanza kukukwepa kila linapokuja suala la kuonana.

Anaweza kuweka mgomo wa kukutana kimwili na hata kuonana kwa maongezi ya kawaida. Anaweza kutafuta kila sababu ya kutokua huku akikupa ahadi hewa za kuonana mfululizo mpaka pale utakapogundua mwenyewe kuwa hataki.

4. Mengi unayofanya yanakuwa mabaya kwake

Mwanamke anaekuchukia huwa anaona mabaya yako tu hata ukijitahidi kuwa mzuri kwake. Unaweza kufanya mambo mazuri ili kuugusa moyo wake, lakini ukaambulia dharau na lawama.

Yani unaweza kujikuta unakosea kila unachofanya, hata kama makosa hayo hayakuhusu.

5. Hakutambulishi kwa watu wake wa karibu

Mwanamke akikupenda kweli huwa ni ngumu kuwaficha watu wake wa karibu kuhusu wewe. Anaweza kuwaambia marafiki zake kuwa yupo kwenye mahusiano, na hata kukutambulisha kwa ndugu zake.

Lakini kama anakuchukia, ni ngumu sana kukutambulisha kwa watu wake au kuwaambia wale walio karibu naye kuhusu uhusiano wenu.

Leave a comment