Jinsi ya kuitambua Picha au Video iliotengenezwa na Ai


Miaka michache iliyopita, ilikua rahisi sana kutambua video au picha zilizotengenezwa na AI (Artificial Intelligence). Mara nyingi, picha au video hizo zilikuwa na makosa mengi ya wazi.
Kwa mfano, mtu kwenye picha angeweza kuonekana na vidole saba, au mikono mitatu, jambo lililofanya iwe rahisi kuelewa kuwa hiyo ni kazi ya AI.

Lakini siku hizi mambo yamebadilika. AI imekua ya kisasa zaidi na makosa yake yamepungua sana. Kwa sasa, ni vigumu sana kutofautisha picha au video halisi na zile zilizoundwa na AI. Kutokana na hilo, mitandao mingi ya kijamii imeanza kuweka alama maalum (label) kwenye maudhui (picha au video) yaliyotengenezwa na AI, ili kuwasaidia watumiaji kutambua kwa urahisi.

Pamoja na hayo, bado kuna ugumu  kwa watu wengi katika kutofautisha picha au video halisi na zile za AI; hasa kama zimeundwa vizuri.

Hapa The Bestgalaxy, tumekuandalia njia rahisi za kuitambua picha au video iliyotengenezwa na AI, ili usipoteze muda au kudanganywa mtandaoni. Pia ni njia ya kujilinda dhidi ya matapeli wanaotumia maudhui ya AI kwa udanganyifu.


Mambo ya Ajabu yanayofanywa na Ai katika ulimwengu wa sasa BONYEZA HAPA>>>

Jinsi ya kuitambua Picha au video iliotengenezwa na Ai



1. Tumia Platform Maalum Kutambua Kazi za AI

Njia ya haraka na rahisi zaidi ni kutumia tovuti maalum zilizoundwa kwa ajili ya kutambua kama picha au video imetengenezwa na AI.
Mfano wa tuvuti kama hii ni Ai or Not. Hii tuvuti inakuruhusu kuweka picha au video, kisha inakupa matokeo ikiwa ni ya AI au halisi.

Hii ni njia nzuri sana lakini kuna baadhi ya picha halisi huwa zinaweza kuonekana ni kazi za Ai kwenye njia hii. Hili linaweza kutokea endapo picha au video halisi itapitishwa kwenye michakato inayohusisha Ai. Michakato hii inaweza kuwa hata kuongeza ubora kwa kutumia Ai tu.

Kwaiyo kiufupi kuna Picha au Video halisi huwa zinaweza kuonekana kama sio halisi(za Ai) kwasababu zimeongeza ubora tu kwa kutumia Ai.

Hii ni website ya Ai or Not ikitoa majibu juu picha. Majibu ya picha hii yamesomeka “Likely AI Generated” ikiwa ni ishara yakwamba picha imetengenezwa na AI.




2. Angalia Vitu Hivi Kwa Macho Yako

Kama hutaki kutumia tovuti au programu maalum, unaweza kutambua mwenyewe kupitia dalili ndogo zifuatazo:

  • Rangi zilizokolea kupita kawaida: Video/Picha za AI mara nyingi huwa na rangi ang’avu kupita kiasi, zisizo za kawaida kuwepo kwenye picha halisi.
  • Mabadiliko madogo kwenye video: Wakati mwingine vitu vidogo hubadilika ghafla, kama sura, madoa ya nguo, macho, au mwanga. Hii ni ishara ya AI.
  • Sauti yenye uroboti: Video za AI (hasa deepfake) mara nyingi zinakuwa na sauti nyepesi au zenye mwangwi kama sauti za roboti (robotic tone).



AI imefika mbali sana lakini bado unaweza kuitambua ukitumia umakini. Ingawa zinatambulika ila kumbuka kuwa sio kila kitu kinachoonekana halisi mtandaoni ni cha kweli. Baadhi ya video au picha zinawezakuwa ni ngumu kutambua mpaka alietengeneza aweke wazi.

Leave a comment