Watu wengi wanaotuma na kupokea pesa kwenye simu zao hapa Tanzania huwa wanatumia huduma za kifedha za mitandao ya simu ikiwemo Mixx by yas kutoka Yas(Tigo).
Mixx by yas imekua moja ya njia nzuri za kutuma na kupokea pesa toka miaka nyuma ambayo ilikua inaitwa “Tigo Pesa”.
Mbali na kutumika kutuma na kupokea pesa, Mixx by yas huwa ina huduma nyingine ndani yake zinahusisha fedha. Katika huduma hizo, kuna huduma ambazo zimelenga kumsaidia au kumuwezesha mtumiaji wao.
Katika Makala hii, tutajikita katika huduma yao ya mikopo inayomuwezesha mtu kukopa pesa zinazoweza kumsaidia kwenye mambo mbalimbali. Ikiwa unahitaji kujua namna ya kukopa pesa katika akaunti yako ya Mixx by yas, basi hapa ndio mahali pake.
Mambo ya kuzingatia unapochukua Mkopo kwenye app za mikopo BONYEZA HAPA>>>
Kukopa Pesa katika akaunti ya Mixx by yas
Kama unahitaji kukopa pesa katika akaunti ya Mixx by yas na uwe huru kuitumia kwenye mambo mbalimbali basi utatakiwa kutumia huduma yao ya “Nivushe plus“. Nivushe plus ni huduma ya Mixx by yas inayokuwezesha mtumiaji kukopa kiwango flani cha pesa na kukilipa katika muda uliochagua kurejesha. Unapewa uhuru wa kuchagua ni muda gani utarejesha(inaweza kuwa baada ya wiki kadha au mwezi mmoja kabisa).
Kama ilivyo mikopo mingine, Nivushe plus pia huwa ina riba ingawa ni kiwango kidogo sana ukilinganisha na baadhi ya huduma za mikopo. Ukiachilia mbali kuwa na riba kidogo, Nivushe plus ni huduma ya haraka sana ya Mkopo kwa watumiaji wa Yas (Tigo).
Jinsi ya kukopa pesa Nivushe plus
Njia rahisi ya kukopa pesa katika Nivushe plus ni kupitia app ya “Mixx by yas“. Kama una app hii kwenye simu yako, fanya yafuatayo:
- Fungua app ya Mixx by yas
- Chagua kipengele Cha “Mikopo” kinachoandikwa “Loans” kwa lugha ya kiingereza.
- Baada ya hapo, chagua “Nivushe plus” kwenye chaguzi zitakazokuja.
- Ukishachagua, utapelekwa kwenye ukurasa maalum wa kuchukua, kuangalia na kurejesha mikopo.

Kwenye ukurasa huo unaweza kukopa Mkopo na kuangalia taalifa nyingi za mikopo. Taalifa hizo ni pamoja na Salio la deni, kiwango chako Cha kukopa na hata historia ya malipo yako.
Kiwango unachoweza kukopa katika Nivushe plus huwa kinaongezeka kutoka na mambo kama miamala unavyofanya kwenye akaunti yako na uaminifu katika kurejesha mikopo. Mara nyingi mtu muaminifu na mwenye miamala mikubwa huwa anakua na kiwango kikubwa cha kukopa. Lakini kitu muhimu zaidi ni uaminifu. Ukiwa vizuri unaweza kukopa hadi milioni 2 (Tsh 2,000,000)