Ikiwa wewe ni kijana mwenye miaka 20 na kuendelea, kuna mambo muhimu sana unatakiwa kujua kuhusu safari ya kufikia ndoto zako.
Kila mtu huwa na ndoto kubwa maishani, lakini ni wachache sana wanaoweza kuzitimiza.
Sababu kubwa inayofanya wengi washindwe si kwa sababu hawana uwezo, bali ni kutokana na kutoanza kuzikimbiza kabisa. Hapa chini tunakupa baadhi ya mambo yanayokwamisha watu wengi kukimbiza ndoto zao. Unaweza kuyapitia ili kuwa na kuelewa kwenye mapambano ya kukimbiza ndoto zako.
Jinsi ya kulinda ndoto zako zisife maishani BONYEZA HAPA>>>
Mambo yanayokwamisha Watu kukimbiza Ndoto zao
1. Kusubiri Wapate Kitu cha Kuanzia
Watu wengi wana mawazo makubwa ya biashara, miradi au mipango ya kubadilisha maisha yao, lakini hawachukui hatua kwa sababu wanasubiri kupata mtaji au kusaidiwa na mtu mwingine ili waanze.
Hii ni moja ya sababu zinazowafanya watu wengi wabaki pale pale walipo kwa miaka mingi, wengine mpaka wanazeeka bila kufanikisha kitu.
Ukweli ni kwamba, ni nadra sana kuona mtu kakupa mkono wa kukuanzishia. Badala ya kusubiri, tafuta njia zako mwenyewe za kuanza hata kidogo.
Usiseme “Nahitaji mtu anipatie milioni 1 ili nifike mbali kibiashara” alafu ukatulia. Bali sema “Nipo napambana kupata pesa kidogo kidogo mpaka nifike kwenye hiyo milioni 1 ili nifike mbali kabisa kibiashara” huku ukifanya hivyo kweli.
Matendo madogo yanayoanza leo, yanaweza kuwa mwanzo wa mafanikio makubwa kesho.
2. Kubadilisha Malengo Mara kwa Mara
Watu wengi huanza mwaka wakiwa na lengo moja, lakini wakifika katikati ya mwaka wanakuwa tayari wamebadilisha mawazo mara kadhaa.
Ni vizuri kuwa na mawazo mapya, lakini kama kila wazo linakufanya usimalize uliloanza, unakuwa unajizungusha pale pale tu bila hatua yoyote.
Kila ndoto inahitaji msimamo na umakini. Usiruhusu malengo mapya yakupotezee mwelekeo wa lengo kuu ulilojiwekea.
Tambua unachokitaka, kisha kifuate bila kuyumbishwa na vitu vidogo vidogo njiani.
3. Kutaka Kuelewa Sana Kabla ya Kuanza Kufanya
Kuna watu hutumia muda mwingi sana kufikiri na kupanga, badala ya kuchukua hatua.
Wanataka kuelewa kila kitu kabla ya kuanza, na matokeo yake wanabaki kufikiri tu bila kufanya chochote cha maana. Kwenye hili; wataalam huwa wanasema “Overthinking Kills Success“, wakiwa na maana “Kufikilia Sana Kunaua Mafanikio”.
Mfano: Wakati wewe unawaza kuanzisha biashara kubwa ya kuuza samaki nchi nzima bila matendo yoyote, mtu mwingine anaamua kuanza kuuza samaki mtaani kwake tu kisha anaanza kuingiza pesa kila siku huku akikua taratibu kibiashara.
Mipango ni mizuri, lakini matendo ndio yanayoleta mabadiliko kwenye maisha.
4. Kutoamini Kwenye Mawazo Yao
Watu wengi wana mawazo mazuri sana, lakini tatizo ni kwamba hawaamini ndani yao kuwa mawazo hayo yanaweza kuleta mafanikio.
Kukosa imani kunazalisha hofu, na hofu inaua ndoto.
Kama huwezi kuamini unachokiwaza, hutachukua hatua, na hutawahi kujua mwisho wake hata kama ni mzuri.
Ndoto hazitimii kwa miujiza, bali kwa hatua ndogo zinazochukuliwa kila siku. Maisha yanabadilika pale unapochukua hatua.