Mambo 5 Mwanaume hapendi kuona kwa Mwanamke katika Mahusiano

Kwenye mahusiano, watu wengi huingia wakiwa wamependana kwa dhati, ingawa siku hizi wapo wanaoingia kwa matamanio au tamaa tu. Na Katika maisha ya mahusiano ya mapenzi, kuna mambo ambayo mwanaume au mwanamke huyaona na kuyapenda, jambo linalowafanya waendelee kubaki pamoja hata kama mwanzo haukuwa na nia ya kweli.

Lakini pia, yapo mambo mengine ambayo mtu akikumbana nayo, huweza kuyachukia kiasi cha kuamua kuondoka kabisa kwenye uhusiano. Makala hii itazungumzia zaidi upande wa mwanaume, kwa kuangazia mambo machache muhimu ambayo kwa kawaida mwanaume hapendi kuyaona kwa mwanamke wake katika mahusiano.

Maswali ya kumuuliza Mpenzi wako Mpya BONYEZA HAPA>>>

Mambo 5 Mwanaume hapendi kutoka kwa Mwanamke

  1. Kukosa Uaminifu

Uaminifu ndio nguzo kuu ya uhusiano wowote. Mwanaume hapendi mwanamke asiyeaminika kwasababu akihisi kwa hutoa siri zake au ana tabia za usaliti, moyo wake huhisi hayupo sehemu salama. Hata kama atabaki kwenye uhusiano kwa muda, mara nyingi itakuwa kwa sababu ya tamaa tu, si kwa upendo wa kweli. Mwanamke anapokuwa mwaminifu, hujenga heshima na kumfanya mwanaume ajisikie yuko na mtu sahihi wa maisha yake.

  1. Dharau

Heshima ni kitu kikubwa kwa mwanaume. Haijalishi mwanamke ni mrembo kiasi gani, mwanaume hatavumilia dharau. Anapenda kujisikia kama kiongozi na mtu muhimu ndani ya uhusiano. Maneno ya kejeli, kutojali maamuzi yake, au kumdharau mbele za watu huumiza moyo wake na kumfanya ajiulize kama kweli yupo sehemu sahihi. Mwanamke anapompa heshima mpenzi wake, hujenga hata misingi ya mapenzi ya muda mrefu.

  1. Uchafu au Kutokujipenda

Mwanaume hupenda mwanamke msafi na anayejipenda. Uchafu au kutojijali kunamfanya mwanaume akose kabisa hamu ya kuwa na mwanamke, hata kama alikuwa amempenda sana. Kujipenda si lazima uwe na nguo za gharama kubwa; hata nguo za kawaida zikivaliwa kwa usafi na mpangilio mzuri humfanya mwanamke avutie. Mwanamke anapojitunza kimwili na kihisia, humvutia zaidi mwanaume na kuimarisha heshima yake.

  1. Kulinganishwa na Wanaume Wengine

Hakuna mwanaume anayependa kulinganishwa na mwingine. Kauli kama, “Mbona fulani kafanya vile alafu wewe umefanya hivi?” ni sumu kubwa kwa mapenzi. Kila mwanaume anapenda kujiona wa kipekee machoni pa mwanamke wake. Kumlazimisha ajione wa hali ya chini kwa kumlinganisha na wengine humfanya ajisikie hafai na kupoteza nguvu ya kupigania uhusiano wengu.

  1. Kutokuwa na Shukrani

Shukrani ni jambo dogo linalobeba uzito mkubwa. Wanaume wengi hujitahidi sana kuhakikisha wapenzi wao wanapata furaha na amani, hata kwa njia ndogo ndogo. Kukosa shukrani au kuchukulia kila kitu kawaida humvunja moyo mwanaume. Neno rahisi kama “asante” linamfanya ajisikie kuthaminiwa na linazidisha upendo ndani ya uhusiano. Akikosa neno hili ndani ya mahusiano, Kuna hatari kubwa ya kuhamia popote atakapolipata nje ya mahusiano.

Mapenzi ya kudumu yanahitaji uaminifu, heshima, kujali na kushukuru. Mwanamke akijitahidi kuepuka mambo haya matano ( kutokuwa mwaminifu, dharau, uchafu, kulinganisha wanaume na kukosa shukrani) anakuwa ameweka msingi mzuri katika mahusiano.

Leave a comment