Kama wewe ni mfuatiliaji wa teknolojia ya AI (Artificial Intelligence), basi unajua kuwa sasa hivi kuna njia nyingi za kutengeneza picha na video kwa kutumia AI. Changamoto kubwa ni kwamba karibu kila platform ya AI maarufu huhitaji malipo kabla hujaweza kufurahia huduma zake.
Kwa mfano, sehemu ya kutengeneza video za AI mara nyingi ndiyo ghali zaidi. Kuna baadhi ya platform zikikugharimu hadi zaidi ya Tsh 200,000 kwa mwezi ili upate uhuru wa kutengeneza video kwa uhuru mkubwa.
Lakini sio kila mtu ana uwezo wa kulipia gharama hizi. Wapo wanaolipia kwa sababu wanatambua thamani yake; hasa wale wanaotumia video au picha za AI kutengeneza brand zao na hata kuingiza pesa kama content creators.
Habari njema ni kwamba sio lazima ulipie! Kuna njia halali na rahisi kabisa ambayo unaweza kutumia kutengeneza picha na video za AI bure na bila kikomo.
Jinsi ya kutengeneza Pesa Facebook BONYEZA HAPA>>>
Njia ya Kutengeneza Picha na Video za AI Bure
Njia hii ni kupitia huduma ya Bing. Hii ni injini ya utafutaji (search engine) inayomilikiwa na kampuni ya Microsoft. Watu huitumia kutafuta vitu mbalimbali kama ilivyo “Google” lakini inamilikiwa na kampuni tofauti.
Ukiachilia mbali kutafuta vitu mbalimbali, katika Bing kuna sehemu ya kutengeneza Video na Picha za Ai bure(Bing Image Creator na Bing Video Creator.). Hii sehemu ndio unaweza kuitembelea ukihitaji kutengeneza video au picha bila kulipia chochote.
- Bing Image Creator: Hii ni sehemu inayokuwezesha kutengeneza picha za AI bure kabisa. Unachotakiwa kufanya ni kutembelea tovuti ya Bing(au Google) na kisha kutafuta “Bing Image Creator”. Hapo utaweza kuandika maelezo ya aina ya picha unayoitaka na AI itakutengenezea papo hapo.
- Bing Video Creator: Kama unataka video, unaweza kutumia “Bing Video Creator”. Hii pia inapatikana mtandaoni bure kupitia Bing. Unachotakiwa kufanya ni kutafuta jina hilo kwenye Bing au Google, kisha utaelekezwa kwenye sehemu ya huduma hiyo.

MUHIMU KUJUA: Ili kutumia huduma hizi, utahitaji kuwa na akaunti ya Microsoft. Kama tayari unayo, unaweza kuingia moja kwa moja. Kama huna, unaweza kufungua akaunti mpya bure kabisa.
Kwa hiyo, kama umekuwa ukitaka kutengeneza picha na video za AI bure bila kikomo, usihangaike tena na gharama kubwa. Bing imekuletea suluhisho kwenye hili.