“Yule mkaka ni mrefu Hadi raha, natamani angekuwa wangu…”
“Alafu hata mimi napenda mwanaume mrefu alafu akiwa mweusi ndio nachanganyikiwa kabisa.”
Haya ni mazungumzo unayoweza kusikia kwenye daladala, mitandaoni au hata mitaani. Lakini swali kubwa ni: kwanini wanawake wengi wanawapenda wanaume warefu?
Je, hii ni kwa sababu ya hisia za kweli, mitazamo wa mtu au ni matokeo ya mila na tamaduni zilizojengeka kwa muda mrefu?
Ukifuatila kidogo; Wengine wanasema ni sayansi ya mwili, huku wengine wakiamini ni ushawishi wa mitindo ya maisha ya kisasa ulioletwa na filamu au mitandao ya kijamii.
Katika makala hii ya The Bestgalaxy, tutachunguza kwa undani sababu kuu zinazofanya wanaume warefu wavutie zaidi kwa wanawake, huku tukikukumbusha kuwa mapenzi ya kweli hayapimwi kwa futi wala sentimita, bali kwa moyo.
Ujumbe mzuri kwa mpenzi wako BONYEZA HAPA>>>
Sababu za Wanawake kupenda Wanaume Warefu
- Hisia za kujihisi salama
Wanawake wengi husema mwanaume mrefu huwapa hali ya kujiamini na kujisikia salama. Wanaume warefu mara nyingi huonekana kuwa na nguvu zaidi kimwili, jambo linalomfanya mwanamke ahisi kwamba yuko na mtu anayeweza kumlinda kwenye hatari. Hata kama si lazima awe na nguvu nyingi, urefu pekee unaleta hisia za usalama kichwani mwa mwanamke.
- Mvuto katika Jamii
Jamii nyingi zimekuwa zikiwapa nafasi kubwa wanaume warefu. Wakati mwingine wanaonekana kama viongozi wa kikundi toka wakiwa wadogo. Mfano, kwenye mikusanyiko hata wa wakubwa, mwanaume mrefu mara nyingi husimama na kuonekana kwa urahisi, kitu kinachoongeza mvuto wake bila hata kusema chochote. Kwa wanawake wengi, hii ni ishara ya hadhi, utawala na mamlaka.
- Sayansi
Watafiti wa saikolojia ya mwili (evolutionary psychology) wanaeleza kuwa urefu ni moja ya sifa ambazo ubongo hutafsiri kama ishara ya afya njema na vinasaba (genes) bora. Mwanamke anaweza asijue, lakini hali yake ya ndani humwambia mwanaume mrefu ana uwezo mkubwa wa kulinda na kuendeleza familia yenye afya. Hii inatokana hata na historia ya nyuma ya kibinadamu ambapo urefu na nguvu vilihusishwa na afya njema.
- Utamaduni na Mitindo
Filamu, muziki, na mitandao ya kijamii zimechangia pakubwa kuunda picha kwamba mwanaume mrefu ndiye “Handsome” Ukifuatilia sinema/movie nyingi, uhusika wakuu wa kiume mara nyingi holewa kwa waigizaji warefu. Hii hujenga taswira akilini mwa watu kwamba urefu ni moja ya vigezo vya mwanaume anayependeza. Kwa hiyo, hata kama mwanamke hakuwahi kufikiria hivyo awali, mazingira na utamaduni hujenga mtazamo huu taratibu.
Jinsi ya kupata Mpenzi mtandaoni BONYEZA HAPA>>>
Mwisho: Si wanawake wote hufuata dhana hii juu ya wanaume warefu. Wengi huweka kipaumbele zaidi kwenye tabia, mawasiliano, na heshima kuliko urefu. Kuna wanaume wafupi lakini wenye mvuto mkubwa kutokana na jinsi wanavyojiamini na jinsi wanavyowajali wapenzi wao. Mapenzi ya kweli hujengwa kwenye uaminifu, mawasiliano, na upendo wa dhati; mambo ambayo hayawezi kupimwa kwa sentimita.