Sms 10 za kiingereza kwaajili ya mpenzi wako

Kila maneno yanayotamkwa kwa makini yanaweza kuwa kioo cha kumwambia mpenzi wako, “Nakupenda, nakutamani, na wewe ni muhimu kwangu.” Katika dunia inayozunguka kwa simu, hata kama muko mbali na mpenzi wako, lakini maneno machache ya mapenzi kupitia SMS, yanaweza kuvunja umbali na kuwaweka pamoja kihisia.

Katika kutuma SMS za mapenzi, Lugha ya Kiingereza inaweza kuwa na ule mkuki wa kupenya roho kwa njia isiyotarajiwa. Sio kwa kuwa ni ya kigeni, bali kwa kuwa ina mafumbo yake yenye kugusa hisia. Kitu kikubwa hapa ni unaemtumia awe anaelewa.

Zingatia haya ili usichokwe na mpenzi wako BONYEZA HAPA>>>

Sms 10 za kiingereza kwaajili ya mpenzi wako


Hapa chini, utapata orodha ya SMS za kiingereza chache unazoweza tumia kuweka wazi hisia zako kwa mwanamke au mwanaume umpendae. Ziangalie vizuri kwa lugha ya kiingereza(English )na kiswahili ili kujua kama zinaenda na hali ya mahusiano yako kabla haujazitumia.

  1. English:
    “Every morning I wake up, my first thought is of you. You are the reason my days feel brighter and my heart feels lighter.”
    Kiswahili:
    “Kilina asubuhi ninapoamka, wazo langu la kwanza ni wewe. Wewe ndio sababu siku zangu zina mwanga na moyo wangu mwepesi.”
  2. English:
    “Your smile is my favorite sight in this world.”
    Kiswahili:
    “Tabasamu lako ndio mandhari niipendayo zaidi hapa ulimwenguni.”
  3. English:
    “No matter where I am, you’re always on my mind and in my heart. Distance means nothing when you mean everything.”
    Kiswahili:
    “Haijalishi niko wapi, daima uko kwenye akili na moyo wangu. Umbali hauna maana wakati wewe ni kila kitu.”
  4. English:
    “Loving you is the easiest and most natural thing I’ve ever done.”
    Kiswahili:
    “Kukupenda ni jambo rahisi na la asili zaidi nimefanya.”
  5. English:
    “You turned my life into a beautiful poem, every line speaks of you.”
    Kiswahili:
    “Umebadilisha maisha yang kuwa shairi zuri, kila mstari unazungumzia wewe.”
  6. English:
    “I never believed in magic until I met you. Now, every day feels like a wonderful spell.”
    Kiswahili:
    “Sikuwahi amini uchawi mpaka nakutana nawe. Sasa, kila siku inahisi nzuri ya kustaajabisha.”
  7. English:
    “You are my today, my tomorrow, and all the days I hope to see.”
    Kiswahili:
    “Wewe ni leo yangu, kesho yangu, na siku zote ninazotumaini kuziona.”
  8. English:
    “Your love is my anchor, it grounds me when I feel lost and lifts me when I feel low.”
    Kiswahili:
    “Upendo wako ni nanga yangu, hutua nikihisi kupotea na kuniinua nikihisi nipo chini.”
  9. English:
    “I cherish the way you love me, the way you understand me, and the way you make ordinary moments extraordinary.”
    Kiswahili:
    “Nathamini vile unavyonipenda, unavyonielewa, na unavyofanya muda wa kawaida uwe wa kipekee.”
  10. English:
    “With you, I’ve found a home that isn’t a place, it’s a feeling. A feeling I never want to lose.”
    Kiswahili:
    “Pamoja nawe, nimepata nyumba ambayo sio mahali, ni hisia. Hisia ambayo sitaki kamwe kuipoteza.”

Huu ni mwisho wa Makala hii lakini ningependa ufahamu kwa sio kila mtu hufurahia kusoma sms za kiingereza kwenye mahusiano. Baadhi ya watu huwa wanafurahia maneno ya kiswahili hata kama wanajua vizuri lugha ya kiingereza. Kwaiyo ni vema ukasoma akili ya mwenza wako vizuri kabla haujazitumia. Na kama unazitumia, usizitumie mara kwa mara.

Leave a comment