RAHA ZA MSAADA (Simulizi fupi ya Kusoma)

Baada ya kuoa nilijua nimepata mke wa kuishi naye na ambaye angeweza kunifanya nipate amani na nilidhike kila ninapomhitaji. Naweza kusema ilianza hivyo, lakini haikuishia hivyo. Mambo yalikuwa hivi;

Baada ya ndoa, nilianza kuishi na mke wangu Neriah kwa furaha kubwa. Alikuwa mwanamke mzuri sana na nilijivunia kumuweka ndani. Ilikuwa ndoto yangu siku zote kumwoa, na japo watu wengi walimuwinda, mimi ndiye nilibahatika. Haikuwa rahisi, kwa sababu hali yangu ya kifedha haikuwa kubwa sanaa, lakini nilijitahidi hata kumwaga pesa kiasi fulani ili anielewe.

Tulipoanza maisha, kila siku nilitoka kazini asubuhi na kurudi mchana, naye akibaki nyumbani kufanya shughuli za ndani. Baada ya muda alianza kuleta marafiki zake wengi nyumbani. Niliporudi kazini mara nyingi niliwakuta, jambo lililonifanya nisiwe huru sana. Nilimueleza juu ya hili, akapunguza kidogo, lakini tabia ikaendelea.

Kadri muda ulivyopita, nilianza hata kuzoeana na baadhi ya marafiki zake. Hata barabarani walinisalimia na wengine walikuwa wakinionesha wanapokaa, wakinikaribisha kwa kusema: “Shemeji karibu, mimi nakaa hapa.” Kwa sababu nilimpenda mke wangu, nilichukulia wote kama mashemeji.

Baada ya miaka miwili, ndoa yangu ikaanza kubadilika. Mke wangu alianza kuwa na makasiriko ambayo mara nyingi yalitokana na ndugu zake. Kwa kuwa sisi ndiyo tulikuwa na uwezo kiasi katika ukoo, alianza kuwasaidia. Mwanzoni alikuwa akiniambia kabla ya kufanya chochote, lakini baadaye akaanza kufanya maamuzi bila kunishirikisha. Alifikia hata kuuza vitu vyetu au kugawa bila ruhusa yangu. Nilijaribu kumkalisha tuzungumze, lakini akawa mkali sana, kama ilivyo tabia ya baadhi ya wanawake wanapokomaa kwenye ndoa.

Wakati huo huo, mambo yangu ya kazi yalikwama. Niliyumba kiuchumi, japo sikupungukiwa chakula. Lakini tabia yake ya kufanya mambo pasipo kuniambia ilinipa mawazo makubwa. Nilivumilia sana, lakini alikuwa haambiliki. Sio kwamba hakunipenda, alinipenda, ila vitendo vyake vilinifanya nisimwelewe. Nilihisi pengine tatizo letu lilikuwa kuchelewa kupata mtoto.

Misukosuko ikaendelea, na hali yangu kifedha ikazidi kuwa mbaya. Kila mara tulipogombana, mke wangu alikuwa akirudi kwao. Nilikua naomba sana ndio anarudi. Nilimweleza mara nyingi atulie ili nipate nafasi ya kutafuta kupambana mambo ya kimaisha vizuri, lakini hakunielewa.

Katika hali hiyo, nilijikuta nikiwa na mawasiliano ya karibu na rafiki zake, hasa mmoja aitwaye Julieth. Wakati mwingine nilimhitaji anisaidie kuniunganisha na mke wangu pale ambapo mke wangu hakuwa tayari kunisikiliza. Hali hii ikatufanya tuzoeane sana.

Julieth alikuwa mwanamke mzuri, mwenye mvuto, lakini kwa kuwa nilimheshimu kama rafiki wa mke wangu, tulidumisha heshima. Lakini, kutokana na ukosefu wa amani katika ndoa yangu, nilijikuta nikiingia kwenye penzi zito naye. Julieth alikuwa single mother akiishi na mtoto wake, na alijipenda sana. Alikua na mwili ulioja kidogo ila ni mzuri utafikili hana mtoto.

Tulipoanza uhusiano, maisha yangu yalianza kuwa na mwanga tena. Nilipata furaha, mambo ya kazini yalienda vizuri kwenye upande WA uchumi na niliweza kuvumilia vituko vya mke wangu bila maumivu makubwa. Mapenzi ya Julieth yalikuwa matamu, hasa kwa kuwa yalikuwa ya siri. Nilikua nikienda kwake nasahua maudhi yote ya mke wangu. Na kwakua alikua anajua kitu gani kina nisumbua kwenye ndoa yangu, alikua hanipi nafasi ya kuwaza.


Lakini Pamoja na kwamba tulikua na mahusiano na Julieth, Bado mke wangu tulikua tuna muheshimu sana. Nakumbuka hata Julieth alikua anasema yupo na mimi kwasababu ya ninayopitia na ukaribu tulioujenga kati yetu. Alikua ananikumbusha mpaka kurudi nyumbani nikiwa nae kwa muda mrefu. Aliwahi pia kuniambia kwa haamini sana kwenye mapenzi kwasababu mtu aliemzalisha wanawasiliana ila anamsumbua sana. Na hakunificha, aliniambia anampenda ila ndio hivyo tu hawapo sawa.
Alikua unaurusha moyo wangu kwa furaha tukiwa kwenye uwanja wetu. Yani nilikua nikizidisha makofi, yeye anakua mtu wa viitikio tu “ooh.. shem” mpaka nachanganyikiwa.

Tuliendelea na mahusiano ya Siri kwa muda flani japo lilikua sio jambo zuri. Lakini baada ya muda, mke wangu alipata ujauzito wangu. Ujio wa mtoto ulikuwa jambo kubwa sana kwenye familia yetu. Kuanzia hapo niliacha kabisa uhusiano na Julieth na kuelekeza nguvu zangu kwa mke wangu. Hatimaye alijifungua na akawa mwanamke wa heshima tena kwangu. Hali hii ilinishangaza ila nikaichukulia kama ilivyo.

Mapenzi kati yangu na Julieth yalikoma, na tukabaki kuheshimiana kwa umbali ghafla tu. Baadaye nikasikia ameolewa na baba wa mtoto wake. Hii ilikua ni habari nje kwangu maana mapenzi yote yalikua kwa mwanamke wangu na mtoto wangu.

Maisha yaliendelea, lakini kipande hiki cha safari ya maisha yangu kilinifundisha mambo makubwa sana. Wewe umejinza nini kwenye sehemu hii ya maisha yangu? Endelea kuwa karibu na The bestgalaxy!

MWISHO

Leave a comment