Karibu kila mwaka, makampuni ya simu huwa yanatoa matoleo mapya ya simu. Makampuni haya ya simu huyatoi tu matoleo ya simu, bali huwa yanashindana kutoa simu zenye maboresho na Teknolojia mpya ilio Bora kwa watumiami.
Watu wengi huwa wanaumiza kichwa sana namna gani wanaweza kupata matoleo haya mapya.
Vijana ambao huwa wanamtindo wa kuhitaji kujaribu vitu vipya, huwa wanahitaji matoleo mapya. Kujaribu vitu vipya ni jambo zuri sana ila ni nzuri zaidi kama liko ndani ya uwezo wako.
Ikiwa hauna uwezo wa kipesa wa kununua kila toleo jipya la simu, basi usiumize sana kichwa juu ya matoleo haya ya simu. Sababu za kutoumiza kichwa sana ni zifuatazo;
Mambo unatakiwa kujua kuhusu simu za mkopo BONYEZA HAPA>>>
Sababu za kutonunua kila toleo jipya la simu
Uzalishaji wa simu upo kibiashara
Fahamu kuwa makampuni ya simu yapo kibiashara na simu ndio moja ya bidhaa wanazouza. Kama zilivyo biashara nyingine, wanahitaji bidhaa ziuzike na wapate faida walioikusudia kisha wauze tena. Kutoa toleo jipya la simu ni sawa na kuingiza mzigo mpya sokoni ili watu wanunue. Hii ndio moja ya sababu simu hutoka kila mara na kuuzwa kama zilivyo bidhaa nyingine.
Kwaiyo endapo utakua hauna uwezo wa kununua toleo jipya la simu, usijisikie kuachwa nyuma. Nasema hivyo kwasababu wao wametoa toleo jipya kwasababu ya faida yao ya kibiashara na sio yako moja kwa moja. Yani kama bidhaa hauwezi ilimiliki, isikunyime usingizi.
Matoleo mapya hushuka bei baada ya muda
Kama umekua karibu na maswala ya kununua simu, utagundua kwasasa simu nyingi huwa zinapungua Bei kwa kasi sana baada ya mwaka moja au mwili toka zitolewe. Yani simu nyingi sana zilizouzwa bei ghali mwaka Jana na mwaka juzi unaweza zikuta kwa bei rahisi mwaka huu. Kuna watu walinunua simu kwa laki 9 kipindi hicho lakini kwa sasa simu walioinunua inapatikana kwa laki 3 tu. Na kadri siku zinapozidi kwenda ndio simu hushuka bei zaidi kutokana na matoleo mapya kuwa mengi na sababu nyingine.
Kwaiyo hapa Naweza kusema kutokimbilia matoleo mapya kunaweza kukufanya uiokoe pesa yako. Unaweza kuwa unasubiri simu mpya zishuke bei ndio ununue kwa bei rahisi.
Baadhi ya matoleo mapya ya simu huja na matatizo
Kwenye historia za simu, kuna matoleo mapya mengi sana yaliokuja na matatizo. Yani simu inaweza kutolewa kipindi hiki lakini baada ya muda mchache, watuamaji wakaanza kukumbana na matatizo ya kiufundi. Mfano wa matatizo yaliowahikutokea sana kwenye historia za matoleo ya simu ni kupata moto sana, vioo kutokwa na mistari, kuzima ghafla na mambo mengine mengi.
Kwaiyo kuchelewa kununua matoleo mapya ya simu kunaweza kukusaidia kuepuka matatizo kama haya. Yani utaona watu wanalalamika juu ya matatizo haya kabla haujatoa pesa yako kuinunua.
Matoleo mapya hayawi tofauti sana na yaliopo
Siku hizi kampuni kama Apple na Samsung huwa zinatoa matoleo kila mwaka lakini haina maana kuna ulazima wa kuchukua kila toleo jipya. Baadhi ya watu kwasasa huwa wananunua hata matoleo ya zamani ya simu za kampuni hizo kwasababu ya kuepuka bei. Mbali na bei, siku hizi kunakua na utofauti mdogo sana wa toleo jipya na toleo la zamani.
Tofauti wanazoweka kwasasa ni Teknolojia ambayo sio ya lazima sana kwa mtumiaji wa kawaida. Mfano; unawezakukuta simu toleo jipya ni bei ghali alafu inasifika kwa kamera inayozoom umbali mrefu sana… Mtumiaji wa kawaida hii itakusaidia nini? Haina umuhimu sana.
Kwa kuangalia hayo yote tuliozungumzia hapo juu, utagundua kunafaida ya kutokimbilia matoleo mapya ya simu. Matoleo mapya ni mazuri lakini kama hauna uwezo wa kununua kila toleo bila Mawazo, basi kuyaacha yapite kwa muda ni chaguo zuri pia.