Jinsi ya kutengeneza Pesa katika channel ya WhatsApp kwa kutumia Opera news hub

Mtandao wa WhatsApp unaweza kufanya uungane na kuwasiliana watu mbalimbali. Lakini katika mtandao huu unaweza pia ukaingiza pesa na kuwa moja ya watu wanaotumia mtandao vizuri.


Watu wengi huwa wanatamani kujua ni jinsi gani mtu anaweza kuingiza pesa mtandaoni. WhatsApp ni moja ya mitandao ambayo mtu anaweza kujifunza kuutumia kutengeneza Pesa na akawa amefanikiwa kuitwa mtu anaetengeneza pesa mtandaoni. Kwaiyo ikiwa wewe ni mmoja wanaotaka kujua namna ya kutengeneza Pesa mtandaoni, mtandao huu unaweza kuwa upande mzuri.

Jinsi ya kutengeneza Pesa kwa kucheza games mtandaoni BONYEZA HAPA>>>



Kwenye Makala hii, unaenda kujifunza namna ya kutengeneza Pesa kwenye Channel ya WhatsApp(WhatsApp channel) na tutatumia Opera news hub kufanya hivyo. Tuanze kwa kufahamu vitu hivi viwili kwanza;

  • Channel ya WhatsApp(WhatsApp channel): Hiki ni kipengele cha WhatsApp ambacho kina kuwezesha mtumiaji wa WhatsApp kuwa na Followers/wafuasi. Unaweza kuwatumia wafuasi Picha, Makala na kushiri nao mambo mbalimbali kama ilivyo kwenye kurasa za Instagram au Facebook. Kila mtumiaji wa WhatsApp anaweza kumiliki channel yake bila shida yoyote.
  • Opera news hub: Hii ni platform ambayo huwa inalipa watu kwa kuandika Makala mbalimbali. Mtu huwa analipwa pesa kutokana makala zake zilizosomwa na watu. Wingi wa wasomaji, unaweza kuwa ndio wingi wa mapato pia. Kusoma zaidi kuhusu hii BONYEZA HAPA>>>

Jinsi ya kutengeneza pesa katika WhatsApp channels kwa kutumia Opera news hub




Iwapo mtu utafanikiwa kumili channel ya WhatsApp yenye wafuatiliaji wengi, Kuna namna unaweza kuitumia kuingia pesa kupitia Opera news hub. Utakua unaitumia channel ya WhatsApp kupata wasomaji wa Makala zako za Opera news hub ili ulipwe na Opera news hub. Utakachotakiwa kufanya ili kufanikisha hayo yote ni kufuata hatua zifuatazo tu;

  • Fungua akaunti ya Opera news hub kisha utaanza kuandika Makala nzuri kwaajili ya followers wako wa Channel ya WhatsApp. Mfano; Unaweza kuandika Makala za Michezo kama channel yako ni kuhusu Michezo.
  • Baada ya hapo, utakua ukizituma link za Makala katika Channel yako ya WhatsApp.
  • Endapo Makala zako zitapata wasomaji wengi wanaozisoma kutoka kwenye channel yako ya WhatsApp, utaingiza pesa kwenye akaunti yako ya Opera news hub.



Kwa kufuata hayo yote, utakua umefanikiwa kuingiza pesa kwenye WhatsApp channel yako kwa msaada wa Opera news hub. Pesa ambazo unaweza kuzitengeneza, zinategemeana na watu ambao ni wasomaji wa Makala zako. Kama utakua na watu wengi wanaozisoma, pesa pia itakua ni nyingi.

One thought on “Jinsi ya kutengeneza Pesa katika channel ya WhatsApp kwa kutumia Opera news hub”

Leave a comment