Maneno mazuri ya kumwambia mpenzi wako ili akupende zaidi

Ingawa vitendo ni muhimu kwenye mahusiano, lakini maneno mazuri huweza kugusa moyo wa mtu wako kipekee na kuimarisha hisia kati ya wapenzi wote wawili. Kwa kutumia maneno sahihi, unaweza kumfanya mpenzi wako ahisi kuthaminiwa, kupendwa na kuwa salama katika penzi lenu.

Watu hutumia njia mbalimbali kuwafikishia wapenzi wao maneno haya ya mapenzi. Wengine huandika ujumbe mfupi (SMS), wengine hutumia sauti katika simu au hata kuandika barua za kimapenzi. Kuna pia wale wanaopendelea kusema uso kwa uso wakitumia sauti ya upole na macho ya upendo. Lakini kilicho muhimu si njia unayotumia, bali ujumbe wenyewe (iwe ni kwa kumwambia “nakupenda”, au kwa kutumia maneno)
Katika makala hii, tumekuandalia orodha ya maneno mazuri ya kumwambia mpenzi wako ili akupende zaidi. Fanya uyaangalie hapa chini;

Maneno mazuri ya kumwambia mpenzi wako ili akupende zaidi

Kila inapofika asubuhi kama hii, nakumbuka kuwa huu ni mwanzo wa siku, na siku yangu njema huanza kwa kujua hali yako kipenzi. Umeamka salama mpenzi wangu?

Kwangu “Maisha Mazuri” yana maana “Mimi kupendana na wewe”. Tukitengana, yatabaki “Maisha” tu alafu “Mazuri” utakua umeondokanayo wewe.

Nikiwa kama Binadamu, sijakamilika na nina nafasi kubwa ya kukosea hapa duniani. Lakini katika yote, naamini sikukosea kukuchangua wewe maishani. Nakupenda na unanipa furaha sana.

Mtu ukiingia kwenye mahusiano mazuri, karibu kila kitu kwenye Dunia kinakua kitumu. Mfano ni Mimi sasaivi; Maisha ni MATAMU, chakula nikila ni KITAMU na hata WEWE kwangu upo hivyo hivyo Mpenzi.

Nilipogundua kuna WEWE kwenye huu ulimwengu, moyo wangu haukua tena na chaguo la kupenda au kuto kupenda. Nilianza kukupenda moja kwa moja mpaka nikashindwa kuuficha ukweli.

Nikikutizama, nakuona kama malaika. Nikikusikiliza, nasikia sauti inayougusa moyo wangu. Nikikufikilia, napata furaha moyoni. Wewe ni Mwanamke ninakupenda na pia waajabu sana maishani mwangu.

Tabasamu lako ni kama humwangia furaha moyo wangu. Siwezi elezea sana ni jinsi gani nakupenda na napenda unapotabasamu, lakini fahamu tu kuwa Nakupenda sana.

Sjui nina mapenzi ya kizamani???… Kama ni hivyo, basi acha tu unione hivyo mpenzi wangu. Natamani tuishi pamoja, tuwalee watoto wetu. Na natamani sana tuendelee kuwa pamoja mpaka mwisho wa maisha yetu.

Kama maisha ni simulizi basi, natamani kuandika simulizi ya Mapenzi na wewe. Simulizi ya watu wawili wanaopenda kwenye kila hali, Wenye mapenzi ya dhati, kusameheana na kushikana mpaka wakafika mbali. Tunaweza iandika pamoja si ndio?

Nahisi umeniweza sasa. Siwezi fikilia maisha yangu bila wewe. Siwezi kuwa ninafuraha nikikukosa hata nikinywa nielewe.

Jambo la muhimu: Ikiwa unataka kuimarisha mahusiano yako, kuongeza ukaribu au kumfanya mpenzi wako aone kuwa yupo na mtu anayemjali kweli, basi maneno haya yatakusaidia sana. Chagua yanayokufaa kwa hali ya mahusiano ya sasa ndio uitumie.

Ujumbe mzuri wa Mke au Mume aliembali BONYEZA HAPA>>

Leave a comment