Opera News Hub: Jinsi ya kufungua akaunti, kutengeneza pesa na kupokea

Opera News Hub ni platform ambayo inawezesha watu kuingiza pesa kwa kutengeneza contents (mahudhui). Kama ni muandishi, hii inaweza kuwa moja ya platform nzuri kuitumia unapokua unahitaji kutengeneza Pesa kwa kuandika ukiwa Tanzania. Kuna kipindi platform hii hilikua haipatikani kwa waandishi wa Tanzania huku baadhi ya nchi jirani wakiwa na uwezo wakuitumia. Lakini kwasasa Mwandishi, ukiwa Tanzania unaweza kufungua akaunti, kutengeneza pesa na kuzipokea bila tatizo.

Jinsi ya kufungua akaunti ya Opera news hub



Ukihitaji kufungua account ya Opera news hub, Anza kwa kutembelea tuvuti ya Opera news hub ambayo ni https://hub.opera.com/ kwenye web browser yako. Baada ya kuingia kwenye tuvuti, utatakiwa kuanza kutengeneza akaunti yako kwa Gmail au Facebook akaunti. Kutumia Gmail ni chaguo zuri zaidi maana unaweza pata matatizo kwenye akaunti yako ya Facebook kirahisi zaidi kuliko Gmail(Gmail ni salama zaidi katika kufungua akaunti).


Kwenye mchakato wa kutengeneza akaunti utatakiwa kujaza taalifa zako kama kama vile majina Kamili, nchi unayotoka na namba za kitambulisho chako na jina unalotaka kuitumia kwenye Opera news hub. Mbali na taalifa hizo kuna namba za wallet utatakiwa kizijaza. Namba hizi za wallet utazipata kwa kupakua app ya Minipay na kufungua akaunti ya Minipay kwa kutumia namba yako ya simu.

Minipay ni app ambayo inatumika kama mfuko wa kupokea hela za mtandaoni. App hii inapatikana kwenye Playstore and hata Appstore ukihitaji kuipakua. Katika ku verify namba yako kwenye Minipa, verification code zitatumwa kwenye WhatsApp hivyo hakikisha namba tunayoitumia, unatumia kwenye WhatsApp pia.

Ukishajaza namba ya wallet na vitu vingine, utafanikiwa kutengeneza akaunti yako Bure kabisa. Utakua na uwezo wa kuingia kwenye akaunti yako ya Opera news hub kwa kutumia simu yako au PC. Uzuri ni kwamba kama unahitaji app ya Opera news hub pia ipo!  Unaweza ichukua Toka Playstore au Appstore.

Jinsi ya kutengeneza pesa katika Opera news hub



Katika Opera news hub, waandishi wanaweza andika Makala zao na kuzichapisha ili zisomwe na watu wengine. Endapo Makala za muandishi zitakua zikisomwa watu, pesa itakua inaingia katika akaunti ya muandishi kwakua amefanya kazi nzuri inayochaguliwa au kupendwa na watu. Hapa nazungumiza zile Makala ambazo zinapata click nyingi (Mibofyo), likes, na hata comments (maoni).


Ili kufanya vizuri zaidi kwenye Opera news hub kama muandishi, ni vema ukawa unatoa Makala za habari na vitu vinavyo trend. Hii itakusaidia kupata wasomaji wengi na kuingiza pesa zaidi. Uwe na uwezo wa kutengeneza hata Makala 5 au 10 kabisa kwa siku ili kutengeneza Pesa nzuri katika mwezi. Pesa zote utakazotengeneza kwenye Makala yako, utakua unaziona kwenye akaunti yako.

Pesa zilizotengenezwa na mmoja wa waandishi wa Opera news hub (Sio kila mtu anaweza tengeneza kiasi hiki)



Jinsi ya kupokea pesa katika Opera news hub


Pesa ulizotengeneza kwenye Opera news hub utakua ukizipokea kila mwezi. Pesa hizo zitakua zinaingia kwenye akaunti yako ya Minipay.

Minipay ni app ambayo inatumika kama mfuko wa kupokelea hela mtandaoni. Uzuri ni kwamba tumeisha iongelea hapo juu, hivyo hatutazungumzia sana hapa.
Kwaiyo pesa zitaingia kwenye akaunti yako ya Minipay na utakua na uwezo wa kuzitoa hata kwenye simu yako tu kupitia Mpesa, Mixx by Yas, Airtel Money na hata Bank ikiwezekana.

Kwa kufanya hayo yote, utakua umefanikiwa kuingiza pesa kwa kuandika mtandaoni kupitia Opera news hub. Mwisho, ningependa kusisitiza kuwa Makala za mambo ya habari na mambo “trend” huwa zina nafasi kubwa ya kufanya vizuri. Ikiwa utakua na Makala mbali na hizo itakuhitaji uweke jitihada zaidi kwenye kuchapisha Makala mpya kila mara.

Muhimu: Maelezo haya yanajitosheleza kabisa kukusaidia wewe kuanza kuingiza pesa endapo utayafuata na kuanza kazi.

Lakini kama utahitaji msaada wa moja kwa moja wa kufunguliwa akaunti na kuunganisha kila kitu bila kupoteza muda, unaweza kutuma ujumbe  WhatsApp +255 622 586 399 tukusaidie kila kitu ili kazi yako inayobaki ni kuandika Makala na kuhesabu mapato yako.

Jinsi ya kutengeneza Pesa Facebook Bonyeza Hapa>>>

One thought on “Opera News Hub: Jinsi ya kufungua akaunti, kutengeneza pesa na kupokea”

Leave a comment