Unaweza kuandika kupitia PC au simu yako ya mkononi? Kama jibu lako ni “Ndio” basi tambua kuwa kuna namna unaweza tengeneza pesa mtandaoni. Kwenye mtandao kuna nafasi ya karibu kila mtu kutengeneza Pesa mtandaoni. Kitu kikubwa na muhimu ni kujua namna gani unaweza fanya hivyo.
Kwa kuandika tu mtu unaweza tengeneza zaidi 1000 $ kwa mwezi ambazo ni sawa na zaidi ya milioni mbili. Lakini pesa inayotengenezwa huwa inategemeana na njia anayotumia, nguvu ulioiweka na sehemu ulioilenga. Kwaiyo haimaanishi kila mtu anaweza tengeneza pesa nyingi kupitia uandishi mtandaoni.
Hapa chini The bestgalaxy tunajaribu kukupa mwanga wa namna gani mtu unaweza tengeneza pesa kwa uandishi. Tutaangalia njia chache mambazo ni nzuri kwa mwandishi kuitumia katika kipindi hiki. Unataka kufahamu? Basi, twende pamoja!
Ujuzi utakaokuwezesha kutengeneza Pesa mtandaoni BONYEZA HAPA>>>
Njia za kutengeneza Pesa mtandaoni kwa kuandika
1. Kutengeneza na kuuza E-books
Unaweza ingiza pesa nyingi kwa kutengeneza na kuuza E-books. E-books ni vitabu vilivyo katika mfumo wa kidigitali na huwa vinanunuliwa na watu wengi mtandaoni. Mtu unaweza kuandika kitabu chako kwa simu au PC kupitia app kama WPS office kisha ukakiuza kwa watu mtandaoni.
Wateja ya ebooks wapo karibia ulimwengu mzima hivyo unaweza kutengeneza na kuuza kitabu chako hata nje ya nchi. Lakini kama tunavyojua; mtu hawezi soma kitabu kisicho mvutia au kisicho kwenye lugha yake. Hivyo ukihitaji kupata wateja wa nchi za nje, utatakiwa kukiandika kitabu chako kwa kuwalenga wanunuzi wa nje pia.
Kama unataka kuuza E-books kwa Africa mashariki, unaweza tumia hata WhatsApp na mitandao mingine ya kijamii tunayoitumia. Lakini ukilenga watu wa nje hapo, ni vema unatumia platform maalum za kuzuia vitabu. Mfano mzuri wa platform za kuzia vitabu mtandaoni hizi ni Amazon KDP.
2. Kuandika kwenye platform zinazolipa waandishi
Unafahamu kuwa kuna platform ambazo zinakulipa moja kwa moja kwa kuandika tu? Kama haujui, basi fahamu hilo kwanzia sasa. Unaweza tengeneza pesa nyingi tu kupitia uandishi wako ingawa itakuhitaji kujitoa sana ili kuweza kuingiza hizo pesa nyingi.
Medium, mtandao wa X(twitter) na Opera news hub ni kati ya platform zinazolipa kwa kuandika. Kwenye hizi platform 3 nilizotaja hapa, Opera news hub ni platform rahisi sana kwa watu wa Africa mashariki kuanza nayo. Inagawa pesa unayoweza tengeneza ni yakawaidi lakini mfumo wa kufanya kazi na kupokea pesa yako, umenyooka zaidi kuliko hizo platform nyingine hapo (Wanalipa pesa kirahisi kupitia app yao ya Minipay).
3. Kutoa huduma za Uandishi kwenye tuvuti za freelancing
Mtindo wa kufanya kazi kwa kuajiriwa kwa muda na wateja tofauti, bila kuwa mfanyakazi rasmi huwa unafahamika kama “freelancing”. Na tuvuti za freelancing ndio sehemu maalum kwa watu wanafanya kazi kwa mtindo huu. Ni kama sehemu ya kukutana na watu wanaoweza kukupa kazi za muda mfupi na kukulipa bila kukuajiri kabisa.
Sasa kama wewe unahitaji kutengeneza Pesa kwa kuandika, basi unaweza Ingia kwenye tuvuti za freelancing ili kupata watu wanaoweza kukupa kazi za kuandika mambo mambo mbalimbali bila kukuajiri moja kwa moja. Hautakua wakwanza kufanya hivyo maana Kuna watu wengi sana Duniani wanaingiza pasa kupitia tuvuti za freelancing kama Fiverr kupata kazi fupi za Uandishi na kuingiza pesa nyingi sana.
Nadhani mpaka hapa umeisha pata picha ya namna unaweza tengeneza pesa mtandaoni kwa kuandika. Asante sana kwa muda wako lakini kabla haujaondoka, ningependa kufahamu kuwana hii sio tu Makala ya kusoma bali ni mwanzo nzuri wa kuelewa jinsi gani unaweza jiajiri mwenyewe mtandaoni.
Endelea kuwa karibu na The bestgalaxy na usisahau kufuatilia simulizi ya MIAKA IJAYO ili kuiweka sawa na mambo yajayo katika ulimwengu.
