Kuna watu wengi hupenda kutazama filamu online. Filamu hizi za online hutoa burudani kwa watazamaji wa rika zote lakini nyingi ni lugha mbali na kiswahili. Si kila mtu anayeweza kuelewa lugha ya filamu hizo, hasa kama ni za Kiingereza, Kihindi au Kichina na ndiyo maana kutafsiri kwa Kiswahili imekuwa msaada mkubwa kwa watazamaji wengi wa Afrika Mashariki.
Kutokana na hitaji hilo kubwa, kumekuwa na sehemu za mtandaoni zinazotoa huduma ya kutafsiri filamu kwa Kiswahili. Sehemu hizi husaidia watu kufurahia movie kwa urahisi huku wakielewa kinachoendelea. Yani kutafsiri movie ni njia nzuri ya kuleta burudani inayowafikia watu wengi zaidi, bila vikwazo vya lugha.
Katika makala hii, tutakuletea orodha ya sehemu mbalimbali za kupata movie ambazo zimetafsiriwa kwa Kiswahili mtandaoni. Iwe unapenda movie za mapenzi, za vita, vichekesho au za kichawi, utajua wapi pa kutembelea ili upate burudani kwa Kiswahili ukiwa na ma DJ unaowapenda.

Sehemu za kupata movie za kutafsiriwa kiswahili mtandaoni
1. Katika YouTube
YouTube ni platform ya video ambayo pia ni sehemu nzuri kwa wapenzi wa filamu kuangalia movie. Katika YouTube unaweza kutana na movie nyingi za Kiingereza lakini baadhi ya movie zilizotafsiriwa kiswahili zipo pia.
Kuna baadhi ya movie nzuri sana unaweza zikuta YouTube zikiwa zimetafsiriwa kiswahili. Movie hizi nyingi huwa ni za zamani maana ndio YouTube wanaweza ziruhusu kidogo. Nyinge huwa na mpya kidogo ila zipo YouTube kutokana na kuchukuliwa kama Creative Commons Licensed movies.
Njia rahisi ya kupata movie hizi ni kuandika neno “Movie za kutafsiriwa kiswahili” katika sehemu ya kutafuta ya YouTube.
2. Group za WhatsApp na Telegram
Njia nyingine ya kupata movie za kutafsiriwa kiswahili mtandaoni ni kuingia katika Group za WhatsApp na Telegram zinazojihusisha na movie za kutafsiriwa. Kuna group hutangazwa na ma “DJ” au watafsiri wa movie kwenye movie zao au kwenye clip zao. Na wakitangaza huwa wanaweka wazi utaratibu wa kujiunga nao. Sasa ikiwa utahitaji movie, unatakiwa kufuata utaratibu wao na kujiunga kwenye hizo group.
Hakikisha unakua makini sana na huyo DJ anae toa namba maana kuna kutapeliwa pia. Ni vema ukaangalia kwanza kama DJ unaemsikiliza anajulikana na kuaminika. Kujilidhisha, fuata utaritibu alikupata huduma yake. Na hii Naweza kusema ni njia nzuri sana kuitumia katika mwaka 2025

3. App za movie za kutafsiriwa
Katika njia ambazo watu wengi walikua wanaotumia kupata movie za kutafsiriwa ni hii. Lakini kwasasa ni njia yenye changamoto sana kutokana na sawa la Copyright.
Ukihitaji app za movie za kutafsiriwa kwasasa unaweza ukapata lakini nyingi hukupa movie chache za zamani na nyingine huwa hazifanyi kazi kabisa. App nyingi za movie zinakufa kwa kutofuata utaratibu wa Copyright wa huku mtandaoni.
Kwakua ni moja ya njia ambayo inatumika, acha tuiweke hapa kama sehemu ya tatu ya kupata movie za kutafsiriwa kiswahili.
ZINGATIA: Makala hii imetolewa kwa lengo la kuelimisha (For education purpose).