Kutoka kimapenzi na Shemeji kuna Madhara gani?

Uhusiano wa kifamilia ni jambo la muhimu sana. Familia hujengwa kwa misingi ya upendo, heshima na uaminifu baina ya wanafamilia. Kila mtu anatarajiwa kulinda mipaka ya heshima ili kuhakikisha amani na mshikamano vinaendelea kudumu ndani ya familia.

Lakini, kuna wakati watu hujikuta wakivuka mipaka hiyo na kujihusisha kimapenzi na shemeji zao. Ingawa hali hii inaweza kuja kwa kushawishiwa, kulazimishwa au chukuliwa kama jambo la kawaida kwa baadhi ya watu, ukweli ni kwamba huleta athari kubwa sana kwa maisha ya mtu binafsi na kwa familia nzima.


Ni muhimu kuelewa kuwa matendo kama haya yanaweza kuathiri sio tu wahusika wawili, bali vizazi na familia yote kwa ujumla. Hivyo, kabla mtu hajachukua uamuzi wa kutoka na shemeji kimapenzi, ni muhimu kujua madhara yanayoweza kutokea. hapa chini kunakupa orodha ya madhara makubwa yanayoweza kukupata au kuikumba familia yako endapo utajihusisha na kitendo hicho.

Jinsi ya kutafuta mpenzi mtandaoni BONYEZA HAPA>>>

Madhara ya kutoka na shemeji kimapenzi

Kupata magonjwa

Mtu kuwa ni shemeji yako haimaanishi yupo salama kwenye upande wa afya. Shemeji yako anaweza kuwa na magonjwa ya kawaida ya zanaa au virusi vya ukimwi kabisa bila wewe kujua. Na endapo utajihusisha nae, unaweza kupata magonjwa hayo kwa urahisi kwakua na imani kuwa ni shemeji wako. Kuna mashemeji wengi wanaume na Wanawake hawapo salama kiafya. Hivyo kujiepusha nao ni kujilinda kiafya.

Kumpoteza mpenzi ulienae na kuvunja familia

Unapokua na mahusiano na shemeji, Kuna hatari kubwa sana ya mahusiano kugundulika. Mahusiano ya Mapenzi ni ngumu sana kuyaficha maana upendo ukizidi mnaweza kifika hatua ya kutojali sana waliowazunguka.


Endapo utagundulika kutoka na shemeji yako, unaweza poteza mpenzi wako(kama unae) na kunivunja familia. Hakuna ndugu anaeweza kukuchukulia vizuri kwa kitendo hicho na utakua umetikisa familia kwa kiasi kikubwa.

Kashfa na Aibu

Watu hawawaamini watu wenye matukio ya kutoka na mashemeji. Sidhani kama na wewe msomaji unaweza muamini mtu unaejua anaweza kutoka na mpenzi wako kwa siri.


Sasa ukitoka na shemeji na kugundulika, utapata kashfa ya “kutembea na mashemeji”. Kashfa hii itakufanya uone aibu na pia hautoaminika na watu kwenye jamii inayojua jambo hilo.

Msongo wa Mawazo

Kutoka na shemeji wa kike au wakiume kunaweza kukupatia msongo wa Mawazo pia. Watu wengi hujikuta kwenye msongo wa Mawazo baada ya kuingia kwenye mahusiano na shemeji zao. Na msongo wa mawazo huu unaweza kuwa unatokana na ujauzito wa Siri, manyanyaso ya kijinsia na vitu vingine kama hivyo.

Sasa kwanini kupitie hayo yote? Ni vema ukajiheshimu na kuheshimu mahusiano ya watu wengine ili kuyaepuka. Endelea kuwa karibu na The bestgalaxy kwa mambo mengi zaidi.

Leave a comment