App ya Gamehub imerahisisha kucheza game za Xbox katika simu

Wachezaji wa games kwenye simu wanazidi kupewa njia rahisi na za kisasa za kufurahia games wanazozipenda kwenye simu. App ya Gamehub ni moja ya suluhisho jipya ambalo limeleta mabadiliko makubwa kwa wapenzi wa games. Kupitia app hii, sasa inawezekana kucheza game za Xbox moja kwa moja kwenye simu yako ya mkononi bila haja ya kuwa na console ya Xbox.

Kama bado haujajua ni kwamba unaweza cheza game za Xbox kwenye simu  lakini hii itakuhitaji utumie huduma ya xcloud. Xcloud ni huduma inayokuwezesha mtu kucheza game za Xbox na nyingine nyingi katika mtandao (Online). Kupitia huduma hii, unaweza cheza game nyingi kubwa kwenye simu yako bila kuwa na simu yenye uwezo sana maana. Kikubwa utakachotakiwa kuwa nacho ni internet yenye kasi tu na tulisha zungumzia juaa ya hilo kwenye makala nyingine hivyo hatauta zungumzia sana hapa.

Game la Fortnite katika Xcloud

Hapa tunakujuza tu kuwa kuna app inaitwa Gamehub imerahisisha zaidi mchakato wa kucheza game za Xbox kupitia hiyo hiyo xcloud.

Kitu kizuri ilicho rahisisha ni kuondoa uhitaji kwa kutumia VPN ikiwa upo nje ya nchi zenye huduma (kama vile US). Yani kupitia app ya Gamehub utaweza kucheza game za Xbox kupitia xcloud popote bila kutumia VPN. Utafanikisha jambo kilo kupitia kipengele cha kuchagua unataka kucheza kama upo sehemu (location). Unaweza fanya yafuatayo kujaribu hiya.

Jinsi ya kucheza game za Xbox kwenye simu kwa app ya Gamehub

Unachohitaji ni kuwa na akaunti ya Xbox, simu yenye uwezo wa kuunganisha intaneti, na app ya Gamehub yenyewe.

  • Fungua app na ujisajiri
  • Baada ya kujisajili, nenda kwenye upande Xbox kwa kubonyeza alama ya Xbox
  • Ukiwa hapo, palasa sehemu ya pembeni katika upande wa kulia, kwenda kushoto kuelekea kulia.
  • Ukifanya hivyo utaletewa sehemu ambayo utachagua location (mahali). Wewe unaweza chagua USA au UK.
  • Baada ya hayo, Chagua game unalotaka kucheza alafu ujisajiri kwa akaunti yako ya Microsoft kama kawaida kwaajili ya kuanza kucheza.

Nakukumbusha tu kuwa kama haujalipia Xbox game pass ultimate, hautaweza kucheza game zaidi ya Fortnite.

Hii ni habari njema kwa watu ambao hawana nafasi au uwezo wa kununua vifaa vya Xbox lakini bado wanatamani kufurahia michezo hiyo.

Leave a comment