Jinsi ya kuepuka au kuondokana na Usingle Mother

Changamoto za mahusiano zimekuwa nyingi, na matokeo yake ni ongezeko la wanawake wanaojikuta wakilea watoto wao peke yao, maarufu kama “single mothers”. Ingawa kuna wanawake wengi walioweka juhudi kubwa kuhakikisha watoto wao wanapata malezi bora hata bila mwenza, ukweli ni kwamba hali hii huja na changamoto nyingi za kiuchumi, kihisia, na hata za kijamii. Kwa wanawake wengi, kuwa single mother siyo chaguo la hiari bali ni matokeo ya mazingira, maamuzi yasiyopangwa, au kuachwa bila msaada.



Kupitia makala hii, hapa chini tutaangalia mambo muhimu ya kuepuka kuwa single mother. Lakini pia kwa wale ambao tayari wako katika hali hiyo, tutaangalia namna ya kujinasua katika Usingle Mother.

Mambo mwanamke hujutia kuchelewa kuyajua BONYEZA HAPA>>>

Jinsi ya kuepuka Usingle Mother

1. Usizae kabla ya mahusiano halali



Baadhi ya watu hupata watoto kabla ya mahusiano kuwa halali na ndio huwa chanzo cha kuwa Single Mother. Sasa ili usiwe mmoja wao, epuka kukubali kupata mtoto kabla mahusiano yenu hayajawa halali. Kama mahusiano yenu ni ya Siri au hayajakomaa, epuka jambo hili kwa kutumia Kinga na njia nyingine nzuri za kuzuia ujauzito.

2. Muelewe mwanaume wako na hali yake



Kabla ya kufanya maamuzi ya kubeba ujauzito wa mtu, tumia muda mrefu sana kumuelewa kwa maneno yake au vitendo vyake. Kama unaona kuna namna hayupo tayari kukuona unapata mtoto nae, usimlazimishe kwa kupata ujauzito. Inasemekana wanaume huwa waonyesha kabisa dalili za kutohitaji mtoto kwa kuongea au vitendo vyao.

Mbali na kumchunguza yeye, angalia na hali yake ya maisha kama inaruhusu yeye kukuhudumia wewe na mtoto. Lakini kuangalia hali yake ya maisha inatakiwa ukuweke mwishoni kabisa maana mtu anaweza kuwa na halia nzuri ya maisha lakini asitake kuwa na mtoto na wewe. Usije ukakurupuka kwenye hili!

3. Yalinde mahusiano yako




Baada ya kupata mtoto, wanawake wengine huingia kwenye Usingle Mother kwasababu hawakua makini kwenye kulinda mahusiano yao na wenza wako. Wanaweza kuwa single Mother kwasababu ya kushindwa kuvumilia tabia flani kwa Mwanaume au kushindwa kuiacha tabia na mambo flani wao wenyewe.


Mwanaume anaweza kuwa na changamoto nyingi sana ambazo baadhi ukiwa kama mwanamke unatakiwa kuzivumilia ili kulinda mahusiano yako(kama hazina madhara sana). Mbali na upende wake, wewe pia unaweza kuwa na mambo flani ambazo ni changamoto kwake.


Hapa kulinda mahusiano yako, unatakiwa mtulivu, msikivu na kutafuta njia za kuyaweka mahusiano yako vizuri badala ya kutumia hasira na kutaka muachane. Unaweza jaribu hata kuomba ushauri kwa watu wanaodumu kwenye ndoa zao ili wakupe mwanga zaidi. Usiombe ushauri kwa watu walioshindwa.


Jinsi ya kuondokana na Usingle Mother





1. Usirudie makosa



Kama unaona kuna kosa ulifanya kwa upande wako ndiomaana umeachwa na kuwa Single Mother, hakikisha haulirudii kwa mtu mwingine. Inaweza kuwa na tabia au matukio ndio yamefanya mutengane na mwenzako wako. Hakikisha haufanyi tena maana kama uliekua nae ameshindwa kuvumilia, kuna hatari ya kushindwana na wengine pia kwaiyo jirekebishe.

2. Usiache kujipenda wewe na mtoto wako



Kupata mtoto sio mwisho wa wanaume wengine kukupenda. Wapo watu wanakupenda na wanatamani wakuchukue wewe na mtoto wako. Lakini hii inategemeana na jinsi unavyojipenda wewe na mtoto wako.
Kujipenda kunaweza kuwa ni kutafuta pesa kwa kujishughulisha, kujiweka kwenye muonekano mzuri wa kuvutia wengine na hata kuwa kwenye mazingira mazuri pia.


Kumpenda mtoto wako pia ni muhimu maana baadhi ya wanaume wanatamani sana mwanamke anaeweza kulea na kukupenda wewe.  Yani ukijipenda wewe na mtoto wako, mwanaume mwingine anaweza kukupenda toka moyoni kabisa na akajikuta anampenda na mtoto wako.

Anaweza kupenda mpaka akaona kama Mwanaume aliekuacha alikua mjinga na hajui thamani yako.

3. Ondoa msukumo wa kupata mtu kwa haraka


Baada ya kuwa single Mother, wengi huwa na msukumo wa kupata mwanaume wa haraka. Hali hii inafanya single Mother hawa kurudia makosa kwa kukubari kuwa na ujauzito wa haraka wa watu wengine. Na baadae wanajikuta wamekua single Mother wenye watoto wa mwanaume zaidi ya mmoja.


Kiufupi msukumo wa kupata mwanaume mwingine hauepukiki ila unatakiwa kupambana kuondoa ili akili yako itulie na kufanya maamuzi sahihi kwenye kila hatua ya kupata mwanaume mwingine. Usiruhusu msukumo ukufanye udandie kila mwanaume kila kufikilia vizuri.

4. Fungua mlango wa watu wengine ila kwa akili sana



Baada ya kuacha na mwanaume mwenye mtoto, kuna uwezekano mkubwa tu wakupata mtu atakae kupenda jinsi ulivyo. Kikubwa unatakiwa kufungua mlango wa watu wengine kuwa na mahusiano na wewe kwa kuweka mazingira ya nayoruhusu kuonesha hisia zao.


Lakini katika hayo yote, unatakiwa kutumia akili sana maana mwanaume ambae atakuchukua ni yule atakae kupenda kwa dhati na kujua taalifa nzuri juu yako.

Endapo utakua ni mtu ambae kila mwanaume anakupata anapokutaka, kuna hatari kubwa ya kufukuza wanaotaka kukuchukua. Tumia akili sana katika kuijenga sifa yako maana wanaume wanatabia ya kupeana taalifa kama mwanamke haujatulia au mwanamke ni rahisi kumpata.


Kama wanaume wengi wanaokufuata watagundua wewe unajielewa, hataki kuwa single Mother na wala hataki kuchezewa, kuna mwanaume anaweza kuja kukuchukua kwasababu ya hizo sababu.

5. Kuwa muwazi kwa mtu mpya na usimrudie wa zamani



Kila mwanaume anaekuja kwenye maisha yako ukiwa kama single Mother, hakikisha anajua wewe una mtoto. Epuka kumficha mtoto ili upendwe. Waache wanaume wakupende jinsi ulivyo na mtoto wako. Ukijiweka vizuri wewe na mtoto wako bila kupoteza mvuto wako, mtu atakupenda kama ulivyo. Mapenzi yakiwa ya kweli, mtoto si tatizo.


Ukimpata anaekupenda, hakikisha haurudi nyuma kwa aliekuacha maana kurudi nyuma kutamuumiza sana mtu mpya aliekupenda jinsi ulivyo. Yani ukirudi nyuma, maumivu anayopata mwanaume alieziba masikio na kukuchukua wewe Single Mother ni makubwa mno.

Kama kunamtu amekubali kukuchukua jinsi ulivyo, muheshimu sana. Anaweza hata kuleta changamoto ndogo ndogo kwenye mahusiano yenu lakini usisahau kuwa anaupendo wa dhati ndio maana amekuchukua.

Leave a comment