UTAMU WA JUMLA 11 (Simulizi ya Maandishi)

Au nimwambie asitume alafu nimwambie kilichotokea?… Hapana, kwasasa siwezi hata kumwambia, ngoja nimtumie namba yangu ya benki ili atume hela humo”. Basi nikafanya hivyo na kabla sijafika nyumbani hela ziliingia alafu nikamshukuru. Ila mawazo hayakuisha kichwani na kiukweli dunia nilikua naiona mbaya sana muda huo.

Nilirudi kwenye chumba nilichopanga nikakuta Salma yupo pale na nikakuta amepika chakula. Nilipofika Salma aliniuliza mbona kama umewahi kurudi, nikamwambia mafunzo yamewahi kuisha. Nilimficha kuhusu mambo yaliotokea na nilikua najaribu kujifanya niko sawa. Alinikaribisha kula chakula alichopika akaniambia hela niliompa ndio ametumia kukiandaa chakula hicho na amenibakizia pia. Nakumbuka nilikaa kama wiki hivi nikijaribu kumficha Salma kilichonikuta lakini sikuweza. kunasiku nilikua nimekaa njee yeye yupo ndani, nikakuta tu ameniita ndani na mimi bila kusita nikaenda ndani. Nikamkuta amekaa kitandani na nilipoingia tu nikamwambia “Unaniitia nini Salma?” akaniambia “Kaa hapa mpenzi wangu” huku akigusa kitandani anapotaka nikae. Mimi nikafanya alichosema, nikakaa nae pale kitandani alafu nikamwambia “Niambie”.

Nikakuta ananishika mkono mmoja alafu anaviingiza vidole vya mikono yake milaini kwenye nafasi ya vidole vya mkono wangu kisha akaniambia “Mpenzi wangu sasahivi umebadilika mpaka najihisi kama nimekukosea hivi… Ila nawaza nimekukosea nini lakini sipati jibu… Unaonekana ni mtu mwenye mawazo sana alafu hata kule unakosema kuna mafunzo unajifunza naona huendi.. Kula nako nakuona hukuzingatii na hata nikipika huwa nakulazimisha sana kula”. Mimi kusikia hivyo, nikafikilia nikaona anachosema ni kweli kabisa nimebadilika maana hata mwili wangu tu kuna jinsi ulianza kupungua kutokana na mawazo lakini nikajaribu kumficha kwa kusema “Ah mbona nipo vizuri tu Salma…Haujanikosea wala nini. Bado nakupenda malaika wangu, usiumize kichwa” nikakuta kasema “Haupo sawa… acha kichwa changu kiumie tu kwaajili yako maana nakupenda. mimi nipo kwenye mahusiano na wewe kwa muda mfupi lakini jinsi ulivyo nijaa kichwani mwangu ni kama nimekaa na wewe muda mrefu… Kuna vitu sivijui toka kwako lakini huwezi nificha hali yako, nakuona kabisa haupo vizuri. Niambie nini tatizo mpenzi wangu”. Bado nilikua mbishi kufunguka kinacho nisumbua mbele yake, nikasema “salma, ondoa hofu niko sawa… Kuna vitu tu vinanisumbua ila haviusiani na mapenzi yetu” akaniambia “Wewe unanificha tu ila tambua kuwa mtu akiwa anamchukia mtu, anakua anajisikia vizuri akiwa na hali mbaya lakini akiwa anampenda hujisikia vibaya kuona yupo kwenye hali mbaya…. sasa mimi ninavyokupenda hivi unafikili nakua kwenye hali gani ukiwa kwenye hali hiyo? Au unataka niondoke ila hutaki kuniambia?”.

Mh mimi mwanzo nilikua naona huenda nikimwambia ataanza kunizarau na kuniacha kwa kuona sina muelekeo ila muda huo mimi nikaona nifunguke tu maana kilikua ni kitu ambacho kinanisumbua akili mpaka nilianza kutamani kifo japo nilikua najaribu kuficha sana. Nilivyomwambia nikakuta ananipa pole na kuanza kunipa naneno mazuri ambayo kiukweli yalinisaidia. Aliniadithia mpaka hadithi za watu ambao anasikia walipitia sehemu ngumu sana katika maisha yao lakini walipambana bila kukata tamaa na mwisho maisha yao yalikua mazuri.

Nashukuru Mungu Salma alikuepo pale na kujaribu kuirudisha akili yangu kwenye mstari kidogo maana kabla ya kufunguka nilikua nahisi niko pekeangu. Tatizo lililonikuta alilichukulia kama limemkuta yeye na alikua upande wangu kwa kunitia moyo. Huenda tatizo hilo lingenikuta wakati salma hayupo maishani mwangu, ningefanya maamuzi mabaya sana kuhusu maisha yangu maana moyo na akili yangu vilikua havitoshi kuvumilia. Kwanzia hapo niliona Salma ni mmoja ya wanawake wenye akili sana. Na baada ya hapo nilijihisi ninanguvu sana tofauti na nilivokua. Nakumbuka baada ya siku mbili nilianza kupanga mipango ya kuanza biashara maana niliona kwakua nimesomea mambo ya biashara bila kupata ajira, huenda nikitumia elimu yangu kufanya biashara zangu naweza nikafika mbali.
Baada ya kupanga mipango, nikaingia kwenye vitendo kwakutumia hela niliotumiwa na wazazi wangu kwaajili ya kupata kazi kwenye yale mafunzo na kuna pesa nyingine niliokuanayo benki kwaajili ya kula nilikua nikiitumia kwaajili ya chakula nyumbani. Wazazi wangu niliwajulisha mambo yalionikuta alafu nikawaambia kwa sasa napambana kwanye biashara tu huku mjini.

Mwanzoni maisha yaliyumba sana na tulichakaa sana ila Salma alikua bado yupo upande wangu. Yani kuna muda nilikua nikimuangalia najisikia vibaya kumchakaza vile mtoto wa watu lakini yeye alikua bado yupo upande wangu na ananionesha upendo na kunishauri ninapotaka anishauri. Nilimshukuru sana mungu kwa kunipa mwanamke wa namna hiyo maana ni wanawake wachache wanaweza fanya hivyo.

Katika kupambana na maisha, sikuwahi kutana na Zuu wala Sara ila niliwahi kutana na Jimmy. Alikua yupo kwenye gari moja kari sana na wala hatukukaa kuongea, alinipungia mkono tu akiwa anaendesha gari kama anawahi sehemu hivi. Aliniacha nafikilia “Sjui aliotea mchongo gani huko?… Dah mwanangu hata kunishtua na mimi niende aliona anachelewa yani… Ila kila mtu na maisha yake hapa duniani acha tu nipambane na maisha yangu”

Basi nikaendelea kupambana na maisha yangu na baada ya muda mambo yalianza kukubali na maisha yalianza kuwa mazuri sana. Mimi na Salma tulifanya utaratibu wa kuwa wanandoa rasmi, tukajenga nyumba nje ya dar na pia nilikua na biashara zenye mafanikio makubwa tu mpaka nikamuingiza Salma kwenye biashara pia.

Nilimshauri aanzishe biashara ya urembo maana alikua anajua sana mambo hayo na alikua anauwezo wa kuwashauri wanawake wenzake kwenye mambo ya urembo. Alikua anafanya vizuri sana upande wa urembo ingawa kipindi hicho alikua anavaa nguo za heshima sana tofauti na mwanzo ila alikua bado anavutia sana. Uzuri wake ulikua haujifichi na baadae tulipata mtoto wa kike alikua mzuri kama yeye. Wakati anamimba ilimllazimu akapime virusi vya UKIMWI na hii iliniogopesha sana kutokana na kazi aliokua anafanya kabla ya kukutana na mimi lakini hakukutwa na virusi vya UKIMWI. Tulienda kupima tena tukiwa wote lakini bado majibu yalikua vizuri. Tulifurahi sana japo ata tungepata isingekua mwisho wa maisha yetu au furaha yetu, ningeendelea kumpenda tu. Namshukuru mungu maisha yetu yanaendelea kuwa mazuri na furaha mpaka sasa. Pia nashukuru mungu kwa kunipa mke bora kwa maisha yangu, nampenda sana salma.

MWISHO

Imetolewa na : The Bestgalaxy

Mawasiliano : +255 715 233 405

Simulizi ya UTAMU WA JUMLA ilio katika maandishi. Ina uhusiano kidogo na Simulizi ya SUKARI YA DADA na MZIGO WA WAKUBWA. Inapatikana katika Sauti pia. Kwaiyo usiishie hapa, Endelea kusoma simulizi nyingine!

Unaweza piga namba +255 715 233 405 au Njoo WhatsApp kwa namba +255 622 586 399 ili kutoa maoni yako juu ya simulizi au kupata maelezo zaidi kuhusu simulizi!

ZINGATIA HII: Tafadhali fahamu kuwa hadithi hii ni mali ya mwandishi. Hairuhusiwi kunakili hadithi yote bila idhini. Unaweza kushiriki au kuchukua sehemu ndogo ya hadithi, lakini si kuichukua hadithi kamili. Asante kwa kuheshimu kazi ya mwandishi!

2 thoughts on “UTAMU WA JUMLA 11 (Simulizi ya Maandishi)”

Leave a comment