Facebook ni moja ya mitandao maarufu sana kwa kutazama na kushare video mbalimbali. Mara nyingi, unaweza kuona video nzuri unayotaka kuihifadhi kwenye simu yako ili uitazame baadaye bila intaneti. Lakini tatizo ni kwamba Facebook haina chaguo la moja kwa moja la kudownload video hizo ziingie kwenye kifaa chako. Kwa bahati nzuri, kuna njia rahisi unazoweza kutumia kupakua video kutoka Facebook bila shida.
Katika ukurasa huu, tutakuelekeza hatua kwa hatua jinsi ya kudownload video za Facebook moja kwa moja kwenye simu yako. Haijalishi unatumia simu ya Android au iPhone, kuna mbinu rahisi ambazo zinafanya kazi kwa wote. Utajifunza jinsi ya kutumia website/tovuti maalum au programu zinazoweza kukusaidia kupakua video hizo kwa urahisi.
Ikiwa umewahi kuona video inayokuvutia kwenye Facebook na ukashindwa kuipakua, basi makala hii ni kwa ajili yako. Fuata mwongozo huu kwa makini ili uweze kuhifadhi video zako unazopenda na kuzitazama wakati wowote bila kuwa na wasiwasi wa data au intaneti.
Jinsi ya kudownload video za Facebook katika simu yako
Kiufupi njia rahisi ya kudownload video za Facebook ni kutumia App au tuvuti maalum kwaajili ya kudownload video hizo. Kuna app na tuvuti nyingi hukuwezesha mtu kupakua video za Facebook. Huwa zanahitaji uzipatie link ya video ambayo unataka alafu baada ya hapo, zinakuwezesha kuchukua video na kuiweka kwenye simu yako.
Mfano wa app za mitindo hii ni app iitwayo Video downloader iliotolewa na Inshot inc. Na kama utahitaji website unaweza tumia tuvuti Fdown.net ikakuwezesha bila tatizo.
Hatua za kudownload ya Facebook kwenye simu
- Copy link ya video ulioiona katika Facebook
- Paste link ya video katika tuvuti au app maalum (katika app ya Video downloader au tuvuti ya Fdown.net)
- Iruhusu app au tufuti kufanya mchakato wake kisha bonyeza kitufe cha kudownload video kitakacho letwa baada ya mchakato.

Kwa kufanya hayo utakua umefanikiwa kupakua video ya Facebook kwenye simu yako. Ila kabla ya kuondoka katika ukurasa huu ni vema kufahamu kuwa upakuaji wa video za watu bira ruhusa ya wamiliki ni kosa ingawa unaweza kufanya ikiwa video ipo katika kundi la video zisizo na madhara.