Jinsi ya kutumia kipengele cha “WhatsApp screen share”


WhatsApp ni mtandao unaoleta pamoja watu kupitia groups, channels na kurahisisha sana mawasiliano. Ni moja ya mitandao mkubwa ulimwenguni milikiwa na Meta. Unatumiwa na watu kuwasiliana na watu wengine walio ndani na nje ya nchi.

Kwenye mtandao wa WhatsApp Kuna vipengele vingi sana mtu unaweza tumia katika kuungana au kuwasiliana na watu wengine. Katika vipengele hivyo, Kuna kipengele kinaitwa “WhatsApp screen share”.

WhatsApp screen share ni kipengele cha WhatsApp kinachowawezesha watumiaji wa WhatsApp kuoneshana Screen za simu zao. Kupitia kipengele cha hiki cha WhatsApp, unaweza kumuonesha mambo yalio katika kioo cha simu yako mtumiaji mwingine wa WhatsApp. Lakini hii inafanyika pindi mnapopigiana video call.

WhatsApp ilikuja na kipengele hiki cha WhatsApp screen share rasimi mwaka 2023 lakini huduma kama Google meet na Zoom zina uwezo kama huu pia. Katika makala hii, tutajikita katika huduma  ambayo inapatikana kwenye mtandao wa WhatsApp.

Jinsi ya kutumia kipengele cha “WhatsApp screen share”



Ukiwa unataka kumuonesha mambo yalio kwenye screen ya simu yako mtu mwingine kwa kutumia WhatsApp Screen share, fuata hatuna zifuatazo;

  • Mpigie au akupigie Video call
  • Mukianza video call, bonyeza Vidoti vitatu
  • Changua “Share screen” kwenye chaguzi zitakazotokea.
  • Baada ya hapo, utatakiwa kukubali kuwa Kila kinachofanyika kwenye screen ya simu yako, kionekane kwa yule mtu ulienae kwenye video call.
  • Ukikubari tu, WhatsApp wataanza kuionesha screen yako kwa yule mtu ulienae kwenye video call.

Kupitia kipengele hiki, unaweza kumuonesha mtu movie/video zililopo kwenye simu yako, kumfundisha Baadhi ya vitu kupitia simu yako na hata rekebisha matatizo kwa kufuata muongozo wake.

Jinsi ya kuona sms za WhatsApp kwenye simu nyingine BONYEZA HAPA>>>

Leave a comment