Sms za kulalamika kwa mpenzi wako (Mwanamke au Mwanaume)



Katika mahusiano ya mapenzi, si kila wakati mambo yanakwenda kama unavyotarajia. Kuna nyakati unaweza gundua kuwa mpenzi wako amebadilika, haonyeshi tena upendo na kujali kama zamani. Labda ameanza kuwa mbali, hajali hisia zako, au hata anaonyesha dalili za kuzingatia katika uhusiano wenu. Hali kama hizi zinaweza kuumiza moyo na kukufanya uhisi huzuni, mashaka, au hata hasira.

Pia, kuna wakati unaweza kugundua kuwa mpenzi wako amekusaliti kabisa. Hakuna kitu kinachouma kama kugundua kuwa mtu uliyempenda kwa dhati ana mtu mwingine au aheshimu uaminifu wenu. Usaliti unaweza kuleta maumivu makubwa na kukufanya ujihisi si wathamani.

Mtu unapopitia katika hali kama hizi, unaweza kuhitaji kumwandikia mpenzi wako ujumbe wa kulalamika, ili aelewe jinsi kitendo chake kilivyokuathiri na, pengine, abadilishe tabia yake , kiwezekana. Kutuma ujumbe wa kuelezea hisia zako kunaweza kuwa moja ya kutoa hisia zako na kufungua mzingo kifuani. Katika makala hii, tumekuandalia orodha ya sms za kulalamika ambazo unaweza kumtumia mpenzi wako ili kuelezea hisia zako kwa bila kupoteza muda.

Simulizi bora za kusoma katika The bestgalaxy BONYEZA HAPA>>>

Ujumbe wa kulalamika kwa mpenzi wako





Moyo wangu upo kwako ni vile tu Umeamua kuubuluza. Unayoyafanya yananiuza na Sina chakufanya kukukumbusha kuwa ulisema milele utanipenda. Ok, Fanya unachofanya ila milele usisahau ninakupenda!



Mimezikumbuka zile siku za furaha , zile siku tulikua tunatafutana kila mara na kuambiana hisia zetu. Na bado nakumbuka tuliambizana “unanipa furaha, sina mwingine, ni wewe tu”. Lakini sasaivi wewe sijui umepata mwingine kakubadilisha… eti ni umesahau???



Ulikuja kama mwanga kuyaangaza maisha yangu, ulileta matumaini na ndoto lakini ghafla unaniacha nikiwa nimevunjika moyo na kukata tamaa ya kupenda tena. Asante kwa yote lakini!



Natamani miaka ambayo nimekaa na wewe isingetokea katika Maisha yangu. Zile kumbukumbu nilizofurahia na wewe zinaniumiza kwasasa. Ninatamani kufuta kila kumbukumbu yako ila ndio hivyo uliniweza, nikakupenda kweli na sasa umenisaliti ninaumia.



Nitajuta milele vile nilikupenda bila kujua dhamira yako na kukuamini. Nilikupa kila kitu nilicho hisi kitakufurahisha; lakini katika malipo, umenitoa machozi kwa maumivu yasio isha.



Najitahidi kila mara kuwaza na kukufanyia mambo yatakayo kupa furaha lakini wewe umekua ukinilipa mambo yanayoniumiza. Najua hii inamaana; Pamoja na kukupenda, Bado haunipendi. Asante sana, naendelea kukupenda ila nimekuelewa!



Nilikupenda bila sharti lolote na bila kuuliza kurudishiwa ila ulichukulia upendo huo kuwa udhaifu wangu. Siwezi sema mengi ila umeniumiza vya kutosha sasa, niache niendelee na maisha yangu.



Nilikuamini kwa moyo wangu wote, lakini umeshindwa kuelewa hilo. Umenifanya nijifunze kuto kumuamini mtu hata nikimpenda sana. Ninakuchukia, lakini nashukuru kwa somo! Nashukuru kwa kunivunja moyo pia!

Huu ndio mwisho wa orodha yetu ila Kuna mambo mengi sana katika The bestgalaxy unaweza furahia. Kikubwa Endelea kuwa karibu nasi ili kujifunza mengi!

Leave a comment