Unaponda sehemu flani ngeni kuishi, unaweza kutana na changamoto au mambo tofauti kwako. Mengine yanaweza kuwa ni yakushangaza na mengine yanaweza kuwa magumu ila baada ya kuishi kwa muda flani na kuyajua vizuri mambo ya hapo, unazoea na kuanza kuishi sehemu hiyo kama ni yakamaaida. Yani hata kama jirani wako umemkuta ni mkorofi, baada ya muda unaweza mchukulia kama alivyo na maisha ya ujirani yakaendelea.
Unapoingia katika mahusiano nako huwa kuna mambo flani hivi yanaweza kuibuka na kuleta changamoto ila wote wapenzi wawili mukiyajua mutaendelea na mapenzi ya muda mrefu bila kuachana. Yani mambo haya kama hata mmoja wenu akiyajua, ataweza kuokoa mapenzi yenu Kila yanapotaka kuvunjika na hata kuyatunza yewe imara. Lakini mukiyajua wote, inakua poa zaidi.
Ujumbe mzuri kwa mpenzi wako BONYEZA HAPA>>>
Mambo ambayo mukijua inakua sio rahisi wewe na mpenzi wako kuachana
Kutoelewana sio mwisho wa mahusiano
Wengi kwenye mapenzi ya sasa huwa wasipoelewana, wanaachana kirahisi sana. Yani wanaweza anzisha mwezi huu mahusiano alafu baada ya mwezi kuisha, wanaishia kwenye kutoelewana alafu wanaachana.
Ukweli ni kwamba kutoelewana kwenye mahusiano hakupingiki, na kama kila mahusiano yangekuua yanaishia pale wapenzi wasipoelewana katika mambo flani, basi kungekua hakuna watu wenye mahusiano ya kudumu.
Ili mahusiano yadumu, inabidi mufahamu kabisa kuwa kuna siku mnaweza kuwa hamuelewani kwasababu ya mambo mbalimbali. Ila nijukumu lenu wote kuyaweka mahusiano vizuri. Mukiwa na uwezo wa kutafutana bila aibu baada ya kutoelewana, mahusiano yenu yatadumu sana.
Kuchepuka kuna hasara kubwa kuliko faida
Asilimia kubwa ya watu wanaochepuka kwa wapenzi wao huishia kujilaumu sana. Na hujilaumu kwasababu kuchepuka kuna hasara kubwa nyingi kuliko faida. Kuchepuka kuna kufanya tuingie kwenye hatari ya magonjwa kama HIV. Alafu mbali na hayo, pia unaweza jiingiza kwenye utumwa wa Siri ambazo zinaweza kukutesa kwa miaka.
Mfano; Unakuta mtu anachepuka alafu kapewa au kumpa mimba mchepuko. Mtoto anazaliwa kwa siri huku mtu aliechepuka anashikiria Siri moyoni mpaka Raha ya maisha anaikosa.
Mukijua mapema haya kama wapenzi, nguvu ya kusalitiana inapungua kidogo.
Kuna muda mnapata hasira kwasababu mnapendana
Mwanamke au Mwanaume anaweza kufoka au kupandwa na hasira kwenye jambo dogo sana. Hizo hasira huwa zinakuja kwasababu ya upendo tu na sio jambo jingine.
Mukijua kuwa kunamuda munatiana hasira kwasababu mioyo yenu inaupendo, mtaweza kuwa kwenye mahusiano kwa muda mrefu sana. Maana asilimia kubwa ya wanaolijua hili, hujielewa kwanza wao alafu huelewa na wapenzi wao wanapokua na hasira.
Mfano; Kwenye ndoa hapa ndio unaweza kukuta mwanamke au mwanaume anakasirika sana na kumrushia maneno mpenzi wake anapochelewa kurudi. Kinachomfanya akasirike sana ni upendo tu na sio jambo jingine. Usipolielewa hili kwa mpenzi wako unaweza muona mbaya kwao.
Maongezi ya usiku ya kila mara ni muhimu
Mukiwa kama wapenzi mnaojenga mapenzi ya muda mrefu, kufanya mazungumzo au mawasiliano ya kila mara usiku ni muhumu sana. Yani kutenga nusu saa au saa moja la kuongea kila siku kutawafanya muwe karibu zaidi kifikra na kihisia.
Mtakua na uwezo wa kupanga mipango yenu pamoja, kujuana zaidi na kujenga imani.
Mbali na hayo, usingizi unaokuja baada ya kuongea na mpenzi wako huwa unakua mzuri sana. Hivyo ni njia moja ya kufanya mulale vizuri.
