Kikawaida, kutengeneza app ni mchakato unaohusisha kuandika “Code” ambazo ni maelezo katika lugha ya computer. Hivyo ukitaka kutengeneza app kwa utaalam zaidi, unapaswa kujua namna ya kuandika Code katika lugha mbalimbali za computer.
Kwa mtu unaetaka kuwa mtaalam wa kutengeneza app za simu, unaweza jifunza lugha za computer kama vile JavaScript, Kotlin, Java, Python, Java na nyinginezo. Ukiwa mtaalam wa lugha za computer na ukawa na uwezo wa kutengeneza app, alafu utaitwa “App developer”.
App developer anaweza kuingiza pesa kwa kuajiliwa sehemu mbalimbali anazoweza kufanya kazi kama “Developer”. Mfano; Kampuni ya Meta ambayo inaumiliki Instagram, Facebook na WhatsApp, huwa zina watu ambao hufaamika kama “Developer” ambao huusika na maboresho ya app hizo. Ni wachache Duniani ila huingiza pesa nyingi sana.
Mbali na kuajiliwa, App developer anaweza ingiza pesa kwa project zake mwenyewe. Yani anaweza pambana kutengeneza kitu anachokiwaza alafu kikamuingizia pesa kwa kukiuza au kukiingiza katika mifumo itakayomuingizia pesa. Mfano mzuri ni Kutengeneza game linalo muingizia pesa au kuwatengenezea watu app za kurahisisha mambo yao ya kibiashara.
Jinsi ya kutengeneza Pesa kwa kucheza games mtandaoni BONYEZA HAPA>>>
Jinsi ya kutengeneza app za simu kwenye simu za bila kujua Code
Pamoja na hayo yote, sio lazima mtu uwe mtaalam ndio utengeneze app za simu. Mtandaoni kuna tuvuti/website nyingi ambazo zimerahisisha mchakato wa kutengeneza app za simu.
Website nyingine zinarahisisha mchakato wa kutengeneza app kiasi ambacho mtu yoyote anaweza kutulia na zitumia kutengeneza app za Simu. Unaweza usijue kabisa maswala ya lugha za computer lakini ukafanikisha kutengeneza app kupitia website hizo.
Ukizitafuta website za mtindo huu katika mtandao, utazikuta nyingi sana lakini asilimia kubwa zinahitaji ulipie pesa. Mfano mzuri ni tuvunti ya Andromo, AppMySite na Appypie. Ni kati ya website rahisi kuzitumia katika kutengeneza app za simu (Android na iOS)lakini ili kupata uhuru kwenye app yako, utatakiwa kulipia.
kutengeneza app za simu kwenye simu BURE
Lakini swala la kulipia, lisikukwamishe maana Kuna tuvuti nyingine zinakupa uhuru mkubwa kabisa bure. Mfano wa tuvuti hizo ni hii hiitwayo “Appcreator24” au tuvuti iitwayo “Appsgeyser“. Website hizi unaweza kuzitumia kutengeneza app za simu kwa urahisi sana na bila kulipia.
Hapa the bestgalaxy tunakupa mwanga wa jinsi ya kutengeneza app ya simu kupitia tuvuti ya Appcreator24. Hapa chini tumekupa hatua muhimu zakuchukua ili kutengeneza app kwenye tuvuti hiyo ila utatakiwa kuwekeza muda wako kujifunza kiundani.
- Ingia kwenye website ya Appcreator24 ujisajili
- Bonyeza “Create app” kuanza kutengeneza app
- Jaza taalifa za app unayotaka na uchague mtindo wake
- Maliza kwa Download app yako ikiwa kama Apk au AAB file
Baada ya hapo utachangua wewe kwa kuipeleka. Unaweza kuiweka kwenye simu yako au kuipeleka sehemu kama Playstore ili watu waipakue kisha upate pesa kwa kuonesha matangazo. Na kama unataka kuiboresha au kuiweka vizuri, basi utaingia kwenye hiyo website ya Appcreator24 ili kurekebisha.

Pamoja na yote hayo, fahamu kuwa website nyingi za kulipia ndio hutumia kutengeneza app nzuri zaidi. Na pia, kujua code kunaweza kufanya uwe bora zaidi katika kuzitumia tuvuti zote za kuunda app. Watu engine hutumia AI kuandika Code katika kuunda app na hufanikiwa kutengeneza app nzuri sana. Lakini sio lazima kufanya hivyo, unaweza tengeneza app bila kujihusisha na code!