Jinsi ya kutafuta Jina la movie kupitia kipande cha video

Kwasasa ukizunguka katika mitandao ya kijamii, unaweza pata video fupi ambazo ni vipande vya movie. Video hizi fupi zinaweza kuonesha sehemu nzuri ya movie flani lakini kupata jina la movie hiyo inaweza kuwa changamoto. Mfano; Kuna siku nimewahi kutana na video katika Mtandao Facebook. Hiyo video ilikua inaonesha sehemu ya kusisimua ya movie. Sehemu hiyo ya movie ilinifanya nitamani kutafuta na kuangalia movie hiyo mwanzo mpaka mwisho. Lakini nilishindwa kufanya hivyo kutokana na kutojua jina la movie yenye kipande hicho.
Sawa hili huwa linapitiwa na watu wengi sana katika kipindi hiki. Watu huona vipande vya movie kwenye TikTok, Facebook na WhatsApp lakini wanashindwa kujua majina ya movie zenye vipande hivyo. Baadhi ya watu huwa wanabahatika kupata Jina la movie kwenye sehemu ya maoni (Comment) japo sio mara zote utapata watu waliotaja jina kwenye sehemu hiyo. Lakini hayo yasikutie shaka maana kuna njia Bora ya kutafuta Jina la movie kupitia kipande kifupi cha video ulichokiona sehemu yoyote. Ukihitaji kujua juu ya hili? soma yafuatayo hapoa chini.

Jinsi ya kutafuta Jina la Movie kwa kipande cha kifupi cha Video

  1. Piga Screenshot sehemu nzuri ya video.

Kitu Cha kwanza unatakiwa kufanya ni kuplay kipande cha video fupi ulionayo alafu upige screenshot sehemu nzuri. Ninapozungumzia sehemu nzuri, ninamaana sehemu ambayo inawaonesha waingizaji na mazingira yao vizuri.
Unaweza piga Screenshot mbili au zaidi ili upate screenshot moja itakayokua vizuri kuliko zote.

  1. Ingiza Screenshot katika Google Lens.

Baada ya kupata screenshot moja nzuri sana, utatakiwa uiingiza Katika Google Lens. Hii Google Lens inakuwezesha kutafuta taalifa za vitu kupitia picha. Mfano; ukiipatia Google Lens Screenshot (picha), itakupa taalifa mbalimbali kuhusu hiyo screenshot. Na kama utaipatia Screenshot ulioipiga katika kipande cha movie, unapata taalifa zinazojumuisha Jina la movie.

App ya Google Lens inapatikana Playstore kwa watu wanaotumia simu za Android(Ina alama ya kamera. Lakini kwa iPhone unaweza tumia Google chrome. Inapatikana kama kipengele kidogo katika Google. Kama unatumia Google kupitia Chrome, utakiona kipengele cha Google Lens kikiwakilishwa na alama ya kamera.
Kutumia Google Lens ni rahisi tu; unaifungua, unachagua picha au screenshot iliopo kwenye simu yako alafu unaiacha ikupe taalifa Toka Google kuhusu hiyo screenshot.

  1. Kupata jina, angalia kwa umakini matokeo ya Google.

Google itakupa matokeo mengi kuhusu hiyo screenshot lakini kwakua unataka jina la movie, utatakiwa kuwa makini kuchambua. Umakini unahitajika maana kama screenshot yako haikua vizuri, unaweza pata taalifa tofauti na unazotafuta.
Lakini kama utajiridhisha kuwa majibu ni sahihi, utakua umefanikiwa kupata jina la movie kama ulivyohitaji.

Jinsi ya Kuangalia movie Bure mtandaoni BONYEZA HAPA>>>

Leave a comment