Kutokana na ukuaji wa Teknolojia, mitandao ya mawasiliano imekua na app za pesa ambazo tunazitumia kwenye simu za smartphone. App ninazozingumia hapa ni app ya Mpesa, My Halo, Mixx by yas, My Airtel na nyingine kama hizo.
Watu wengi wenye smartphone hutumia app hizi na zimekua zikirahisisha sana mchakato wa kutuma pesa kwa ndugu na marafiki zao. Uzuri wa app hizi katika kutuma pesa ni huwa zinarahisisha mchakato mzima wa kutuma pesa. Zinapunguza na changamoto ambazo hujitokeza mara nyingi mtu anapotuma pesa.
Mfano wa changamoto hizo ni kukosea na namba ya mtumiajia na kupata lile tatizo la “Invalid MMI code.” Unapochelewa kufanya uchaguzi katika Menu za kawaida.
Ukiwa unatumia app, kunakuwa na uwezekano mdogo wa kukosea namba ya mtu maana unaweza ichukua moja kwa moja kwenye majina uliotunza.
Sasa mbali na mambo ya kutuma pesa kwa ndugu na marafiki, app hizi Kuna mambo zimeyarahisisha sana. Kama unatumia moja ya app hizi, basi angalia orodha ya mambo mazuri unayoweza fanya kwa urahisi kupitia app hizi za pesa.
Jinsi ya kutafuta simu iliopotea au kuibiwa BONYEZA HAPA>>>
Mambo mazuri unayoweza fanya kwa app ya mtandao wako wa Mawasiliano
Kutafuta wakala waliokaribu na wewe
Kama unatumia app za pesa za Makampuni ya mawasiliano, kwasasa unaweza tafuta Mawaka waliokaribu na wewe kwenye eneo ulilopo. Yani hatakama umefika kwenye eneo geni kwako, unaweza fungua app na kuangalia mawakala waliopo kwenye eneo lako na unaweza hata kuwapigia. Kipengele hiki ni kizuri zaidi kwa watu wanaosafiri kwenda sehemu mbalimbali wasizozijua vizuri.
Kubook ndege
Ukitaka kupata ticket za ndege kwa haraka na urahisi, unaweza tumia app hizi pia. Tumewahi zungumzia jinsi ya kubook ndege kwa app ya Mpesa, hivyo jambo hili linaweza kuwa sio jambo geni. Ila kama haujasoma makala iliozungumzia hayo, basi fahamu kuwa unaweza kubook na kupata Tiketi za ndege kupitia app ya Mpesa na app nyingine zenye kipengele cha kulipia ticket za ndege kwasasa.
Kulipia kwenye tuvuti za mtandaoni
Katika tuvuti nyingi ulimwengu huwa zinaweka mfumo wa kulipia kwa kutumia Visa au Mastercard. Mfano; ukihitaji kulipia bidhaa katika tuvuti ya Amazon au AliExpress kwasasa, utahitajika kuwa na Visa au Mastercard. Jambo la kupata Visa au Mastercard limerahisishwa sana kwenye app za pesa za mitandao ya mawasiliano tunayotumia. Unaweza zitengeneza kwa urahisi kupitia App ya Mpesa, Mixx by yas na app nyingine ndani ya dakika 5 tu. Jifunza za zaidi swala hili hapa.
Kusimamia, kuwekeza pesa au Kukopa pesa
Ukitaka kusimamia vizuri pesa zako unazotunza kwenye simu, ni vema ukawa unatumia app maana zimeweka urahisi. Unaangalia Salio la akaunti yako kirahisi na hata kufanya miamla ukiwa nje nchi. Kiufupi usimamizi wa pesa yako unakua ni rahisi zaidi.
Mbali na usimamizi, app hizi kwasasa zinakupa uwezo wa kuwekeza pesa kwa urahisi ili kuizalisha. Ukiachana na kuwekeza, unaweza hata kukopa pia.
Ni hayo tu tuliokuandalia katika makala hii, Endelea kuwa karibu na The bestgalaxy kwa mengine zaidi.