Katika maisha ya mahusiano ya kimapenzi, kuna nyakati ambapo hisia za kumkumbuka mpenzi wako zinakuwa nyingi sana. Hali hii hutokea pale mnapokuwa mbali au hata wakati mnakuwa karibu lakini shughuli za kila siku zinawazuia kuwa pamoja. Kumkosa mtu unayempenda kwa muda ni huleta hali ngumu sana hata mnapokua na mapenzi ya dhati. Lakini ni jambo zuri ni kwamba, kuieleza hali hiyo kwa mpenzi wako hufanya ajue umuhimu wake kwako na hata kukupenda zaidi. Yani unaweza kumtumia hata ujumbe wa sms mzuri wa kumueleza jinsi gani umemiss na akafurahi na kujua unamuhitaji.
Mfano; Ujumbe mdogo wa “Nimekukumbuka mpenzi wangu, natamani niwe karibu na wewe” unaweza kubeba uzito wa hisia zako zote na kuonyesha jinsi gani unamuhitaji mpenzi wako. Wakati mwingine, huenda mpenzi wako anajihisi mpweke au hana uhakika wa hisia zako ila akiwa anapata ujumbe wako wa kummiss, anaweza kuwa ni faraja anayoihitaji. Ni jambo dogo kulifanya lakini lenye nguvu ya kuimarisha uhusiano na kuonyesha kwamba unamjali.
Mambo yasiofaa kuwambia marafiki kuhusu Mpenzi wako BONYEZA HAPA>>>
Katika makala hii, tumekusanya orodha ya SMS bora ambazo unaweza kumtumia mpenzi wako kumjulisha jinsi unavyomkumbuka. Unaweza zitumia bura kuleta furaha kwenye mahusiano wako.
SMS za kumiss mpenzi wako
- Nipo hapa nimetulia ila kila nikifikilia jinsi nafurahia nikiwa karibu yako, natamani nikufuate ulipo. Nakumiss sana mpenzi, natamani niwepo ulipo.
- We ni ile tamu waliosema “haionjwi” kwasababu mtu akionja hunogewa. Tangu nilipo onja ukaribu wako, nautamani kila mara. Nakumiss sana.
- Upo mbali mpenzi wangu, lakini moyo haujawahi punguza upendo wako. Bado nahitaji wewe uwe wangu, na Bado nahitaji niendelee kuwa wako.
- Unauzuri wa kushangaza kama nyota angani. Nikiangalia nyota na vitu vingine vyenye uzuri wa kushangaza, huwa nakukumbuka sana wewe.
- Kuna muda unaweza waza eti nitakuacha na maumivu niende mbali. Huko mbali nafika vipi bila wewe? Moyo unakuhitaji kila dakika. Hata sasa nimekumiss nakuwaza wewe…
- Nakupenda sana. Tafadhali njoo unijaze furaha ya uwepo wako Kipenzi. Moyo wangu umemiss zile hisia za kuwa karibu yako.
- Huku Moyo uliokupenda unanisumbua kuhusu wewe. Umekukumbuka sana mpenzi wangu, natamani uje useme nao kwa ukaribu. Umechoka, uhitaji kukuona wewe Tabibu.
- Njoo niyaone yale macho yako mazuri Mpenzi. Njoo unilishe kile chakula mimi hupenda. Nimekumiss mpaka onaona giza, siioni furaha bila ya wewe ninaekupenda.
- Kile na hitaji nikiwa na huzuni, ni wewe. Na hata kile nile nahitaji nikiwa na furaha, ni wewe. Kiufupi, maisha yangu nayaona ni mzuri nikiwa na wewe. Nimekumiss mpenzi wangu.
- Nakupenda na ninakutaka karibu nami zaidi ya kitu chochote ulimwenguni. Nakuhitaji zaidi ya chupa ya maji jangwani. Uko wapi mpenzi?
Sms hizi za kumiss ni nzuri kwa walio kwenye ndoa (Mume au mke) na hata kwa wasio kwenye ndoa (Wapenzi). Kikubwa unatakiwa kuchagua sms au ujumbe unapenda na hali yenu. Na pia ni muhimu kujua ni wakati gani wa kumtumia sms huyo umpendae.