UTAMU WA JUMLA 08 (Simulizi ya Maandishi)






Nikatoka pale dirishani nikakaa kitandani nawaza “Dah ila huyu mwanamke mzuri… ila simuelewi, inamaana yeye ndio Tausi kweli? na mambo yaliokua yanaendelea hapo ni mambo gani sasa?”.

Nilikaa kama dakika 30 mule ndani nikiwa nimeduwaa nawaza lakini ghafla nikasikia mlio wa ndoo kama zimegongana hivi pale nje. Nikachungulia dirishani nikamuona Salma amevaa khanga ametoka kuoga alikua anaweka ndoo ya kuogea pale nje na baada ya kuweka nikakuta kama anatembea anakuja kama kwenye chumba changu hivi. Nilishtuka sana, nikatoka pale dirishani alafu nikakaa haraka huku nikiwa nawaza “Anakuja huku au?” huku nimetega sikio zote mbili mlangoni. Nikasikia visauti vya mlango ukigongwa kidogo pamoja na sauti ndogo ya Salma “Hodi”.

Mimi moyo ukadunda “Duh!” nikaitikia “Karibu” huku nikiweka akili na macho yangu yote mlangoni kuona kama anataka mimi niende mlangoni nikamsikilize au ataingia ndani maana mlango nilikua sijaufunga, Niilikua kama nimeufunga hivi ila niliacha kinafasi kidogo. Baada ya sekunde chache nikaona mlango unasukumwa, Salma huyo anaingia ndani. Mtoto alikua kajifunga khanga na haijafika hata magotini. Paja zilikua nene na kwakua alitoka kuoga kwenye ngozi yake nyeupe kulikua kama kuna vitone vidogo vidogo sana vya maji. Sura yake ilikua nzuri lakini kwa muda huo macho yake yalikua yamevimba alafu mekundu kutokana na kulia. Hata nilivyokua nikimuangalia muda huo alikua ni mtu ambae anataka kulia lakini anajikaza. Laikini bado alikua ni mzuri sana.  

Basi akasimama mbele yangu alafu akaniangalia usoni kidogo na akaniambia “Mambo” kisha akaangalia chini kwa aibu huku akijiminya minya vidole vya mikono. Mimi nikamwambia “Fresh Salma, Niambie” akajibu “Safi” huku akiwa anaendelea kuangalia chini mara ajikune shingo kidogo. Mimi nilikua sijajua amefuata nini hapo muda huo maana sikumuita hivyo nikataka kumuuliza alichofuata lakini kabla sijamuulliza nikakuta anaanza kusema “Sa… Samahani… nilikua naomba unisaidie ile hela nilio irudisha.  Sasa hivi nipo tayari kukupa ulichokua unahitaji”.



Mh mimi kusikia hivyo nikashtuka sana maana pamoja nakwamba nilikua nasikia watu wanasema yeye ni Tausi na kazi yake ni kujiuza nilikua bado siamini sana maana nilikua nampenda sana na sikuzani kuwa ni mtu wa hivyo kabla ya kuuweka moyo wangu kwake. Sikumbuki nilitaka neseme nini baada ya kuambiwa hivyo ila nakumbuka jasho la ajabu lilinishuka ghafla. Nahisi Salma aliona hali yangu maana nikakuta tu kabla sijaongea chochote, Salma akaanza kudondosha mimachozi huku akisema “Ila mimi ngoja nikwambie tu ukweli… Mimi sasa ivi sipo kama watu wanavyonifikilia… Kuna sehemu ya maisha yangu natamani niibadilishe ila sijui pakuanzia maana hata nikiikimbia naona inanikimbilia. Kuna muda naona hata nikiielezea kwa watu hakuna atakae nisaidia ila naona bora nikwambiie tu wewe maana ndio mtu ambae nimekupenda kwa sasa japo sijui utakavyo nichukulia”

Alivyokua akiongea hivyo niliganda nilikuwa namsikiliza kwa makini kweli maana alikua anaonekana anatoa maneno toka moyoni mwake kabisa yani. Salma aliendelea kuongea, akasema “Mimi naitwa Salma na hilo ni jina langu kabisa japo wengi hunijua kwa jina la Tausi hapa mjini. Nilipewa jina la Tausi na dada mmoja ambae alinileta hapa mjini toka kwa bibi yangu huko Tanga.  Huyu dada alikua anaitwa Mariam na kwasasa hayupo hapa Dar, alipata fulsa ya kwenda kufanya kazi Kanada na sina mawasiliano nae toka aende huko. Alinitoa kule Tanga kuja huku Dar akidai kuna kazi nzuri anaifanya na atanifundisha maana yeye kule alikua anakuja kusalimia wazazi wake tu na hao wazazi walikua wanaishi karibu na bibi yangu. Mimi nilikua nakaa kwa bibi kwasababu wazazi wangu walifariki kwa ajari ya gari wakati hawana hata nyumba na ndugu wengine hawakua na msaada kwangu kiasi kwamba nilishindwa kumaliza hata shule ya sekondari.
Huyo dada ni kama alikua ananisaidia hivi kidogo niwe na uwezo wa kujitegemea maana nilifika kwenye umri ambao nilitakiwa nijipende, niwe na muonekano msafi lakini sina pesa hata ya kununua mahitaji yangu. Alivyonileta hapa mjini akanifundisha kazi aliokua akiifanya ambayo nikuuza mwili. Nilikua naogopa sana pindi alipokua akinifundisha maana kilikua ni kitu cha ajabu sana kwangu ila mazingira alioniweka yaliniondoa hofu kidogo maana jirani zetu na marafiki zetu walikua wanafanya kazi hiyo hiyo. Baadae niliingia mpaka kwenye makundi ya watu wanaofanya kazi hiyo na makundi hayo yalikua yana utaratibu wa kuchangisha pesa kwa kila mwanakikundi na kununuliana vitu. Usipokua unapeleka pesa kwa muda mrefu inakua kama unadaiwa hivi, wanakuja kuchukua vyombo au vitu vyako na kukutoa katika kikundi. Njia kuu ya kupata pesa za kupeleka kwenye kikundi ni kujiuza tu, wanakikundi wote wanajua hilo.


Mimi kiukweli kazi hii niliifanya kwa miezi michache sana na moyo ukaanza kukataa kuendelea lakini nilikua naogopa kuacha kila nikiwaangalia watu walionizunguka au nikifikilia pesa ninazotakiwa kutoa ili mambo yangu yaende vizuri. Ikafika wakati watu wengi wanajua najiuza na wananiita majina ya hovyo na kunisema vibaya karibu kila kona ninayofahamika. Watu wengine wananisema vibaya ila hawajawahi uona mwili wangu. 
         
Nilichoshwa na hayo mambo, nikaamua toka moyoni kuiacha hiyo kazi. Nilijaribu kutafuta mtu ambae atanioa ili nitulie lakini kila nikikutana na mwanaume anakua ananichukulia mimi ni mtu ninaejiuza hivyo anakua hana mpango na mimi. Wengine wanaweka mipango lakini inaharibika kutokana na watu kuwambia kuwa najiuza wakati mimi nataka kuacha.

Nina miezi sasa nimejitenga na marafiki wanaojiuza, nimepanga chumba huku ambako watu hawanijui sana na nilianza mpaka kuuza nguo za watoto ili kuondokana na kazi ya kujiuza lakini leo mambo yamebadilikatena. Rafiki zangu wamekuja kubeba vitu walivyoninunulia na mbaya zaidi wameondoka mpaka na nguo ninazouza. Hapa sina kitu cha maana kwenye chumba changu, sina hela na sielewi pakuipata kwa haraka zaidi ya kuingia tena kwenye biashara ya kujiuza na ndio maana nimekuja kwako hivi.

Samahani kama unanipenda kweli, najua utakua umeumia kujua mambo yangu ila naomba utambue kuwa na mimi nakupenda sana lakini maisha yangu mimi siyaelewi. Natamani kutoka kwenye maisha haya na kuwa na mwanaume mmoja maishani atakae nielewa lakini kila nikijaribu, vitu vinaingilia kati, nadondoka tena kwenye kazi ya kujiuza. Nikifanikiwa kutoka kwenye maisha haya mabaya, sitatamani kurudi tena. Natamani kuitwa mke, natamani kuheshimiwa kama watu wengine na natamani nifute vitu vyote vibaya nilivyowahi fanya lakini nashindwa.”



INAENDELEA…

One thought on “UTAMU WA JUMLA 08 (Simulizi ya Maandishi)”

Leave a comment