Nilikaa kitandani nikaanza kuwaza “Yaani inamaana Tausi ndio huyu Salma?… Na inamaana wale madada ulioniamsha nikiwa nimelala walikua wanamtaka Salma ambae ndie huyo Tausi?… alafu huyo tausi anajiuza?… Ah hapana, Mpenzi wangu Salma sio huyo Tausi wao”
Lakini nikaanza kufikilia tena “Au kweli anaitwa Tausi na anajiuza ndio maana kila nikimtaka tulale wote anakataa? huenda anataka hela huyu…. Dah ila ananiumiza moyo huyu mwanamke. Sijui kwasababu nampenda?… Mbona moyo wangu unaumia hivi nikiwaza kuwa ni kweli anajiuza?… Mh Ila kama ni kweli Salma anajiuza basi siku zote hizi alikua ananiona mshamba na mapenzi yangu ya maneno haya… Yani nabembeleza na kuogopa kabisa kumbe mtu mwenyewe anataka hela na sio maneno” nilpokua nafikilia hivyo moyo ulikua unaumia na nikaanza kuona mpaka kizungu zungu. Nikalala kitandani huku nikijiona mshamba kweli. Siku hiyo nilikua humo ndani mpaka Salma akarudi. Salma alivyorudi alisalimiana na mimi nikiwa ndani huku yeye akiwa nje.
Sikutaka kupiga nae stori kabisa siku hiyo. usiku ulipoingia alikua akinitumia ujumbe kwenye simu lakini sikua na jibu maana nilikua na mawazo alafu nahisi kama Salma ananiona mshamba na vitu vyote anavyofanya ni kama ananiigizia hivi. Nilikua nazisoma kabisa ila sijibu na alivyona sijibu nikakuta amenitumia sms akisema “Njoo tulale wote” lakini nikaipuuzia. Nikakuta tena akasema “Njoo basi, nakusubiri hapa mlangoni kwangu”. Mh mimi kuona hivyo tamaa ikaniingia kidogo nikawaza “Mh ngoja niende tu na nikipata nafasi ya kula tunda ntakula tu maana pamoja nakwamba anajiuza bado namtamani… Ngoja nikamkunje mpaka hasira ziishe, huenda naweza punguza hata mawazo kwa kufanya hivyo”. Nikatoka pale kitandani nilipo jilaza ili nitoke nje niende kwa Salma lakini kabla sijaenda kwa Salma, akili ikaniambia “Nenda na hela maana anauza huyo… Usije ukaumbuka huko”. Na mimi kweli nikachukua hela za kutosha na kutoka nje kuelekea mlangoni kwa Salma.
Nilipofika mlangoni kwake tu nikakuta mlango wake unafunguliwa ili niingie lakini kabla sijaingia alinisimamisha pale pale kwa mapozi ya kimahaba hivi akiwa amevaa kinguo kimoja chepesi kilichokua kimeacha aslimia kubwa mikate yake nje. Nikakuta ananiambia kwa sauti ya upole “Kwanini haujibu sms zangu?… nimekukosea nini?” basi mimi nilivyo muona anaongea hivyo nikaona ndio ananiona mshamba kabisa yani maana nimeambiwa yeye anaangalia hela tu. Sikupoteza muda kumjibu, nikachukua hela nilizokujanazo nikamshikisha mkononi mwake alafu nikamwambia “Samahani, unaweza kunihudumia usiku wa leo mpaka asubui?”. Nikakuta kashtuka, kaiangalia ile hela kisha kaniangalia mimi husoni kwa sekunde chache alafu akafunga mlango wake na kuniacha nimesimama pale mlangoni.
Baaada ya kuona hivyo mimi nikaona nirudi kwenye chumba changu tu na niliporudi nikakaa kama dakika moja hivi hali yangu nikiwa siielewi. Ghafla ikaingia SMS ya toka kwa Salma “Mimi sio mtu wa hivyo, kwanini unanichukulia hivyo?” mimi nikaona ananiigizia huyu, nikamjibu “We Tausi acha kunizungusha,mimi nipo tayari kulipia… si ndio kazi yako hiyo?” Yeye akasema “Nani Tausi? Mimi sio tausi” alafu hapo hapo kabla sijamjibu akasema “Njoo uchukue hela yako, nimeiweka chini mlangoni kwangu. wakiiba usinidai”. Mh mimi nikaona niangalie kama kweli ameiweka chini hela yangu, nikakuta kweli ipo chini pale mlangoni kwake. Nikaichukua ile hela pale mlangoni kwake alafu nikarudi kwenye chumba changu. Sikujibu SMS yoyote muda huo mpaka akapiga simu akawa anaongea mambo yasio eleweka kwa sauti kama ya kulia hivi eti “Wasikudanganye hao… nakupenda… mimi sio wa hivyo… Tausi sio jina langu, naitwa Salma… Watu wananiongelea vibaya. Mbona huongei sasa? wewe huongei?” mimi nilikua simjibu, alikata simu.
Sikutaka kumjibu chochote siku hiyo mpaka asubui ikafika, nikajiandaa kwenda kwenye mafunzo yalionileta mjini hapo alafu nikaondoka kwenda kwenye mafunzo. Nilivyokua naondoka niliacha mlango wa Salma haujafunguliwa na ulikua ukionekana kama Salma bado yupo ndani hajaamka. Sikua namjali sana Salma muda huo maana nilikua naona ananiumiza japo moyoni bado nampenda.
Kule kwenye mafunzo nilikua sijaenda siku za nyuma na nilivyoenda siku hiyo nilikuta kumbe katika siku ambazo sikwenda kampuni ilisema kila mtu anaetaka kuajiriwa pindi mafunzo yatakapoisha inatakiwa alipie Milioni 10 pindi mafunzo yatakapoisha ila watakao toa ndani ya wiki hiyo milioni 5 hawatatakiwa kulipa tena. Hiyo ni kama punguzo kwa watu watakaolipia mapema. Basi mimi nikaona imebaki siku moja tu ofa iishe na nilipokua narudi toka mafunzoni nikawa nawaza kwamba nikifika nyumbani nikawapigie simu wazazi na kuwajulisha juu ya hili. Nilipokua nafika kwenye nyumba niliokua nakaa nikakuta watu wengi kidogo maeneo yale na tena ni wanawake alafu wapo maeneo ya chumba cha Salma.
Nilikua sielewi wamefuata nini pale ingawa nilikua naona wanatoa kitanda na vitu vingine ndani ya chumba cha salma. Sikutaka kujihusisha nao, nikaelekea moja kwa moja kwenye chumba changu na kukaa humo ila nilipokua nimekaa nikawa nasikia uko nje watu wakitupa maneno kama “Tumekutafuta sana… Kwenye simu hupatikani una mwezi sasa… Kama yamekushinda yaache yaende na raha zake… mwanamke huna haya”. Nikaona ngoja nichungulie dirishani labla nitaona vizuri kinachoendelea, nikaona watu wanabeba vitu wanaondoka navyo na kumuacha Salma amekaa mlangoni kwake kama anajizuia kulia hivi ila machozi kiasi yana mdondoka. Watu hao walikua wakiondoka huku wakitupa maneno ya dharau sana na kulitaja jina la Tausi na sio Salma.
Nikatoka pale dirishani nikakaa kitandani nawaza “Dah ila huyu mwanamke mzuri… ila simuelewi, inamaana yeye ndio Tausi kweli? na mambo yaliokua yanaendelea hapo ni mambo gani sasa?”.
INAENDELEA…
One thought on “UTAMU WA JUMLA 07 (Simulizi ya Maandishi)”