Maneno matamu yana nguvu ya kipekee ya kugusa moyo wa mtu. Unaweza muumiza mtu kwa maneno au kumfurahisha. Kwenye mapenzi, unaweza tumia maneno kumfurahisha mpenzi wako na kuimarisha uhusiano wenu. Hata ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) unaweza kuwa njia rahisi na ya haraka ya kuonyesha hisia zako za dhati na kumfurahisha mpenzi wako. Unaweza usiwe naye kwa muda wote, lakini maneno yako yanaweza kuunganisha mioyo yenu hata mkiwa mbali.
Mapenzi si tu kumfanyia mpenzi wako matendo makubwa, bali pia ni kuhusu kufanya mambo madogo madogo kila siku. Mambo kama kumtumia ujumbe mzuri uliojaa upendo unaweza kuwa ni kuonesha mapenzi pia. Kumwambia mpenzi wako neno “Ninakufikiria,” au “Unanifanya nijisikie furaha.” Kupitia sms kunaweza fanya some huo ujumbe na kufikilia mambo mengi chanya juu ya upendo wenu. Yani kuna ujumbe hata ukimfikia mpenzi akiwa anawasiwasi au ameweka jambo baya moyoni, akiusoma moyo wake unakua vizuri ghafla na kusahau yote.
Hapa sisi kama kawaida, tumekuandalia maneno ya mapenzi unayoweza tumia. Haya ni yale maneno matamu ambayo unaweza kumwambia mpenzi wako kwa njia ya SMS. Maneno haya yamebeba hisia, yanayowaweka wapenzi karibu, na kufurahisha.
Mpenzi anaekupenda sana anaweza kukuacha kwasababu hizi BONYEZA HAPA>>>
Maneno matamu ya kumwambia mpenzi wako kwa sms
- Walimwengu bhana… Watakuja kukudanganya, watajifanya hawajui kuwa tunapendana, wanajifanya wanakupenda sana ila nia yao waharibu penzi letu alafu wapate cha kusema. Najua kupendana kwetu ni huzuni kwao, ila sitaacha kukupenda.
- Huenda kiumbe unaye muogopa hapa Duniani ni mwanaume ila naomba usiniogope mimi. Nakupenda sana na nipo kufuta maumivu yote umepitia malkia wangu.
- Wakiniambia niwaweke moyoni, nitawambia moyoni upo wewe na funguo za moyo nimepoteza.. siwezi kukutoa na wala siwezi waingiza
- Na jua kuna nyakati tunaweza pita zikawa ngumu kidogo kuamini kuwa tunapendana. Ila usisahau kuwa nakupenda hata kwenye nyakati hizo wangu.
- Siku njema kwangu ni ile ninayojua upo salama na bado unanipenda. Ukiwa salama nakua na Amani, ukiwa unanipenda nakua nina furaha mpenzi.
- Tuhesabu 1 mpka 5 alafu ntakwambia kitu. Haya tuanze sasa. Moja, Mbili, tatu, nne, tano, Anaesoma ujumbe huu ndie ameuteka moyo wangu. Nampenda sana.
- Umewahi jaribu kuhesabu nyota? Ukiwa unahesabu nyota angani, unaweza anza kwa kuziona chache mwanzoni lakini ukizingatia, nyingine hua kama zinaibuka na kuwa nyingi kiasi cha kutohesabika. Ninasababu nyingi za kukupenda ila ni ngumu kuhesabu kama ilivyo kwenye nyota. Kila muda unavyoenda, nazidi kupata sababu nyingi za kukupenda.
- Moyo wangu unanisukuma nikwambie nipo tayari kufanya chochote hapa Duniani kwaajili yako. Yote ni sababu unaupa furaha mpaka siku hizi unadunda sana likitajwa jina lako.
- Mbali na uhai nilionao, penzi lako ndio kitu cha thamani maishani mwangu. Naweza potezea chochote ila nikabaki na furaha sababu wewe unanipenda.
- Nakupenda sana mpenzi. Moyo wangu Nimekupa mazima kama zawadi ya upendo. Na ikitokea siku nikakwambia unauumiza, Sina maana unirudishie, ninamaana uubembeleze.
- Maana sahihi ya mapenzi nimeijua nilipokupata wewe. Penzi lako limenipeleka ulimwengu uliojaa Raha, kwenye Giza umekua ni taa mpaka najivunia kuwa na wewe.
- Unataka kujua wewe ni nani kwangu? Wewe ni yule ambae tukikosana nakua sina furaha. Yule ambae nikifikilia anavyonipenda huwa natabasamu. Yule alienionesha kuwa Asali ladha yake halisi ni utamu. Yule natamani niwe nae hilele maishani mwangu.
- Nakupenda sana na natamani ujue kuwa walimwengu wanataka tuachane wakati sisi tunataka tuwe wote milele. Tukiyasikiliza ya walimwengu tutafika wanapotaka tufike na tukisikilizana, tufika tunapotaka kufika.
- Umejaa kwenye kila sehemu ya moyo wangu. Unaweza kuwa Sababu ya huzuni au furaha yangu.
- Unaweza kaa bila kuvuta pumzi ila sio kwa muda mrefu. Na ndivyo naweza kaa bila ukaribu na wewe ila sio kwa muda mrefu. We ni mtu muhimu kwangu, nakupenda.
Ni hayo tu katika ukurasa huu, unaweza tembelea ukurasa mwingine na kusoma sms za mapenzi nyingine kama hizi zitakua sio chaguo zuri kwako. Endelea kuwa karibu na The bestgalaxy kwa mambo mengine zaidi.