Dubai ni mji maarufu duniani unaovutia watalii kutoka kila pembe ya dunia. Una mandhari za kuvutia, teknolojia ya kisasa, utajiri na ni mahali panapopendwa sana na watu. Lakini, kama ilivyo kwa miji mingine mikubwa, kuna sheria, desturi, na kanuni za kipekee ambazo wageni wanapaswa kuziheshimu. Kutozingatia mambo kama hayo ukiwa Dubai, kunaweza kusababisha usumbufu au matatizo makubwa hatakama ni mgeni.
Kama mgeni unayeitembelea Dubai kwa mara ya kwanza, ni muhimu kujua mambo unayotakiwa kujiepusha nayo ili kuhakikisha safari yako ni ya kufurahisha na sio matatizo. Mji huu una mchanganyiko wa mila za Kiislamu na tamaduni za kisasa, ambazo zote zinahitaji heshima kutoka kwa wageni wake. Kutokujua sheria za msingi kunaweza kusababishia migogoro isiyo ya lazima.
Katika makala hii, tutakupa mwongozo wa mambo unayopaswa kuepuka unapokuwa Dubai. Kwa kuzingatia mwongozo huu, utakuwa na fursa ya kufurahia safari yako bila wasiwasi na kuonyesha heshima kwa wenyeji wa mji huu wa kuvutia.
Jinsi ya kupata Ticket za ndege za bei rahisi BONYEZA HAPA>>>
Mambo Usiotakiwa Kufanya Ukiwa Dubai
Usile hadharani kipindi cha Ramadan
Kipindi cha Ramadan ni takatifu kwa Waislamu, na kula, kunywa, au kuvuta sigara hadharani wakati wa mchana ni marufuku kwa wote, wakiwemo wageni. Ni muhimu kujizuia na kuheshimu ibada ya kufunga kwa wenyeji. Kama ukiwa katika mji huo kipindi cha Ramadan, basi kuwa mtulivu na ufuate utaratibu wao.
Usilale na mpenzi wako chumba kimoja kwenye baadhi ya hoteli
Hoteli nyingi katika Dubai zina sera zinazofuata sheria za Kiislamu, na wanandoa wasiooana hawaruhusiwi kulala chumba kimoja. Hakikisha unafahamu sera za hoteli kabla ya kufanya malipo. Kuna hotel nyingine huruhusu wageni kulala pamoja hatakama hawajaoana na ndio unapaswa kuzitumia ili kuepuka usumbufu.
Kunywa pombe hadharani
Ingawa pombe inaruhusiwa lakini ni kwenye maeneo maalum kama baa na hoteli zinazoiruhusu. Kujiachia na kunywa au kuionyesha hadharani kunaweza kusababisha matatizo makubwa, ikiwa ni pamoja na faini au kifungo. Swala hili linatakiwa kuzingatiwa kila siku na sio siku za Ramadan tu kama ilivyokua kwenye kula.
Kusalimia kwa kutumia mkono wa kushoto
Katika tamaduni za Kiarabu, mkono wa kushoto unachukuliwa kama mchafu, na hivyo ni vyema kutumia mkono wa kulia unapotoa au kupokea kitu, au hata kusalimiana. Fanya havyo maana Dubai ina utamaduni wa kiarabu na nivema ukauheshimu unapokuna wenyeji.
Hatumaini hayo wamekupa mwanga na mwongozo juu ya jinsi gani unatakiwa kuwa au kufanya huko Dubai. Mbali na kuyajua hayo, ni vema ukawa chini ya mtu mwenyeji atakea kusaidia kujua zaidi mambo ya kufanya katika mji huo ili kuhakikisha haukosei.