UTAMU WA JUMLA 06 (Simulizi ya Maandishi)





Walivyoondoka tu nikajisemea “Bora wameniamsha maana simu nimeiweka pabaya kiasi kwamba mwizi angepita maeneo haya angechukua simu bila mimi kujua”. Baada ya hapo mawazo ya Salma yakaanza kuteka kichwa changu. Nikaanza kuwaza “Dah Salma nae sijui kaenda wapi?… Naanza mpaka kukosa raha yani. Na hii ndoto nilioiota hapa ni ukweli au imesababishwa na makelele ya waliokua wananiamsha tu? Itakua ni hawa mbwa wameniletea lindoto la ajabu… ila sasa mbona hayupo na hakuniambia jana kwamba hatokuepo leo?”Niliwaza mambo mengi sana hapo lakini kichwa kilikua hakinipi majibu ya moja kwa moja, nilikua najiuliza maswali yanayo zaa maswali tu.


Mida ya saa 7 mchana hivi nikiwa palepale mlangoni nilikuta Salma anarudi na anarudi na mzigo mkubwa kiasi kwenye pikipiki. Nilivyomuona Moyo ukadunda kwa furaha “Nduh” alafu nikaendelea kuwaangalia yeye na dereva wa pikipiki wakifika pale. Walipofika nikasalimiana na dereva wa pikipiki pamoja na Salma pia alafu nikasaidia kutua mzigo na kumuwekea mlangoni kwake maana alishakua malaika wangu muda huo, vitu vyake vigumu na vizito lazima nijihusishe navyo.

Baada ya hapo dereva wa pikipiki aliondoka na kutuacha pale na mimi hapo nilimuuliza alikua wapi akaniambia alikua kununua mzigo wa nguo za watoto anataka kuanza kuuza maana alikua hana kazi ya kufanya hapo mjini. Aliponijibu tu hivyo mimi sikumchimba sana kwenye mambo ya kazi huko, nikajikuta moyo umekua mwepesi alafu nikawa na furaha ya ajabu kumuona malaika wangu Salma amerudi.


Siku hiyo tukaendelea kuongea mambo ya mahusiano yetu na mambo mengine ya kijinga kijinga mpaka jua linazama.  Usiku uliingia na katika kutumiana nae ujumbe usiku huo nilimuomba aje tulale wote lakini alikataa, nikamuomba nimfuate nikalale kwake lakini bado alikataa. Nikajua huenda ni mwanamke muoga na anaogopa kukubari kirahisi kuwa na mwanaume, hivyo nikamuacha siku hiyo, sikumsumbua sana. Na hata kulivyokucha niliendelea kuwa nae vizuri tu kimaongezi ila sikuingizia swala la yeye kukataa kulala na mimi usiku. Sikwenda kwenye mafunzo siku hiyo ili tu nibaki na yeye nyumbani.



Siku ya pili usiku katika kuchati nikaamua kujaribu tena kumshawishi tulale wote usiku huo chumbani kwangu ili angalau nipate nafasi ya kumkamata na kumgusa panapotakiwa. Nakumbuka nilimwambia “Salma, njoo ulale kwangu leo… Natamani tulale wote” lakini hakukubari, akajibu “Ah hapana, huko siji hahaha”. Nilijaribu pia kumwambia anifungulie mlango wa chumba chake ili niende nikalalale kwenye chumba chake lakini hakuniruhusu kufanya hivyo, alikataa. Siku hiyo nilijisikia vibaya kidogo maana ilikua ni mara ya pili kunigomea lakini nikajitahidi kupuuza alafu tukaendelea kuongelea mambo mengine. Kulivyokucha, tulikua tunaongea mambo ya mapenzi na vitu vingine kama kawaida lakini sikua naingizia mambo ya yeye kukataa kulala na mimi usiku. Na kiukweli nilikua siwezi muuliza “Kwanini hutaki kulala na mimi?” akiwa mbele ya macho yangu kwakua nilikua kwa kiasi flani namuogopa na pia kichwani nilikua nawaza “Nisiwe na haraka, huenda usiku unaofuata atakubari”. Jambo hili lilinipa mawazo sana mpaka nikashindwa tena kwenda kusoma mafunzo, nikabakia tu nyumbani na yeye.


Siku ya tatu usiku pia alinigomea na siku hiyo niliumia sana maana ilikua ni mara ya tatu hiyo najaribu kumshawishi na hanikubalii. Lakini usiku huo nilijikaza tena nikaendelea kuongeanae mambo mengine tu. Na baada ya kukucha nikakutananae kama kawaida na tulikua kama wapenzi kabisa katika kusalimiana na kuongea. Siku hiyo nilibaki nyumbani ili niongee nae tena kama kawaida lakini sikupata nafasi ya kukaa nae muda mrefu maana mida ya saa 3 asubui alikua anaenda kuuza nguo za watoto na aliniaga na aliniambia anaweza kurudi jioni.
Hiyo siku Salma alivyoondoka na kuniacha pale nyumbani nilikumbwa na mawazo mengi sana juu yake kwakua nilikua simuelewi kabisa. Nakumbuka niliingia ndani ya chumba changu nikakaa nikawanawaza “Huyu dada mbona ananitesa hivi? Au ndo ameanza mambo aliokua ananifanyia Zuu kipindi nipo chuo?  yaani nashindwa kumuelewa maana mchana tukikutana anakua kama ni mpenzi wangu ambae anaweza kubali chochote ninachomwambia lakini nikimwambia usiku tulale wote anakataa… Inamaana na haelewi ninachomaanisha au? Mh itakua huyu Salma hanipendi ila ananiigizia… Itakua ananiigizia tu huyu maana pamoja nakwamba nashindwa kumwambia moja kwa moja ninachotaka lakini jinsi ninavyomwambia tulale wote, yeye ilibidi aelewe tu nataka nini. Au mimi ndio nakosea kumwambia? Mh labla ila bado nampenda acha anisumbue tu akili yangu… Kuna siku ataniruhusu tu kugusa mtunda wake ule… yani mdada mweupee, mzuri sura alafu kapewa umbo lenye mamizigo ya kutosha… mmh acha anitese tu ila nikikamata nitambana mpaka atafurahi”


Wakati nimo ndani mule naendela kuwaza nikasikia kama kunamtu nje anapiga hodi hivi, Nilipotoka nje nikakutana na  majamaa watatu. Mmoja kati yao niliposalimiana nae akajitambulisha kuwa yeye ndie mwenye kile chumba ambacho nilikikuta kwenye nyumba hiyo wakasema mwenye nacho amesafiri. Alisema amekuja hapo kuchukua vyombo vyake na ameishaongea na mwenye nyumba. Mimi nikamkubalia na baada ya dakika chache nikawa nawashuhudia wakifungua mlango na kuanza kutoa vitu kuvipeleka kwenye gari ambalo lilisimama mbali kidogo na kwenye nyumba.

Baadae na mimi nikaona nisiishie kuwaangalia tu, nikajumuika nao kuwasaidia kutoa vyombo na kupeleka kwenye gari. Basi tukaanza kupiga stori huku tukifanya kazi kama ilivyo kawaida kwa wanaume kupiga stori nyingi hatakama hatujajuana sana. Tulifanikiwa kupakia kila kitu kwenye gari na jamaa akaanza kuniaga. Nakumbuka yule jamaa alisema “Asante sana, mimi nimehamia mtaa wa mbele hapo kunajumba linawapangaji wengi, Hiyo nyumba ni ya mama mmoja tajiri sana anafahamika kama Mama Suzi anakaa kwenye jumba lake huko… Ukiwa na muda unaweza ukanitembelea mzee” basi mimi nikaitikia “Anh sawa, usiwaze”. Baada ya mimi kusema hivyo akasema “Poa bwana, utaniagia huyu Tausi maana naona hayupo sjui kaenda kujiuza huko hahaha”.

Mh mimi nikashtuka, nikamuuliza “Tausi yupi huyo?” akasema “huyo dada mweupe mwenye chumba hicho”. Mh nilishangaa nikajikuta naropoka “Anaitwa Tausi huyo?”. Huyo jamaa akajibu “Ndio.. kwani vipi? si ndio jina lake ilo au?” Muda huo niliona niseme tu “Ndio” ili tukaete maengezi. Nikamsikia jamaa akisema huku akiondoka “Nasikia huyo dada ni hela yako tu… ukimpa hela, anakupa chungawa. Kuna mitaa niliwahi muona wanamjua sana ila sijui mitaa ya huku kaamia kufanya nini… Kwaheri bwana”. Mimi sikua na maneno mengi hapo nikajibu “Sa.. sawa” alafu nikaenda haraka ndani kupumzisha akili maana hali yangu iliishaanza kuwa mbaya. Nilikaa kitandani nikaanza kuwaza “Yaani inamaana Tausi ndio huyu Salma?… Na inamaana wale madada ulioniamsha nikiwa nimelala walikua wanamtaka Salma ambae ndie huyo Tausi?… alafu huyo tausi anajiuza?… Ah hapana, Mpenzi wangu Salma sio huyo Tausi wao”…





INAENDELEA….   

One thought on “UTAMU WA JUMLA 06 (Simulizi ya Maandishi)”

Leave a comment