Jinsi ya kutengeneza Video za katuni kwa simu (Tumia kupata Pesa mtandaoni)

Pengine unaweza kuwa ni mtu unaempenda kujua namna gani utaweza tengeneza katuni Bora kupitia simu. Jambo hili sio jepesi sana kulifanya kama unataka kutengeneza katuni zenye ubora wa hali ya juu. Asilimia kubwa ya utengenezaji wa katuni zenye ubora huwa ni mgumu kidogo kuliko zisizo na ubora. Lakini habari njema ni kwamba, kwasasa unaweza tengeneza katuni zenye ubora kirahisi kwa msaada wa Al. Yani kuna huduma za AI ambazo zinaweza kutumika kwenye mchakato wa kutengeneza katuni zenye ubora ili kurahisisha mchakato mzima.

Hapa The bestgalaxy tunaenda kukuelezea kila hatua unayotakiwa kuichukua ili kutengeneza video za katuni kwa kutumia simu. Ili kuelewa mchakato mzima, utatakiwa kuwa na ujuzi kidogo kwenye mambo ya kuedit picha, video na uelewa kwenye matumizi ya AI. Kama upo vizuri kwenye upande huo, fuata maelezo yafuatayo ili kutengeneza video za katuni.

Ujuzi utakao kuwezesha kuingiza pesa mtandaoni BONYEZA HAPA>>>

Jinsi ya kutengeneza video za katuni kwa kutumia simu

Kwanza kabisa utatakiwa kuwa na app ya PicsArt, Chat GPT na Motion Ninja kwenye simu yako. Baada ya kupata app hizo kwenye simu yako, fuata hatua zifuatazo ili kutengeneza video za katuni:

Hatua ya kwanza; Tengeneza katuni muhusika na mazingira yake.

Hapa utatakiwa kutengeneza kwanza Katuni ambae atakua muhusika kwenye video pamoja na mazingira atakayokuepo. Kufanya hivi ingia kwenye app ya Chat GPT, fungua akaunti kisha itumie kuunda picha ya katuni muhusika. Unaweza muunda katuni huyo kwa kuandika “Create an image of cartoon character sheet” alafu utapewa picha za huyo katuni akiwa kwenye hali tofauti tofauti.
Baada ya kutengeneza huyo muhusika, utatakiwa kutengeneza au kuunda Picha ya mazingira yake ambayo inaitwa Background image. Kuiunda hiyo picha, unaweza andika “Create background image” hapo hapo kwenye ChatGPT alafu ukaletewa.

Hapa kwenye kuunda Picha, ujuzi wa kutumia AI ndio unahitajika zaidi. Na baada ya kuunda Picha hizo kupitia ChatGPT, fanya kudownload/kupakua zote ziwe kwenye simu yako.

Hatua ya pili; Tengeneza picha inayounganisha muhusika na mazingira yake.

Katika hatua hii, utatakiwa kutumia app ya PicsArt kutengeneza picha ambayo imeunganisha katuni muhusika na mazingira yake. Yani fanya kuedit picha iwe inamuonesha yule katuni akiwa kwenye mazingira ya picha ulioiunda (Background image). Hii inabidi uwe na ujuzi kidogo katika upande wa kuedit picha.

Baada ya kufanikiwa kupata picha nzuri ilio oanisha mazingira na muhusika, fanya kuitunza picha hiyo kwenye simu yako kwaajili ya hatua nyingine.

Hatua ya tatu; Badilisha picha kuwa vipande vya video za muhusika akifanya mambo mbalimbali

Katika hatua hii, utatakiwa kutumia huduma ya AI ambayo inaitwa Kling AI (KlingAI.com) ili kugeuza picha ulioitengeneza kuwa vipande vya video. Kling AI inakuwezesha mtumiaji kugeuza picha kuwa video. Unaweza itumia kling kufanya picha yako igeuke video inayoonesha muhusika akikimbia, akiongea, akicheza na mambo mengine unayohitaji.
Kwenye hiyo huduma, wewe tengeneza video fupi hata 3 tu zikionesha muhusika akifanya matendo yanayo endana. Mfano; unaweza kutengeneza video 2 za muhusika akiongea alafu 1 ikawa inamuonesha muhusika akiondoka.

Baada ya kuunda video hizo kupitia Kling AI, fanya kuzidownload kwenye simu yako kwaajili ya hatua nyingine.

Hatua ya nne; Unganisha vipande vya video na kuingiza Sauti

Hatua hii ni hatua ya mwisho kabisa ambayo itakuhitaji utumie app ya Motion Ninja kuunganisha video zote ulizounda, ziwe video moja. Inabidi unapounganisha uziweke kwenye hali ambayo italeta maana kwa mtazamaji. Usiishie kuunganisha tu, weka na sauti katika video hizo. Ikamilishe video kwa kuweka mambo yote unayoona yanaweza kufaa.


Baada ya video kukamilika, basi utakua tayari umefanikiwa kutengeneza video ya katuni kwa kutumia simu yako. Njia hii ni rahisi sana kuliko njia nyingine.

Uzuri wa kutengeneza katuni kwa mtindo huu ni kwamba unaweza tengeneza kitu kikubwa kulikuo unavyofikilia. Yani hizi ni katuni ambazo ukiamua kuzitengengeza na kuzisimamia vizuri, utaweza kuzitumia kuingiza hata brand na hata pesa kupitia mitandao ya kijamii. Kwaiyo kujua hiya inaweza kuwa na hatua nzuri ya kumiliki vitu vikubwa mtandaoni na kutengeneza pesa pia.

Kama unataka kufundishwa kwa ukaribu zaidi jinsi ya kutengeneza katuni kwa mtindo huu na kuingiza pesa, tuma Neno “Kujifunza katuni” kwenda namba 0715 233 405 ili ujulishwe pindi masomo haya yatapoanza (Sio Bure).

Leave a comment