UTAMU WA JUMLA 05 (Simulizi ya Maandishi)

Ila kama huyu ni mke wa mtu basi waliosema mke wa mtu mtamu hawajakosea kabisa… Ngoja nimuulize” nikaifuta ile SMS niliotaka kuituma. Nilivyofuta nikamwambia tu “Salma, nikuulize Swali?” alafu ikapita kama dakika moja nikakuta anajibu “Ah hapana usiniulize, nijibu kwanza swali langu”….

Basi mimi nikamwambia “Skia Salma, nijibu kwanza swali ntakalokuuliza alafu ndio nitakwambia” nikakuta tu kaniambia “Nina hamu” nilipo soma nikawa nawaza “Anamaanisha nini huyu? mbona kama ametangulia mbele sana huyu… Neno tata hili… Anamanisha nini kusema hivi usiku huu? Dah sijui nimjibu nini sasa hapa?” kabla sijapata cha kumjibu nikakuta ametuma SMS nyingine imeandikwa “Nina hamu ya kumjua huyo anaenipenda”. Nilipoona amesema hivyo, nikamuelewa alichokua akimaanisha ila alikua ameishaniingiza tamaa juu ya kumpata maana aliposema tu anahamu akili yangu ikawa inaniletea picha za jinsi alivyoumbika, Salma alikua ni dada flani mzuri wa sura na amebalikiwa umbo.

Nikajikuta nimetupia mbali wazo la kumuuliza mambo ya kuolewa, nikamwambia “Sawa, huyo mtu anaekupenda ni mimi”. Alikaa kama dakika 3 hivi bila kujibu mpaka nikaanza kuwaza “Au nimekosea kumwambia? Mbona hajibu? Au anaandika ujumbe mrefu huyu… Dah” lakini ghafla nikakuta kajibu “Mmh Haya, lakini samahani, sijakuelewa vizuri unanipenda kivipi yani?”. Mh alivyosema hivyo nikawanawaza mbona kama anataka kukataa huyu wakati alikua kama anaelewa ninachotaka kumwambia?… Kwamba hajaelewa kweli?… Dah liwalo na liwe, ngoja nimuelekeze tu”. Basi nikatulia nikaandika “Salma, nakupenda sana na upendo wangu kwako nashindwa hata niuelezee vipi kwako ila tambua tu nahitaji tuwe wapenzi. nimejikuta tu nakupenda Salma, nahitaji nafasi katika moyo wako maana moyo wangu umeishauteka.” alafu nikamtumia. Akatulia kama dakika 2 hivi bila kujibu na mimi nikawa nasubiri huku moyo wangu unadunda “Nduh Nduh Nduh”.

Nakumbuka baada ya ukimya wa dakika chache akasema “Kitu gani umependa kutoka kwangu?” nikafikilia ninavyompenda nikaona siwezi elezea kitu gani nampendea maana nimejikuta tu napenda jinsi alivyo hivyo nikamjibu “Nakupenda jinsi ulivyo tu”. Akakaa tena kama dakika 4 ivi alafu akasema “kwani nikoje?” mimi nikamwambia “Ni dada falni mzuri, msafi, unajielewa na mtulivu pia, nahisi ni mungu aliniumbia… Nimejikuta navutiwa kua na wewe ikiwezekana maishani Salma. Naona nakua na furaha nikiwa na wewe. Alafu sijaanza leo kukupenda, nakupenda tangu nakutia machoni siku ile tuliokutana hapo nje”. Nilivyo mwambia hivyo, akaniambia “Kwani siku ile tuliokutana hapo nje ilikua ndio siku yako ya kwanza kuniona?” nikamjibu “Ndio salma, nilipokuona nilihisi nimekutana na malaika”. Basi nikakuta kanijibu ujumbe wa kucheka “Hahahaha” mimi nikamwambia “Kweli tena, sitanii”

Akakaa tena kama dakika 4 hivi alafu akasema “Sawa, mimi mwenyewe nakupenda ila naogopa usijekua unanidanganya mwisho ukaniumiza” mimi kwa haraka haraka nikawa na furaha nikamwambia “Siwezi fanya huo ujinga, Nakupenda sana Salma”. Nikakuta kanijibu “Haya, Nakupenda pia” nilipata furaha ya ajabu mpaka nikataka nipige kelele usiku huo mule ndani. Niliona kama ni bahati kuwa na mahusiano na dada huyo maana alikua ni mzuri na anajipenda sana kiasi kwamba ukimuona barabarani huwezi zani anatokea kwenye nyumba za kupanga, unaweza hisi ni mke wa mtu mwenye pesa sana au ni wale wadada wazuri wa kwenye video.

Basi usiku huo ulikua wa furaha sana na nilikua na hamu tukutane pindi kutakapokucha maana muda huo mvua ilikua inanyesha sana na ulikua muda mbaya tayari. Na kweli kulikucha ila nilichelewa kidogo kuamka kutokana na kuchelewa kulala na kitu cha kwanza kukifanya kilikua ni kumtumia Salma SMS lakini ilionesha kuwa hapatikani kwa muda huo. Nilipotoka nje nikakuta mlango wa Salma unaonekana kama Salma hayupo ndani maana umefungwa kwa nje. Nilivyona hivyo nilikua na vimaswali kichwani mpaka nikaamua nisiende kwenye mafunzo ya kampuni siku hiyo. Nilikaa tu chumbani kwangu, ukafika muda wa kula chakula nikaenda kununua alafu nikarudi nikakaa mlangoni kwangu nikawa nacheza gemu kumsubiri. Kwenye mida ya kama saa 4 asubui hivi nilikua nimechoka kushika simu, niliegemea pembeni ya mlango pale nje, usingizi ukanichukua.

Huko usingizini nikaanza kuota nipo na Salma sehemu nisioijua hata vizuri napambana kumshika na kumkumbatia Salma lakini nashindwa sababu yeye ananisukuma huku akinifokea kama hanijui kwa kusema “Hebu niachie… Wewe Mkaka vipi!… We mkaka!”. Dah ndoto hiyo ilifanya nishtuke toka usingizini na nilipofungua macho mbele yangu nikakuta Madada wawili wamesimama mbele yangu pale mbele ya mlango wangu wananiangalia huku wakiniamsha kwa kusema “Wewe kaka… Wewe kaka”. Basi mimi nikasema “Naam” huku nikiwa najaribu kuyaweka macho vizuri ili niwaone vizuri maana macho yangu yalikua usingizini na hao madada sikujua watakuwepo mbele yangu. Nikawaangalia sura zao haraka haraka nikakuta sura zao ni ngeni.

Basi nikakuta wananisalimia na mimi nikaitikia alafu wakauliza “Samahani kaka, tulikua tunaulizia anapokaa dada mmoja hivi anaitwa Tausi… tunasikia anakaa mitaa hii”. Mimi kwakua nilikua mgeni kidogo kwenye maeneo hayo na nilikua sijafahamiana sana na watu wa mtaa huo, sikuweza mtambua mtu wanaemuulizia hivyo nikawaambia “Ah mimi sijui watu wengi mtaa huu ila hapa hakuna mtu anaitwa tausi” wakanishukuru alafu wakawa wanaondoka. Madada hao walikua wasafi na wamevaa vinguo vifupi vinavyotega macho ya wanaume. Mimi kwa haraka haraka nilivyoona muonekano wao nilihisi huenda wanafanya kazi ya kuuza miili yao maana walikua wameanika vitu nje nje alafu hawajiwazii.

Walivyoondoka tu nikajisemea “Bora wameniamsha maana simu nimeiweka pabaya kiasi kwamba mwizi angepita maeneo haya angechukua simu bila mimi kujua”. Baada ya hapo mawazo ya Salma yakaanza kuteka kichwa changu. Nikaanza kuwaza “Dah Salma nae sijui kaenda wapi?… Naanza mpaka kukosa raha yani. Na hii ndoto nilioiota hapa ni ukweli au imesababishwa na makelele ya waliokua wananiamsha tu? Itakua ni hawa mbwa wameniletea lindoto la ajabu… ila sasa mbona hayupo na hakuniambia jana kwamba hatakuepo leo?”

INAENDELEA….

One thought on “UTAMU WA JUMLA 05 (Simulizi ya Maandishi)”

Leave a comment