Mh alikua amejisogeza karibu yangu na tulikua tumegusana kabisa kiasi kwamba nilikua najikuta nahisi vitu tofauti na kitu ninachokifanya muda huo. Mwili wake mlaini ulileta joto la ajabu mwilini mwangu alipokua karibu yangu maaana alikua ni mwanamke mwenye kila sifa ya kuamsha hisia kwa mwanaume. Ukiachana na hayo yote, alikua ananukia vizuri.
Basi siku hiyo nilifanikiwa kumrushia nyimbo kwenye simu yake na tulipeana hata namba za simu ili tuweze kuwasiliana kwenye simu. Baada ya hapo tulikua tunaurafiki nae na urafiki huo ulikua kama unaelekea kuwa wa kimapenzi hivi japo nilikua sijawahi mwambia nampenda wala yeye hajawahi niambia hivyo.
Kuna siku tulikua tumekaa sehemu moja tunaongea pale nje mlangoni kwangu mida ya jioni… Nakumbuka tulikua tunapiga stori za kawaida huku mimi nimeshika simu yangu naangalia video za vichekesho. Salma alikua pembeni yangu kidogo upande wa kulia. Niliona video moja ikanichekesha sana mpaka nikasema “Hahah angalia video hii” Salma akasogea zaidi kwangu ili aone lakini katika kusogea kwake aliingia mpaka mwilini kabisa, mimi nikawa namuonesha video huku akili ikiwa imehama kutokana na yeye kuja mwilini mwangu. Nakumbuka aliangalia video ile alafu nikamuona akicheka “Hahaha…. wasumbufu hawa” huku akiyatoa macho yake kwenye simu na akaniangalia usoni.
Kwakua mimi akili ilikua haipo tena kwenye video ipo kwake, tukajikuta tumekaa kimya kwa sekunde chache tunaangaliana alafu tunataka kama kusogezeana midomo yetu hivi. Ilikua kama tunataka kuikutanisha midomo hivi lakini ghafla Salma akazuga kwa kushtuka na kusema “Ivi mziki huo unalia wapi?” huku akitoka mwilini mwangu. Na mimi nikajiweka vizuri na kusema “Mh Itakua huko nyuma” na baada ya hapo tukaendelea na stori nyingine ila kiukweli ilibaki kidogo sana kuanza kupimana joto la mwili.
Ukiachana na siku hiyo, kuna siku nyingine tulikaa pamoja sehemu na tulikua tumegusana miili yetu alafu alikua amevaa kinguo kilaini kifupi ambacho kinaonesha mpaka sehemu za juu ya magoti. Tulikua tunaongea mambo ya kawaida tu ila mimi mawazo yangu ya kahama kabisa maana alikua ananigusa gusa ila yeye yupo bize kuongea ongea.
Nilikua namuangalia anavyoongea alafu kichwani nawaza “mwanamke ananukia vizuri huyu… Midomo yake mizuriii… Dah… ananipa majaribu na mapaja yake… Sijui niyaguse? Mh ngoja nijifanye kama nayagusa bahati mbaya maana natamani balaa”. Uvumilivu ukanishinda, nikajikuta tu mkono wangu nimeuweka kwenye moja ya paja lake na lilikua limejaa sana nikaanza kulipapasa kama natafuta vitu hivi. Nakumbuka muda huo alikua anataja nyimbo anazozipenda na kabla hajamaliza, nikauweka mkono wangu. Nilivyo fanya hivyo akaacha kuongea na alishtuka kidogo na akasema kwa kisauti cha chini “OOh.. iiii… Wewe… mkaka nini?… Mbona unafanya hivyo?” Mimi ujasiri ukanikimbia nikazuga nikasema “Ku… Kuna kitu nimeona kama kimedondokea hapa” huku nikiutoa mkono.
Basi aliniangalia usoni kidogo alafu akayatupa macho yake chini kwa aibu huku akiguna “MMh”. Mimi mwenyewe nilifanya kitendo hicho kwa msukumo wa hisia zangu juu yake tu hata sikujielewa, nilipoutoa tukakaa sekunde chache alafu tukaendelea kupiga stori kama kawaida. Salma alikua ni mwanamke mzuri na alikua ananivutia ila uzuri wake ulikua unaniogopesha mpaka kumwambia nakupenda maana alikua anateka hisia mpaka akili zangu zinahama, pia nilikua nahisi ni mke wa mtu na mme wake huenda amesafiri hivyo naweza kutwa nae muda wowote.
Nilikaa kama miezi miwili hivi nilikuwa naongea nae, ninamazoea nae lakini sijamwambia kama nampenda. Ila katika hiyo miezi miwili nilikua kunavitu sivielewi kabisa kwenye maisha yake. Nilikua namuona anaishi peke yake, Sijawahi muona na mwanaume na wala Hafanyi kazi yoyote inayoonekana na karibu kila siku anapika na kula. Nilikua najiuliza hela “Anatoa wapi?” maana hata kutoka nyumbani huwa hatoki mara kwa mara, anaweza kwa wiki akatoka mchana masaa mawili kwa siku moja au mbili tu akarudi nyumbani. Usiku pia huwa anatoka na anarudi asubuhi ila hii katika miezi hiyo miwili niliwahi muona akitoka usiku mara moja tu na alirudi na mchubuko kidogo kwenye paji lake la uso. Nikamuuliza aliniambia alikua kwenye sherehe na kuna mtu alimuumiza kwa bahati mbaya.
Siku moja katika mida ya saa 5 usiku hivi nilikua nikitumiana nae SMS kwenye simu yeye akiwa kwenye chumba chake alicho panga na mimi kwenye chumba changu. Kimvua kilikua kinanyesha siku hiyo nje na kilianza mida ya saa 4 usiku hivi. Nakumbuka katika kutumiana SMS Salma aliniambia “Yani mvua ya leo imeleta baridi hatari… yani nimejifunika shuka mbili nzito lakini bado nahisi baridi” mimi nikasema “Ah mimi huku nina shuka moja jepesiii, fikilia baridi ninayoihisi hapa ni kiasi gani” akasema “hahah wewe basi unatia huluma, Au nikupe shuka moja zito unipe lako jepesi?”. Basi mimi nikajibu “Njoo unipe utakua umenisaidia sana Salma” alafu nikawa nasubiri atakachojibu. Nikakuta anachelewa kujibu nikaanza kuwaza kichwani “Eh mbona anachelewa kujibu huyu, anakuja kweli nini?… Mh kwajinsi alivyoumbika sita mruhusu atoke… Mh na ile mizigo yake aliobeba nitakavyoifanya hata amini…. Mtoto msafi balaa”.

Wakati nikiwaza hayo nikakuta SMS toka kwa Salma imeingia, moyo wangu ukadunda pigo moja kubwa “Nduh” nilipoona SMS imeingia na nilipoifungua nikakuta amesema “Mh ningekuja kukupa ila naogopa”. Nikamjibu “Unaogopa nini sasa?” akajibu “nakuogopa wewe” mimi kama utani nikamwambia “Haha kwanini sasa unamuogopa anaekupenda?” akachelewa kidogo kunijibu alafu akaja kujibu “Mh wewe acha kunirusha roho bana… nani huyo ananipenda?”. Alivyosema hivyo mimi nikapumua kwa nguvu kama mara mbili hivi alafu nikatuliza kichwa nikaandika “Mimi hapa nakupenda. alafu nilitamani ujue hili toka nakuona kwa mara ya kwanza. Nakupenda sana Salma, umeukamata moyo wangu mpaka nashindwa elewa jinsi ya kuelezea upendo nilionao kwako, sitamani nikukose… Nataka uwe mpenzi wangu”. Baada ya kuiandika nikawa kama nimeituma hivi alafu nikaiweka simu pembeni ya kitanda changu kisha nikalala chali nikawanaangalia juu huku nikiwanawaza “Dah sijui atakubali huyu… Akikubali nitamfaidi kweli na ile mizigo ya nyuma alafu Kabinuka… Kifua chake tu kizuri sijui ndani atakuaje. Mtoto namuona mtamu kabla sijamla Dah… nilipanga kutokumpa moyo mwanamke ila huyu sjui kaniibia moyo?” alafu hapo hapo nikaanza kuwaza tena “Mh ila huyu mwanamke nikimtongoza na akikubali alafu baadae mtu akaja kusema natembea na mke wake si nitaharibu kilakitu nilichojia huku Dar?… Wazazi wangu wakisikia nimepata matatizo kwasababu ya kutembea na mke wa mtu watanionaje? wataendelea kutupa hela zao kwaajili yangu kweli? Mh sidhani”.
Nikakuta Ghafla SMS toka kwa Salma imeingia imeandikwa “Wewe, mbona kimya?” nikashtuka nikaangalia vizuri nikakuta SMS nilioiandika kumbe sikuituma, hivyo haikwenda. Nikajicheka kidogo huku nikijisemea “Bora hata haikwenda, ngoja nimuulize maswala ya kuolewa vizuri maana ananitamanisha lakini nikienda kichwa kichwa naweza umia mimi. Ila kama huyu ni mke wa mtu basi waliosema mke wa mtu mtamu hawajakosea kabisa… Ngoja nimuulize” nikaifuta ile SMS niliotaka kuituma. Nilivyofuta nikamwambia tu “Salma, nikuulize Swali?” alafu ikapita kama dakika moja nikakuta anajibu “Ah hapana usiniulize, nijibu kwanza swali langu”….
INAENDELEA….
One thought on “UTAMU WA JUMLA 04 (Simulizi ya Maandishi)”